Kumbukizi ya miaka 20 ya Moses Nnauye imetegua vitendawili vingi

Kumbukizi ya miaka 20 ya Moses Nnauye imetegua vitendawili vingi

Apart from hayo makundi, unadhani hakuna watanzania wengine wenye karama ya uongozi, sasa unajiita raisi ajaye alafu unaishi kwa kutegemea kudra za waliokupatia sh 100 kwenye bil walizochota then unaona wanakujali
Sio lazima niwe Raisi wa Tanzania Hata Burundi,Rwanda na Congo panafaa!Nitawatumia Boys 2 men kusimikwa huko!!!
 
Kwenye Urais Makamba mtoe! Naweza kukubaliana na wewe kwa wengine,na usije shangaa Rais akaja kua Ridhiwan!

Kuhusu Sauti zao kunaswa,hata Sauti ya Kikwete ilinaswa kwenye yale maongezi,sema kwa sababu yakutunza heshima za Kikwete haikuweza kutolewa,lakini Jiwe aliwahi kupiga dongo,kwamba kuna wastaafu wanawashwa washwa,badala wakae watulie zao na maisha yao

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Hiyo kauli ya kuwashwawashwa mbona aliitoa kitambo kabla ya sauti kuvuja?
 
Umeniwahi kuandika huu uzi. Ila kila kitu kina mwanzo na mwisho.

Wakiendeleza siasa zao za kujiona wengine hawafai kuongoza hii nchi kifuatacho ni kuwaachia chama chao.

Hii nchi inaenda kukombolewa 2025. JPM hakuwamaliza wahuni.
So na nyie sasa mnataka katiba mpya? Au wahuni mtawaondoaje?
 
ABUU KAUTHAR

Tukio la kawaida la mkusanyiko wa watu kumkumbuka mpendwa wao limenifumbua akili na kuyajua mambo mengi kuhusu siasa za nchi hii na asili ya uhusiano wa karibu wa baadhi ya watu.

Nazungumzia kumbukizi ya miaka 20 tangu kufariki kwa mmoja wa viongozi mahiri wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Brigedia Jenerali Moses Nnauye, ambaye, kama cheo kinavyojieleza, pia aliwahi kuhudumu serikalini, jeshini huku akikumbukwa zaidi kwa kipawa chake cha muziki.

Ukiacha familia ya Nnauye mwenyewe (mjane na watoto), walikuwepo pia Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, na Makatibu wakuu wa CCM wastaafu Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba.

Orodha hii ikanikumbusha tukio lile enzi ya awamu ya tano ziliponaswa sauti zikimsema vibaya marehemu Rais wa Awamu ya Tano, John Pombe Magufuli. Ni wazee hawa, (ukimuondoa Kikwete) ndio waliosikika wakimsema vibaya marehemu. Pia alikuwemo Nape, ambaye katika mazungumzo na Mzee Makamba alisikika akimuita ‘baba’ kwa heshima zote.

Hawa jamaa pamoja na marehemu ambaye walijikusanya kumkumbuka, wametoka mbali na sio ajabu kwamba wanazeeka wakiwa na ukaribu mkubwa, sio wao tu bali hata familia zao! Naamini wapo sahihi watu waliosema kuwa kuna ‘family coalition’ (muungano wa familia) unaosaidiana kuhakikisha wanatawala nchi hii.


Wote watatu niliowataja licha ya kulelewa ndani ya chama, pia walikuwa wanajeshi mahiri, enzi hizo wakati chama kimeshika utamu na hatamu zikiitangulia sio tu serikali bali hata jeshi. Kikwete, hadi anatoka jeshini alikuwa Luteni., Kinana alikuwa Kanali na Makamba alikuwa Luteni huku marehemu waliyekuwa wakimuadhimisha akiwa Brigedia Jenerali. Hii inaelezea hisia za kujiona wanastahili zaidi kukamata uongozi wa nchi wanayoona kuwa wameipigania chamani, jeshini na serikalini.

Ukiangalia historia zao, walianza kwenye chama pamoja,wakahudumua tena pamoja jeshini na kisha serikalini. Nnauye na Makamba walikuwa na mengine ya kuwaunganisha: sanaa. Wote walikuwa waimbaji enzi hizo. Kwa kweli, sikuwa najua kuwa Nnauye alikuwa ndio John Komba wa kwanza!

Hotuba ya Makamba ilifichua siri nyingi, ambapo alielezea ukaribu wake mkubwa na Nnauye kiasi kwamba bosi wake huyo wa zamani alimfia mkononi, akimsaidia kumtamkisha neno muhimu kwa Muislamu kulitamka kabla ya kifo: Laa Ilaaha Illa llah (Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu).

Kinana alisema katika hotuba yake kuwa Nnauye aliacha mafunzo mawili makubwa: Kwanza kiongozi huandaliwa na pilli, mafanikio huja kwa kuwa na ‘organization’ nzuri katika taasisi. Kwangu, kauli hizi ni dongo kwa marehemu JPM ambaye anajulikana kama kiongozi aliyekosa malezi ya chama na ambaye hakuna na weledi katika organization ya chama na badala yake alikuwa mtu wa ‘matamko’.

Wapo watu waliotafsiri kusanyiko lile kuwa sio tu ni maadhimisho ya kumbumbuka Mzee Nnauye bali pia shukrani kwa kundi lile kwa Mwenyezi Mungu wao kwa kuwatoa kifungoni baada ya kuwekewa alama ya X na JPM. Sio siri kuondoka kwa JPM kumewapa ahueni Mzee Makamba na Kinana ya walau kufurahia uhuru na kutoishi kwa wasiwasi tena! Sio siri pia kuwa kuondoka kwa JPM kumefufua matumaini ya kupanda kisiasa kwa wakina Nape, Ridhwani na Januari.


Ninachokiona ni kuwa hizi familia ziko ‘connected’ mno na kuna makubaliano mengi ya kifamilia. Nani alijua kuwa kumbe wakina Nape walikabidhiwa kwa Makamba awalee baada ya kufariki kwa mzee wao? Nani hajui kuwa Kikwete kambeba sana Januari na kumlea kisiasa? Kinana naye akawa karibu na Nape enzi zao chamani akimpa madini ya ‘organization’ ambayo naye alijifunza kwa Mzee Nnauye? Yapi mengine hatuyajui katika mikataba hii ya kifamilia?

Nikiangalia mustakbali wa nchi, nikirejea sauti zile zilizovuja za kumponda JPM hasira zao sitashangaa hawa wababe wakiichukua nchi baada ya Rais Samia kustaafu. Tayari kuna tetesi kuwa Rais Samia anapokea ushauri kutoka Mzee wa Chalinze, ambaye ndiye mzee wa hawa vijana.

Halafu vijana wako vizuri na wamejipanga hasa Januari ambaye anajulikana kama kipenzi cha watu wa mitandaoni hasa Twitter (Twitter darling), ingawa kwa upande mwingine sio siri rekodi yake ya utendaji haivutii, haishtui.


Bila vikwazo vingine njiani, naiona serikali huko mbele ya Rais Januari, Waziri Mkuu Nape huku wakina Ridhwan, Bashe wakipewa majukumu kubwa katika Baraza la Mawaziri.

Tusubiri na tuone


Nani sasa aliyewapa hati miliki ya kutawala? Tuwape watu madaraka kwa uwezo na sifa zao. Sio kurithishana
 
Katiba mpya utaipata wapi ndugu? Katiba haipatikani kwa maneno laini.

Jifunze hata kwa kuangalia nchi zote zilizofikia hatua ya kuandika katiba mpya nini kilitokea kwanza?
Walibondana hadi wale wabishi walioshika hatam walipofumuliwa 0713... ndo katiba ikapatikana
 
Ujinga tu! Kwani Nnauye ni maarufu kuliko Rashid Kawawa? Ni maarufu kuliko Oscar Kambona? Ni maarufu kuliko akina Kasela bantu. Hapa kuna kiwewe na kuandaa urithi wa madaraka. Siku hizi namuona Nape ana panic kila wakati, anaona amesahaulika. Bahati mbaya Nchimbi ambaye ni adui yake namba moja amerudishwa. Katikati kuna ndumila kuwili, Kikwete.

Ni hivi Nnauye alikuwa na nafasi kama wengine katika chama. Aliwabeba akina makamba baada ya kufukuzwa ualimu kwa kumpa mwanafunzi mimba, na leo hii hasemi ujinga wake. Walikuwepo akina kanali Mwasomola ambao leo hii hawasikiki, akina Kolimba. Mwinyi alipopata urais Kikwete alikuwa katibu wa CCM wa wilaya Masasi au Nachingwea ambako alifahamiana na Nnauye. Nnauye ndo mtu aliyemuombea uwaziri Kikwete bna kwa upendeleo wa kidini ndani yake, Mwinyi akamteua kuwa Naibu waziri akitokea wilayani, siyo hata mkoani!
Leo hii Kikwete anamtukuza Nnauye siyo kwa umaarufu wa kisiasa, bali kwa kumshika mkono na kumtambulisha kwa Mwinyi. Nnauye naye alilindwa na Kikwete akapewa mkuu wa wilaya na kumuepusha na uadui wake na Nchimbi. Wakati huo huo Nchimbi anajiona ni raifiki sana wa Kikwete. Undumila kuwili huo!!!!
Uadui wa Nchimbi na Nape ulianzia wapi mkuu kama hutojari nifumbue macho wengine siasa imetupita pembeni.
 
Walibondana hadi wale wabishi walioshika hatam walipofumuliwa 0713... ndo katiba ikapatikana
Ewaaaaa! Bila hayo kufanyika hakuna katiba halisi inaweza kuandikwa. Pigia mstari neno HALISI.

Kunaweza kuandikwa katiba ya kisanii lkn Ikawa si ile inayojibu changamoto za nchi husika bali inayompendelea mtawala.
 
Sisi Sukuma Gang hatutakubali kabisa lazima turudi ulingoni tena, afe beki afe kipa,ujinga wakati wa kwenda tu,tumeshajua kila kitu walichofanya hawa Msoga Gang.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums
Genge la Wasukuma hawatafika popote, hawana uwezo wa kifedha lakini wanao wingi wa watu. Hata kipindi ya JPM walikuwa wamegawanyika na kuanza kuwa na ubaguzi wa kimaeneo.
 
Sisi Sukuma Gang hatutakubali kabisa lazima turudi ulingoni tena, afe beki afe kipa,ujinga wakati wa kwenda tu,tumeshajua kila kitu walichofanya hawa Msoga Gang.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Dawa yenu ni kuwaamsha wananchi kuwakataa wote make nia zenu si njema... mnawachezea wananchi wanafikiri ccm ni chama kumbe ni genge la kinafiki na ujambazi...
 
Katiba mpya iliyo thabiti ndio itatoa fursa sawa hata kwa mtoto wa muuza vitumbua kupenya hadi katika meza kuu yenye keki ya taifa.
Vingenevyo ni maumivu tu.
Mbona John Pombe Magufuli na Samia Suluhu Hassan wamepenya hadi hightable kwa Katiba hii mbovu
 
Ama kweli nchi hii ni ya wenye nchi.

Sukuma gang watapukutishwa sana siku za mbeleni.

Nawaonea huruma sana sukuma gang!
Kati ya vitu tunavyo weza kuja kuvijutia baadaye ni haya majina tunayo yaandika sana Sukuma gang ,Msoga gang na mengine yanayo fanana na hayo.

Nchi yetu ni ya watanzania wote bila kujari mkoa au Kijiji anacho tokea.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom