Kumbukumbu ya Iftaar Nyumbani kwa Balozi Ramadhani Kitwana Dau Yanga Kids Walipofuturu Pamoja

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Utangulizi
Kuna wako wanaomtazama Dr. Dau kama ''Lecturer'' Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Kuna wengine wanamtazama Dr. Dau kama Mkurugenzi wa Masoko Tanzania Ports Authority (TPA) na wengine wanamtazama kama Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.

Wako wanaomtazama Dr. Dau kwa kujenga daraja maarufu la Kigamboni.
WanaKariakoo tunapenda kuliita daraja lile ''Daraja la Dau.''

Hawa wenye kumjua Dr. Dau na sasa Balozi Dau kwa sifa hizi ni wengi sana.

Lakini tupo tunaomtambua Ramadhani kwa kuwa mmoja wa vijana wadogo katika timu ya Yanga Kids katika miaka ya 1970.

Timu hii imeacha historia ya pekee katika soka la Tanzania na inawezekana Afrika.

Inatosha.
Siku kama ya leo mwaka uliopita 2023 Balozi Dau alitualika nyumbani kwake kufuturu.

Nimefuturu nyumbani kwa Dr. Dau mara nyingi sana lakini futari hii ilikuwa ya aina yake.

Hii ilikuwa futari ya ''Wananchi.''

Watu baki nadhani tulikuwa watatu hivi: Mimi, Matimbwa Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es Salaam na Mshike.

Waliobakia wote wenyewe - Dar Young Africans na Pan Africa.

Kuna mshairi alikuwa anatunga shairi na mwanzo wa ubeti akajiuliza, ‘’Wapi ninaanza kueleza historia hii?’’

Akaendelea kuandika, ‘’Wapi ninaanza kueleza historia hii, historia iliyojaa majonzi na furaha?’’

Najiuliza wapi nitaaza kueleza historia ya vijana wenzangu niliwajua kwa miaka mingi toka utotoni wengine kwa karibu na wengine kwa mbali?

Na wengine hatuko nao wametangulia mbele ya haki.
Bado najiuliza wapi naanza kueleza historia ya Yanga Kids.

Naanza na Kocha Victor Stanslaus?

Au naanza na Balozi Dr. Ramadhani Dau aliyetualika futari nyumbani kwake Kisota, Kigamboni?

Wengine huita Kizota.
Panastahili jina hilo.

Niliyoshuhudia kwa macho yangu na kuyasikia kwa masikio yangu hayajapata kunipitikia hata kwa mbali katika fikra zangu.

Hii ni kumbukumbu katika kumbukumbu zangu nzuri za futari.
Nimesali Maghrib na kufuturu na nyota wa mpira wa Tanzania.

Wangapi wamepata bahati hii?

Baraza ya mbele ya nyumba ya Balozi Dau siku ile ilikuwa Majlis ya aina yake.
Balozi Dau kama nilivyotangulia kusema alikuwa mchezaji wa Yanga Kids.

Leo nduguze wamemwitika na Balozi karudi udogoni yuko Jangwani na Adolf, Kassim Manara, Mkweche, Godian Mapango, Carlos Mwinyimkuu, Mohamed Selugendo, Juma ‘’Mensah’’ Pondamali na marehemu Tostao.

Sunday ‘’Computer’’ Manara yuko kaka pembeni ya Balozi lakini yeye wakati ule wa Yanga Kids yeye tayari ni ‘’Senior Player.’’

Wanakumbushana kelele za Kocha Victor anawapigia kelele Yanga Kids wakiwa na mpira kuhama sehemu moja ya uwanja wafanye mashabulizi kutoka upande mwingine.

Kocha Victor anapiga kelele, ‘’Change,’’ yaani mpira uondoshwe huko uende kwengine.

Hapa wanamwiga Kocha Victor Stanslaus.

Mohamed Selugendo na Balozi Dau nawasikia wakikumbushana maelezo ya Kocha Victor kuwa pasi itolewa baada ya kuangalia inapigwa kwa nani ili izae matunda.

Mohamed Selugendo yeye akicheza Winger na anakumbuka sana pasi alizokuwa kimdondoshea Kassim Manara juu kwa kufunga magoli ya kichwa.

Walikuwa siku ile hawa ndugu zangu wamerudi utotoni kabisa.

Baraza ya mbele ya nyumba ya Balozi Dr. Dau ilikuwa sawa na Bunge la wacheza mpira na takriban wote walikuwa nyota kwanza katika timu ya Yanga Kids, timu ya watoto wadogo wa Yanga kisha wakacheza timu ya wakubwa kwa kiwango kilekile.

Hawa kwa weledi na wakacheza Yanga na baadae wakiwa wakubwa kushiriki katika mashindano makubwa ya makombe ya Afrika.

Katika ya haya wengi wao walivaa jezi za Taifa Stars.
Hata hivyo huu haukuwa ndiyo mwisho wao.

Walivuka mipaka ya Tanzania na kucheza soka la kulipwa Ulaya na kwengineko.

Utapenda kumsikia Juma ‘’Mensah’’ Pondamali anavyoeleza mechi ya mwaka wa 1980 waliyocheza Ndola siku Taifa Stars ilkipocheza na Zambia ilivyoshinda kucheza fainali la Kombe la Mataifa ya Afrika, Nigeria.

Rais Kaunda yuko uwanjani mkono wake wa kulia ameshika kitambaa cheupe na uwanja umejaa mashabiki wanaishangilia timu yao, Pondamali anatueleza.

Utapenda kumsikiliza Juma Pondamali akieleza kipigo cha mashuti makali alichokipata kutoka kwa washambuliaji wa Zambia na jinsi alivyokuwa anapangua mashuti ambayo kwa hakika yangekuwa magoli.

‘’Nilikuwa nahema kama mchezaji wa ndani na kipindi cha mapumziko nikamuomba Mahadhi aje anisaidie maana nilikuwa na hofu nitafungwa tu.’’

Juma Pondamali anasema, Mahadhi alikataa.

Aliyoyaona kwa Pondamali yaliyokuwa yanamkuta mlinda mlango mwenzake yalimtosha.

Taifa Stars ilikuwa inahitaji ushindi wa goli moja tu kuingia kwenye fainali za Kombe la Afrika.

Ilikuwa katika kuelemewa kama huku alikoeleza ndipo Juma Mensah anasema alidaka mpira wachezaji wa Zambia wakiwa wamewaelemea wamejazana golini kwao na yeye kwa haraka baada ya kudaka tu akampigia mpira mrefu Peter Tino katikati ya Uwanja.

Peter Tino alipoupokea mpira ule hakusubiri akaupeleka mbele kwa kasi na ghafla akajikuta amewaacha walinzi wa KK 11 nyuma na yeye yuko mbele yao analiangalia goli la Zambia.

Yaliyobakia ni historia.

Pondamali anazungumza kwa nguvu na hisia kiasi unajiona kama uko uwanjani unaangalia pambano uwanjani, Ndola.

Adolf Rishard utafurahi na utacheka kumsikiliza akieleza changamoto alizokuwa akikutananazo kama nahodha wa ama katika Timu ya Taifa au Pan Africa.

Adolf anaongea kwa utulivu na taratibu na anapanga vyema maneno yake kwa staili ya kukufanya wewe ucheke vipi Pondamali anafukuzana uwanjani na waamuzi.

Anaeleza shida iliyokuwa ikimkuta kumtuliza Pondamali asifanya jambo likasababisha matatizo kwake na kwa hiyo kuathiri timu nzima.

Pondamali anamweleza Adolph, ‘’Umeona Sabu na Masimenti wamenikumba wameniingiza kwenye nyavu na wamefunga goli.’’

Captain Adolph anamjibu mlinda mlango wake kuwa, ‘’Tulia hazipiti dakika tano tutarudisha hili goli.’’

Hakika goli linarudishwa.

Bila kuambiwa na mtu nimeshuhudia mapenzi ambayo bado yangalipo kati ya nyota hawa miaka mingi baada kumaliza kucheza soka.

Mbali na tulipokuwa tunazungumza barazani nimeona tulipokuwa ndani tumekaa tunafuturu wanavyosemezana wenyewe kwa wenyewe.

Nimewasikia pale Majlis Kassim Manara akilaumu kitendo cha uongozi wa Yanga kuivunja Yanga Kids kwa kuwatoa wao kidogo kidogo na kuwatia timu kubwa kinyume na maelekezo ya Kocha Victor kuwa timu hiyo iachwe kama ilivyo hadi ifikie upeo kuwa sasa timu yote imekuwa ndiyo timu ya Yanga.

Adolph anaeleza mechi sasa wametoka Yanga baada ya mgogoro wa mwaka wa 1975 wako Pan Africa walizocheza Afrika ya Magharibi na kwengineko kwa fasaha utadhani anasoma kutoka kitabuni.

Nina ugomvi na Adolph kwa ukaidi wake wa kufanya ajizi kuandika kumbukumbu zake za maisha yake katika soka la Tanzania.

Adolph na Juma Mensah wana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika na siasa zake kuanzia kupata wachezaji hadi vipi timu na viongozi wa soka Afrika wanavyoendesha mambo ya mpira.

Wawili hawa wamecheza soka pamoja toka wakiwa makinda na hakuna wasichokijua.

Mwili utakusisimka ukiwasikia wakieleza saikolojia ya uchawi katika mpira na nafasi yake katika kupatikana ushindi hali kadhalika nafasi ya hongo.

Yapo mengi sana yanayotangulia mechi ndani ya uwanja kabla mpira haujaanza.

Sikuwanajua kuwa wachezaji wanajuana vizuri sana kiasi wanajua nani anafaa kumkaba nani na wakamweleza kocha na kocha anakubali ushauri.

Captain Adolf kaeleza mengi na vipi Taifa Stars walikuwa wanafanya uchaguzi katika mabeki kama watatu hivi kati ya Kajole, Amasha na mwingine nani acheze.

Halikadhalika kuficha uwezo wa washambuliaji kwa mabeki ili wasitishike na yeye.

Alieleza vipi Mayanga mshambuliaji hatari wa Zaire alivyotulizwa na kijana mdogo Ahmed wa Pan Africa juu ya sifa zake nyingi za kutisha.

Adolph anaeleza changamoto za nyakati hizo za wachezaji kuzuiwa kutoka nje ya mipaka kucheza soka la kulipwa na jinsi walivyokuwa wakinyang’anywa pasi za kusafiria kwa kuogopa wasitoroke.

Adolph ana kisa cha kusisimua cha yeye kukamatwa Uwanja wa Ndege Nairobi.

Balozi Dau siku zote yeye ‘’adui’’ yake ni Sunday Manara.

Kila mtu akifika akikaribishwa na kukaa kitako swali lake kwake litakuwa, ‘’Hebu tumalizie ubishi huu Kassim Manara na Sunday nani alikuwa na mpira mkubwa?’’

Balozi atacheka sana akisikia jibu kuwa Kassim ngoma yake ilikuwa nzito kuliko ya Sunday kaka yake.

Kassim anasema Timu ya Uholanzi ya Kombe la Dunia walikwenda Austria
kufanya mazoezi na wakacheza na timu yao.

Kassim alipangwa kucheza Sunday alikuwa kakaa kwenye bench.

Nimewaona kabla ya futari waandishi wa michezo wakihangaika na camera zao wakifanya mahojiano na Sunday na Kassim Manara.

Naamini watatuletea vipindi vya kuburudisha kutokana na waliyoyasikia katika mkusanyiko huu na katika mahojiano hayo.

Wakati wa kufturu nilibahatika kukaa na Carlos Mwinyimkuu na katika mazungumzo alinifahamisha kuwa ana maktaba nyumbani kwake ya picha nyingi za mpira alizozihifadhi vizuri.

Alinifahamisha kuwa amehifadhi pia historia yake ya mpira.

Anasema kacheza mechi 16 za mashindano makubwa zote kacheza dakika 90.

Sunday Manara yeye kanifahamisha kuwa mshabiki wake mmoja amemuuzia hazina kubwa ya picha kutoka magazeti ya zamani ambayo alikusanya miaka ile.

Sunday amehifadhi picha hizi baada ya kuzifanyika ''scanning.''

Hizi ni habari nzuri sana kwa TFF ikiwa watataka kutengeneza maktaba yake ya mpira wa Tanzania.

Halikadhalika pia hizi ni taarifa nzuri kwa waandishi wa michezo na vyombo vya habari kwa ujumla.

Nimesikitika sana sikuweza kumpata Kassim Manara kwa tete a tete hata ya nusu dakika kwani baada ya kufuturu hakukaa sana aliondoka kutokea hapo kukimbilia uwanja wa ndege kwa safari ya kurejea Austria.

1712434798510.png

Kulia: Kassim Manara, Mohamed Mkweche, Adolph Rishard, Godian Mapango, Mwandishi, Balozi Ramadhani Dau na Taufiq Kazaliwa.
1712434974475.png

Kulia: Mshike na Juma Pondamali
1712435048599.png

1712435120666.png

Kulia ni Mohamed Selugendo​
 
Sh Mohamed
Leo umenikumbusha miaka yangu ya odogoni, timu yangu ilikuwa Pan Africa
Umemtaja mtu ambae nilikuja kusikia karibuni tu kuwa amefariki nae ni Mohamed Yahya Tostao, Mwenyeezi Mungu amsamehe makosa yake
Kweli usemayo hakika team ile ya Young kids haitotokea kwa miaka ya karibu
Dr Dau, sina la kusema juu yake kwani nitaharibu haiba yake
Naikumbuka mechi ya A.S Vita ya Zaire na Pan Africa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha

Nakupa shukurani sana kwa kunikumbusha ya zamani

Mwenyeezi Mungu akupe kila lenye kheri
 
Adolph anaeleza changamoto za nyakati hizo za wachezaji kuzuiwa kutoka nje ya mipaka kucheza soka la kulipwa na jinsi walivyokuwa wakinyang’anywa pasi za kusafiria kwa kuogopa wasitoroke.

Adolph ana kisa cha kusisimua cha yeye kukamatwa Uwanja wa Ndege Nairobi.
Kumbe mpira ulikuwa unaharibiwa na siasa toka zamani
Shukran kwa historia nzuri...
 
1.Juma Pondamali 2. Jaffar Abdulrahman 3.Mohammed Mkweche 4. Leodgar Tenga 5. Jella Mtagwa 6. Mohammed Rishard " Adolf" 7.Gordian Mapango 8.Muhaji Mukhi 9. Kitwana Manara 10.Mohammed Yahya "Tostao" 11.Kassim Manara
 
Mohamed Said,

..bila shaka Adolf Rishard alikuwa akimzungumzia Mayanya Maku, left winger wa AS Vita ya Zaire, iliyocheza na Pan Africa uwanja wa Sheikh Amri Abeid ktk mashindano ya kombe la washindi wa Afrika. Katika mechi hiyo Pani walishinda bao 2 -- 1 lakini walitolewa ktk mashindano kwasababu walifungwa bao 1--0 walipocheza Kinshasa.
 
Adolph ambaye Umesema kwenye picha hafanani ninayemjua. Labda kanzu na kofia aliyovaa imenichanganya. Hawafanani
 
Sh Mohamed
Leo umenikumbusha miaka yangu ya odogoni, timu yangu ilikuwa Pan Africa
Umemtaja mtu ambae nilikuja kusikia karibuni tu kuwa amefariki nae ni Mohamed Yahya Tostao, Mwenyeezi Mungu amsamehe makosa yake
Kweli usemayo hakika team ile ya Young kids haitotokea kwa miaka ya karibu
Dr Dau, sina la kusema juu yake kwani nitaharibu haiba yake
Naikumbuka mechi ya A.S Vita ya Zaire na Pan Africa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha

Nakupa shukurani sana kwa kunikumbusha ya zamani

Mwenyeezi Mungu akupe kila lenye kheri
Wandugu,
Pan Africa Swahili na Mafia nyumbani kwa Bi. Hanifa ilikuwa barza yangu.
 
historia nzuri kwa sisi wapenda soka,angalau tunapata machache kwenye mengi yaliyojiri huko nyuma kutoka kwa wasakata kabumbu wa Tanzania,hakika siku hazigandi.🙏
 
Mohamed Said,

..bila shaka Adolf Rishard alikuwa akimzungumzia Mayanya Maku, left winger wa AS Vita ya Zaire, iliyocheza na Pan Africa uwanja wa Sheikh Amri Abeid ktk mashindano ya kombe la washindi wa Afrika. Katika mechi hiyo Pani walishinda bao 2 -- 1 lakini walitolewa ktk mashindano kwasababu walifungwa bao 1--0 walipocheza Kinshasa.
Mechi ile naikumbuka sana. Pan walikuwa wazuri sana katika ''off side trick''. Yaani wanahama unajikuta uko peke yako.

Mohamed, kwavile ilikuwa barza ya 'kids' lakini ingenoga zaidi kama Abdallah Kibaden Mputa angelikaa kando ya Sunday Manara. Hawa watu waliitikisa sana Afrika Mashariki.

Mo umenikumbusha Mkweche, Mapango, Pondamali , Adolf n.k. Nimewakumbuka pia akina Maulid Dilunga, Abbas Dillunga. Mohamed Kajole, Omar Mahadhi, Salihina na Nasor Mshoto wa Zanzibar, Mohamed Chuma , Gibson Sembuli, n.k. Ukitamtaja Sembuli hapo Mbaraka Mwinshehe anakuja maana alimtungia wimbo baada ya kifo.

Mohamed Chuma alichezea Bandari Mtwara na ni mchezaji aliyeichezea Taifa Stars kwa miaka 10 mfululizo.
Huko Mtwara natamani wangempa hadhi ya Mtaa au Barabara.

Mohamed Said Ramadhani inakwisha, lini Iftar kwako tujuliane hali ! usinisahau Sheikh
 
Ukimtaja Balozi Dr.Dau nakumbuka Mafia juu ya ukarimu,uzalendo alioufanya kwa watu wa Mafia kipindi naishi kule karibu kabisa na nyumbani kwake Tereni.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sh Mohamed
Leo umenikumbusha miaka yangu ya odogoni, timu yangu ilikuwa Pan Africa
Umemtaja mtu ambae nilikuja kusikia karibuni tu kuwa amefariki nae ni Mohamed Yahya Tostao, Mwenyeezi Mungu amsamehe makosa yake
Kweli usemayo hakika team ile ya Young kids haitotokea kwa miaka ya karibu
Dr Dau, sina la kusema juu yake kwani nitaharibu haiba yake
Naikumbuka mechi ya A.S Vita ya Zaire na Pan Africa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha

Nakupa shukurani sana kwa kunikumbusha ya zamani

Mwenyeezi Mungu akupe kila lenye kheri
Pan Africa ndio team yangu mpaka kesho.

Ngoja nikurejeshe nyuma kidogo.
Pan Africa walichagua Mji wa Arusha kama uwanja wao wa nyumba kwasababu Dar ilishatekwa na team za Simba na Dar Young Africa.

Naikumbuka mechi kati ya Pan Africa na Vita ya Zaire wakati huo sasa Congo.
Team zilisha salimia watazamaji katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
1. Juma Pondamali
2. Mohamed Mkweche
3. John Faya.
4. Jafary Adrahaman / Leordiga Tenga sikumbuki nani alianza.
5. Jella Mtagwa huyu Mwamba picha yake iliwahi kutoka katika stamp.
6. Mohamed Rishad Adolf
7. Godian Mapango huyu Mwamba alikuwa mfupi machachari sana.
8. Moahamed Yahaya Tostao
9. Kassim Manara
10. Muhaj Muki
11. Ally Katolila.

Mechi inakaribia kuanza wachezaji wa pande zote mbili wameshasalia watazamaji ghafla BENZ inaingia kwa kasi kubwa uwanjani anashuka Sunday Manara nadani akitokea Nairobi au KIA wakati huo Sunday akicheza mpira kama kumbukumbu zangu zipo sawa Australia.Muhaj Muki anampisha Sunday Manara anaingia huku akivaa kezi ya Pan Afrika uwanja mzima unalipuka kwa shangwe kubwa.

Mpira unapigwa si mchezi Vita ikiwa na washambuliaji wakubwa Lofombo na Mayanga wanapata bao la kuongoza.Sunday anakokota mpira anampasia ndugu yake Kassimu wanasawazisha na baadae wanaongeza bao la pili.

Wakati huo Marehemu Sammy Mdee Mkurugenzi wa AICC na Ndollanga Mkurugenzi wa TAWICO hawa wakuu ndio waliokuwa wakiratibu mipango yote ya PAN AFRICA FC.

Nakumbuka kuna kipindi timu yetu ya taifa kuanzia number hadi number 11 wote walitoka Pan Africa FC.Kwa hakika Pan Africa ilisheheni wachezaji wa kiwango cha juu na kubwa zaidi wote walikuwa wazawa.
 
Mechi ile naikumbuka sana. Pan walikuwa wazuri sana katika ''off side trick''. Yaani wanahama unajikuta uko peke yako.

Mohamed, kwavile ilikuwa barza ya 'kids' lakini ingenoga zaidi kama Abdallah Kibaden Mputa angelikaa kando ya Sunday Manara. Hawa watu waliitikisa sana Afrika Mashariki.

Mo umenikumbusha Mkweche, Mapango, Pondamali , Adolf n.k. Nimewakumbuka pia akina Maulid Dilunga, Abbas Dillunga. Mohamed Kajole, Omar Mahadhi, Salihina na Nasor Mshoto wa Zanzibar, Mohamed Chuma , Gibson Sembuli, n.k. Ukitamtaja Sembuli hapo Mbaraka Mwinshehe anakuja maana alimtungia wimbo baada ya kifo.

Mohamed Chuma alichezea Bandari Mtwara na ni mchezaji aliyeichezea Taifa Stars kwa miaka 10 mfululizo.
Huko Mtwara natamani wangempa hadhi ya Mtaa au Barabara.

Mohamed Said Ramadhani inakwisha, lini Iftar kwako tujuliane hali ! usinisahau Sheikh
Nguruvi,
Nimecheka peke yangu kama mwehu.
Mfungo unakatika hatuna siku tena.
 
Utangulizi
Kuna wako wanaomtazama Dr. Dau kama ''Lecturer'' Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Kuna wengine wanamtazama Dr. Dau kama Mkurugenzi wa Masoko Tanzania Ports Authority (TPA) na wengine wanamtazama kama Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.

Wako wanaomtazama Dr. Dau kwa kujenga daraja maarufu la Kigamboni.
WanaKariakoo tunapenda kuliita daraja lile ''Daraja la Dau.''

Hawa wenye kumjua Dr. Dau na sasa Balozi Dau kwa sifa hizi ni wengi sana.

Lakini tupo tunaomtambua Ramadhani kwa kuwa mmoja wa vijana wadogo katika timu ya Yanga Kids katika miaka ya 1970.

Timu hii imeacha historia ya pekee katika soka la Tanzania na inawezekana Afrika.

Inatosha.
Siku kama ya leo mwaka uliopita 2023 Balozi Dau alitualika nyumbani kwake kufuturu.

Nimefuturu nyumbani kwa Dr. Dau mara nyingi sana lakini futari hii ilikuwa ya aina yake.

Hii ilikuwa futari ya ''Wananchi.''

Watu baki nadhani tulikuwa watatu hivi: Mimi, Matimbwa Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es Salaam na Mshike.

Waliobakia wote wenyewe - Dar Young Africans na Pan Africa.

Kuna mshairi alikuwa anatunga shairi na mwanzo wa ubeti akajiuliza, ‘’Wapi ninaanza kueleza historia hii?’’

Akaendelea kuandika, ‘’Wapi ninaanza kueleza historia hii, historia iliyojaa majonzi na furaha?’’

Najiuliza wapi nitaaza kueleza historia ya vijana wenzangu niliwajua kwa miaka mingi toka utotoni wengine kwa karibu na wengine kwa mbali?

Na wengine hatuko nao wametangulia mbele ya haki.
Bado najiuliza wapi naanza kueleza historia ya Yanga Kids.

Naanza na Kocha Victor Stanslaus?

Au naanza na Balozi Dr. Ramadhani Dau aliyetualika futari nyumbani kwake Kisota, Kigamboni?

Wengine huita Kizota.
Panastahili jina hilo.

Niliyoshuhudia kwa macho yangu na kuyasikia kwa masikio yangu hayajapata kunipitikia hata kwa mbali katika fikra zangu.

Hii ni kumbukumbu katika kumbukumbu zangu nzuri za futari.
Nimesali Maghrib na kufuturu na nyota wa mpira wa Tanzania.

Wangapi wamepata bahati hii?

Baraza ya mbele ya nyumba ya Balozi Dau siku ile ilikuwa Majlis ya aina yake.
Balozi Dau kama nilivyotangulia kusema alikuwa mchezaji wa Yanga Kids.

Leo nduguze wamemwitika na Balozi karudi udogoni yuko Jangwani na Adolf, Kassim Manara, Mkweche, Godian Mapango, Carlos Mwinyimkuu, Mohamed Selugendo, Juma ‘’Mensah’’ Pondamali na marehemu Tostao.

Sunday ‘’Computer’’ Manara yuko kaka pembeni ya Balozi lakini yeye wakati ule wa Yanga Kids yeye tayari ni ‘’Senior Player.’’

Wanakumbushana kelele za Kocha Victor anawapigia kelele Yanga Kids wakiwa na mpira kuhama sehemu moja ya uwanja wafanye mashabulizi kutoka upande mwingine.

Kocha Victor anapiga kelele, ‘’Change,’’ yaani mpira uondoshwe huko uende kwengine.

Hapa wanamwiga Kocha Victor Stanslaus.

Mohamed Selugendo na Balozi Dau nawasikia wakikumbushana maelezo ya Kocha Victor kuwa pasi itolewa baada ya kuangalia inapigwa kwa nani ili izae matunda.

Mohamed Selugendo yeye akicheza Winger na anakumbuka sana pasi alizokuwa kimdondoshea Kassim Manara juu kwa kufunga magoli ya kichwa.

Walikuwa siku ile hawa ndugu zangu wamerudi utotoni kabisa.

Baraza ya mbele ya nyumba ya Balozi Dr. Dau ilikuwa sawa na Bunge la wacheza mpira na takriban wote walikuwa nyota kwanza katika timu ya Yanga Kids, timu ya watoto wadogo wa Yanga kisha wakacheza timu ya wakubwa kwa kiwango kilekile.

Hawa kwa weledi na wakacheza Yanga na baadae wakiwa wakubwa kushiriki katika mashindano makubwa ya makombe ya Afrika.

Katika ya haya wengi wao walivaa jezi za Taifa Stars.
Hata hivyo huu haukuwa ndiyo mwisho wao.

Walivuka mipaka ya Tanzania na kucheza soka la kulipwa Ulaya na kwengineko.

Utapenda kumsikia Juma ‘’Mensah’’ Pondamali anavyoeleza mechi ya mwaka wa 1980 waliyocheza Ndola siku Taifa Stars ilkipocheza na Zambia ilivyoshinda kucheza fainali la Kombe la Mataifa ya Afrika, Nigeria.

Rais Kaunda yuko uwanjani mkono wake wa kulia ameshika kitambaa cheupe na uwanja umejaa mashabiki wanaishangilia timu yao, Pondamali anatueleza.

Utapenda kumsikiliza Juma Pondamali akieleza kipigo cha mashuti makali alichokipata kutoka kwa washambuliaji wa Zambia na jinsi alivyokuwa anapangua mashuti ambayo kwa hakika yangekuwa magoli.

‘’Nilikuwa nahema kama mchezaji wa ndani na kipindi cha mapumziko nikamuomba Mahadhi aje anisaidie maana nilikuwa na hofu nitafungwa tu.’’

Juma Pondamali anasema, Mahadhi alikataa.

Aliyoyaona kwa Pondamali yaliyokuwa yanamkuta mlinda mlango mwenzake yalimtosha.

Taifa Stars ilikuwa inahitaji ushindi wa goli moja tu kuingia kwenye fainali za Kombe la Afrika.

Ilikuwa katika kuelemewa kama huku alikoeleza ndipo Juma Mensah anasema alidaka mpira wachezaji wa Zambia wakiwa wamewaelemea wamejazana golini kwao na yeye kwa haraka baada ya kudaka tu akampigia mpira mrefu Peter Tino katikati ya Uwanja.

Peter Tino alipoupokea mpira ule hakusubiri akaupeleka mbele kwa kasi na ghafla akajikuta amewaacha walinzi wa KK 11 nyuma na yeye yuko mbele yao analiangalia goli la Zambia.

Yaliyobakia ni historia.

Pondamali anazungumza kwa nguvu na hisia kiasi unajiona kama uko uwanjani unaangalia pambano uwanjani, Ndola.

Adolf Rishard utafurahi na utacheka kumsikiliza akieleza changamoto alizokuwa akikutananazo kama nahodha wa ama katika Timu ya Taifa au Pan Africa.

Adolf anaongea kwa utulivu na taratibu na anapanga vyema maneno yake kwa staili ya kukufanya wewe ucheke vipi Pondamali anafukuzana uwanjani na waamuzi.

Anaeleza shida iliyokuwa ikimkuta kumtuliza Pondamali asifanya jambo likasababisha matatizo kwake na kwa hiyo kuathiri timu nzima.

Pondamali anamweleza Adolph, ‘’Umeona Sabu na Masimenti wamenikumba wameniingiza kwenye nyavu na wamefunga goli.’’

Captain Adolph anamjibu mlinda mlango wake kuwa, ‘’Tulia hazipiti dakika tano tutarudisha hili goli.’’

Hakika goli linarudishwa.

Bila kuambiwa na mtu nimeshuhudia mapenzi ambayo bado yangalipo kati ya nyota hawa miaka mingi baada kumaliza kucheza soka.

Mbali na tulipokuwa tunazungumza barazani nimeona tulipokuwa ndani tumekaa tunafuturu wanavyosemezana wenyewe kwa wenyewe.

Nimewasikia pale Majlis Kassim Manara akilaumu kitendo cha uongozi wa Yanga kuivunja Yanga Kids kwa kuwatoa wao kidogo kidogo na kuwatia timu kubwa kinyume na maelekezo ya Kocha Victor kuwa timu hiyo iachwe kama ilivyo hadi ifikie upeo kuwa sasa timu yote imekuwa ndiyo timu ya Yanga.

Adolph anaeleza mechi sasa wametoka Yanga baada ya mgogoro wa mwaka wa 1975 wako Pan Africa walizocheza Afrika ya Magharibi na kwengineko kwa fasaha utadhani anasoma kutoka kitabuni.

Nina ugomvi na Adolph kwa ukaidi wake wa kufanya ajizi kuandika kumbukumbu zake za maisha yake katika soka la Tanzania.

Adolph na Juma Mensah wana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika na siasa zake kuanzia kupata wachezaji hadi vipi timu na viongozi wa soka Afrika wanavyoendesha mambo ya mpira.

Wawili hawa wamecheza soka pamoja toka wakiwa makinda na hakuna wasichokijua.

Mwili utakusisimka ukiwasikia wakieleza saikolojia ya uchawi katika mpira na nafasi yake katika kupatikana ushindi hali kadhalika nafasi ya hongo.

Yapo mengi sana yanayotangulia mechi ndani ya uwanja kabla mpira haujaanza.

Sikuwanajua kuwa wachezaji wanajuana vizuri sana kiasi wanajua nani anafaa kumkaba nani na wakamweleza kocha na kocha anakubali ushauri.

Captain Adolf kaeleza mengi na vipi Taifa Stars walikuwa wanafanya uchaguzi katika mabeki kama watatu hivi kati ya Kajole, Amasha na mwingine nani acheze.

Halikadhalika kuficha uwezo wa washambuliaji kwa mabeki ili wasitishike na yeye.

Alieleza vipi Mayanga mshambuliaji hatari wa Zaire alivyotulizwa na kijana mdogo Ahmed wa Pan Africa juu ya sifa zake nyingi za kutisha.

Adolph anaeleza changamoto za nyakati hizo za wachezaji kuzuiwa kutoka nje ya mipaka kucheza soka la kulipwa na jinsi walivyokuwa wakinyang’anywa pasi za kusafiria kwa kuogopa wasitoroke.

Adolph ana kisa cha kusisimua cha yeye kukamatwa Uwanja wa Ndege Nairobi.

Balozi Dau siku zote yeye ‘’adui’’ yake ni Sunday Manara.

Kila mtu akifika akikaribishwa na kukaa kitako swali lake kwake litakuwa, ‘’Hebu tumalizie ubishi huu Kassim Manara na Sunday nani alikuwa na mpira mkubwa?’’

Balozi atacheka sana akisikia jibu kuwa Kassim ngoma yake ilikuwa nzito kuliko ya Sunday kaka yake.

Kassim anasema Timu ya Uholanzi ya Kombe la Dunia walikwenda Austria
kufanya mazoezi na wakacheza na timu yao.

Kassim alipangwa kucheza Sunday alikuwa kakaa kwenye bench.

Nimewaona kabla ya futari waandishi wa michezo wakihangaika na camera zao wakifanya mahojiano na Sunday na Kassim Manara.

Naamini watatuletea vipindi vya kuburudisha kutokana na waliyoyasikia katika mkusanyiko huu na katika mahojiano hayo.

Wakati wa kufturu nilibahatika kukaa na Carlos Mwinyimkuu na katika mazungumzo alinifahamisha kuwa ana maktaba nyumbani kwake ya picha nyingi za mpira alizozihifadhi vizuri.

Alinifahamisha kuwa amehifadhi pia historia yake ya mpira.

Anasema kacheza mechi 16 za mashindano makubwa zote kacheza dakika 90.

Sunday Manara yeye kanifahamisha kuwa mshabiki wake mmoja amemuuzia hazina kubwa ya picha kutoka magazeti ya zamani ambayo alikusanya miaka ile.

Sunday amehifadhi picha hizi baada ya kuzifanyika ''scanning.''

Hizi ni habari nzuri sana kwa TFF ikiwa watataka kutengeneza maktaba yake ya mpira wa Tanzania.

Halikadhalika pia hizi ni taarifa nzuri kwa waandishi wa michezo na vyombo vya habari kwa ujumla.

Nimesikitika sana sikuweza kumpata Kassim Manara kwa tete a tete hata ya nusu dakika kwani baada ya kufuturu hakukaa sana aliondoka kutokea hapo kukimbilia uwanja wa ndege kwa safari ya kurejea Austria.

View attachment 2955920
Kulia: Kassim Manara, Mohamed Mkweche, Adolph Rishard, Godian Mapango, Mwandishi, Balozi Ramadhani Dau na Taufiq Kazaliwa.
View attachment 2955930
Kulia: Mshike na Juma Pondamali
View attachment 2955935
View attachment 2955936
Kulia ni Mohamed Selugendo​

View: https://www.youtube.com/watch?v=eh87Ox4iBfo
 
Dau alitakiwa kuwa segerea kaliibia sana NSSF kilichomiokoamagufuli asimfunge ni viwili,walikula wote mali ya wizi,pili kumshawish lipumba ajitoe ukawa kupunguza kura za Lowassa,ila dauni fisadi kama mafisadi wengine tu
 
Back
Top Bottom