Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Paskali,
Mimi sina tatizo na historia ambayo nyie mngependa iwe.

Aliyesema kaanzisha AA ni yeye mwenyewe Kleist na mswada wake umechapwa kitabu toka 1973.

Historia hii nimeeleza kama ilivyokuwa na wajuzi wameiafiki na leo ndiyo historia isomweshayo kote vyuoni na mwaka 2011 ikaingizwa katika Dictionary of African Biography.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio lisemwalo ndilo liwalo, bali liandikwalo ndilo!.
Asante kwa hadithi nzuri za simulizi za historia.

P.
 
Yericko,
Si lazima uamini ninachosema.

Tumeishi miaka mingi na historia ya Chuo Cha Kivukoni.

Si lazima ujibu maswali niliyokuuliza.
Kukaa kimya pia ni jibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Akae kimya ili ujichukulie wajinga wengi km wale wanaojiita wasomi ktk vyuo vya umma?Wamelisha watz ujinga miaka nenda rudi hadi watz sasa kufikiri hawawezi , ingawa wanapata shida kujua mbona wasomi wetu wana tuangusha kila mahali na visingizio bado haviishi?Walipiga sana kelele kuwa tafitii zao hasifanyiwi kazi, baadae wakasingizia wanahujumia na mataifa.Sasa hawajui waseme nini, zaidi kudai chuo chao kinatambulika.Ila ukiwauliza kinatambulika vitu, wanakuja juu. Hata wewe ,kuingiza vitabu library kihuni kupitia mitandao yenu ya kiharakati na madai ya kugombea uhuru,umeshafikia kutumia km ushahidi wa ubora, ukweli wa ulichoandika.
 
Mzee wetu anazeeka na imani yake kuwa Tanu ni Wasauzi
Mzee ni mhanga wa uongo, hawa ndio assets za CCM .CCM ni wahanga wa uongo wao kuliko wapinzani.Kwao anayeongea anatosha kumfanya msomi aamini hiyo habari kuliko kuamini akili yake hata km taarifa anayoisoma mkononi ile ile anayoelezwa ila kwa upotofu. Huyu mzee anashikwa mara nyingi sana off-guard km wabunge wa ccm, viongozi wao. most of the time watu waliokuwa wakiumbuka km Mkama ktk msiba wa Bob Makani.Si kwamba walikuwa wanadanganya tena makusudi ila walishaamini uongo kiasi cha kufanya wasiwe na uwezo tena wa kuwa na tahadhari ya kujua ni uongo na usingefaa pale. Hiyo ni phenomenon inayotokea kwa binadamu kuathirika na mazingira. Huwa ni mbaya zaidi ,huyo mtu akiwa na vitu fulani vinavyomfanya kuwa too biased kwa kiasi cha kupoteza uaminifu pale jambo lipo upande tofauti na mapenzi yake.
 
Mzee unaua saja jamii unayodhani unaipigania.Kuwapa fikra mbaya ni kuwazuia kuingia karne mpya kwa ushindani.Mtaishia kupambana kuzuia sababu ya kifo cha marehemu, badala ya kuzuia maambukizi yanayowarudisha makaburini kila siku. Wewe unadhani kuwa na babu yako kunakufanya uwe msomi au uwe mkweli kiasi cha kuweza sema kweli n akweli tuu?Especially kwa mtu asiey na uwezo wa kujua kamba za babu kwa mjukuu na pia uwezo wa wewe na babu yako kujua kweli na uaminifu wa kuisema kweli.Kumbuka kukosa uaminifu kwa zaidi ya mtu mmoja kuna effects kubwa sana ktk kupitisha historia. Zinabadili kweli kuwa hadithi ya kutunga.

Hivi mzee ktk jamii yako nani ataaminika akielezea habari ya ghaddafi ,na akielezea habari ya Israel?Watoto wenu watabaki kuwa victims.Na hiyo mentality ita wablock sana kupata mema ya nchi kwa vile siku zote hawataona pale wanaodhani kuwa maadui kuwa wamekuja waokoa.
 
Wana Majlis,
Hivi mnajua kuwa Mwalimu Nyerere ameandika kuhusu AA na hakupingana na yale aliyoandika Kleist Sykes?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio lisemwalo ndilo liwalo, bali liandikwalo ndilo!.
Asante kwa hadithi nzuri za simulizi za historia.

P.
Paskali,
''Mapema asubuhi moja kile kilichoanza kama mipango ya siri dhidi ya makampuni ya Wazungu bandarini, kililipuka na kuwa mapambano ya dhahiri. Watu katika mitaa jirani ya alipoishi akikaa Abdulwahid walikuwa hawajatoka vitandani mwao alifanjiri moja waliposikia vishindo na makelele vimetanda mtaani. Makuli, baadhi yao wakiwa vidari wazi, walikuwa wameizingira nyumba ya Kleist, wakipiga makelele wakimtaka Abdulwahid atoke nje. Makuli wale walipiga kwata njia nzima kutoka bandarini huku wakitoa maneno ya kupinga ukoloni na wakiimba kupandisha morali zao. Tukio hili halikuwa na kifani. Ilikuwa ni mara ya kwanza nchini Tanganyika kwa wananchi kushuhudia katika mitaa ya Dar es Salaam uasi wa dhahiri kama huo dhidi ya serikali ya kikoloni. Abdulwahid, wakati ule kijana mdogo kabisa, akichungulia kupitia dirisha la chumba chake alichokuwa amelala, alishangazwa kuona umati mkubwa wa watu nje ya nyumba yao. Aliweza kuwatambua baadhi ya wenzake katika kamati ile ya siri iliyokuwa inapanga mipango ya mgomo. Alipotoka nje kuonana nao makuli wenye hasira walimfahamisha kuwa mgomo ulikuwa umeanza na wasingerudi kazini hadi madai yao yote yamekubaliwa.

Mgomo huo ulioenea kama moto wa makumbi ulikumba nchi nzima kwa kasi ya ajabu. Ilikuwa kama vile wafanyakazi wa nchi nzima wametaarifiana. Wafanyakazi wa Tanganyika Railways huko Tabora wakiongozwa na Salum Abdallah Popo waliingia kwenye mgomo tarehe 11 Septemba, 1947. Chama cha African Association mjini Tabora kilimteua Mwalimu Pinda, aliyekuwa akifundisha shule ya St Mary, kuwa 'mshauri' wa wafanyakazi waliogoma. Asubuhi ya siku ya mgomo wafanyakazi wa Tanganyika Railways walikusanyika kwenye kiwanja cha mpira chaTown School, wakakaa chini ya miembe kujikinga jua. Tabora ni maarufu kwa miti hiyo. Tangu siku hiyo kiwanja hiki kikawa ndicho uwanja maalum kwa mikutano yote ya siasa.''

Historia hii imeandikwa kwanza na John Iliffe: ‘'A History of Dockworkers of
Dar es Salaam,'’ TNR, Dar es Salaam, 71, 1970,'' mimi sikuridhika na maelezo
yake nikafanya utafiti wangu kwa kumhoji Islam Barakat aliyekuwa Labour
Inspector wa kwanza Mwafrika aliyeshuhudia kwa macho yake haya yote.

Niliongeza mengi katika kitabu cha Abdul Sykes ambayo Iliffe yalimpita.
 
Lipi jipya kwenye hii copy na paste yako?

Inaitwa plagiarism.

 
Wana Majlis,
Hivi mnajua kuwa Mwalimu Nyerere ameandika kuhusu AA na hakupingana na yale aliyoandika Kleist Sykes?

Sent using Jamii Forums mobile app
Paskali,
''The Tanganyika African National Union is, in one sense, a new organisation, but in another it is an old organisation. It was taken over from what was formerly called the Tanganyika African Association, which was founded in 1929, largely as a social organisation. The Tanganyika African National Union, which took over from the African Association about ten months ago, is a new organisation in the sense that it is a political organisation, where as the former was semi-political.''

[6] Julius K. Nyerere, Tanganyika African Association, to Governor Edward Twining, 10 th August, 1953. Sykes' Papers.
 
Haya mambo haya, ni balaa, Huyo Mohamed Said naye ni wakuja tu, wametoka Congo wakaishia Musoma, kisha wakaja Mzizima, naye ni wakuja tu, so hiyo history anayoandika ni story ya wazee wake wahamiaji sio wana Mzizima
Hivi ulikuwa huelewi kuwa Dar ni multi ethnic city toka enzi na enzi?

Laiti ungelielewa maana ya Dar Es Salaam usingekurupuka.
 
Hivi ulikuwa huelewi kuwa Dar ni multi ethnic city toka enzi na enzi?

Laiti ungelielewa maana ya Dar Es Salaam usingekurupuka.
haikuwa multi ethnic city mpaka pale wahamiaji kutoka Congo, Sudan kidogo na group dogo la Wayao, Wanyasa na wazulu na wala sio muda mrefu unaosema enzi na enzi
 
haikuwa multi ethnic city mpaka pale wahamiaji kutoka Congo, Sudan kidogo na group dogo la Wayao, Wanyasa na wazulu na wala sio muda mrefu unaosema enzi na enzi
Hatakuelewa, atakupinga daima, hajui ni juzi tu mjerumani akahamisha makao toka Bagamoyo na kuleta Mzimzima....
 
Kosa kubwa unalolifanya tangu miaka yote ya ubishi wetu hapa, nikuwa rejea zinatoka chanzo kimoja tu kiitwacho Sykes to Sykes.... Chanzo chenye maumivi na chenye kifua kikali chenye hasira na Julius Nyerere
 
haikuwa multi ethnic city mpaka pale wahamiaji kutoka Congo, Sudan kidogo na group dogo la Wayao, Wanyasa na wazulu na wala sio muda mrefu unaosema enzi na enzi
Nimekusomesha juu hapo lakini somo halijakuingia. Kaisome tena post uliyoijibu.
 
Kosa kubwa unalolifanya tangu miaka yote ya ubishi wetu hapa, nikuwa rejea zinatoka chanzo kimoja tu kiitwacho Sykes to Sykes.... Chanzo chenye maumivi na chenye kifua kikali chenye hasira na Julius Nyerere
Yericko,
Kleist Sykes (1894 - 1947) ndiyo aliyeandika maisha yake na mswada ukatufikia na ukachapwa kitabu.

Nyaraka nyingine ni nyaraka kama nyaraka zilivyo na hakuna katika nyaraka zilizoko katika kitabu changu zilichomtaja Baba wa Taifa kwa ubaya.

Pitia notes zote kwenye kitabu na onyesha iliyokuwa na taarifa mbaya kwa Mwalimu Nyerere.

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Watu wengine wanasoma au wanasikiliza bila kujua kuna kitu kinaitwa critical thinking

Kuna hoja mbili kuhusu hili

1.Mohamed ameondoa ushiriki wa watu makusuadi katika historia anayosema ni ya Tanganyika, ingawa mambo yakibana husema ya wazee wake na ikiwa ngumu zaidi husema ya Waislam

Kosa ambalo Kivukoni walifanya kwa kutotambua michango mingine, kwake lina uhalali

2. Historia ina formula, kuieleza au kuiandika kwa mujibu wa matukio na wakati kama ilivyo
Jaribio la ku ''interject'' personal feelings or ideas, historia husota madole ya machoni dhahir shahir

Kwa waliosikiliza video, Mohamed anasema Kleist Sykes aliunda AA na kisha Jamii fil Islamiya 1933. Mohamed hakueleza chochote kuhusu Cecil Matola.

Kumtaja Cecil ni kumtaja Rais wa kwanza na hivyo hoja ya Kleist kuunda AA inakufa.
Katika maandishia anasema, Kleist aliunda kwasababu alikuwa na pesa na mashuhuri.

Mohamed haelezi Cecil Matola alikuwa msomi na 'immunity' dhidi ya Wakoloni kuliko Kleist
Tendo la kutomtaja Matola, historia haikukaa kimya imemnyooshea kidole

3. Mohamed anasema Abdul Aliunda TANU, Nyerere akiwa Rais wa TAA kabla ya 1954.

Kitendo cha kumuondoa Nyerere, historia inamzaba kibao Mohamed.
Huwezi kuwa Rais wa chama asiyejua transformation. Abdul hakuunda TANU, alishiriki

1929 cecil akiunda AA hadi uchaguzi katika miaka ya 1950 Abdul ni takribani miaka 23.
Kleist na Mwanawe Abdul walibaki na uana harakati kwa miaka 23.

Nyerere aliandika katiba ya TANU katika transformation ya chama kuwa ya kisiasa
Akafungua milango UN kwa kutumia usomi, na kupata Uhuru katika miaka 10

Mohamed hasemi hilo, lakini historia inamsuata bila mtu kuandika kitabu kingine

Miaka 23 Kleist na mwanae Abdul Sykes hawakuwa na wazo la kuandika katiba
Wazo amekuja nalo Nyerere. Ndio maana Mohamed hajibu hoja za nani aliandika katiba
Hataki kumsikia Nyerere mtu anayemchukia sana katika dunia hii

Mohamed anasema hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na kamati ya watu watano.
Katika hao Mohamed hamtaji Nyerere aki back date kuandikwa kwake.

Historia inamshataki Mohamed, kama hotuba iliandikwa kabla ya Nyerere ni nani aliyetarajiwa kwenda UN?

Historia inasema kama kamati iliandika hotuba, kulikuwa na tatizo gani ikiwa lilikuwa suala la chama?
Kuna shida gani chama kuandika hotuba kubwa kama ya UN na kumkabidhi mhusika!

Mohamed anaingiza hoja kuonyesha Nyerere alisoma tu bila kujua maudhui ili kumdhalilisha.

Historia inamtetea Nyerere. Wakati hotuba inaandikwa yeye ni mmoja wa watu wachache sana waliokuwa na degree katika kiwango cha Master. Alishakuwa exposed katik siasa za dunia

Mohamed anaweza kumdhalilisha Nyerere atakavyo, wanaosoma kwa critical thinking watakuwa na rafiki yao mmoja anayeitwa Historia atakayewasaidia kuchambua chuki na ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…