Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Mnabaduhe,
Umesema kweli lakini huwezi kuondoa ukweli kuwa Uislam ulitumika sana.

Mkutano wa Kura Tatu ulifanyika Parish Hall lakini hiyo ni 1958 TANU ina
nguvu kila mtu anaifata sasa kwani walijua uhuru uko njiani.

Uliza ilikuwaje kabla ya hapo nikuwekee historia nzima kama nilivyoieleza
katika kitabu cha Abdul Sykes.
 
Ha ha ha

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mzee Mohamed Said! Hao unaodai ni wazee wako! ni wazee wetu pia! Ni Wazalendo wa taifa hili! wewe sio wa Kwanza kuandika 'Oral History' Prof. Israel Katoke aliwahi kuandika The Karagwe Kingdom: A history of the Abanyambo of North Western Tanzania c.1400-1915 ! Haikuleta shida ndio maana mpaka leo,kitabu chake kinatumika University ! aliandika historia ya wazee wake pia( historia hiyo haijawahi kuwagawa watu) Ila Unachoaandika wewe kinahatari kubwa ya Kuwagawa watanzania kwa minajiri ya Udini.
Every Great Historian Knows that! Including You Sheikh Mohamed Said.
 
Shida ni kwamba, hao unaowaita wazee wako, utakuta ni ndugu zako katika dini.

Kama kivukoni walipotoka kwa kuandika uongo, ilikuwa ni busara kutambua wakichokifanya ili tuwe na kitu halisi.

Anyway, najaribu kutafakari mfumo wa:-

1. Thesis-kivukoni
2. Ant-thesis-Mohamed Said and the like
3. Synthesis-Perhaps Yerico Nyerere, Nguruv nk.

Tunahitaji wa kubalance story, isionekane historia ya uhuru ni one sided movement, wakati wamekufa wengi sana bila kujali itikadi zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnababuduhe,
Huko katika kuwagawa watu wala tusiende.
Nyakati hizi ni ngumu kidogo lakini soma kitabu cha Abdul Sykes.

Prof. Haroub Othman ndipo alipotaabika.
Hilo ulilogusia ni mojawapo ya yaliyomtaabisha.

Ndipo walipoamua kuwapa kazi Prof. Shivji na wataalamu wenzake
waje na kitabu kingine labda kinaweza kurekebisha historia niliyoandika
na ndiyo maana wakajakunihoji.


Kulia: Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Othman aliyekaa chini Mohamed Said

Huko kwa kuwagawa Watanzania wala tusiguse ndugu yangu.
Inaelekea wewe mgeni katika mambo haya.
 
Ntamaholo,
Historia ndivyo ilivyokuwa na hayo yote yalifanywa na watu hao.

Kuwa historia iliwasahau ndiyo maana nimeandika habari zao na
leo mko hapa mmetatazika sana.

Akili inakataa kuamini.
Hilo la kuweka mizani hakuna anaekuzuia.
 
Ha ha ha yaani dharau za kisukuma zipo dhahiri shahiri. Aksante Mayala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ntamaholo,
Mikutano ya kwanza ya TANU Sheikh Suleiman alikuwa anaomba dua
kisha ndiyo Nyerere anapanda jukwaani kuhutubia.

Huu ni katika utamaduni wa Waislam.
Wewe huwezi kuelewa haya.

Dua inafuta Qadar.
 
Soma kisha useme walioachwa ni akina nani na utupe historia yao ya Uhuru. Halafu pia ukiona watu wametajwa au kuwekwa ambao hawakustahili basi utupe historia yao mbadala.

Yanini unaandikia mate na wino upo?
Great woman wa JF Faiza

1. Thesis.
Tuseme tu kuwa ndo historia ya kwanza ya uhuru kuandikwa na watu wa kivukoni. Sijawahi kuiona hivyo sina cha kusema. Kama imepotoshwa, tunatarajia kuletwa story ambayo ni dhahiri. Lakini badala yake, tumeletewa habari ya kupinga kila kitu na kuletewa kitu kipya.

2. Antithesis. Badala ya kutuletea ukweli, sasa tunalazimishwa kuoneshwa kuwa ni waislam pekee waliohusika. Ni kama MH anakataa kila kitu cha kivukoni, analeta jambo jipya kabisa. Sasa hapa tutahitaji atakaye kuwa mkweli.

3. Synthesis-Tunahitaji mtu wa kutuunganisha sasa mara baada ya kivukoni kuharibu, mohamed naye akaharibu, sasa Nyerere labda atuunganishe.

Mi naamini hostoria ya tanganyika, siyo single sided movement, bali ni mult-side movement.

Kama Mohamed Said kila kitu anakibariki kwa dua ya kiislam, hata wapigania uhuru walibariki kwa dua za kiislam, kikristo na kijadi.

Kijadi ng'ombe na mbuzi zilikufa just kuwatakia heri wapigania uhuru.

Tunahitaji mtafiti wa kutuunganisha sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti, nani aliasisi kuandika katiba ya TANU?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paskali,
Soma kitabu cha Abdul Sykes.
Mengi hapo juu umeyakosea.

Nyerere hakushinda kwa kura nyingi na hapa napuuza lugha yako
isiyopendeza.

Msome Judith Listowel kaeleza uchaguzi ule kwa kirefu sana.
Dr. Kyaruzi nishaeleza mara nyingi historia yake hapa nk. nk.

Abdul aliingia TAA katika uongozi baada ya sakata la makuli.

Nimekuwekeeni historia yote labda hukuioma na kama umeisoma
unakaa kimya basi imekutisha kama ilivyomtisha John Iliffe.

AA iliasisiwa 1929.

Msome Kleist anaeleza kila kitu vipi aliasisi AA 1929 baada ya kukutana
na Dr. Aggrey 1924.

Cecil Matola hakukaa sana katika AA alifariki 1933 na President akawa
Mzee bin Sudi.

Lakini hii isitukwamishe mnaweza kuendelea kuamini hivyo hakuna shida.

Naona hii imekuumeni sana ya Kleist kuasisi AA na wanae TANU.
Inachoma kweli kweli.

Prof. Haroub Othman alitaka kupata wazimu kwa historia hii mji
mzima anapita anauliza nani huyu Abdulwahid Sykes?

Mwishowe akaenda kwa Nyerere.
Allah muweza.

Angalia hizi rejea ndani ya kitabu cha Sykes:

...written with the help of a paper by Aisha Daisy Sykes presented as seminar paper at the University of Dar es Salaam in 1968. Daisy wrote this paper with the assistance of her father Abdulwahid Sykes, from an original manuscript written by Kleist Sykes. Other information on Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika is from Tewa Said Tewa’s unpublished manuscript, ‘A Probe In the History of Islam in Tanganyika’. Other information is from Ali Mwinyi Tambwe, secretary Al Jamiatul Islamiyya in the early 1940s.

Daisy Sykes Buruku, ‘The Townsman: Kleist Sykes’, in Iliffe (ed) Modern Tanzanians, Nairobi, 1973, pp. 95-114.
 
Ungekuwa unaeleza hivi usingepingwa. Maana hapa ni zaidi ya wazee wako.

Kaswali kingine kalikoulizwa hujakajibu, ni kuwa, Historia ya babu zako, kwa nini hukumtafta na Nyerere na yeye akatoa yake na uzoefu wake?

Au yeye siyo mzee wako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Namba mbili si kweli.

Umekisoma kitabu cha Mohamed Said?

Hukumsoma humo Nyerere? Hukumsoma humo John Rupia? Hukumsoma Chief Kidaha Mwakaiah? Hukumsoma humo Dr Michael Lugazia, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, Patrick Aoko na wengi wengine? Hao nao ni Waislam?

Historia ya kivukoni imeshindwa kumuweka hata mtu aliyempokea na kumpa makazi na malazi Nyerere.

Hivi Nyerere alikuwa hana watu kule mission quarter?
 
Mzee wa dua ya kiislam pekee. Hajui kama na dua za Kristo zilihusika. Hataki kukiri hata dua za mizimu zilizohitaji damu ya mafahari wa mbuzi, kuku, kondoo na ng'ombe nazo zilikuwa sehem ya harakati.

Yeye na uislam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ntamaholo,
Majibu yote hayo ninayo na zaidi.

Kasome kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza tatizo lililomfika Abdul
katika mradi wa TANU wa kuandika historia yake mara tu baada
ya uhuru.

Jibu lake lipo hapo.
Lakini hebu kwanza ingia hapo chini:
Mohamed Said: KUTOKA JF: MAREHEMU HASSAN UPEKA (TANU INTELLIGENCE 1956) NA UANDISHI WA HISTORIA YA TANU
 
Ntamaholo,
Hili nilishalieleza.

Ile dua ya kwa Mzee Tambaza ilikuwa dua ya Kiislam na kule kuchinja
ni katika dua.

Dua yoyote nzito hufuatiliwa na kuchinja na nyama ikagawiwa sadaka.

Nyerere yeye hakuwa mweledi katika mila hizi za Kiislam ndipo aliposema
aliyosema.

Nikimjua vyema Mzee Tambaza na wanae na wajukuu zake hivi sasa.
Na nawajua kuwa dini wanaifahamu vizuri.

Hawawezi kuabudu mizimu.

Hawa wazee wengi wao walikuwa chini ya Sheikh Hassan bin Amir
aliyekuwa Mufti wa Tanganyika.
 
Ntamahalo kwani nani kakupingia hilo?
Mimi nimeeleza hizo dua nawe eleza wapi zilifanyika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…