Kumbukizi ya miaka 20 ya Moses Nnauye imetegua vitendawili vingi

View attachment 2035696
ABUU KAUTHAR

Tukio la kawaida la mkusanyiko wa watu kumkumbuka mpendwa wao limenifumbua akili na kuyajua mambo mengi kuhusu siasa za nchi hii na asili ya uhusiano wa karibu wa baadhi ya watu.

Nazungumzia kumbukizi ya miaka 20 tangu kufariki kwa mmoja wa viongozi mahiri wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Brigedia Jenerali Moses Nnauye, ambaye, kama cheo kinavyojieleza, pia aliwahi kuhudumu serikalini, jeshini huku akikumbukwa zaidi kwa kipawa chake cha muziki.

Ukiacha familia ya Nnauye mwenyewe (mjane na watoto), walikuwepo pia Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, na Makatibu wakuu wa CCM wastaafu Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba.

Orodha hii ikanikumbusha tukio lile enzi ya awamu ya tano ziliponaswa sauti zikimsema vibaya marehemu Rais wa Awamu ya Tano, John Pombe Magufuli. Ni wazee hawa, (ukimuondoa Kikwete) ndio waliosikika wakimsema vibaya marehemu. Pia alikuwemo Nape, ambaye katika mazungumzo na Mzee Makamba alisikika akimuita ‘baba’ kwa heshima zote.

Hawa jamaa pamoja na marehemu ambaye walijikusanya kumkumbuka, wametoka mbali na sio ajabu kwamba wanazeeka wakiwa na ukaribu mkubwa, sio wao tu bali hata familia zao! Naamini wapo sahihi watu waliosema kuwa kuna ‘family coalition’ (muungano wa familia) unaosaidiana kuhakikisha wanatawala nchi hii.

Wote watatu niliowataja licha ya kulelewa ndani ya chama, pia walikuwa wanajeshi mahiri, enzi hizo wakati chama kimeshika utamu na hatamu zikiitangulia sio tu serikali bali hata jeshi. Kikwete, hadi anatoka jeshini alikuwa Luteni., Kinana alikuwa Kanali na Makamba alikuwa Luteni huku marehemu waliyekuwa wakimuadhimisha akiwa Brigedia Jenerali. Hii inaelezea hisia za kujiona wanastahili zaidi kukamata uongozi wa nchi wanayoona kuwa wameipigania chamani, jeshini na serikalini.

Ukiangalia historia zao, walianza kwenye chama pamoja,wakahudumua tena pamoja jeshini na kisha serikalini. Nnauye na Makamba walikuwa na mengine ya kuwaunganisha: sanaa. Wote walikuwa waimbaji enzi hizo. Kwa kweli, sikuwa najua kuwa Nnauye alikuwa ndio John Komba wa kwanza!

Hotuba ya Makamba ilifichua siri nyingi, ambapo alielezea ukaribu wake mkubwa na Nnauye kiasi kwamba bosi wake huyo wa zamani alimfia mkononi, akimsaidia kumtamkisha neno muhimu kwa Muislamu kulitamka kabla ya kifo: Laa Ilaaha Illa llah (Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu).

Kinana alisema katika hotuba yake kuwa Nnauye aliacha mafunzo mawili makubwa: Kwanza kiongozi huandaliwa na pilli, mafanikio huja kwa kuwa na ‘organization’ nzuri katika taasisi. Kwangu, kauli hizi ni dongo kwa marehemu JPM ambaye anajulikana kama kiongozi aliyekosa malezi ya chama na ambaye hakuna na weledi katika organization ya chama na badala yake alikuwa mtu wa ‘matamko’.

Wapo watu waliotafsiri kusanyiko lile kuwa sio tu ni maadhimisho ya kumbumbuka Mzee Nnauye bali pia shukrani kwa kundi lile kwa Mwenyezi Mungu wao kwa kuwatoa kifungoni baada ya kuwekewa alama ya X na JPM. Sio siri kuondoka kwa JPM kumewapa ahueni Mzee Makamba na Kinana ya walau kufurahia uhuru na kutoishi kwa wasiwasi tena! Sio siri pia kuwa kuondoka kwa JPM kumefufua matumaini ya kupanda kisiasa kwa wakina Nape, Ridhwani na Januari.

Ninachokiona ni kuwa hizi familia ziko ‘connected’ mno na kuna makubaliano mengi ya kifamilia. Nani alijua kuwa kumbe wakina Nape walikabidhiwa kwa Makamba awalee baada ya kufariki kwa mzee wao? Nani hajui kuwa Kikwete kambeba sana Januari na kumlea kisiasa? Kinana naye akawa karibu na Nape enzi zao chamani akimpa madini ya ‘organization’ ambayo naye alijifunza kwa Mzee Nnauye? Yapi mengine hatuyajui katika mikataba hii ya kifamilia?

Nikiangalia mustakbali wa nchi, nikirejea sauti zile zilizovuja za kumponda JPM hasira zao sitashangaa hawa wababe wakiichukua nchi baada ya Rais Samia kustaafu. Tayari kuna tetesi kuwa Rais Samia anapokea ushauri kutoka Mzee wa Chalinze, ambaye ndiye mzee wa hawa vijana.

Halafu vijana wako vizuri na wamejipanga hasa Januari ambaye anajulikana kama kipenzi cha watu wa mitandaoni hasa Twitter (Twitter darling), ingawa kwa upande mwingine sio siri rekodi yake ya utendaji haivutii, haishtui.

Bila vikwazo vingine njiani, naiona serikali huko mbele ya Rais Januari, Waziri Mkuu Nape huku wakina Ridhwan, Bashe wakipewa majukumu kubwa katika Baraza la Mawaziri.

Tusubiri na tuone

Hii mbombo si mchezo 😁😁
 
Kila taifa kuna loyal family katika utawala ukianza Marekani kuna Rais George Bush Senior na George Bush Junior wote wametawala kwa wakati tofauti huko Kenya kuna Rais Jomo Kenyatta na Rais Uhuru Kenyatta. Si ajabu na hapa Tanzania tukapata Rais kutoka kwenye mfumo huo.
hata hapa wapo, Mwinyi- Mwinyi; Karume-Karume nk. Hatukatai utawala wa namna hii, hoja yetu ni kuwa taratibu sahihi za kuingia madarakani zimefuatwa? Ukiangalia Bush walivyoingia - sawa kabisa; je Kenyatta ilikuwaje? Tunayataka hayo?
 
Sioni tatizo kwa wao kuwa na muunganiko na uhusiano wa karibu. Ni utamadauni wa kawaida wa mwafrika hasa Tanzania kuwa na undugu. Sisi sote ni ndugu.
 
Unafahamu wagombea urais wa Marekani hawapatikani kwa watu kuja kamati kuu na majina yao mfukoni?
Umewahi kujua mtoto mmojawapo wa Bush alishindwa vibaya na Trump kwa KURA ZA WANACHAMA?
Tafsiri ya jina la mfukoni linakuwa tafauti kwa kutegemea nchi. Hata la Bush junior lilikuwa la mfukoni ndiyo likaenda kwenye kamati zao za chama. Na hata huko USA unategemea magodfather wako wa kwenye chama kukusupport kwa uzito wa maneno yao na fedha zao. Na akifanikiwa lazima alipe hisani.
 
Tatizo waTz wanafukia vichwa mchangani kiwiliwili kinabaki juu halafu wanasema wamejificha!
Mambo yapo wazi kama hatutaamua kuforce mabadiriko yajayo yameshajulikana mbona!
 
ABUU KAUTHAR

Tukio la kawaida la mkusanyiko wa watu kumkumbuka mpendwa wao limenifumbua akili na kuyajua mambo mengi kuhusu siasa za nchi hii na asili ya uhusiano wa karibu wa baadhi ya watu.

Nazungumzia kumbukizi ya miaka 20 tangu kufariki kwa mmoja wa viongozi mahiri wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Brigedia Jenerali Moses Nnauye, ambaye, kama cheo kinavyojieleza, pia aliwahi kuhudumu serikalini, jeshini huku akikumbukwa zaidi kwa kipawa chake cha muziki.

Ukiacha familia ya Nnauye mwenyewe (mjane na watoto), walikuwepo pia Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, na Makatibu wakuu wa CCM wastaafu Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba.

Orodha hii ikanikumbusha tukio lile enzi ya awamu ya tano ziliponaswa sauti zikimsema vibaya marehemu Rais wa Awamu ya Tano, John Pombe Magufuli. Ni wazee hawa, (ukimuondoa Kikwete) ndio waliosikika wakimsema vibaya marehemu. Pia alikuwemo Nape, ambaye katika mazungumzo na Mzee Makamba alisikika akimuita ‘baba’ kwa heshima zote.

Hawa jamaa pamoja na marehemu ambaye walijikusanya kumkumbuka, wametoka mbali na sio ajabu kwamba wanazeeka wakiwa na ukaribu mkubwa, sio wao tu bali hata familia zao! Naamini wapo sahihi watu waliosema kuwa kuna ‘family coalition’ (muungano wa familia) unaosaidiana kuhakikisha wanatawala nchi hii.

Wote watatu niliowataja licha ya kulelewa ndani ya chama, pia walikuwa wanajeshi mahiri, enzi hizo wakati chama kimeshika utamu na hatamu zikiitangulia sio tu serikali bali hata jeshi. Kikwete, hadi anatoka jeshini alikuwa Luteni., Kinana alikuwa Kanali na Makamba alikuwa Luteni huku marehemu waliyekuwa wakimuadhimisha akiwa Brigedia Jenerali. Hii inaelezea hisia za kujiona wanastahili zaidi kukamata uongozi wa nchi wanayoona kuwa wameipigania chamani, jeshini na serikalini.

Ukiangalia historia zao, walianza kwenye chama pamoja,wakahudumua tena pamoja jeshini na kisha serikalini. Nnauye na Makamba walikuwa na mengine ya kuwaunganisha: sanaa. Wote walikuwa waimbaji enzi hizo. Kwa kweli, sikuwa najua kuwa Nnauye alikuwa ndio John Komba wa kwanza!

Hotuba ya Makamba ilifichua siri nyingi, ambapo alielezea ukaribu wake mkubwa na Nnauye kiasi kwamba bosi wake huyo wa zamani alimfia mkononi, akimsaidia kumtamkisha neno muhimu kwa Muislamu kulitamka kabla ya kifo: Laa Ilaaha Illa llah (Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu).

Kinana alisema katika hotuba yake kuwa Nnauye aliacha mafunzo mawili makubwa: Kwanza kiongozi huandaliwa na pilli, mafanikio huja kwa kuwa na ‘organization’ nzuri katika taasisi. Kwangu, kauli hizi ni dongo kwa marehemu JPM ambaye anajulikana kama kiongozi aliyekosa malezi ya chama na ambaye hakuna na weledi katika organization ya chama na badala yake alikuwa mtu wa ‘matamko’.

Wapo watu waliotafsiri kusanyiko lile kuwa sio tu ni maadhimisho ya kumbumbuka Mzee Nnauye bali pia shukrani kwa kundi lile kwa Mwenyezi Mungu wao kwa kuwatoa kifungoni baada ya kuwekewa alama ya X na JPM. Sio siri kuondoka kwa JPM kumewapa ahueni Mzee Makamba na Kinana ya walau kufurahia uhuru na kutoishi kwa wasiwasi tena! Sio siri pia kuwa kuondoka kwa JPM kumefufua matumaini ya kupanda kisiasa kwa wakina Nape, Ridhwani na Januari.

Ninachokiona ni kuwa hizi familia ziko ‘connected’ mno na kuna makubaliano mengi ya kifamilia. Nani alijua kuwa kumbe wakina Nape walikabidhiwa kwa Makamba awalee baada ya kufariki kwa mzee wao? Nani hajui kuwa Kikwete kambeba sana Januari na kumlea kisiasa? Kinana naye akawa karibu na Nape enzi zao chamani akimpa madini ya ‘organization’ ambayo naye alijifunza kwa Mzee Nnauye? Yapi mengine hatuyajui katika mikataba hii ya kifamilia?

Nikiangalia mustakbali wa nchi, nikirejea sauti zile zilizovuja za kumponda JPM hasira zao sitashangaa hawa wababe wakiichukua nchi baada ya Rais Samia kustaafu. Tayari kuna tetesi kuwa Rais Samia anapokea ushauri kutoka Mzee wa Chalinze, ambaye ndiye mzee wa hawa vijana.

Halafu vijana wako vizuri na wamejipanga hasa Januari ambaye anajulikana kama kipenzi cha watu wa mitandaoni hasa Twitter (Twitter darling), ingawa kwa upande mwingine sio siri rekodi yake ya utendaji haivutii, haishtui.

Bila vikwazo vingine njiani, naiona serikali huko mbele ya Rais Januari, Waziri Mkuu Nape huku wakina Ridhwan, Bashe wakipewa majukumu kubwa katika Baraza la Mawaziri.

Tusubiri na tuone

Mkuu hata sauti za JK Zilinaswa sema tu jpm aliamua kumwachia mungu wamseme tu ndiyo maana alikuwa kila siku anasema wamuombee
 
Ujinga tu! Kwani Nnauye ni maarufu kuliko Rashid Kawawa? Ni maarufu kuliko Oscar Kambona? Ni maarufu kuliko akina Kasela bantu. Hapa kuna kiwewe na kuandaa urithi wa madaraka. Siku hizi namuona Nape ana panic kila wakati, anaona amesahaulika. Bahati mbaya Nchimbi ambaye ni adui yake namba moja amerudishwa. Katikati kuna ndumila kuwili, Kikwete.

Ni hivi Nnauye alikuwa na nafasi kama wengine katika chama. Aliwabeba akina makamba baada ya kufukuzwa ualimu kwa kumpa mwanafunzi mimba, na leo hii hasemi ujinga wake. Walikuwepo akina kanali Mwasomola ambao leo hii hawasikiki, akina Kolimba. Mwinyi alipopata urais Kikwete alikuwa katibu wa CCM wa wilaya Masasi au Nachingwea ambako alifahamiana na Nnauye. Nnauye ndo mtu aliyemuombea uwaziri Kikwete bna kwa upendeleo wa kidini ndani yake, Mwinyi akamteua kuwa Naibu waziri akitokea wilayani, siyo hata mkoani!
Leo hii Kikwete anamtukuza Nnauye siyo kwa umaarufu wa kisiasa, bali kwa kumshika mkono na kumtambulisha kwa Mwinyi. Nnauye naye alilindwa na Kikwete akapewa mkuu wa wilaya na kumuepusha na uadui wake na Nchimbi. Wakati huo huo Nchimbi anajiona ni raifiki sana wa Kikwete. Undumila kuwili huo!!!!
Unayajua mambo! Ona Nape na Undumila kuwili! Si huyu JK aliyesitisha ufadhili wake pale chuo cha Diplomasia? Si Malecela aliyemtoa jalalani wakati huo hta kumtafutia gari Landcruiser la kufanya kampeni nchi nzima ili apambane na Nchimbi?
 
Sisi Sukuma Gang hatutakubali kabisa lazima turudi ulingoni tena, afe beki afe kipa,ujinga wakati wa kwenda tu,tumeshajua kila kitu walichofanya hawa Msoga Gang.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Hii Mada sukuma GANG inawasorokota tumboni na kupanda kichwani, na vile hawajuhi walitendalo, watapata uchizi na kupuyana uchi .
 
Kila taifa kuna loyal family katika utawala ukianza Marekani kuna Rais George Bush Senior na George Bush Junior wote wametawala kwa wakati tofauti huko Kenya kuna Rais Jomo Kenyatta na Rais Uhuru Kenyatta. Si ajabu na hapa Tanzania tukapata Rais kutoka kwenye mfumo huo.
Dr Mwinyi
 
Jeshi lichukue hatua gani kama wananchi hamto act kwanza[emoji28]! Jeshi ni la wananchi Tanzania.

Kwa ubinafsi unaoendelea na lack of solidarity tutaendelea kuminywa kende mpaka kiama chetu! Watu wachache wamejimilikisha utawala wao na familia zao ndio maana miaka nenda rudi sura ni zile zile [emoji28] licha ya maraisi kubadilika[emoji28]!

Atachukua January marope na kumpa Nape uwaziri mkuu ni mwendo wa kubunya tozo tu za wanyonge[emoji1787]! Trend inaendelea ni kuwapa watoto wao life na jamaa zao sie tutaota mvi na kufa [emoji41]
Yale mazindiko na kafara za watu unafikiri mchezo!!

Akili za watu zinafungwa tunabaki mazuzu tu!!!
 
Aiseh!tukubali yaishe!sema hawa jamaa huwa wanatujali walau kidogo!!!Kikwete na Mwinyi senior wametujali angalau!!
 
Ujinga tu! Kwani Nnauye ni maarufu kuliko Rashid Kawawa? Ni maarufu kuliko Oscar Kambona? Ni maarufu kuliko akina Kasela bantu. Hapa kuna kiwewe na kuandaa urithi wa madaraka. Siku hizi namuona Nape ana panic kila wakati, anaona amesahaulika. Bahati mbaya Nchimbi ambaye ni adui yake namba moja amerudishwa. Katikati kuna ndumila kuwili, Kikwete.

Ni hivi Nnauye alikuwa na nafasi kama wengine katika chama. Aliwabeba akina makamba baada ya kufukuzwa ualimu kwa kumpa mwanafunzi mimba, na leo hii hasemi ujinga wake. Walikuwepo akina kanali Mwasomola ambao leo hii hawasikiki, akina Kolimba. Mwinyi alipopata urais Kikwete alikuwa katibu wa CCM wa wilaya Masasi au Nachingwea ambako alifahamiana na Nnauye. Nnauye ndo mtu aliyemuombea uwaziri Kikwete bna kwa upendeleo wa kidini ndani yake, Mwinyi akamteua kuwa Naibu waziri akitokea wilayani, siyo hata mkoani!
Leo hii Kikwete anamtukuza Nnauye siyo kwa umaarufu wa kisiasa, bali kwa kumshika mkono na kumtambulisha kwa Mwinyi. Nnauye naye alilindwa na Kikwete akapewa mkuu wa wilaya na kumuepusha na uadui wake na Nchimbi. Wakati huo huo Nchimbi anajiona ni raifiki sana wa Kikwete. Undumila kuwili huo!!!!
Ni kweli Brig. Nnauye alikufa bila nyumba?
 
Back
Top Bottom