Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mnabaduhe,Mzee Said Mohamed! wakati wa kupigania Uhuru wa Nchi hii hakuna Mtu aliyewaza kuhusu Imani yake na nafasi ya Imani yake katika kulikomboa taifa Hili! waislam,wakristo,wapagani,wahindu,wachawi walisimama pamoja kudai uhuru wa nchi hii.
Ungelijua UAMUZI WA BUSARA WA TABORA Ulifanyikia Wapi? usinge litaja abadani suala la Udini ulioung'ang'ania.
Umesema kweli lakini huwezi kuondoa ukweli kuwa Uislam ulitumika sana.
Mkutano wa Kura Tatu ulifanyika Parish Hall lakini hiyo ni 1958 TANU ina
nguvu kila mtu anaifata sasa kwani walijua uhuru uko njiani.
Uliza ilikuwaje kabla ya hapo nikuwekee historia nzima kama nilivyoieleza
katika kitabu cha Abdul Sykes.