Kumbukizi ya miaka 20 ya Moses Nnauye imetegua vitendawili vingi

Wakati Sukuma Gan wanapukutishwa, jiulize wewe na uzao wako mtafaidika vipi akina Nape na January wakiwa wanakula keki ya taifa?
Asee siku hizi JF imevamiwa na watoto wengine ID za zamani lakini michango yao kama ushabiki wa Alikiba na Diamond. Eti sukuma gang wakome nchi ina watu wazima wenye akili timamu zaidi ya mil 10 then watu wanashabikia circle ya watu wasiozidi 1000 wanajiona wajanja. Mbaya zaidi unakuta kundi analoshabikia mtu hawamjui na hana direct benefits endapo watashika madaraka
 
Huwa nasikitika sana nionapo mtu mwenye akili timamu anapoacha kufikiria maslahi mapana ya nchi hii; badala yake anasifia na kushangilia siasa za hovyo as if hili ni jambo jepesi au anaweka ushabiki kama wa mpira.
 
What do we say to the god of death? (Not today)
 
Sisi Sukuma Gang hatutakubali kabisa lazima turudi ulingoni tena, afe beki afe kipa,ujinga wakati wa kwenda tu,tumeshajua kila kitu walichofanya hawa Msoga Gang.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Tatizo mnatumia maguvu ya Kisukuma wenzenu wamewekeza kwenye akili na mipango madhubuti ya muda mrefu. Kamwe hamtawaweza mpaka mshapigwa bao. Ushauri wangu if you can't defeat them join them.
 
Mnajidanganya, kabla ya 2025 tutakuwa tumesharudisha himaya yetu.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kama baba yako ni fundi viatu, akakuandaa kuwa fundi viatu, ukawa fundi viatu wenye viatu watakusifia kweli...." Yaani fundi kama baba yake"

Hata sasa kuna watu wanaandaliwa na system kuwa raisi wa JMT 2035-2045. Sasa wewe mtoto wa fundi cherehani kaa hapo ukijifunza cherehani ukifikiri katiba ndo itakupa nafasi ya kugombea uraisi sababu wewe ni Mtanzania. Hii ni nchi sio kikoba.
 
Katiba mpya iliyo thabiti ndio itatoa fursa sawa hata kwa mtoto wa muuza vitumbua kupenya hadi katika meza kuu yenye keki ya taifa.
Vingenevyo ni maumivu tu.

Bado haitafua dafu
Hao watu waone ivo ivo
Kachemka JPM sembuse Katiba ambayo ni makaratasi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wakati Sukuma Gan wanapukutishwa, jiulize wewe na uzao wako mtafaidika vipi akina Nape na January wakiwa wanakula keki ya taifa?
Kiroho changu tu kitasuuzika. Maana sukuma gang mlijawa na maneno ya kifedhuli, inda na ubaladhuli
 
ABUU KAUTHAR

Tukio la kawaida la mkusanyiko wa watu kumkumbuka mpendwa wao limenifumbua akili na kuyajua mambo mengi kuhusu siasa za nchi hii na asili ya uhusiano wa karibu wa baadhi ya watu.

Nazungumzia kumbukizi ya miaka 20 tangu kufariki kwa mmoja wa viongozi mahiri wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Brigedia Jenerali Moses Nnauye, ambaye, kama cheo kinavyojieleza, pia aliwahi kuhudumu serikalini, jeshini huku akikumbukwa zaidi kwa kipawa chake cha muziki.

Ukiacha familia ya Nnauye mwenyewe (mjane na watoto), walikuwepo pia Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, na Makatibu wakuu wa CCM wastaafu Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba.

Orodha hii ikanikumbusha tukio lile enzi ya awamu ya tano ziliponaswa sauti zikimsema vibaya marehemu Rais wa Awamu ya Tano, John Pombe Magufuli. Ni wazee hawa, (ukimuondoa Kikwete) ndio waliosikika wakimsema vibaya marehemu. Pia alikuwemo Nape, ambaye katika mazungumzo na Mzee Makamba alisikika akimuita ‘baba’ kwa heshima zote.

Hawa jamaa pamoja na marehemu ambaye walijikusanya kumkumbuka, wametoka mbali na sio ajabu kwamba wanazeeka wakiwa na ukaribu mkubwa, sio wao tu bali hata familia zao! Naamini wapo sahihi watu waliosema kuwa kuna ‘family coalition’ (muungano wa familia) unaosaidiana kuhakikisha wanatawala nchi hii.

Wote watatu niliowataja licha ya kulelewa ndani ya chama, pia walikuwa wanajeshi mahiri, enzi hizo wakati chama kimeshika utamu na hatamu zikiitangulia sio tu serikali bali hata jeshi. Kikwete, hadi anatoka jeshini alikuwa Luteni., Kinana alikuwa Kanali na Makamba alikuwa Luteni huku marehemu waliyekuwa wakimuadhimisha akiwa Brigedia Jenerali. Hii inaelezea hisia za kujiona wanastahili zaidi kukamata uongozi wa nchi wanayoona kuwa wameipigania chamani, jeshini na serikalini.

Ukiangalia historia zao, walianza kwenye chama pamoja,wakahudumua tena pamoja jeshini na kisha serikalini. Nnauye na Makamba walikuwa na mengine ya kuwaunganisha: sanaa. Wote walikuwa waimbaji enzi hizo. Kwa kweli, sikuwa najua kuwa Nnauye alikuwa ndio John Komba wa kwanza!

Hotuba ya Makamba ilifichua siri nyingi, ambapo alielezea ukaribu wake mkubwa na Nnauye kiasi kwamba bosi wake huyo wa zamani alimfia mkononi, akimsaidia kumtamkisha neno muhimu kwa Muislamu kulitamka kabla ya kifo: Laa Ilaaha Illa llah (Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu).

Kinana alisema katika hotuba yake kuwa Nnauye aliacha mafunzo mawili makubwa: Kwanza kiongozi huandaliwa na pilli, mafanikio huja kwa kuwa na ‘organization’ nzuri katika taasisi. Kwangu, kauli hizi ni dongo kwa marehemu JPM ambaye anajulikana kama kiongozi aliyekosa malezi ya chama na ambaye hakuna na weledi katika organization ya chama na badala yake alikuwa mtu wa ‘matamko’.

Wapo watu waliotafsiri kusanyiko lile kuwa sio tu ni maadhimisho ya kumbumbuka Mzee Nnauye bali pia shukrani kwa kundi lile kwa Mwenyezi Mungu wao kwa kuwatoa kifungoni baada ya kuwekewa alama ya X na JPM. Sio siri kuondoka kwa JPM kumewapa ahueni Mzee Makamba na Kinana ya walau kufurahia uhuru na kutoishi kwa wasiwasi tena! Sio siri pia kuwa kuondoka kwa JPM kumefufua matumaini ya kupanda kisiasa kwa wakina Nape, Ridhwani na Januari.

Ninachokiona ni kuwa hizi familia ziko ‘connected’ mno na kuna makubaliano mengi ya kifamilia. Nani alijua kuwa kumbe wakina Nape walikabidhiwa kwa Makamba awalee baada ya kufariki kwa mzee wao? Nani hajui kuwa Kikwete kambeba sana Januari na kumlea kisiasa? Kinana naye akawa karibu na Nape enzi zao chamani akimpa madini ya ‘organization’ ambayo naye alijifunza kwa Mzee Nnauye? Yapi mengine hatuyajui katika mikataba hii ya kifamilia?

Nikiangalia mustakbali wa nchi, nikirejea sauti zile zilizovuja za kumponda JPM hasira zao sitashangaa hawa wababe wakiichukua nchi baada ya Rais Samia kustaafu. Tayari kuna tetesi kuwa Rais Samia anapokea ushauri kutoka Mzee wa Chalinze, ambaye ndiye mzee wa hawa vijana.

Halafu vijana wako vizuri na wamejipanga hasa Januari ambaye anajulikana kama kipenzi cha watu wa mitandaoni hasa Twitter (Twitter darling), ingawa kwa upande mwingine sio siri rekodi yake ya utendaji haivutii, haishtui.

Bila vikwazo vingine njiani, naiona serikali huko mbele ya Rais Januari, Waziri Mkuu Nape huku wakina Ridhwan, Bashe wakipewa majukumu kubwa katika Baraza la Mawaziri.

Tusubiri na tuone

Uzi hai kwa miaka 30 ijayo
 
Point of correction.
JK ametoka jeshini akiwa ni Luteni kanali na sio luteni.
Kuna tofauti kubwa kwa rank kati ya luteni na luteni kanali.
Jeshini kwa maafisi rank ya kwanza ya kuingia ni
Luteni Usu
Luteni
Kateni
Meja
Luteni Kanali
Kanali then vinaanza vyeo vya kijenerali
Brig. Jenerali
Meja Jenerali
Luteni Jenerali, na cheo cha juu kabisa ni
Jenerali ambae mara nyingi pia ndio Mkuu wa Majeshi (Chief of Defense Forces)

Ni vema kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja, ikumbukwe rank aliyofikia JK sio ilikuwa juu ukimlinganisha na mzee Makamba.
 
Shukran
 
ni mimi tu au? maana waliohudhudria hafla hii mbona naona kama wamechaguana chaguana, kuna kundi silioni kama limetuma mwakilishi.
 
Wakati Sukuma Gan wanapukutishwa, jiulize wewe na uzao wako mtafaidika vipi akina Nape na January wakiwa wanakula keki ya taifa?
Wakati wa Mwinyi na Kikwete sisi wazee shamba na biashara tulifaidi sana tu.Kipindi cha Kikwete mtu ulikuwa ukilima zako ekari 2 tu za zao lolote,ulikuwa unapiga pesa maana bei sokoni ilikuwa vizuri.
Lakini tawala zingine na hiyo ya Magu,kila kitu kikafa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba nitumie kiingereza ili uelewe namaanisha nini. I meant you feel happy to be defiled. Kikwete, and co are desecrating our country yet we have people like you who feel the sweetness of their acts! What a shame!
Sidhani kama kuna mtu aliyeinajisi nchi kama Magufuli...
 
Kila taifa kuna loyal family katika utawala ukianza Marekani kuna Rais George Bush Senior na George Bush Junior wote wametawala kwa wakati tofauti huko Kenya kuna Rais Jomo Kenyatta na Rais Uhuru Kenyatta. Si ajabu na hapa Tanzania tukapata Rais kutoka kwenye mfumo huo.
Labda km zenj si sehem ya nchi hii,lkn picha tayr ishachoreka huko na ilifanywa kimkakati si kwa baht nasib
 
Back
Top Bottom