Kumbukizi ya Nyerere: Familia ya Mwalimu Nyerere yawataka wasanii kuacha kutumia jina la Baba wa Taifa kama ubin wao

Familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere imewataka wasanii wanaoigiza sauti za viongozi akiwemo Baba wa Taifa kuanza kutumia majina yao halisi badala ya kujitambulisha kwa majina ya viongozi wanaoigiza sauti zao na kuleta mkanganyiko.

Msemaji wa familia hiyo ambaye ni mtoto wa sita wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage, Madaraka Nyerere ameyasema hayo wakati akipokea tuzo ya Mwalimu iliyotolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Milambo, (Amsha) kijijini Mwitongo wilayani Butiama mkoani Mara.

Madaraka amemtolea mfano Steve Mengele maarufu kama "Steve Nyerere" na kumtaka msanii huyo na waandishi wa habari kuanza kutumia jina lake halisi ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza kwa baadhi ya watu pamoja na familia kwa ujumla kwani na wao wana mwanafamilia aitwae Steven.

Familia hiyo pia imewataka viongozi na watu mbalimbali wanaofika nyumbani kwa Mwalimu Kijijini Butiama kwa ajili ya masuala mbalimbali ikiwemo kumuenzi Baba wa Taifa kutoa ushirikiano kwa familia hiyo hata baada ya kilichowapeleka kutamatika.

Familia hiyo imesema baadhi ya viongozi na watu mbalimbali hufika nyumbani hapo kufanya walichokusudia na baada ya hapo hupotea na kukata mawasiliano.

Madaraka Nyerere amesema kabla ya watu hao kufika nyumbani hapo huwa na mawasiliano mazuri lakini wakishakamilisha jambo lao hupotea kabisa.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Madaraka amesema italeta maana zaidi kwa wanaokwenda Butiama na kuhusisha familia kuacha kukata mawasiliano kama kweli wanamuenzi Baba wa Taifa.

Amesema wanapopiga simu kwa viongozi hao kwa kuwa kunaweza kuwa na jambo la muhimu kujadiliana au ni taarifa muhimu mara nyingi watu hao hawapokei simu utadhani si wale waliokuwa 'wanawasumbua' wakitaka ushirikiano wao katika kumuenzi Mwalimu Nyerere.

USSR
hivi nyerere katika nchi hii alikuwa mmoja tu?
 
Madaraka aache kujificha ficha aingie kwenye siasa afanye Kaz kama Baba yake, wapo watu wengi sana wa kumsaidia kutunza hizo kumbukumbu hapo...

Anagombea jimbo anaanza kutema cheche.. umri umeenda sana kuishia kutoa statements za jumla jumla .. kwani hao wasanii hawafahamiki Ili muwalime barua
Politics si ya kila mtu, na si kila mtu ana interest za kuwa politician
 
Tanzania kuna koo nyingi, kuna ukoo wa kichaga mfano Mushi na masawe, meaning nchini kuna watu wengi tu wanajiita masawe au mushi. ukienda songea kuna ngonyani, komba, ndunguru, nchimbi n.k, ndani yake kuna maelfu ya kina nduguru na nchimbi, sio ukoo unaomilikiwa na mtu mmoja.

swali nililouliza ni je? Nyerere alikuwa mmoja tu? hapakuwa na nyerere wengine toka kwenye familia tofauti na ya huyu aliyekuwa rais? kama jibu ni kwamba walikuwepo na wapo hadi leo, hawa watoto wa nyerere wanapata wapi hakimiliki ya jina hilo? na mtu akijiita nyerere, anamaanisha nyerere baba yao tu au inawezekana anamaanisha nyerere wengine tofauti na huyo baba yao?
 
Safi Sanaa

Familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere imewataka wasanii wanaoigiza sauti za viongozi akiwemo Baba wa Taifa kuanza kutumia majina yao halisi badala ya kujitambulisha kwa majina ya viongozi wanaoigiza sauti zao na kuleta mkanganyiko.

Msemaji wa familia hiyo ambaye ni mtoto wa sita wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage, Madaraka Nyerere ameyasema hayo wakati akipokea tuzo ya Mwalimu iliyotolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Milambo, (Amsha) kijijini Mwitongo wilayani Butiama mkoani Mara.

Madaraka amemtolea mfano Steve Mengele maarufu kama "Steve Nyerere" na kumtaka msanii huyo na waandishi wa habari kuanza kutumia jina lake halisi ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza kwa baadhi ya watu pamoja na familia kwa ujumla kwani na wao wana mwanafamilia aitwae Steven.

Familia hiyo pia imewataka viongozi na watu mbalimbali wanaofika nyumbani kwa Mwalimu Kijijini Butiama kwa ajili ya masuala mbalimbali ikiwemo kumuenzi Baba wa Taifa kutoa ushirikiano kwa familia hiyo hata baada ya kilichowapeleka kutamatika.

Familia hiyo imesema baadhi ya viongozi na watu mbalimbali hufika nyumbani hapo kufanya walichokusudia na baada ya hapo hupotea na kukata mawasiliano.

Madaraka Nyerere amesema kabla ya watu hao kufika nyumbani hapo huwa na mawasiliano mazuri lakini wakishakamilisha jambo lao hupotea kabisa.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Madaraka amesema italeta maana zaidi kwa wanaokwenda Butiama na kuhusisha familia kuacha kukata mawasiliano kama kweli wanamuenzi Baba wa Taifa.

Amesema wanapopiga simu kwa viongozi hao kwa kuwa kunaweza kuwa na jambo la muhimu kujadiliana au ni taarifa muhimu mara nyingi watu hao hawapokei simu utadhani si wale waliokuwa 'wanawasumbua' wakitaka ushirikiano wao katika kumuenzi Mwalimu Nyerere.

USSR
Hii imekaa Safi Sanaa.

Nukuu ya baba wa taifa.
""UTII UKIZIDI SANAA HUZAA UOGA, UOGA UKIZIDI SANA HUZAA UNAFIKI NA KUJIPENDEKEZA NA MWISHO WAKE NI MAUTI""
 
NISINGEKUBALI kabisa
Mtu chawa asiejielewa
Yule mtu mfupi inatakiwa abadilishe jina maana ubongo wake Una hitilafu

Mwalimu hakua chawa chawa Tu oyaoya

Sasa huyu mtu mfupi anaharibu jina la teacher
 
Huyo Madaraka kajiaibisha sana
Sikutegemea mtu mzima kuongea hayo
Mpaka malaika tumechukua majina yao itakuwa baba yake
Hatujasahau tulipokosa hata sanda za kuwazikia wapendwa wetu
 
Kinachouma zaidi picha ya baba ipo hela lkn wewe mtoto huna hizo hela😂🤣🤣
 
Huyu kunguni akome kutumia jina la mwalimu hana sifa wala maarifa yoyote na huwa kanajifanya kuwa na hekima kwenye hamna.yaani mpaka misiba kanaona ni fursa.
 
Mh ana hekima sanaaa

Amemshauri kijana kuheshimu mzazi aliemzaa kwa kutumia jina la baba yake naa ache kutumia majina ya watuw wasiomhusu
 
Back
Top Bottom