Mateo Kovasic
JF-Expert Member
- Aug 9, 2022
- 420
- 335
BALOZI wa Tanzania nchini Malawi, Mheshimiwa Humphrey Polepole ameweka wazi mambo manne ambayo unaweza kufanyiwa Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi unayesimamia haki na ukweli bila kupindisha maneno.
“Kwenye Chama cha Mapinduzi ukiwa umenyooka hivi yaani umenyooka hivi rula inasubiri mambo 4 wanaweza kukufanyia wahuni, sababu wahuni wapo kwenye CCM, wako wahuni kwenye Chama cha Mapinduzi na mimi nimeshiriki na wenzangu kwenye uongozi kupambana nao na umesikia sasa hivi viongozi wetu wanahangaika kusema wahuni wasivuruge uchaguzi wa mwaka kesho uchaguzi wa chama”.
Kwa mujibu wa PolePole ndani ya CCM ukiwa mkweli na msimamia haki na kunyoosha maneno mithili ya rula ndani ya CCM utafanyiwa mambo makuu manne yafuatayo
Vitu vyote hivi kwangu vimeshindikana kwa kuwa namtegemea sana Mungu wa mbinguni ndio maana watu wanatapatatapa.
- Watakupiga Fitna, Fitna kupeleka maneno ya uongo na nini kwa viongozi
- Wakishindwa fitna utashushiwa zengwe, zengwe linatengenezwa Skendo lisilokuwa na kichwa wala miguu linashushwa
- La tatu utalogwa unakufa, unapigwa stroke hivi hivi
- Watakuja wajaribu kukuumiza kwa hiyo unatakiwa kuwa makini
CHANZO: Dar24 Online
Tuwekee video yake.