Kumbukumbu Kutoka Maktaba 1989 Askofu Mkuu Marko A Mgulunde, Pd. W. Slaa na Mama Getrude Mongela

Kumbukumbu Kutoka Maktaba 1989 Askofu Mkuu Marko A Mgulunde, Pd. W. Slaa na Mama Getrude Mongela

Mhashamu Askofu Mkuu Marko A Mgulunde akimpongeza Mama Getrude Mongela mara baada ya kutoa mada yake iliyohusu uhusiano wa kanisa na serikali kwenye warsha ya Caritas; huku Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Pd. W Slaa (kushoto) akiangalia. [PICHA Pd. Anthony Chilumba].

Kiongozi Toleo la Kwanza December 1989

Lakini kupata picha kamili tambua na uelewe kuwa Pd. W. Slaa huyo hapo juu pichani akiwa nje ya uongozi wa kanisa alichaguliwa na chama chake CHADEMA kugombea urais wa Tanzania akipambana na Jakaya Mrisho Kikwete wa CCM mwaka wa 2010.

(Picha hiyo hapo juu inatoka katika ''scrap book'' yangu ambayo sasa ina umri wa miaka 46 ingawa imeacha kufanya kazi kwa miaka mingi.

Imestaafishwa na computer).​
Ingependeza zaidi ukaenda kuisha Somalia.
 
HUko juu.picha zote geresha tu
Picha ya university of khartoum na mavazi yenu ni kusudio kubwa
Bal...
Mimi si mtu wa ghilba.

Niko JF kwa jina langu halisi kwa sauti na picha.

Sijajificha.

Niulize chochote kuhusu mimi nitakujibu bila hofu.
 
Hiyo picha ya Mwisho hapo University of Khartoum inaumiza ukifikiria kinachoendelea Leo huko Sudan

..inasemekana wanaofadhili vita vya Sudan ni UAE.

..UAE wamekuja kama Wakoloni mambo leo wenye nia yakuhodhi bandari na njia za usafiri ktk bara la Afrika.

..kwa Tanzania UAE wamekuja kwa jina la DP world na kugawiwa gati ktk bandari ya Dsm.

..Usije ukashangaa chama fulani cha siasa kupewa mapesa ya kampeni na UAE / DP world.

..ikionekana sanduku la kura halitasaidia chama kibaraka cha UAE / DP world musishangae wakianza kufadhili vita kama Sudan.

..
 
Mohamed Said Babu Natamani kujua machache kuhusu John Okelo field marshal .

Nini kilimkuta baada ya mapinduzi ya Zanzibar?

Kwanini hakupata wadhifa wowote baada ya mapinduzi.
Aliondoka kwa kupenda au walimtimua?

Alihongwa chochote?
Okello alitupwa mbali huko baada ya kuona kaz yake waliyompatia ya kutangaza mapinduzi imekwisha,hvo hakuwa na kaz ikabidi wampandishe ndege had kwao.

Huko kwao Iddi Amin akaanza kusema "naona Uganda sas ina field marshal wawili" [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Kilichomkuta okello sasa ni noma unaambiwa kazikwa km mbuzi watu wawili watatu tu na hkn kutangaza habari zake kuanzia hapo. Ndio hvo
 
Mhashamu Askofu Mkuu Marko A Mgulunde akimpongeza Mama Getrude Mongela mara baada ya kutoa mada yake iliyohusu uhusiano wa kanisa na serikali kwenye warsha ya Caritas; huku Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Pd. W Slaa (kushoto) akiangalia. [PICHA Pd. Anthony Chilumba].

Kiongozi Toleo la Kwanza December 1989

Lakini kupata picha kamili tambua na uelewe kuwa Pd. W. Slaa huyo hapo juu pichani akiwa nje ya uongozi wa kanisa alichaguliwa na chama chake CHADEMA kugombea urais wa Tanzania akipambana na Jakaya Mrisho Kikwete wa CCM mwaka wa 2010.

(Picha hiyo hapo juu inatoka katika ''scrap book'' yangu ambayo sasa ina umri wa miaka 46 ingawa imeacha kufanya kazi kwa miaka mingi.

Imestaafishwa na computer).​
Huyu mzee ni wakulindwa kwa gharama yyte ile ndgu zangu watanzania, kwa sababu anatuelimisha vijana wa kileo ili tujue ukweli wa mambo ulivo.

Sisi vijana wa zama hizi sio wadadisi ,hatuna hamu ya kujifunza vitu vipya,hatuna muamko wa kujisomea vitabu kw sababu wanasema " kusoma ni kuutafuta ukweli" sisi hilo hatuna.

Binafsi amenifundisha mengi sana kupitia mabandiko yake hapa jf.

Namuombea kwa Mungu azidi kumpa siha njema na umri mrefu ili sisi vijana tunaojielewa na kujitambuwa tuzidi kunufaika kimaarifa kutokana na yeye.

Tujivunie huyu mzee jamani wakat huu akiwa hai kwa sababu " KILA MZEE ANAEKUFA AFRIKA NI SAWA NA MAKTABA MZIMA KUTEKETEA NA MOTO"

Sasa hapa kwa mzee saidi naweza sema kuna maktaba zaidi ya mia. hvo itakuw hasara kubwa sana kwetu endapo hatujaitumia vzr library hii ikiwa hai.
 
Yoso,
Hakika Uislam naupenda mno.

Huu ni mwaka wa 26 toka nilipoandika kitabu changu cha kwanza: ''The LIfe and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.''

Kitabu hiki kimebadili maisha yangu na kimebadili historia ya uhuru wa Tanganyika na kimebadili pia historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Jina la kitabu liliwashtua wengi.

Kama kupenda Uislam kuna uhusiano na kufuga majini mimi nimekuwa hivi toka udogoni na kuwa hivi ni malezi yetu.

Kufuga majini ni ilm maalum nimeelezwa watu wanajifunza.

Majini ni viumbe kama sisi wameumbwa na Allah.
Nilipokuwa mtoto nilimfahamu Sheikh mmoja jina lake Mwalimu Bakari.

Mwalimu Bakari alikuwa mtu maarufu mitaa ya Gerezani akiishi Mtaa wa Livingstone na Kirk Street (Lindi Street).

Mwalimu Bakari walimpa jina lingine wakazi wa Dar es Salaam.
Walimwita Mwalimu Bakari ''Sethabari.''

Maana ya hili jina lingine ni kuwa mjuzi wa yale ambayo hayaonekani na macho.

Mimi alitokea kunipenda kwa kuwa nilikuwa nimefiwa na mama yangu nikiwa na umri wa miaka minne.

Akiniona alikuwa ananishika kichwa na kuniombea dua na kunifariji kwa kunipa fedha.

Hii ilikuwa kawaida yake.

Mwalimu Bakari watu wakihadithia mengi kuhusu yeye kuwa alikuwa anaweza kuzungumza na majini na kuwatuma kazi na wakamtii.

Kwa hakika ni ilm ambayo sijakutana na mtaalamu akanieleza hasa undani wake.

Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika katika Baraza la Wazee wa TANU alikuwa Sheikh Issa Nasr kutoka Bagamoyo.

Sheikh Issa Nasr nimeambiwa alikuwa ujuzi mkubwa wa ilm ya majini.

Katika utafiti wangu wa kitabu cha Abdul Sykes nilifahamishwa kuwa Sheikh Issa Nasr alikuwa mmoja wa ''walinzi maalum' wa Mwalimu.

Wanasema popote alipokuwa Nyerere yeye atakuwa karibu yake na mpashaji habari wangu anasema hapo yuko na ''askari'' zake ambao hawaonekani.

Huyu aliyekuwa akinipa taarifa hizi ameniambia yeye akimjua Sheikh Issa Nasr toka udogoni kwake Bagamoyo na wao walipokuwa watoto wakimuona Sheikh Nasr amekaa nje ya nyumba yake walikuwa wanabadilisha njia kwa kumuogopa.

Mimi nikaamua kufanya utafiti kuangalia picha za Nyerere kama nitamuona Sheikh Issa Nasr karibu ya Mwalimu akipiga doria na jeshi lake la askari maalum.

Niliweza kuona picha mbili na zote tawire.
Sheikh Issa yuko pembeni ya Mwalimu Nyerere.

Picha ya kwanza ni ile ya Baraza la Wazee wa TANU iliyopigwa mwaka wa 1957.

Angalia picha hiyo hapo chini Sheikh Issa Nasr ni huyo aliyechutama miguuni kwa Nyerere na fimbo begani.

Picha ya pili ni ya mwaka wa 1961 siku Ian Macleod Waziri wa Makoloni alipotoa siku ya uhuru wa Tanganyika Karimjee Hall mwaka wa 1961.

Angalia picha hiyo utamuona Nyerere kabebwa mabegani na Sheikh Issa Nasr yuko pembeni yake.

View attachment 3157803
Sheikh Issa Nasr huyu chini ya Mwalimu Nyerere ni wa pili kushoto baada ya aliyevaa koti jeusi
View attachment 3157809
Kulia ni Sheikh Issa Nasr​
huyu mzee anatisha tu kwa kumuona. inasemekana tanga walifanyq dua wakasema mzee ruka shimo hili. alivoruka na wazee wakasema bas mkolon kwisha
 
Back
Top Bottom