Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Mag3 na Yericko Nyerere

Kuna kitendawili cha umiliki wa jengo alilotoa gavana. Sina kumbu kumbu kama tuliwahi kujadili hadi mwisho! Nadhani kulikuwa na utata. Mwaweza nikumbusha kidogo!
Katika tafiti zangu nyingi sijaona panapothibitisha kuwa pale palikuwa pa Kleist Sykes au Cecil Matola au Ramadhan Ali au mweusi yoyote, lakini bado ushahidi toka vyanzo vingi nilivyovibaini unaonyesha Sir Cameron kama serikali ndie aliyetoa jengo na eneo hilo litumiwe na Cecil Matola na watu wake katika AA, hii ni baada ya miezi kadhaa ya kuanzishwa AA ikiwa inafanyia shughuli zake nyumbani kwa Matola, zingatia kwa Matola rais wa AA sio Kleist Sykes wala Plantan na wahamiaji haramu wengine...
 
Ulishakisoma kitabu bibie au unamjadili Yericko sio kitabu chake?

Maaana sisi hapa hatumjadili Mahame Said bali historia yake katika kitabu chake...
 
maswali haya msaidie mzee mwenzako kujibu kakimbia!


1.Nani aliandika katiba ya TANU

2. AA au TAA zilikuwa na katiba ipi, iliandikwa na nani na mwaka gani

3. Kabla ya Nyerere nani aliandika katiba ya chama?
Hawawezi kukujibu hayo, ukiwabana sana watakwambia unawaonea kisa waislamu...
 
Katiba ya TANU wame Copy kutoka Convention People's Party (CPP) chama cha kina Kwame Nkrumah's .

Nakushauri ungetulia kwenye huu mnakasha ungejifunza vingi.

Kuliko kujifanya unajua wakati hamna kitu.
Je ni Abdul Sykes na wale wazee wenu ndio waliokwenda kwa Nkurumah kukopi katiba au ni Nyerere? Unadhani kwa nini walikwenda kukopi Ghana ilihali hapa unatuambia AA na TAA vilikuwa na katiba? Kwanini isingehuishwa katiba iliyokuwepo tu?

Tumia akili, tukiwaambia AA na TAA vilikuwa vilabu vya gongo muwe mnaelewa...
 
Kwanza nikushukuru kwa kuchangia mjadala huu, pili nikushauri kabla ya kuchangia soma mtiririko wa mjadala ulivyo...

Na mwisho nakushukuru kwa kunishauri...
 
Yericko hicho kitabu kitakuwa kichekesho.

Unasema kinahusu ujasusi sasa vipi kitabu cha ujasusi kitakuwa kitabu cha historia ya Tanganyika?

Hebu nitajie nani publisher wa kitabu chako au ndiyo hivyo tena?



Sent using Jamii Forums mobile app
Ukijua maana ya ujasusi wala hautashangaa kuona historia ya Mkwawa, Israel, USA, Urus, Tanganyika, Zanzibar, AA, TAA, TANU na CCM...

Ujasusi ni ulimwengu mwingine wenye maisha kama haya haya.... Hivyo sio kuvaa suti na bastola kiunoni tu
 
Shukrani kubwa sana kwakutupa machache haya yanayosherehesha na kutufunza mengi... Nakiri wewe historia unaijua, bahati mbaya una matatizo yanayoonekana ni madogomadogo lakini yana madhara makubwa sana...nayo ni udini na chuki dhidi ya Julius Nyerere.

Nimefurahishwa zaidi ambapo leo umekiri rasmi kuwa Cecil Matola ndie mwasisi wa AA, na katibu wake ni Kleist Sykes. Hili lilikuwa ugomvi wetu wa muda mrefu, na umekiri baada ya kubanwa sana hivi... Mengine tuendelee kujadiliana...
 
Hivi ndivyo ulivyoelewa?
 
Yericko,
Hakika hili la ''uasisi,'' limekuzongeni sana.
Sijakataa kuwa Cecil Matola alikuwa rais wa AA.

Kleist alikuwa na uwezo mkubwa sana wa oganaizesheni na hii nafasi ya
secretary ilimwenea sana.

Maisha yake yote alikuwa mjumbe wa Maulid Commitee katika mji wa
Dar es Salaam.

Hata alipokuja kuasisi Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mwaka wa
1933 yeye akawa secretary na president Mzee bin Sudi.

Baada ya Matola kufariki Mzee bin Sudi akawa president.

Sababu kubwa ya nafasi ya secretary kuwa yake ilikuwa kwanza alikuwa
anajua kupiga taipu kitu nadra sana kwa Mwafrika katika miaka ile ya
1920s na pia akijua kusema Kijerumani na Kiingereza.

Lakini kikubwa zaidi kilichompembua katika uongozi ni kuwa Kleist alikuwa
na uwezo mkubwa wa fedha na alikuwa mtu karimu sana.

Kuna mwaka kulikuwa na mgogoro katika Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika
ambayo ndiyo ilikuwa ikisimamia maulid na pakawa na tatizo la kuchangisha
fedha kwa ajili ya maulid.

Kleist alimaliza tatizo lile la kukusanya fedha kwa kutoa hela zote ili maulid
isiache kusomwa mwaka ule.

Barazani kwake nje ya duka lake watu walikuwa hawapungui na pia vikombe
vya kahawa na mmoja wa marafiki zake wakubwa alikuwa Aziz Ali Mwafrika
tajiri na ''contractor,'' wa kujenga majumba.

Sasa sijui hii ''kukiri,'' kuhusu Matola umekusudia kitu kipi labda unifafanulie.

Tatizo lenu nyie ni kuwa hamjui, ''background,'' habari za ziada za hawa watu
na ndiyo maana wakati mwingine mie huwa nacheka nikikusomeni.

Hawa mimi ni babu zangu na babu yangu Salum Abdallah alikuwa mmoja wa
wana-barza.

Unaposhikilia kuwa Matola aliasisi, aliasisi, aliasisi...
Mtu wa Mission Quarter enzi zile hawezi kumtangulia mtu kutoka Kariakoo.

Hizi ndizo zilivyokuwa siasa za kikoloni, wabague uwatawale yaani, ''divide
and rule.''

Hii ilikuwa sehemu imewekwa kando na Waingereza kwa ajili ya Wakristo
peke yao na sehemu peke yake Dar es Salaam ambako kulikuwa na kanisa.

TANU ndiyo ilikuja kuondoa hizi fitna.

Mimi huwa nachukua muda mwingi kueleza mambo zaidi ili nyie mjue hali
ya Dar es Salaam ya miaka ile ilikuwaje.

Kuwa mimi naijua historia ya wazee wangu hili wala si jambo kubwa sana
kwangu.

Wewe kama ungekuwa kizazi cha watu hawa nawe kama mimi ungeyajua
haya yote hata bila ya kufanya juhudi kubwa.

Sasa katika hali kama hii mtie Kleist na Matola katika mizani uwapime hapo
ndipo utakapoweza kujua ukweli.

Nayajua mengi sana na yapo ambayo sijapatapo kuyaeleza hapa.

Sasa soma kwanza historia ya watu wa Dar es Salaam na mji wenyewe kabla
ya kunyanyua kalamu kuandika.

Usifanye pupa kwani utafiti unataka subra.
 
Ukijua maana ya ujasusi wala hautashangaa kuona historia ya Mkwawa, Israel, USA, Urus, Tanganyika, Zanzibar, AA, TAA, TANU na CCM...

Ujasusi ni ulimwengu mwingine wenye maisha kama haya haya.... Hivyo sio kuvaa suti na bastola kiunoni tu
Yericko,
Unazungumza na mtu ambae maisha yake yote toka udogoni alikuwa
analala na vitabu mchagoni.

Huwezi kunifunza kitu katika uwanja huu.
Ngoja nikupe mchapo.

Siku moja sasa tushakuwa wakubwa tulikuwa Saigon Club tunazungumza.

Mimi nikawa nasikitika kuwa sikuweza kutimiza ndoto yangu ya kucheza
''competitive football,'' Simba na kisha Timu ya Taifa.

Jumanne Masimenti ambae alikuwa mchezaji wa Cosmopolitan, Simba
na Timu ya Taifa akaangua kicheko kile cha kebehi akasema, ''Hivi wewe
Eusobio (zamani sote tukijipa majina ya wachezaji wakubwa wa Ulaya wa
wakati wetu nami nilichagua jina hili) ungecheza mpira gani wewe.

Mazoezini sisi tukipiga danadana kabla ya mazoezi uko pembeni na vitabu
vyako unasoma.''

Tulikuwa tukicheza mpira hapo Mnazi Mmoja.
Hii ni miaka ya mwanzo ya 1960.

Jamaa wote kwa kuwa walikuwa wanaijua hii tabia yangu na ikiwaudhi sana
wakaangua kicheko.

Hivi ndivyo nilivyokuwa... Shakespeare to Irving Wallace na wengine wengi.
 
Yericko,
Ahsante kwa mchango huu.
 

Wewe kwanini usiandike historia ya hao wengine?

Mohamed Said kishaandika kuhusu Abdul Rauf Songea Mbano, kishaandika kuhusu Abdallah Mkwawa. Hao wote ni Wamanyema?

Pia kwenye kitabu chake Cecil Matola yumo, John Rupia yumo, Nyerere yumo, na wengine wengi ambao hujawahi kuwasikia isipokuwa kwa Mohamed Said, wote hao ni Wamanyema?

Nyie mlisema na kutuaminisha mtaungana mje na historia mpya, ndiyo hii ya "Sesilia Matola"?

Hapo sasa.
 
Wewe usingesoma kitabu cha Mohamed Said ungeuliza hayo?

Fanya tafiti uje na historia mbadala. Mbona Mohamed Said alipoona historia ya kivukoni imewaacha watu waliounda TANU na waliompokea Nyerere Dar akaja na kitabu ambacho kimekuwa mashuhuri sana. Vipi wewe unabaki kwenye JF kukosoa usiyoyajuwa?

Au ndiyo mambo ya "Sesilia Matola"?
 
jibu hoja alizouliza wacha kubwabwaja na kuhorojeka,njia ya muongo fupi mzee wa soga kwenye vijiwe vya kahawa kaumbuka!
*hiki ni kizazi cha kuhoji sio kila kitu 'hewala'
 
Yeriko katika historia ya AA hadi TAA na kufikia TANU hizi ndizo sehemu zilipo nyaraka zake yaani vyanzo vya kupata historia yake.

Kwanza ni Nyaraka za Sykes ambazo hadi leo wenyewe hawajazitoa kwa umma ukiacha kipindi kifupi Abdul Sykes alipokuwa yu hai na akampatia bint yake Daisy mwisho ya miaka ya 1960 ili amuonyeshe John Iliffe wa History Department Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Pili ni Maktaba ya CCM Dodoma.

Tatu Tanzania National Archives (TNA) na,

Nne kwa watu binafsi waliokuwa katika uongozi wa TAA na TANU na wengi wao wameshatangulia mbele ya haki.

Mimi kote huko nimepita na nimegundua mengi kiasi nimeandika paper, "Lost Documents."

Hii paper naitafuta maktaba sijaipata ilichapwa na Africa Events miaka ya 1980.

Hebu nifahamishe hizo "source," zako ni zipi tupate kulinganisha, "notes."

Lakini kote huko hakuna kulikokuwa na nyaraka za maana kushinda nilizoziona kwa akina Sykes.

Yericko hebu soma tena kipande hicho hapo
chini msikilize mdogo wake Abdul Sykes, Ally mwenye kadi ya TANU No. 2 akizungumza:

‘’I got in touch with Makatta Mwinyi Mtwana one of very influential and rich African businessmen in Tanga who had been a friend of my father. Makatta had established his business in Tanga. He was an importer of khanga and was competing with Indians.

Every weekend I used to travel to Tanga to visit him.

At that time Tanga was the seat of the settler community. Almost all the sisal estates in Tanganyika were in Tanga Province.

During weekends the settlers, almost all of them members of the Sisal Growers Association of Tanganyika, would drive to town from their estates and meet at Planters Hotel, which was exclusive to Europeans to discuss politics of the day. When nationalist politics began they met at the same hotel to plot against TANU.

I got in touch with Mwalimu Kihere to see if we could open a branch in Tanga but unfortunately there was not much I could do there because at that time Tanga was involved in its own internal social conflicts, which prevented the formation of a political party. One day I received a message from Makatta that on Friday at 5 p.m. the Tanga police would come to my house to search me for TANU documents.

I put whatever TANU papers I had in a box and went to hide them at a place where no one would think of searching. I hid the papers at Akena’s house. When a white police officer and three black policemen raided my house that day they found nothing.

They tore my mattresses and pillows, they combed the room but they could not find any paper to incriminate me.

How was Makatta informed of the raid against my house?

TANU had sympathisers in many places in the colonial administration. One of them tipped him off.

I stayed at Korogwe for eight months until when I became sick with a serious kidney ailment as a result of polluted water. I was referred to Dar es Salaam Sewa Haji Hospital for treatment. I needed an operation but there was no qualified kidney expert in Tanganyika to perform the operation. I was put on medication to relieve the pain.

The operation came to be performed in Dar es Salaam 1962 after independence by one Dr. Lean from Britain.

I did not return to Korogwe after getting well as I was transferred to Moshi Labour Office. I immediately began to organise for TANU. By then TANU had sent Nyerere to the United Nations in New York to plead for Tanganyika’s independence.

At the United Nations, Nyerere was not articulating anything new since his speech was from the very recommendations of the memorandum which the TAA Political Subcommittee had prepared and submitted to the Constitutional Development Committee of Governor Edward Twining in 1950 which were however ignored by the Governor.

Twining instead pursued a multiracial representation in the Legislative Council and to keep up with its stand, the government sent a multiracial delegation composed of I.C. Chopra, an Asian, Sir Charles Phillips a European, and Liwali Yustino Mponda, an African member of the Legislative Council for Newala, to oppose TANU at the United Nations.

We were determined to show the government that TANU had clout.’’

(Alphonce Akena alikuwa katika Jeshi la Polisi na baada ya uhuru akawa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai).

Nani leo hata hapo Maktaba ya CCM Dodoma anaeweza kukupa taarifa hizi.

Mimi nina sauti ya Ally Sykes akieleza haya katika tapes.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…