"Mohamed Said, post: 22765533, member: 12431"]Jackline,
Kuna tofauti kati ya mjadala wa heshima na ufedhuli.
Hakuna matusi, unajaribu kutafuta sababu
Tena wewe ndiye bingwa, mimi nikiwausia watu watumie lugha za stara haa vijana wako
Unatafuta sababu, lakini tupo pale pale, nani aliandika katiba ya TANU. Kabla ya hapo AA au TAA zilikuwa na katiba ipi zilitumika wapi na nani aliandika
Kuna mahali umesema Nyerere alipokea uongozi hivyo ni ushahidi vyama vilikuwa vya siasa
Well, pale Ilala katika ile kona kuna bango la Pepsi na chini kuna kuku. Tuna mkusanyiko wetu wa Arsenal na Man U. Hiyo haitoshi kuwa sisi ni klabu ya michezo! Tuna viongozi wetu lakini si ushahidi ni klabu
Mtu mwenye hasad katika roho yake huwa hajifichi vile vitu vinavyochoma
moyo wake huwa anavidhihirisha.
Hasad ni ile kwa nini neema hii kapewa yeye sikupata mie?
Kwa nini haimuondokei hii nema na yeye akawa kama watu wengine?
Mimi sikujui wala hatujuani, hasad ya nini? Napata riziki kwa njia zangu hasad ya nini?
Haya ni maneno ya kushindwa hoja sasa unatetwa na kugeuza jamvi kama eneo la mipasho.
No, turudi kwenye hoja
Jicho la husda linakausha hata mgomba uliokuwa unanawiri.
Watu kama hawa ukiwajua unawakimbia.
Wakimbie lakini usikimbie hoja. Umeleta mashtaka, umewasomea wahusika tunakuuliza ushahidi unasema Abdul kasema! whaat? Abdul ni kwako siyo international Unit.
Mimi toka utoto mama yangu akinitahadharisha kuhusu husda na athar zake.
Husda ni zaidi ya wivu.
Jibu hoja, hayo yako na mzazi wako ni huko nyumbani kwenu
Husda katika hii historia ilionekana tangu zamani sana.
Hakuna husda kuna matundu , kunauzushi. Hiyo haifanyi kuwa historia si kweli, ila hatuwezi kuruhusu kugeuzwa ndondocha hata kwa yale tunayojua. Jibu hoja
Nimeweka hapa jinsi gazeti la Africa Events lilivyokusanywa kwa kuwa tu
limemtaja Abdul Sykes kuwa alihusika sana katika kuunda TANU.
Haya hayajibu hoja yatafutie eneo
Nimeeleza kisa cha Paula Parks alivyofukuzwa nchini kwa kuandika makala
kuhusu TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika baada ya kufanya mahojiano
na Ally Sykes.
Sawa sawa,. lakini hayajibu hoja zilizoko mbele.
Nimeeleza jinsi historia ya TANU ilivyoandikwa na Abdul Sykes jina lake likawa
halipo.
Hawakumtendea haki kwakweli. Turudi kwenye hoja
Kichekesho mimi nikae hapa nakejeliwa na mtu ambae wala sijui anakotokea wala
hajakuwa na ujasiri hata wa kujitokeza kwa jina lake dhahir awe kila kukicha ni
kejeli na ''Cambridge,'' haimtoki mdomoni.
Unatumia Cambridge ili sisi tuliofeli darsa la saba tukuogope.
Tumekuchukua na kukupeleka Cambridge, halafu tumekuweka stoo huko cambridge, ukirudi utakuwa umekwenda Cambridge. Nilikutahadharisha mapema, tunaojua vitoga na N'gonda ni sisi si Cmabridge
Jibu hoja tuache hayo. Nani aliandika katiba ya TANU, kabla ya hapo ni katiba ipi iliyokuwepo na iliandikwa na nani
Ninalolijua nalisema nisilojua nasema hili silijui.
La katiba unalijua au hulijui?