Elsa Marie
JF-Expert Member
- Jul 7, 2017
- 2,284
- 5,596
Wapo wengi.Hujawahi kuona watu wenye ukoo tofauti lakn wana majina yanafanana kama Massawe Mushi etc
Sasa huyu ukoo wake ni Mangele ( kama sijakosea) sio Nyerere.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wapo wengi.Hujawahi kuona watu wenye ukoo tofauti lakn wana majina yanafanana kama Massawe Mushi etc
Aibu tupu, hakuna mwenye umiriki wa jina, mtu yeyote anaweza kutumia jina lolote,
Familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere imewataka wasanii wanaoigiza sauti za viongozi akiwemo Baba wa Taifa kuanza kutumia majina yao halisi badala ya kujitambulisha kwa majina ya viongozi wanaoigiza sauti zao na kuleta mkanganyiko.
Msemaji wa familia hiyo ambaye ni mtoto wa sita wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage, Madaraka Nyerere ameyasema hayo wakati akipokea tuzo ya Mwalimu iliyotolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Milambo, (Amsha) kijijini Mwitongo wilayani Butiama mkoani Mara.
Madaraka amemtolea mfano Steve Mengele maarufu kama "Steve Nyerere" na kumtaka msanii huyo na waandishi wa habari kuanza kutumia jina lake halisi ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza kwa baadhi ya watu pamoja na familia kwa ujumla kwani na wao wana mwanafamilia aitwae Steven.
Familia hiyo pia imewataka viongozi na watu mbalimbali wanaofika nyumbani kwa Mwalimu Kijijini Butiama kwa ajili ya masuala mbalimbali ikiwemo kumuenzi Baba wa Taifa kutoa ushirikiano kwa familia hiyo hata baada ya kilichowapeleka kutamatika.
Familia hiyo imesema baadhi ya viongozi na watu mbalimbali hufika nyumbani hapo kufanya walichokusudia na baada ya hapo hupotea na kukata mawasiliano.
Madaraka Nyerere amesema kabla ya watu hao kufika nyumbani hapo huwa na mawasiliano mazuri lakini wakishakamilisha jambo lao hupotea kabisa.
Akizungumza kwa niaba ya familia, Madaraka amesema italeta maana zaidi kwa wanaokwenda Butiama na kuhusisha familia kuacha kukata mawasiliano kama kweli wanamuenzi Baba wa Taifa.
Amesema wanapopiga simu kwa viongozi hao kwa kuwa kunaweza kuwa na jambo la muhimu kujadiliana au ni taarifa muhimu mara nyingi watu hao hawapokei simu utadhani si wale waliokuwa 'wanawasumbua' wakitaka ushirikiano wao katika kumuenzi Mwalimu Nyerere.
USSR
Inawezekana una hoja, ila ukienda kwa Pilato wataangalia kwenye historia lini huyu Steve alianza kutumia jina hilo, watakuta ni pale alipoanza kuigiza sauti ya Mwalimu Nyerere. Ndiyo maana katika clip hii Madaraka amesema zaidi ya mara moja, imefika wakati inakuwa kama ni upotoshaji maana wengine hawakuwa wamezaliwa kujua historia hii matokeo yake ni kuleta mkanganyiko. Madaraka amekuwa sahihi pia kuwakosoa waandishi wa habari, wanapoandika jina la Steve, hili jina la Nyerere linapaswa kuwekwa hivi "Nyerere" au kusema "anayejulikana kwenye sanaa kama Steve Nyerere" au "almaarufu Steve Nyerere".Madaraka labda hajui kuwa Tanzania hakuna jina linalozuiwa mtu kujiita.
Mimi naweza kuamua kujiita Jitu Jiwe kama (Given names) si lazima Jiwe liwe ni surname.
Sasa Steve Nyerere kaamua kujiita Steve Nyerere kwa nini hutaki ajiite anavyotaka yeye?
Hakuna mahali Steve Nyerere kajiita mtoto wa Nyerere
Na wewe kabadili jina ujiite Samia Suluhu Hassan uone kitakachokutokea.Aibu tupu, hakuna mwenye umiriki wa jina, mtu yeyote anaweza kutumia jina lolote,
Nchi inakabuliwa na Mambo mengi, kila sekta hawa watoto wa Nyerere wanachoona ni jina tu,! kenge kabisa, kenge hawana mchango wowote katika nchi, hawana ma kampuni, sio academician,sio ma engineer, sio marubani, yapo yapo tu, kuna moja lilikufa kutokana na matumizi ya pombe ya muda mrefu,
Y anaishi kwa handout za, serikali, mtoto wa Baba wa Taifa,sawa huna ukwasi, lakini hata kuwa profesa mkubwa chuo kikuu umeshindwa, yanalia Lia tu kusubili kuteuliwa, so pathetic
Kakuwadia sana viongz kwa kutumia hilo jinaa 😄Steven Mangele anatia Watu Aibu 🤣 🤣
Ila sio Steve MangeleMkoa wa Mara una watu wenye jina la Nyerere kwa maelfu kama sio malaki
Unaacha kutumia jina la mzazi (baba) wako unakwenda kutumia jina la kiongozi huo ni uzuzu! Unafikiri baba yake mzazi anajisikiaje mtoto wake kutotumia jina lake na badala yake anatumia jina la Nyerere ambaye si baba yake?Wasajiri hilo jina basi
Huyo msanii Steve baba yake anaitwa Nyerere? Tatizo Steve amekuwa akijitambulisha kama baba yake ni Nyerere wakati siyo.Mkoa wa Mara una watu wenye jina la Nyerere kwa maelfu kama sio malaki
Kweli kabisa, ni aibu kubwa mno, wachangiaji wengi hawajaiona hoja na uzito wake. Aliye na wajibu wa kulinda Legacy ya mtu wa kwanza ni mtoto wake, wengine watafanya kadri watakavyowwza.Ni aibu kufikia wenye jina wanakuambia uache kulitumia.
Nyerere alipoitwa baba wa taifa, Hao watoto wake wangekataa, Nyerere alishavuka level za kuwa mali ya familia. Kama wao hawatumii jina la baba yao vizuri, ni ujinga wao.Huyo msanii Steve baba yake anaitwa Nyerere? Tatizo Steve amekuwa akijitambulisha kama baba yake ni Nyerere wakati siyo.
Sheria hii hii hairuhusu kutumia jina la mwenzio, kumbuka hapo imejitanabalisha kuwa kuna mwanandugu ambaye ana majina yote 3 yanayotumiwa na huyo msanii. Ingekuwa jina 1 au 2 sawa, ila yote 3 khaa..., haijakaa sawa..Siafiki hata kidogo
Kwani kuna Ubaya gani
Mbona kawaida
Wanajiita diamond ni wengi
Wengine wanajiita kondeboy
Kuna Dada huku anaitwa Ray c
Kuna akina Beyonce wengi tu
Kuna watu wanaitwa Mayele
Yote hiyo ni kuonesha upendo tu
Na riziki wanapatia humo humo
Kwanza unakataza kwa msingi gani, sheria gani
Tatizo la huyu bwana alichukua hilo jina kama utambulisho wa kisanii.Nyerere alipoitwa baba wa taifa, Hao watoto wake wangekataa, Nyerere alishavuka level za kuwa mali ya familia. Kama wao hawatumii jina la baba yao vizuri, ni ujinga wao.
Kila mtanzania anaweza kuwa na ubini wa Nyerere kama akitaka.
Nyerere alipoitwa baba wa taifa, Hao watoto wake wangekataa, Nyerere alishavuka level za kuwa mali ya familia. Kama wao hawatumii jina la baba yao vizuri, ni ujinga wao.
Kila mtanzania anaweza kuwa na ubini wa Nyerere kama akitaka.
Kwanini uache ubini wako uanze kutumia ubini wa kiongozi!! Huo ni zaidi ya uchawa. Mwambieni ndugu wa Mwalimu wamemkataa aendelee na ubini wakwao. Kwanza ana mdhalilisha sana baba yake.Nyerere alipoitwa baba wa taifa, Hao watoto wake wangekataa, Nyerere alishavuka level za kuwa mali ya familia. Kama wao hawatumii jina la baba yao vizuri, ni ujinga wao.
Kila mtanzania anaweza kuwa na ubini wa Nyerere kama akitaka.
Hao ndugu ni wajinga, wakati wa utawala wa baba yao elimu ilikuwa bure, hawakusoma, madaraka akaishia kwenye ulevi na upromota wa ngumi, Makongoro gari yake muda wote imejaa pombe, imebidi mfumo ukamfiche maporini Huko Katavi kuepuka aibuKwanini uache ubini wako uanze kutumia ubini wa kiongozi!! Huo ni zaidi ya uchawa. Mwambieni ndugu wa Mwalimu wamemkataa aendelee na ubini wakwao. Kwanza ana mdhalilisha sana baba yake.