Kumbukumbu ya Dar es Salaam dockworker's union 1948 katika Nyerere square 2022

Kumbukumbu ya Dar es Salaam dockworker's union 1948 katika Nyerere square 2022

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KUMBUKUMBU YA DAR ES SALAAM DOCKWORKER'S UNION 1948 KATIKA NYERERE SQUARE DAR ES SALAAM 2022

Hapo Nyerere Square palipojengwa jengo la kuvutia mwaka wa 1948 palikuwa na jengo la mbao na paa la mabati.

Katika jengo hilo ndipo ilipokuwa ofisi ya Abdul Sykes Secretary General wa Dar es Salaam Dockworker’s Union.

Katika jengo hilo ndipo viongozi wa Dar es Salaam Dockworker’s Union wakiongozwa na Abdul Sykes kwa upande mmoja na wawakilishi wa makampuni ya meli na Muingereza G. akisaidiwa na Labour Inspector Ahmed Barakat kwa upande wa pili walipokuwa wakifanya mikitano yao.

Hamilton aliletwa Tanganyika kutoka Uingereza kuja kuwafunza Waafrika wengi wao wakiwa Wazaramo, Wandengereko, Warufiji, Wang’indo waliokuwa wameshika kazi za ukuli namna ya kufanya majadiliano kati ya tajiri na muajiriwa kujadili maslahi yao wapakua mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam.

Hii ni historia ya kusisimua na nimeieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Mikutano hii ilikuwa migumu ya kutiishana na ilikuwa kushindwa kwa majadiliano haya ndipo kulikosababisha mgomo wa mwaka wa 1950 mgomo ambao makuli walipambana katika mitaa ya Dar es Salaam na vikosi vya wakoloni vya kuzuia fujo watu wa pwani wakiwaita askari wale ‘’Kavirondo,’’ na damu ikamwagika.

Kavirondo 19 waliuliwa.
Kavirondo maana yake ilikuwa mtu mshenzi.

Hawa walikuwa askari katili kutoka bara wasio na mila waliokuwa wakitumiwa na wakoloni kama mbwa wakali kupambana na Waafrika wenzao waliokuwa wanapigana kujitoa katika minyororo ya dhulma.

Mwezi June 1950 baada ya mgomo huu serikali iliipiga marufuku Dar es Salaam Dockworker’s Union.

Nikawa nimesimama Mtaa wa Mansfield naiangalia Nyerere Square fikra nyingi zikinipitia kuhusu historia ya wazalenso hawa waliojitolea kupambana na kila aina ya dhulma ya ukoloni lakini leo hakuna anaejua habari zao.

Historia imewasahau.

Abdul Sykes baada ya kutoka Dockworker’s Union ndiyo baada ya kifo cha baba yake 1949 akaingia TAA kwa juhudi kubwa ku kuendeleza mapambano ya kutafuta uhuru wa Tanganyika.

Ndipo mwaka wa 1950 yeye na Hamza Mwapachu wakitumia ujana wao wakafanikiwa kuuondoa uongozi wa Thomas Plantan na Clement Mtamila uliokuwa umepigwa na umri wakaichukua TAA na kufanya mabadiliko makubwa yaliyokuja kusimamisha TANU mwaka wa 1954.

Haya yote yanapita kichwani kwangu nikiiangalia Nyerere Square.

Taratibu nilijivuta kutoka hapo nikasogea mbele nikapiga picha Matasalamat Building.

Baba yangu aliniambia yeye mara ya mwisho kumuona Abdul Sykes walikutana Matasalamat Building wakazungumza kwa muda kisha wakaagana
Abdul Sykes akamuaga baba kwa kumwambia, ‘’Bukra,’’ neno la Kiarabu maana yake kesho.’’

1669264184140.png
1669264237592.png
 
Back
Top Bottom