Umar Mukhtar alifika katika kijiji ambacho askari wa Kitaliani walikivamia kuua na kufanya ufisadi ulio vuka mipaka nje ya kanuni za vita. Akasema ni nani awezae kupigana na adui mshenzi kama huyu asiyechunga mipaka? Si kama jeshi lake halikuwa na uwezo wa kulipiza la hasha, kwake yeye kufanya hivyo kungemshusha na yeye kuingia katika ushenzi. Hapa nawasoma watu wasiochunga ndimi zao na inakuwa tabu kujibu matusi kwa matusi.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ndugu zangu wana Majlis,
Uzuri wa JF ni huu ni kuwa unaweza umemkusudia mtu fulani maelezo
akaja mtu mwingine akakujibu.
Lakini kwa kuwa hapa ni uwanja wazi mpata mpatae huwezi kumwambia
kuwa sikukusudia wewe.
Ikiwa unataka kumkwepa labda kwa kuwa unajua hana moja la maana na
hakuna tija kufanyanae mjadala njia nyepesi ni ''shifting,'' yaani unahama.
Maalim Haruna sheikh wangu aliyenisomesha adab za mnakasha, yaani
majadiliano alinifunza namna ya ''kumfunza mjinga,'' na hili ndilo neno
alilokuwa akitumia - ''mjinga.''
Maalim Haruna Allah amrehemu alikuwa anaanza mhadhara wake
kwa nukuu ya
Imam Shafi inayosema kuwa
Imam Shafi amesema
kuwa yeye anaweza kusimama hata na watu mia moja kwa hoja lakini
akashindwa na mjinga mmoja.
Hili neno ''mjinga,'' likawa linanipa shida sana siku moja nikamuuliza
sheikh hili neno naweza kulitumia hadharani si tusi?
Maalim Haruna alikuwa na hulka moja.
Ukiuliza swali la kijinga huwa ananyamaza kimya kwa dakika mbili tatu
hivi hasemi kitu anakutazama.
Akakaa kimya...
''Kesho mie nitakuwa sipo utakwenda kumuuliza nani swali kama hilo?
Sasa mimi nakuuliza wewe mjukuu wa
Sheikh Mohamed Mvamila,
wewe akili yako inakutuma vipi hili neno, ''mjinga,'' ni tusi?''
Pale pale nikajua kosa langu.
Huyu mzee Allah atamlipa.
Akitufunza kutumia akili zetu.
Sasa nikawa jibu lishakuja na nikataka nijibu katika njia
Maalim
Haruna afurahi.
''Mjinga ni ''jahil,'' na hilo neno sikuzote tunalisema ndani ya masjid
na katika madrasa na hafla zetu haliwezi likawa tusi.''
Jibu langu lilimfurahisha sana
Maalim Haruna.
Basi alitufunza namna ya kumsomesha mtu mjinga.
Anasema sheikh, ikiwa umeleta ushahidi mmoja katika kujibu masaala
na mwenzio bila ya kuja na hoja akaja na maneno matupu kukupinga,
unakuja na ushahidi mwingine na mwingine na mwingine na mwingine.
Sheikh akamaliza kwa kusema ukifanya hivi utakuwa unamsaidie yeye
kwa vitu viwili.
Kwanza kumpa elimu asiyokuwanayo na pili unamdhihirishia ule ujinga
wake.
Nimeweka hapa historia ya
Ally Sykes katika siku za mwanzo baada ya
kuundwa TANU akapewa adhabu ya uhamisho akapelekwa Korogwe na
jinsi alivyovamiwa na makachero nyumbani kwake na vipi
Mzee Makatta
Mwinyimtwana alivyomnusuru.
Sasa soma alipopelekwa uhamisho Moshi baada ya kutolewa Korogwe
nini kilitokea:
''I was able to convince Hamza Aziz and Iddi Mwajasho to attend the Machame meeting in which Nyerere spoke. Hamza Aziz and Mwajasho were young police officers stationed at the Police Training College. After this meeting the two were reprimanded by the government for getting involved in politics contrary to service regulations. In organising the Machame meeting I had earned for myself the wrath of the colonial administration.
Soon after this meeting I was arrested for allegedly taking bribes. One day a white officer and an African Inspector walked into my office and arrested me. There was no evidence to back the allegations. I was suspended and taken to court on trumped up corruption charges. One of the people who was used by the government to frame me was Joseph Kimalando, one of the TANU founding members from Northern Province. I had crossed swords with Kimalando when we were transforming TAA into TANU at the headquarters. I had backed Yusuf Olotu and other patriots and advised them to sideline him and register the new party. Although among the founders of TANU in Dar es Salaam, once back in Moshi Kimalando refused to register the party in Kilimanjaro.
Reports reaching TANU headquarters were that Kimalando was collaborating with the colonial government to frustrate registration of the party. He was ousted from the party and he joined UTP.
Kimalando was a seasoned politician having been in politics since the early days of the African Association. He claimed to be among the founder members of the Association together with Sheikh Hussein Juma who was later to be Vice President of the United Tanganyika Party, UTP, an opposition party formed by the British to oppose TANU. When I was transferred to Moshi from Korogwe in 1957 Kimalando, then outside the mainstream of the struggle and a member of the UTP, framed me against the government.
My mother and Abdulwahid contacted Annur Kassum recently returned from studies in Britain where he had studied law to defend me. Our parents had known each other in Dar es Salaam for many years. My father in his early business career had tried to join the Chamber of Commerce, which was dominated by Indians at that time. My father could not fit in that all Indian organisation and left to form his own African Traders Association, which was shortlived. It is during that period at the Chamber of Commerce that he came to be acquainted with Annur Kassums’s father.
Annur Kassum flew to Moshi by a Dakota plane of the East African Airways and appeared in court the following day. The two policemen who had arrested me did not appear in court but the magistrate asked the prosecutor to proceed with the case. Kassum objected and insisted that the two police officers who had made the arrest must appear as witnesses. For some unknown reasons the prosecution was not very keen to have the two policemen interrogated by my defence council and the magistrate had no choice but to dismiss the case. By then I had been suspended from work for six months. I was given four months leave from work and I used this opportunity to go to Accra to attend Ghana’s independence celebrations in 1957.''
Kutoka, ''Under the Shadow of British Colonialism.'' (Hakijachapwa)