Kumbukizi: Sokoine ndiye alibomoa uchumi wa nchi, na utawala wa sheria. Sioni chochote cha kumsifu, urathi wake uandikwe upya

Toka tumepata uhuru kuna kipi cha maana chini ya utawala upi tumekifanya? Wakoloni mfano walijenga shule kubwa na nzuri ambazo sisi kwa karne hii nyingine tumezigeuza vyuo vikuu wakati ni shule za sekondari.
 
Hhh mkuu unakatisha tamaa..Shule YouTube
Hapana mkuu, mim nasema ukweli tu. Japo ukiangalia juu juu unaweza ona ni jambo la maana lakini tumeua elimu yetu kwa mambo ya kisiasa. Weka shule chache zenye tija na walimu wa kueleweka. Shule ya kata walimu wa Voda fast( crushing program) kama wakumbuka
 
Uchumi uliporomoshwa na vita vya Kagera. Tulioshiriki vita vile runajua mengi acha kabisa. Kutoka Kagera hadi mpaka wa Sudan kwa Mguu huku tukisafisha vichaka. lshia hapo hapo dogo.
Tulikuwa wazalendo wa kweli.
Huyu ni kichaa mwenye simu ya android asamehewe.
 
Mkuu yawezekana wewe ni 'mtoto wa 2000' kwa namna ya uandishi wako na ulivyoelezea jambo hilo kinafiki.

Kifupi ni kwamba, baada ya 'vita vya Kagera' na Nyerere kutangaza waTz 'kujifunga mkanda miezi 18', wafanya biashara mafisadi walitumia slogan hiyo kuficha bidhaa muhimu ionekane ugumu wa maisha umebarikiwa na Serikali.

Hali hiyo ilivuruga kabisa uchumi na maisha ya raia.

Hali ilikuwa ngumu mno takribani kwa miaka mitano(1980-1984).
Maduka yalikuwa totally empty, nguo sukari, sabuni, C. Oil etc etc havikuwepo madukani vilifichwa.

Sokoine alikuja kuchukua hatua ya kuwabana mafisadi walioficha bidhaa, ninasema walikuwa wameficha kwa sababu walivyosikia kuna operesheni hiyo wakavitoa vitu kwenye maghala yao usiku na kwenda kuvitupa.

Bidhaa nyingi zilitupwa zikiwemo na magunia ya pesa wakihofia kutiwa nguvuni wakikwepa mkono wa sheria.

Maelezo ya kisa hiki ni marefu sana,
Itoshe kusema kwamba kumlaumu Sokoine bila kupongeza juhudi zake za kupigania maisha ya waTz ni kumtendea dhulma.

Aliwabana mafisadi kwa manufaa ya waTz na siyo kusema kwamba katika zoezi hilo alitia mkono kujinufaisha kama viongozi wa sasa wanavyofanya, hapana.

na kifo chake kilikuwa ni pigo kuu kwa Raia na kilitikisa nchi.

Tangia kifo chake 1984 hadi leo sijawahi kusikia ama kusoma popote mtu kaandika akimlaumu Sokoine kwa ubaya wowote alioifanyia nchi na raia wake, isipokuwa wewe tu!

Karudie tena kusoma historia yake, ukiendelea kuleta ubishi wa kijuaji na stori zako za uongo hapa tutaelewa kuwa unatumika, kuna watu wapo nyuma yako kuchafua legacy ya Sokoine Waziri mkuu aliyependwa sana kwa dhati kabisa na raia wa Tz kutokana na utumishi wake uliotukuka.
 
Nchi Ina utajiri wa Mashujaa mitandaoni, kulalamika na kukosoa kazi rahisi Sana.
 
Siku tukiamua kuwa wa kweli na kujifunza kutokana na makosa itakuwa rahisi zaidi kusonga mbele.
VAN ARKADIE, BRIAN. β€œTHE TANZANIAN SOCIALIST EXPERIMENT: SERIOUS OPTION OR ROMANTIC DREAM?” PERSPECTIVES ON POLITICS, PRODUCTION AND PUBLIC ADMINISTRATION IN AFRICA: ESSAYS IN HONOUR OF OLE THERKILDSEN, edited by Anne Mette KjΓ¦r et al., Danish Institute for International Studies, 2015, pp. 255–71. JSTOR, http://www.jstor.org/stable/resrep30721.20. Accessed 2 Oct. 2024.
 
Kipindi anafanya hayo yote,Mwalimu alichukua hatua gani? Kulinda uchumi wa nchi ?
Hii Ni kweli, kukawa na kipindi Cha mikingamo redio Tanzania. Ila Ni waziri mkuu aliyependwa kuliko wote. Warioba ndiye aliyekuwa waziri wa sheria na mwanasheria mkuu wa Serikali, alichukua jukumu gani kwa sheria zile? Angejiuzulu ningemwelewa
 
Uchumi uliporomoshwa na vita vya Kagera. Tulioshiriki vita vile tunajua mengi acha kabisa. Kutoka Kagera hadi mpaka wa Sudan kwa Mguu huku tukisafisha vichaka. lshia hapo hapo dogo.
Tulikuwa wazalendo wa kweli.
Nina Mzee Mtaani hapa ana sema yeye ndio walikua Front line, ktk vita, baada ya vita Nyerere aka waambia sina cha kuwalipa
 
Uchumi uliporomoshwa na vita vya Kagera. Tulioshiriki vita vile tunajua mengi acha kabisa. Kutoka Kagera hadi mpaka wa Sudan kwa Mguu huku tukisafisha vichaka. lshia hapo hapo dogo.
Tulikuwa wazalendo wa kweli.
Ni upuuzi tupu.

Kwani kulikuwa na ULAZIMA gani kwa Tanzania katika kupigana vita hiyo?? Nchi ilinufaika na Nini au ilipata faida gani kutokana na vita hiyo?

Aliyewahi kuwa Rais wa Marekani Bw.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…