Kumbukizi ya Nyerere: Familia ya Mwalimu Nyerere yawataka wasanii kuacha kutumia jina la Baba wa Taifa kama ubin wao

Kuchagua jina ni hiyari ya mtu.
Kuna jamaa alikataa jina la ukoo wake akaamua kujiita.
Malcom X, na akakubalika bila shida.
Jina la Nyerere ni jina kama majina mengine.
Kwetu Nyerere ni jina la kwanza la mtu na Lina maana ya Sisimizi.
 
Mtu kama unafanya mambo mazuri katika jamii sidhani wahusika wataona aibu ukijihusisha na ubini wao.

Sasa bwana Steve naona hujakubalika na wahusika wa jina la Nyerere.

Jichunguze kuna kitu unakifanya wazi wazi au sirini hakina sifa nzuri kwa jamii.
Exactly 💯...
Na Mkuu ni kwamba kama unafanya mambo mazuri lazima utataka utambulike kwa ukoo wenu kwani hiyo sifa ni vizuri irudi kwenye ukoo wenu kama kumbukumbu.
Huyu Steve Mengele ni tapeli tu..akae mbali na Ukoo wa Mwalimu.
Kuelekea uchaguzi Mkuu ndio mtamjua....
Huyu Lofa hakawii kuita press alivyo kilaza amdhalilishe Madaraka hakika nakuambia subiri uone...
 
Familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere imewataka wasanii wanaoigiza sauti za viongozi akiwemo Baba wa Taifa kuanza kutumia majina yao halisi badala ya kujitambulisha kwa majina ya viongozi wanaoigiza sauti zao na kuleta mkanganyiko.

Msemaji wa familia hiyo ambaye ni mtoto wa sita wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage, Madaraka Nyerere ameyasema hayo wakati akipokea tuzo ya Mwalimu iliyotolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Milambo, (Amsha) kijijini Mwitongo wilayani Butiama mkoani Mara.

Madaraka amemtolea mfano Steve Mengele maarufu kama "Steve Nyerere" na kumtaka msanii huyo na waandishi wa habari kuanza kutumia jina lake halisi ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza kwa baadhi ya watu pamoja na familia kwa ujumla kwani na wao wana mwanafamilia aitwae Steven.

Familia hiyo pia imewataka viongozi na watu mbalimbali wanaofika nyumbani kwa Mwalimu Kijijini Butiama kwa ajili ya masuala mbalimbali ikiwemo kumuenzi Baba wa Taifa kutoa ushirikiano kwa familia hiyo hata baada ya kilichowapeleka kutamatika.

Familia hiyo imesema baadhi ya viongozi na watu mbalimbali hufika nyumbani hapo kufanya walichokusudia na baada ya hapo hupotea na kukata mawasiliano.

Madaraka Nyerere amesema kabla ya watu hao kufika nyumbani hapo huwa na mawasiliano mazuri lakini wakishakamilisha jambo lao hupotea kabisa.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Madaraka amesema italeta maana zaidi kwa wanaokwenda Butiama na kuhusisha familia kuacha kukata mawasiliano kama kweli wanamuenzi Baba wa Taifa.

Amesema wanapopiga simu kwa viongozi hao kwa kuwa kunaweza kuwa na jambo la muhimu kujadiliana au ni taarifa muhimu mara nyingi watu hao hawapokei simu utadhani si wale waliokuwa 'wanawasumbua' wakitaka ushirikiano wao katika kumuenzi Mwalimu Nyerere.

USSR
Nilitegemea hoja hii kutoka familia ya mwalimu nyerere siku nyingi ila kwa ustaarabu wao wamevumilia muda mrefu. Wasanii kujiita jina la nyerere eti kwa kuigiza sauti yake tu sio sahihi kabisa. Stephen Mengele amesikia asite mara moja kujiita Stephen Nyerere. waandishi wa habari mumesikia. Baadhi ya wasanii wana maadili mabaya wengine wameshiriki dili za ovyo kama huyu Mengele kutetea kuuza bandari za taifa kwa dubai. Unakuta anashambuliwa jina linatajwa stephen nyerere. Mtu wa ovyo anaitwa Nyerere kwa vile tu anajua kuigiza sauti yake. Hakika haipendezi.
 
Kweli..majina nickname sio ishu..ila ya ukoo..fikiria jina lenu la ukoo kuna mtu anaanza kulitumia wakat hana hata undugu nanyi
Kwani wao ni wamiliki wa lugha iliyotumika kutengeneza hilo jina? UKIULIZWA LEO NYERERE lina maana gani na ukapata jibu labda ukute linamaana ya msimu wa mvua. Sasa msimu wa mvua kuitwa kwa kizanaki halafu ndio utune na kusema hilo jina ni miliki yenu? HUO NI UBINAFSI
 
Eti watu wangine wanakuja hapa ila wakishaondoka hawapokei simu Tena na wanapotea..... Kwenye haya maisha usijipe umuhumu kwenye maisha ya watu Wala usitake kupendwa... Hapa huyu Madaraka alitaka tu kutoa hisia zake kwamba hawathaminiki na hawapewi kipaumbele familia yao especially yeye, ningekua yeye ikifika Nyerere day nazima simu na sipatikani ili wasinizoee tena.

Kutumia jina Nyerere ni jina kama majina mengine Kila mtu ana haki ya kuitwa au kujiita... Mohammed, Mwakyambiki, Yesu, Mkapa, Obote, Kassim yote hayo ni majina unajichagulia unalotaka,, Hata huyo Nyerere baba ake kuna watu waliitwa Nyerere kabla yake...
 
Familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere imewataka wasanii wanaoigiza sauti za viongozi akiwemo Baba wa Taifa kuanza kutumia majina yao halisi badala ya kujitambulisha kwa majina ya viongozi wanaoigiza sauti zao na kuleta mkanganyiko.

Msemaji wa familia hiyo ambaye ni mtoto wa sita wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage, Madaraka Nyerere ameyasema hayo wakati akipokea tuzo ya Mwalimu iliyotolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Milambo, (Amsha) kijijini Mwitongo wilayani Butiama mkoani Mara.

Madaraka amemtolea mfano Steve Mengele maarufu kama "Steve Nyerere" na kumtaka msanii huyo na waandishi wa habari kuanza kutumia jina lake halisi ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza kwa baadhi ya watu pamoja na familia kwa ujumla kwani na wao wana mwanafamilia aitwae Steven.

Familia hiyo pia imewataka viongozi na watu mbalimbali wanaofika nyumbani kwa Mwalimu Kijijini Butiama kwa ajili ya masuala mbalimbali ikiwemo kumuenzi Baba wa Taifa kutoa ushirikiano kwa familia hiyo hata baada ya kilichowapeleka kutamatika.

Familia hiyo imesema baadhi ya viongozi na watu mbalimbali hufika nyumbani hapo kufanya walichokusudia na baada ya hapo hupotea na kukata mawasiliano.

Madaraka Nyerere amesema kabla ya watu hao kufika nyumbani hapo huwa na mawasiliano mazuri lakini wakishakamilisha jambo lao hupotea kabisa.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Madaraka amesema italeta maana zaidi kwa wanaokwenda Butiama na kuhusisha familia kuacha kukata mawasiliano kama kweli wanamuenzi Baba wa Taifa.

Amesema wanapopiga simu kwa viongozi hao kwa kuwa kunaweza kuwa na jambo la muhimu kujadiliana au ni taarifa muhimu mara nyingi watu hao hawapokei simu utadhani si wale waliokuwa 'wanawasumbua' wakitaka ushirikiano wao katika kumuenzi Mwalimu Nyerere.

USSR
Ujinga tu , nchi zilizoendelea hayo majina ya watu yanatumika sana na akuna tatizo tz sijui uwa Kuna nn
 
Mtu kama unafanya mambo mazuri katika jamii sidhani wahusika wataona aibu ukijihusisha na ubini wao
Kila ukoo ujitahidi kutoka kimaisha ili ujivunie ubini wao

Ubini wa Huyo Steve wa Mengele ni maskini wa kutupwa ndio maana kaamua akimbie huo ubini atumie ubini wa watu ubini wa Nyerere

Ukoo wa Mengele mkae chini mjitathimini kumaliza tatizo la ulofa kwenye ukoo wa Mengele ili watoto na wajukuu na vitukuu wajisikie fanatic kutumia jins la ubini ls Mengele badala ya kulikimbia na kwenda kuokota majina ya ubini ya watu sababu anaona jina la ubini la baba yake halina maana yoyote zaidi ya ulofa

Kaeni kikao mjadiliane hilo
 
Eti watu wangine wanakuja hapa ila wakishaondoka hawapokei simu Tena na wanapotea..... Kwenye haya maisha usijipe umuhumu kwenye maisha ya watu Wala usitake kupendwa... Hapa huyu Madaraka alitaka tu kutoa hisia zake kwamba hawathaminiki na hawapewi kipaumbele familia yao especially yeye, ningekua yeye ikifika Nyerere day nazima simu na sipatikani ili wasinizoee tena.

Kutumia jina Nyerere ni jina kama majina mengine Kila mtu ana haki ya kuitwa au kujiita... Mohammed, Mwakyambiki, Yesu, Mkapa, Obote, Kassim yote hayo ni majina unajichagulia unalotaka,, Hata huyo Nyerere baba ake kuna watu waliitwa Nyerere kabla yake...
hakulelewa kuzima simu na kutokuwasikiliza viongozi wa nchi ndugu
 
Back
Top Bottom