Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Asante kwa hadithi nyingine nzuri na tamu ya Salum Abdallah Popo, ila
kama umesema urongo kuwa Sykes alianzisha AA wakati sii kweli, mwanzilishi wa AA ni Cecil Matola, mwaka 1927, Sykes alikaimu urais mwaka 1933 baada ya Matola kufariki.

Kisha ukasema urongo Sykes alianzisha TAA, wakati mwanzilishi wa kweli wa TAA ni Dr. Vedastus Kyaruzi.
Urongo huo kama hautoshi, ukasema urongo mwingine kuwa Sykes alianzisha TANU, wakati mwanzilishi wa TANU ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ukasema urongo mwingi kuhusu babu zako na harakati za uhuru, wakati ukweli halisi shujaa wa uhuru na mkombozi wa taifa hili dhidi ya wakoloni ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pekee!.

Hivyo hii taarifa yako kuwa babu yako yeye ndiye aliyeongoza mgomo wa kwanza wa Tanganyika mwaka 1947 dhidi ya Waingereza katika majimbo ya kati ya Tanganyika needs collaboration, vinginevyo pia inaweza kuwa ni urongo, sio urongo uliotunga weye bali ni urongo wa aliyekusimulia hadithi ya urongo.

Kama babu yako alikuwa mmoja wa wazalendo wa kwanza wakati wa ukoloni kuanzisha harakati za vyama vya wafanyakazi, this also needs collaboration, tulivyofunzwa sisi, waanzilishi wa harakati za migomo ya wafanyakazi ni kina Michael Kamaliza na Rishidi Kawawa .

Hili la kusema kuwa alikuwa kati ya watu wa mwanzo kuiunga mkono Tanganyika African National Union (TANU), chama cha kizalendo kilichopigania na kunyakua uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1961 bila kumtaja shujaa pekee wa TANU na uhuru wa Tanganyika ni omission!, some omissions za makusudi nazo pia ni urongo!.

Bahati mbaya sana sisi wengine hatukujaliwa kipaji cha kusimulia hadithi za wazee wetu tulizo simuliwa, ila hata mimi Mzee wangu, Andrew Mayalla ni miongoni wa Watanganyika walioongoza vikosi vya polisi kwenye parade ya uhuru na mama yangu alifanya kazi bomani, picha zipo, hivyo mimi na wewe kwa kiasi fulani tunafana, ni watoto wa wapigania uhuru, ila mimi sina urongo wowote kuhusu wazee wangu.

Urongo unafuata kanuni ya samaki kwenye tenga la samaki, samaki mmoja akioza... hivyo hata kama kuna ukweli wa asilimia 99% katika simulizi zako, urongo wa asilimia 01% unatosha kabisa kuharibu tenga la samaki wote, ila kitu kizuri, hadithi zako kwanza ni tamu, pili ni elimishi, hivyo licha ya urongo na zile sumu ndani ya simulizi zako, so far you are the best story teller humu jf, in fact you are an orator na narrator!.

Thanks, keep it up, ninakusoma sana na enda ikawa one day nikawa mwanafunzi wako kwenye oratorio skills.

Paskali
Paskali,
Mimi sina tatizo na historia ambayo nyie mngependa iwe.

Aliyesema kaanzisha AA ni yeye mwenyewe Kleist na mswada wake umechapwa kitabu toka 1973.

Historia hii nimeeleza kama ilivyokuwa na wajuzi wameiafiki na leo ndiyo historia isomweshayo kote vyuoni na mwaka 2011 ikaingizwa katika Dictionary of African Biography.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paskali,
Mimi sina tatizo na historia ambayo nyie mngependa iwe.

Aliyesema kaanzisha AA ni yeye mwenyewe Kleist na mswada wake umechapwa kitabu toka 1973.

Historia hii nimeeleza kama ilivyokuwa na wajuzi wameiafiki na leo ndiyo historia isomweshayo kote vyuoni na mwaka 2011 ikaingizwa katika Dictionary of African Biography.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio lisemwalo ndilo liwalo, bali liandikwalo ndilo!.
Asante kwa hadithi nzuri za simulizi za historia.

P.
 
Yericko,
Si lazima uamini ninachosema.

Tumeishi miaka mingi na historia ya Chuo Cha Kivukoni.

Si lazima ujibu maswali niliyokuuliza.
Kukaa kimya pia ni jibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Akae kimya ili ujichukulie wajinga wengi km wale wanaojiita wasomi ktk vyuo vya umma?Wamelisha watz ujinga miaka nenda rudi hadi watz sasa kufikiri hawawezi , ingawa wanapata shida kujua mbona wasomi wetu wana tuangusha kila mahali na visingizio bado haviishi?Walipiga sana kelele kuwa tafitii zao hasifanyiwi kazi, baadae wakasingizia wanahujumia na mataifa.Sasa hawajui waseme nini, zaidi kudai chuo chao kinatambulika.Ila ukiwauliza kinatambulika vitu, wanakuja juu. Hata wewe ,kuingiza vitabu library kihuni kupitia mitandao yenu ya kiharakati na madai ya kugombea uhuru,umeshafikia kutumia km ushahidi wa ubora, ukweli wa ulichoandika.
 
Mzee wetu anazeeka na imani yake kuwa Tanu ni Wasauzi
Mzee ni mhanga wa uongo, hawa ndio assets za CCM .CCM ni wahanga wa uongo wao kuliko wapinzani.Kwao anayeongea anatosha kumfanya msomi aamini hiyo habari kuliko kuamini akili yake hata km taarifa anayoisoma mkononi ile ile anayoelezwa ila kwa upotofu. Huyu mzee anashikwa mara nyingi sana off-guard km wabunge wa ccm, viongozi wao. most of the time watu waliokuwa wakiumbuka km Mkama ktk msiba wa Bob Makani.Si kwamba walikuwa wanadanganya tena makusudi ila walishaamini uongo kiasi cha kufanya wasiwe na uwezo tena wa kuwa na tahadhari ya kujua ni uongo na usingefaa pale. Hiyo ni phenomenon inayotokea kwa binadamu kuathirika na mazingira. Huwa ni mbaya zaidi ,huyo mtu akiwa na vitu fulani vinavyomfanya kuwa too biased kwa kiasi cha kupoteza uaminifu pale jambo lipo upande tofauti na mapenzi yake.
 
Paskali,
Hii si hadithi hii ndiyo kweli yenyewe.

Kwa mara ya kwanza iliwashtua wengi waliochukuliwa na historia mfano
wa Chuo Cha Kivukoni.

Mmoja katika wale wenye akili zilizopea aliamua kuzungumza na mimi.
Kwanza alitaka kujua historia yangu.

Nikamweleza historia ya babu yangu katika harakati za kupambana na
ukoloni:

''(Babu yangu) Salum Abdallah Popo alikuwa muasisi wa harakati za vyama vya wafanyakazi na alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kuanzisha upinzani na kuunga mkono juhudi za kuupinga utawala wa kikoloni. Mwaka 1947 aliongoza mgomo wa kwanza Tanganyika wa wafanyakazi wa Tanganyika Railways katika majimbo ya kati ya nchi. Tanganyika ilipopata uhuru wake mwaka 1961 Salum Abdallah Popo aliachana mkono na Nyerere kama wengi walivyofanya na aliwekwa kizuizini na serikali chini ya sheria ya Preventive Detention Act of 1962 kwa ajili ya msimamo wake wa kuamini kuwa vyama vya wafanyakazi viwe huru. Akiwa mwenyekiti wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) alipinga vyama vya wafanyakazi kuwekwa chini ya Tanganyika African National Union (TANU) chini ya Rais Julius Nyerere.''

Paskali
Huyu ni babu yangu na alikuwapo toka siku ya kwanza TANU inaundwa
na ni mmoja kati ya wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora.

Salum Abdallah si ''character,'' katika kitabu cha hadithi.

''Halikadhalika natoa shukurani kwa marehemu Rashid Mussa ambae katika mazungumzo yetu, yeye bila kufahamu kuwa mimi ni mjukuu wa Salum Abdallah Popo alinieleza habari za babu yangu wakati anaanza siasa na jinsi alivyoongoza mgomo wa kwanza wa Tanganyika nzima pale Tabora mwaka 1947...

Ingawa vitabu vya historia havimtaji, lakini babu yangu yeye ndiye aliyeongoza mgomo wa kwanza wa Tanganyika mwaka 1947 dhidi ya Waingereza katika majimbo ya kati ya Tanganyika. Babu yangu alikuwa mmoja wa wazalendo wa kwanza wakati wa ukoloni kuanzisha harakati za vyama vya wafanyakazi. Vilevile alikuwa kati ya watu wa mwanzo kuiunga mkono Tanganyika African National Union (TANU), chama cha kizalendo kilichopigania na kunyakua uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1961...

TAA ilipofanya mkutano wa siri katika shule moja pale Tabora ili kuchangisha fedha kumwezesha katibu wa TAA Jimbo la Magharibi Germano Pacha kusafiri Dar es Salaam kuhudhuria mkutano mkuu wa kuanzishwa TANU Julai mwaka 1954 mchango, mkubwa kupita yote ilikuwa shilingi ishirini. Fedha hizi alitoa babu yangu. Mkutano huu ulihudhuriwa na watu maarufu wa Tabora pamoja na baadhi ya waalimu kama Abubakar Mwilima, Harub Said na George Magembe. Hawa walikuja kuwa watu muhimu sana wakati wa harakati za kudai uhuru. Hata hivyo, babu yangu alitupana mkono na Julius Nyerere kama wengi walivyofanya, na alitiwa kizuizini na serikali mara baada ya uhuru chini ya Preventive Detention Act ya mwaka 1962...

Babu yangu Salum Abdallah na Kleist Sykes walikuwa majirani katika miaka ya 1930 nyumba zao zikitazamana katika Mtaa wa Kipata (sasa Kleist Sykes), na wote wakiwa wameajiriwa na Tanganyika Railways. Babu yangu akifanya kazi katika karakana ya kuyeyusha chuma. Lango kuu la kuingia loko shedi kama sehemu hiyo ilivyokuwa ikijulikana ilikuwa limeelekea katika mtaa ambao sasa unajulikana kama Mtaa wa Nkrumah. Hii ndiyo ilikuwa karana kuu ambayo treni na mabehewa yake yalikuwa yakifanyiwa matengenezo na vipuli kutengenezwa hapo. Kazi yake ilikuwa ngumu inayohitaji kufanyika katika hali ya joto la juu kabisa kutoka katika moto ambao ulihitajika ili kukunja chuma kwa moto mkali. Hii ilikuwa kazi ngumu iliyohitaji nguvu na afya nzuri, kazi hasa iliyomfaa babu yangu kwa tambo lake kubwa la Kimanyema. Kleist alikuwa amesoma katika shule ya Wajerumani. Kwa ajili hii basi alikuwa na kazi isiyokuwa na sulubu, wakati ule akiajiriwa kama karani wa mahesabu. Kleist na Salum Abdallah, baba yangu alinifahamisha, hawakuwa kwa hakika watu waliopendana sana. Wazulu wanafahamika kwa sifa ya shari kama walivyo Wamanyema. Lakini watoto wa Kleist na Salum Abdallah Popo, walikuja kujenga urafiki ambao ulidumu miaka mingi.

Wakati nakua, nilikuja kujua kuhusu watu hawa na mambo yaliyotokea Dar es Salaam hata kabla sijazaliwa mwaka wa 1952. Baba yangu, ndugu zake na watu wengine wa Dar es Salaam walikuwa ndiyo walikuwa walimu wangu kwa yote niliyojifunza kuhusu mji wenyewe na historia yake...''

Paskali,
Hii ndiyo ilikuwa, ''credential,'' yangu kwa huyu msomi.
Historia yangu ilimdhihirishia kuwa najua ninachoandika.

Sikulazimishi kuamini historia hii.

Tumeishi kwa miaka mingi sana na historia ya Chuo Cha Kivukoni na
hakuna aliyedhurika kwa kuamini historia ile.

Hayo yote niliyoweka hapo juu nimetoa katika kitabu cha Abdul Sykes.
Mzee unaua saja jamii unayodhani unaipigania.Kuwapa fikra mbaya ni kuwazuia kuingia karne mpya kwa ushindani.Mtaishia kupambana kuzuia sababu ya kifo cha marehemu, badala ya kuzuia maambukizi yanayowarudisha makaburini kila siku. Wewe unadhani kuwa na babu yako kunakufanya uwe msomi au uwe mkweli kiasi cha kuweza sema kweli n akweli tuu?Especially kwa mtu asiey na uwezo wa kujua kamba za babu kwa mjukuu na pia uwezo wa wewe na babu yako kujua kweli na uaminifu wa kuisema kweli.Kumbuka kukosa uaminifu kwa zaidi ya mtu mmoja kuna effects kubwa sana ktk kupitisha historia. Zinabadili kweli kuwa hadithi ya kutunga.

Hivi mzee ktk jamii yako nani ataaminika akielezea habari ya ghaddafi ,na akielezea habari ya Israel?Watoto wenu watabaki kuwa victims.Na hiyo mentality ita wablock sana kupata mema ya nchi kwa vile siku zote hawataona pale wanaodhani kuwa maadui kuwa wamekuja waokoa.
 
Mzee unaua saja jamii unayodhani unaipigania.Kuwapa fikra mbaya ni kuwazuia kuingia karne mpya kwa ushindani.Mtaishia kupambana kuzuia sababu ya kifo cha marehemu, badala ya kuzuia maambukizi yanayowarudisha makaburini kila siku. Wewe unadhani kuwa na babu yako kunakufanya uwe msomi au uwe mkweli kiasi cha kuweza sema kweli n akweli tuu?Especially kwa mtu asiey na uwezo wa kujua kamba za babu kwa mjukuu na pia uwezo wa wewe na babu yako kujua kweli na uaminifu wa kuisema kweli.Kumbuka kukosa uaminifu kwa zaidi ya mtu mmoja kuna effects kubwa sana ktk kupitisha historia. Zinabadili kweli kuwa hadithi ya kutunga.

Hivi mzee ktk jamii yako nani ataaminika akielezea habari ya ghaddafi ,na akielezea habari ya Israel?Watoto wenu watabaki kuwa victims.Na hiyo mentality ita wablock sana kupata mema ya nchi kwa vile siku zote hawataona pale wanaodhani kuwa maadui kuwa wamekuja waokoa.
Wana Majlis,
Hivi mnajua kuwa Mwalimu Nyerere ameandika kuhusu AA na hakupingana na yale aliyoandika Kleist Sykes?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio lisemwalo ndilo liwalo, bali liandikwalo ndilo!.
Asante kwa hadithi nzuri za simulizi za historia.

P.
Paskali,
''Mapema asubuhi moja kile kilichoanza kama mipango ya siri dhidi ya makampuni ya Wazungu bandarini, kililipuka na kuwa mapambano ya dhahiri. Watu katika mitaa jirani ya alipoishi akikaa Abdulwahid walikuwa hawajatoka vitandani mwao alifanjiri moja waliposikia vishindo na makelele vimetanda mtaani. Makuli, baadhi yao wakiwa vidari wazi, walikuwa wameizingira nyumba ya Kleist, wakipiga makelele wakimtaka Abdulwahid atoke nje. Makuli wale walipiga kwata njia nzima kutoka bandarini huku wakitoa maneno ya kupinga ukoloni na wakiimba kupandisha morali zao. Tukio hili halikuwa na kifani. Ilikuwa ni mara ya kwanza nchini Tanganyika kwa wananchi kushuhudia katika mitaa ya Dar es Salaam uasi wa dhahiri kama huo dhidi ya serikali ya kikoloni. Abdulwahid, wakati ule kijana mdogo kabisa, akichungulia kupitia dirisha la chumba chake alichokuwa amelala, alishangazwa kuona umati mkubwa wa watu nje ya nyumba yao. Aliweza kuwatambua baadhi ya wenzake katika kamati ile ya siri iliyokuwa inapanga mipango ya mgomo. Alipotoka nje kuonana nao makuli wenye hasira walimfahamisha kuwa mgomo ulikuwa umeanza na wasingerudi kazini hadi madai yao yote yamekubaliwa.

Mgomo huo ulioenea kama moto wa makumbi ulikumba nchi nzima kwa kasi ya ajabu. Ilikuwa kama vile wafanyakazi wa nchi nzima wametaarifiana. Wafanyakazi wa Tanganyika Railways huko Tabora wakiongozwa na Salum Abdallah Popo waliingia kwenye mgomo tarehe 11 Septemba, 1947. Chama cha African Association mjini Tabora kilimteua Mwalimu Pinda, aliyekuwa akifundisha shule ya St Mary, kuwa 'mshauri' wa wafanyakazi waliogoma. Asubuhi ya siku ya mgomo wafanyakazi wa Tanganyika Railways walikusanyika kwenye kiwanja cha mpira chaTown School, wakakaa chini ya miembe kujikinga jua. Tabora ni maarufu kwa miti hiyo. Tangu siku hiyo kiwanja hiki kikawa ndicho uwanja maalum kwa mikutano yote ya siasa.''

Historia hii imeandikwa kwanza na John Iliffe: ‘'A History of Dockworkers of
Dar es Salaam,'’ TNR, Dar es Salaam, 71, 1970,'' mimi sikuridhika na maelezo
yake nikafanya utafiti wangu kwa kumhoji Islam Barakat aliyekuwa Labour
Inspector wa kwanza Mwafrika aliyeshuhudia kwa macho yake haya yote.

Niliongeza mengi katika kitabu cha Abdul Sykes ambayo Iliffe yalimpita.
 
Lipi jipya kwenye hii copy na paste yako?

Inaitwa plagiarism.

Mzee Mohamed

Wewe ni muongo sana, Nyerere ndie alikuwa rais wa TANU akiwa na uzoefu wa kimataifa akifahamiana na waingereza wengi na akiwemo John,

Nyerere ndie aliyeratibu na kuuleta ugeni huo Tanganyika, leo unasema alikuwa kijijini Mwitongo???

Aisee wewe ni muongo sijawahi kuona mzee wangu....

Hebu tujikumbushe hapa yaliyomo kwenye kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

_________________________________________________

Mwl. Julius Kambarage Nyerere, alipendwa na kuheshimika sana ndani na nje ya nchi. Mwaka 1985, aliamua kwa hiari yake mwenyewe, kuacha uongozi wa Taifa ili apumzike. Alizunguka nchi nzima kuwaaga Watanzania. Kwa mapenzi makubwa, wakampa zawadi za kila aina. Wananchi walionesha wazi huzuni waliyokuwanayo kwa uamuzi aliouchukua. Walimuaga wakilia machozi!
Kumbukumbu muhimu ni hutuba yake, ya kuwaaga Watanzania, ya ter. 5 Novemba, mwaka 1985, kabla hajastaafu Urais aliyoitoa mbele ya wazee wa Dar es Salaam:
Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam, na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana, mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza, Oktoba 1952, miaka thelathini na mitatu (33) nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi (ushee). Niliporudi, nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini, nikiwa shuleni Chuo Kikuu nilijua. Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ya siasa. Niliamua hivyo. Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda na kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.
Niliporejea nchini, hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari, nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi, anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Alishaniambia habari hizo, tangu nikiwa Makerere, Chuo Kikuu, nikiwa mwanafunzi.
Pale (Makerere), mimi na wanafunzi wenzangu tulianzisha chama kinachoitwa, Tanganyika African Welfare Association (TAWA), cha wanafunzi wa Tanganyika, mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.
Tukaona kwa nini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na si Tanganyika nzima? Kwa hiyo, nikawaandikia baadhi ya watu, Tanganyika. Nikasema, jamani eeh, tumeanzisha chama, kwa nini msianzishe huko matawi ya chama hicho?
Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia (nikiwa Makerere), akasema: “Wewe, kwa nini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).”
Kwa hiyo, la maana si kuanzisha matawi, maana Chama kipo na matawi yameenea. La maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.
Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo, mimi nikawa katibu wa katawi la TAA, hapo Makerere. Niliporudi Tabora, na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora. Kwa hiyo, nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo. Nilipelekwa na Kasela Bantu, ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.
Wakati huo, mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo, Anautouglou. Kwenye mkutano huu, wakanichagua kuwa Rais wao, wa TAA. Ninasema yote haya, kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo, Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana―cha matatizo.
Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana―katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.
Baada ya miezi kumi na mitatu (13), hapo mwaka 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani (Vita Kuu ya Pili ya Dunia) huko Burma. Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu, nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa miguu, kila Jumamosi. Baadaye, wazee wakanipa baiskeli, nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu, kufanya mikutano.
Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz, (na wengine wengi) waliokuwa ni wazee.
Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: “Wazee na Ndugu zangu!” Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU. Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa. Hawakuyumba hata kidogo. Vijana walikuwa na mashaka. Wengine walikuwa na vikazi vyao, waliogopa kuvipoteza. Nalo jambo lenyewe ni la hatari, la kuzungumzia uhuru! Unaweza ukakosa kazi, na wapo waliopoteza kazi. Wengine wakaacha kazi. Akina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.
Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.
Nilikwenda Songea mwaka 1955, mara baada ya kujiuzulu. Huko, wazee walinipokea na kunielewa. Nilianza safari za kuitembelea Tanganyika nzima. Nilikwenda Mbeya. Mkutano wangu, niliufanya na wazee kikundi kidogo cha wazee, ndani ya nyumba ya mtu.
Kwa mkutano huu wa Mbeya, wazee wakauliza: Unatafuta nini? Nikawaambia natafuta uhuru. Wale wazee, kwa sababu ya Vita vya Maji Maji, na wanakumbuka, kabisa. Wakaona, mimi ninatafuta jambo la hatari. Tulifanya mkutano wa makini kweli. Wakauliza: Wewe unawezaje kuleta uhuru? Wewe una njia gani kudai uhuru na usitiwe kitanzi na Waingereza? Tulielezana. Nikawaambia ninyi wazee, Waingereza wanawadanganya. Waingereza wametumwa na ule Umoja wa Mataifa, uliokufa (League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari, watuachie tujitawale. Waingereza wanafanya ujanja, hawasemi. Vita vimekwisha (vya Pili) na Umoja wa Mataifa mwingine, mpya (United Nations Organisation UNO), umewakabidhi Tanganyika kwa shabaha ileile. Sisi siyo koloni lao. Wamepewa dhamana tu.
Kwa hiyo, nikawaambia wazee, hakuna haja ya kumwaga damu. Tuwaseme tu! Tuwashitaki kwa waliowaleta hapa kwamba hawafanyi kazi yao, wamesahau kabisa!
Wazee wakauliza: “Eeh, inawezekana?” Nikasema, inawezekana. Kazi yetu ya kwanza, ilikuwa kuwaambia watu kwamba uwezekano wa kujitawala upo. Hilo lilikuwa la kwanza. Wazee walijua maana ya kujitawala. Walitamani kujitawala, lakini hawakujua waanzie wapi. Vijana hawakuwa na habari kwamba kujitawala kunawezekana. Kwa hiyo, kwa wazee sikuwa na matatizo. Wao hawakuwa na kazi, hawakumwogopa Mwingereza. Hawakuogopa kufukuzwa kazi. Baadhi walikuwa wafanyabiashara.
Mzee John Rupia (marehemu), alikuwa mfanyabiashara na kaidi kidogo. Aliwahi kutishwa na kunyang’anywa leseni yake ya biashara. Akaambiwa akiendelea kushirikiana na kijana mwenda wazimu (Julius Nyerere), atanyang’anywa leseni moja kwa moja. Rupia aliwajibu: “Potelea mbali!”. Nasema yote haya ikiwa njia ya kutoa shukrani kwa wazee na imani yao kwa vijana wakati huo.
Imani hujenga imani. Na mambo haya makubwa ya nchi, kama hayana baraka za wazee hayaendi. Magumu sana. Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani. Tangu awali kabisa.
Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: “Leo wazee wanakutaka.” Wapi? “Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku.” Nikasema, haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo(u), wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza. Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilizomalizika, zilikuwa za Kurani. Sasa, zikaja dua za wazee, za jadi. Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku naambiwa, “Twining (Twainingi) umekwisha!” (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: “Tambuka!” Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: “Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!”
Sasa mimi Mkristo(u), hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini, tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo, nilitambuka pale na kuambiwa: “Nenda nyumbani salama. Twaining hawezi tena!” Wazee wangu wengine, wanakumbuka. Tulikuwa tunakwenda Bagamoyo (kwenye makaburi). Kwenye makaburi kule, tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.
Baadhi yetu mtakumbuka safari moja, jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu), walishitakiwa. Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo. Tufunge! Tukafunga. Hakuna kula. Na siku ya kufunga, tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko. Tukafanya mkutano hadi saa 12 (za) jioni.
Baada ya mkutano, tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia. Mimi nikamuuliza mzee: “Sheikh, una Aspro?” Akajibu: “Kwa nini unataka Aspro?” Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kweli kweli. Akasema, S”ubiri.” Tulisubiri hadi saa ya kufuturu. Tukafuturu vizuri. Mzee Ramia, akaniuliza: “Bado unataka Aspro?” Nikajibu, “Kichwa sasa hakiumi!” Kumbe ilikuwa njaa. Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee.





Nyuma ya pazia, Mwl. Nyerere amebeba alama muhimu na rekodi za kipekee duniani. Alama hizo zinamfanya kuwa binadamu wa kipekee kabisa Afrika katika Karne ya Ishirini na Moja ( 21), alama hizo ni:
Alizaliwa tar. 13 Aprili, mwaka 1922, Butiama na kufariki tar. 14 Oktoba, mwaka 1999, London, Uingereza. Ni Rais wa kwanza Afrika kuachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe.
Ni Rais wa kwanza kuhama Ikulu na kwenda kuishi kwenye nyumba aliyoijenga kwa mkopo yake akiwa bado Rais.
Ni kati ya Marais aliyekuwa analipwa mshahara mdogo duniani, na pengine kati ya rais aliyewahi kulipwa mshahara mdogo barani Afrika mpaka sasa.
Ni Mtanganyika wa kwanza kusoma Chuo Kikuu nchini Uingereza, akiwa Mwafrika wa pili kupata Shahada nje ya Afrika: akisomea English, Political Economy, Social Anthropology, British History, Economic History, Constitutional Law, and Moral Philosophy.
Ni kiongozi aliyeisaidia China kuingia Umoja wa Mataifa na hutuba yake maarufu akisema kwamba,”Umoja wa Mataifa si serikali ya dunia, bali ni sehemu ambayo dunia nzima inakutana. Kwa hiyo, kumtoa China katika umoja wa mataifa ni kumtoa kuwa sehemu ya dunia.”
Ndiye mwanzilishi wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini (Anti Apartheid Movement), mwaka 1959, pamoja na Trevor Huddleston, nchini Uingereza.
Ni mmoja kati ya waanzilishi wa Umoja wa Afrika, 1963.
Amezisaidia nchi nyingi za Afrika kupata uhuru kuliko mtu mwingine yeyote katika historia ya ukoloni. Nchi hizo ni: Zambia (1964), Malawi (1964), Botswana (1966), Lesotho (1966), Mauritius (1968), Swaziland (1968) and Seychelles (1976) na baadae 1975, (Mozambique), (Angola), 1980 (Zimbabwe), 1990 (Namibia) na 1994 (South Africa).
Mwaka 2009, alitajwa na rais wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kama, Shujaa wa Waulimwengu Kuhusu Haki za Kijamii (World Hero of Social Justice).
Amepokea shahada mbalimbali kutoka Vyuo mbalimbali ambavyo ni: University of Edinburgh (UK), Duquesne University (USA), University of Cairo (Egypt), University of Nigeria (Nigeria), University of Ibadan (Nigeria), University of Liberia (Liberia), University of Toronto (Canada), Howard University (USA), Jawaharlal Nehru University (India), University of Havana (Cuba), National University of Lesotho, University of the Philippines, Fort Hare University (South Africa), Sokoine University of Agriculture (Tanzania) na Lincoln University (PA, USA).
Alipokea Tuzo ya Order of José Marti Cuba (1975), Order of the Aztec Eagle (Collar) Mexico (1975), Order of Amílcar Cabral, Guinea Bissau (1976), the Nehru Award for International Understanding (1976), the Third World Prize (1982), Order of Eduardo Mondlane Mozambique (1983), the Nansen Medal for outstanding services to Refugees (1983), Order of Agostinho Neto, Angola (1985), Sir Seretse Khama SADC Medal (1986), Joliot-Curie Medal of Peace (1988), the Lenin Peace Prize (1987), the International Simón Bolívar Prize (1992), the Gandhi Peace Prize (1995), Statesman of the 20th century by the Chama Cha Mapinduzi (2000), Order of the Companions of O. R. Tambo (Gold), South Africa (2004), Royal Order of Munhumutapa, Zimbabwe (2005), Most Excellent Order of the Pearl of Africa (Grand Master), Uganda (2005), Order of Katonga, Uganda (2005), National Liberation Medal, Rwanda (2009), National Liberation Medal, Rwanda (2009), Campaign Against Genocide Medal, Rwanda (2009), Order of the Most Ancient Welwitschi Mirabilis, Namibia (2010), Tanzania Professional Network Award (2011), Order of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Tanzania (2011), National Order of the Republic (Grand Cordon), Burundi (2012) na Order of Jamaica, Jamaica.
Mwaka 2007, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alimpa tuzo ya Katongo ambayo ni Medali ya juu kuliko zote ya Jeshi la Uganda, kwa heshima ya upinzani wake dhidi ya ukoloni na serikali ya Idi Amin.
Mitaa, barabara, majengo, vituo, shule, vyuo na vitu vilivyopewa jina lake; Daraja la Nyerere Kigamboni, Julius Nyerere University of Kankan, in Kankan, Guinea, Nyerere Drive, Gaborone (1.6 km) in Botswana, Nyerere Avenue, Mombasa (1.5 km) na Nyerere Road, Kisumu (2 km) nchini Kenya, Julius Nyerere Street, Windhoek (1.1 km) nchini Namibia, Julius Nyerere Street, Durban (0.5 km) nchini South Africa, Nyerere Road, Kitwe (1.4 km) nchini Zambia, Julius Nyerere Way, Harare (1 km) nchini Zimbabwe, Julius Nyerere International Airport, Julius Nyerere International Convention Centre, Nyerere Day- Public Holiday (14/10), Nyerere Cup, Nyerere Road, Unguja, Zanzibar (6.5 km), Nyerere Secondary School, Mwanga District na J.K. Nyerere Secondary School, Moshi, Kilimanjaro Region, Mwalimu J. K. Nyerere Secondary School, Mbozi District, Mbeya Region, Nyerere Memorial School, Korogwe, Tanga Region, Nyerere High School Migoli Iringa Region, Nyerere Secondary School, Unguja, Zanzibar, Mwalimu Nyerere Foundation, Mwalimu Nyerere Museum Centre na Mwalimu Nyerere Memorial Academy- Tanzania.

Baadhi ya vitabu alivyoviandika ni, Freedom and Unity (Uhuru na Umoja), Freedom and Socialism (Uhuru na Ujamaa), The Arusha Declaration, Education for self-reliance, The Varied Paths to Socialism, The purpose is man, Socialism and development, Freedom and Development (Uhuru Na Maendeleo), Ujamaa, Crusade for Liberation, Education for Self-Reliance, Uongozi na Hatima ya Tanzania, na Tujisahihishe.
Pamoja na kujulikana kama Baba wa Taifa la Tanzania, Nchi za Kusini mwa Afrika zinamtambua kama Baba wa Ukombozi wa Nchi za Kusini.
Pamoja na kujua lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa Ufasaha, pia alifahamu lugha ya Kigiriki na Kilatini.
Julius Nyerere ameandikwa kwenye kitabu cha Enyclopidia kama mtu pekee duniani katika historia ya Karne ya 21, aliyeweza kuwafanya watu wa makabila, dini, asili na historia tofauti kujiona kama watu wamoja.
Binadamu pekee aliyeasisi Muungano wa aina yake duniani wa Tanganyika na Zanzibar (wa serikali mbili) na kisha kuikalia kijasusi Zanzibar kwa Nusu Karne.

Yote aliyoyaanza tangu utoto wake, makuzi yake, harakati zake, utuuzima wake, uzee wake, yalifikia kikomo tar. 14 Oktoba, mwaka 1999, alipoaga dunia kwenye kitanda cha Hospitali ya Mtakatifu Thomas, mjini London, alikokwenda kwa matibabu. Kabla hajafariki dunia, aliwakumbuka Watanzania wake akisema: “Najua nitakufa, sitapona ugonjwa huu. Ninasikitika kuwaacha Watanzania wangu, najua watalia sana. Lakini nami nitawaombea kwa Mungu.” Naam, Watanzania wake walilia sana, walipopata taarifu za kifo chake. Mwili wake ulipoletwa nchini, waliomboleza kwa uchungu mno. Mwl. Julius Kambarage Nyerere alizikwa kijijini kwake, Mwitongo Butiama, kwa heshima zote na wananchi wa Tanzania na wmataifa mbalimbali wakiwemo viongozi mashuhuri, waliokuja kwa ajili ya mazishi.
Ni dhahiri, msingi wa yale yote aliyoyaamini na kuyasimamia, utaendelea kudumu ndani ya mioyo ya kizazi chake, kizazi hiki na vizazi vijavyo kutokana na mchango mkubwa alioutoa akiwa muasisi na Baba wa Taifa katika kujenga taifa la Tanzania. Huyo ndiye mtoto aliyezaliwa siku ya mvua, na kupewa jina la mzimu wa mvua, KAMBARAGE; mwana wa Chifu, Nyerere Burito na Mgaya wa Nyang’ombe. Ni dhahiri, tar. aliyozaliwa 13 Aprili, mwaka 1922, Mgaya hakujua kwamba ajifungua mtoto ambaye angekuja kuwa kiongozi mashuhuri sana Afrika na duniani, aliyewapenda binadamu wote na kuwatumikia Watanzania kwa moyo wake wote, akili na nguvu zake zote.
 
Wana Majlis,
Hivi mnajua kuwa Mwalimu Nyerere ameandika kuhusu AA na hakupingana na yale aliyoandika Kleist Sykes?

Sent using Jamii Forums mobile app
Paskali,
''The Tanganyika African National Union is, in one sense, a new organisation, but in another it is an old organisation. It was taken over from what was formerly called the Tanganyika African Association, which was founded in 1929, largely as a social organisation. The Tanganyika African National Union, which took over from the African Association about ten months ago, is a new organisation in the sense that it is a political organisation, where as the former was semi-political.''

[6] Julius K. Nyerere, Tanganyika African Association, to Governor Edward Twining, 10 th August, 1953. Sykes' Papers.
 
Haya mambo haya, ni balaa, Huyo Mohamed Said naye ni wakuja tu, wametoka Congo wakaishia Musoma, kisha wakaja Mzizima, naye ni wakuja tu, so hiyo history anayoandika ni story ya wazee wake wahamiaji sio wana Mzizima
Hivi ulikuwa huelewi kuwa Dar ni multi ethnic city toka enzi na enzi?

Laiti ungelielewa maana ya Dar Es Salaam usingekurupuka.
 
Hivi ulikuwa huelewi kuwa Dar ni multi ethnic city toka enzi na enzi?

Laiti ungelielewa maana ya Dar Es Salaam usingekurupuka.
haikuwa multi ethnic city mpaka pale wahamiaji kutoka Congo, Sudan kidogo na group dogo la Wayao, Wanyasa na wazulu na wala sio muda mrefu unaosema enzi na enzi
 
haikuwa multi ethnic city mpaka pale wahamiaji kutoka Congo, Sudan kidogo na group dogo la Wayao, Wanyasa na wazulu na wala sio muda mrefu unaosema enzi na enzi
Hatakuelewa, atakupinga daima, hajui ni juzi tu mjerumani akahamisha makao toka Bagamoyo na kuleta Mzimzima....
 
Paskali,
''The Tanganyika African National Union is, in one sense, a new organisation, but in another it is an old organisation. It was taken over from what was formerly called the Tanganyika African Association, which was founded in 1929, largely as a social organisation. The Tanganyika African National Union, which took over from the African Association about ten months ago, is a new organisation in the sense that it is a political organisation, where as the former was semi-political.''

[6] Julius K. Nyerere, Tanganyika African Association, to Governor Edward Twining, 10 th August, 1953. Sykes' Papers.
Kosa kubwa unalolifanya tangu miaka yote ya ubishi wetu hapa, nikuwa rejea zinatoka chanzo kimoja tu kiitwacho Sykes to Sykes.... Chanzo chenye maumivi na chenye kifua kikali chenye hasira na Julius Nyerere
 
haikuwa multi ethnic city mpaka pale wahamiaji kutoka Congo, Sudan kidogo na group dogo la Wayao, Wanyasa na wazulu na wala sio muda mrefu unaosema enzi na enzi
Nimekusomesha juu hapo lakini somo halijakuingia. Kaisome tena post uliyoijibu.
 
Kosa kubwa unalolifanya tangu miaka yote ya ubishi wetu hapa, nikuwa rejea zinatoka chanzo kimoja tu kiitwacho Sykes to Sykes.... Chanzo chenye maumivi na chenye kifua kikali chenye hasira na Julius Nyerere
Yericko,
Kleist Sykes (1894 - 1947) ndiyo aliyeandika maisha yake na mswada ukatufikia na ukachapwa kitabu.

Nyaraka nyingine ni nyaraka kama nyaraka zilivyo na hakuna katika nyaraka zilizoko katika kitabu changu zilichomtaja Baba wa Taifa kwa ubaya.

Pitia notes zote kwenye kitabu na onyesha iliyokuwa na taarifa mbaya kwa Mwalimu Nyerere.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paskali,
''The Tanganyika African National Union is, in one sense, a new organisation, but in another it is an old organisation. It was taken over from what was formerly called the Tanganyika African Association, which was founded in 1929, largely as a social organisation. The Tanganyika African National Union, which took over from the African Association about ten months ago, is a new organisation in the sense that it is a political organisation, where as the former was semi-political.''

[6] Julius K. Nyerere, Tanganyika African Association, to Governor Edward Twining, 10 th August, 1953. Sykes' Papers.


Watu wengine wanasoma au wanasikiliza bila kujua kuna kitu kinaitwa critical thinking

Kuna hoja mbili kuhusu hili

1.Mohamed ameondoa ushiriki wa watu makusuadi katika historia anayosema ni ya Tanganyika, ingawa mambo yakibana husema ya wazee wake na ikiwa ngumu zaidi husema ya Waislam

Kosa ambalo Kivukoni walifanya kwa kutotambua michango mingine, kwake lina uhalali

2. Historia ina formula, kuieleza au kuiandika kwa mujibu wa matukio na wakati kama ilivyo
Jaribio la ku ''interject'' personal feelings or ideas, historia husota madole ya machoni dhahir shahir

Kwa waliosikiliza video, Mohamed anasema Kleist Sykes aliunda AA na kisha Jamii fil Islamiya 1933. Mohamed hakueleza chochote kuhusu Cecil Matola.

Kumtaja Cecil ni kumtaja Rais wa kwanza na hivyo hoja ya Kleist kuunda AA inakufa.
Katika maandishia anasema, Kleist aliunda kwasababu alikuwa na pesa na mashuhuri.

Mohamed haelezi Cecil Matola alikuwa msomi na 'immunity' dhidi ya Wakoloni kuliko Kleist
Tendo la kutomtaja Matola, historia haikukaa kimya imemnyooshea kidole

3. Mohamed anasema Abdul Aliunda TANU, Nyerere akiwa Rais wa TAA kabla ya 1954.

Kitendo cha kumuondoa Nyerere, historia inamzaba kibao Mohamed.
Huwezi kuwa Rais wa chama asiyejua transformation. Abdul hakuunda TANU, alishiriki

1929 cecil akiunda AA hadi uchaguzi katika miaka ya 1950 Abdul ni takribani miaka 23.
Kleist na Mwanawe Abdul walibaki na uana harakati kwa miaka 23.

Nyerere aliandika katiba ya TANU katika transformation ya chama kuwa ya kisiasa
Akafungua milango UN kwa kutumia usomi, na kupata Uhuru katika miaka 10

Mohamed hasemi hilo, lakini historia inamsuata bila mtu kuandika kitabu kingine

Miaka 23 Kleist na mwanae Abdul Sykes hawakuwa na wazo la kuandika katiba
Wazo amekuja nalo Nyerere. Ndio maana Mohamed hajibu hoja za nani aliandika katiba
Hataki kumsikia Nyerere mtu anayemchukia sana katika dunia hii

Mohamed anasema hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na kamati ya watu watano.
Katika hao Mohamed hamtaji Nyerere aki back date kuandikwa kwake.

Historia inamshataki Mohamed, kama hotuba iliandikwa kabla ya Nyerere ni nani aliyetarajiwa kwenda UN?

Historia inasema kama kamati iliandika hotuba, kulikuwa na tatizo gani ikiwa lilikuwa suala la chama?
Kuna shida gani chama kuandika hotuba kubwa kama ya UN na kumkabidhi mhusika!

Mohamed anaingiza hoja kuonyesha Nyerere alisoma tu bila kujua maudhui ili kumdhalilisha.

Historia inamtetea Nyerere. Wakati hotuba inaandikwa yeye ni mmoja wa watu wachache sana waliokuwa na degree katika kiwango cha Master. Alishakuwa exposed katik siasa za dunia

Mohamed anaweza kumdhalilisha Nyerere atakavyo, wanaosoma kwa critical thinking watakuwa na rafiki yao mmoja anayeitwa Historia atakayewasaidia kuchambua chuki na ukweli
 
Back
Top Bottom