KUMBUKIZI: Ukiwa mkweli ndani ya CCM, Mambo 4 yatakukuta - Humphrey Polepole

Wanaeafanyia hata wasio ccm, pale wanapogusia keki ya taifa. Mfano ni kwa hili jambo la Dp world, wale wanaokosoa mkakati wamewekwa kwenye line ya kupatia hizo dozi...
 
Ni lazima ukiwa tofauti watakudhuru kwa sababu huwezi kubadilika kutoka fisi na kuwa swala lazima wakutafune tu

Taifa hili bila wote bungeni kuwa na msimamo mmoja na kukemea wizi na rushwa, hongo, kubebana labda mtafika mbali

Ila kama mmoja au wawili watataka kubadilika basi wataitwa viherehere tena mpaka top watawaita hivyo
 
Kayasema hayo yeye akiwa anatesekea wapi
 
Mbona alisema kitambo sana kabla hata ajawa balozi wewe ndo unaleta leo huu uzi
 
Sasa nimeanza kuelewa kwanini utawala wa Samia ulifuta Shule ya Uongozi ya Hamfrey Pole pole , na kumfurusha kutoka Kwenda kumpa kazi Mbali huko Cuba.

Katika series ya shule za uongozi kutoka kwa Hamfrey Pole pole ni kama alikuwa akitoa siri kali sana za ndani, kufichua maovu ya serikali ya CCM, Kiukweli ukienda kupitia Shule ya Uongozi utagundua yote aliyosema Pole Pole ndo haya tunayaona. Kuna kikundi cha watu ndo Kinaendesha nchi na Rais yeye ni kama mwanasesere amekaa pale ila hana maamuzi, alinukuliwa, kwa akili za wazi huwezi kufikiri kwa Roho na Moyo wake Mama Samia anaweza kuagiza watu kuua au Kubaka, bali ni kikundi ambacho ndo kimeishikilia nchi, ambacho hata Pole pole na wana CCM wanakitambua, na kinaogopesha kweli kweli. Na Hicho kikundi cha Watu wachache kinachoendesha Serikali ndo kilimuondosha Magufuli, ambacho hata hivyo magufuli angemaliza miaka mitano angekifurusha mana kilishaishiwa nguvu kidogo, sasa kimeamka na kina nguvu kweli kweli.

Tafuteni vipindi vile kuna mengi sana aliongea, leo naamua kuongelea Moja ya Vitu alitoa Pole pole katika shule ya Uongozi, alisema CCM Ukiwa umenyooka na msimamo wa Haki , thabiti kuliko rula basi mambo manne yatakukuta, ambayo ni kama ifuatavyo
1. Utapigwa Fitna
2. Utashushiwa Zengwe, Skendo utaletewa
3. Utalogwa , stroke
4. Utatekwa, utaumizwa

Sasa haya mambo ndio anayopitia Mpina na Gwajima, CCM Sio chama , ni chama cha majasusi. Sasa Gwajima ana Siri nyingi sana Za CCM ila sasa ndo wanamzibiti.


View: https://youtu.be/I7lAYC-LRU4?si=7krm2MV4c0GIsRZB
Pia naendelea Kusema , katika maraisi wote ambaye angeamua kubadili katiba na angefanikiwa basi alikuwa Magufuli, Maraisi wengine walikuwa too weak. Inawezekana walitaka kubadili , ila walikuwa too weak, Na Mama Hilo la katiba haliwezi , si jasiri kiasi Hiko, sidhani mama Angeweza kuanzisha Mradi wa bwawa la nyerere, wala mradi wa reli, mana unapingana na ineterest za wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…