Nichangie kidogo,yoote tutazunguka ila kubwa linaachwa kwamba tangu awali kulikuwa na mpango wa kumtumia Mwalimu kama ngazi ili baadaye hao waliompokea waitie nchi kwenye Udini na mwalimu aling'amua hili na kukibadilisha chama kwenda TANU na hatimaye Uhuru.
Hii kusema Serikali haina Dini ila watu wake ndiyo wana Dini ni njia ya Mwalimu kuwadhibiti "Wadini" ,kiukweli kuna upotoshaji mkubwa kwa waandishi wa vitabu vya kina Sykes.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Jeisuiti Katika Mwelekeo wa Dunia:
Maamuzi yoyote ya mwelekeo wa dunia hutokea baada ya kukubaliwa ama kuratibiwa na Kanisa kupitia shirika la Jeisuiti ambalo utendaji wake ni wa siri zaidi. Karne ya Kumi na Sabaa (17), kanisa lilikuja na mpango madhubuti wa kuisaka haki ya kibinadamu katika ulimwengu wa kikoloni. Ijapokuwa, mpango huo ulikuwa ukibadilika malengo kila nyakati kulingana na mahitaji ya Karne. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Shirika la Wajeisuiti lilikuwa na nguvu na lilikuwa tayari sehemu ya tawala nyingi duniani, hivyo kufanya kisiwepo kitakachofanyika bila majasusi hawa kujua ama kuhusika, hasa juu ya mstakabali wa dunia ijayo. Walikuwa na bado wanauoni mkubwa wa mambo yajayo.
Wazo la kuwa na Shirikisho la Mataifa lilitolewa kwa mara ya kwanza, na mwanafalsafa Mjerumani Immanuel Kant, mnamo mwaka 1795. Wazo la Kant lilirudiwa na wanafalsafa mbalimbali. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza Ya Dunia, rais wa Marekani, Woodrow Wilson, alipendekeza hatua za kuanzisha shirikisho hili kwa kusudi la kuzuia vita za wakati ujao baada ya mwisho wa vita ile. Kant alikuwa wakala wa ujasusi wa Wajeisuiti akiripoti kwa Karl Theodor von Dalberg. Karnt alizaliwa mjini Königsberg (sasa: Kaliningrad), mnamo tar. 22 Aprili, mwaka 1724, akiwa mtoto wa fundi. Mamake alimsomesha kweye shule ya sekondari, akaendelea kusoma theolojia, falsafa, sayansi, fizikia na hisabati. Tasnifu yake ya kwanza haikupokelewa na Profesa Msimamizi wake, mwaka 1746. Ndipo, akageukia kufanya kazi ya ualimu kwenye nyumba ya matajiri na makabaila mbalimbali kwenye mazingira ya Königsberg. Mwaka 1754, alirudi Chuo Kikuu, akamalizia masomo yake. Tangu mwaka 1755, alikuwa mwalimu na ilipofika mwaka 1804, akawa profesa kamili kwenye Chuo Kikuu cha Königsberg. Hakuoa. Aliishi na mtumishi wa nyumbani tu hadi kifo chake kilipomfika, akiwa na umri wa miaka themanini kamili (80). Kaburi lake ni kando ya Kanisa Kuu la Königsberg. Limetunzwa, hata baada ya kufukuzwa kwa Wajerumani na kuwa sehemu ya Urusi.
Katiba ya Shirikisho la Mataifa, ilikuwa sehemu ya mkataba wa Versailles ya mwaka 1919. Nchi washindi au mataifa ya ushirikiano zilijiunga na umoja huo mpya. Baada ya kukubaliwa na nchi za kutosha, shirikisho lilianza rasmi tarehe 10 Januari, mwaka 1920. Katiba hiyo, ilikuwa na madhumuni yafuatavo:
Fitina zote kati ya nchi, zitasuluhishwa kwa njia ya amani kwa maazimio ya kamati au mahakama ya kimataifa
Nchi wanachama, zote zitaungana dhidi ya nchi yoyote itakayoanzisha vita mpya au kukataa azimio la mahakama ya kimataifa
Nchi kupunguza jeshi yao na idadi ya silaha zilizopo
Mkutano mkuu wa wawakalishi wa nchi zote wanachama, itakuwa Bunge la Shirikisho
Kamati kuu au halmashauri ya nchi wanachama nne (baadaye sita) na nafasi nne (baadaye 9) za nchi zinazobadilishana kwa zamu
Ofisi kuu inayoongozwa na Katibu Mkuu
Mahakama ya kimataifa itaundwa (ilishaundwa), ya kutoa azimio katika matatizo kati ya madola
Mkataba wa Versailles ulianzisha aina mpya ya maeneo yaliyowahi kuwa ama koloni au majimbo ya nchi zilizoshindwa katika vita. Koloni zote za Ujerumani pamoja na sehemu kubwa ya majimbo ya Milki ya Osmani ya awali, ziliwekwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa na kukabidhiwa kwa nchi washindi wa vita. Zilipewa hali ya pekee kama maeneo ya kudhaminiwa. Tofauti na koloni za kawaida, nchi wadhamini hazikupewa mamlaka yote jinsi iliyokuwa katika koloni zao za kawaida bali zilipokea maeneo ya kudhaminiwa chini ya masharti fulani pamoja na kulinda haki kadhaa za wenyeji na kuziandaa nchi hizi kwa uhuru. Hapo mwanzoni tofauti kati ya koloni na eneo la kudhaminiwa haikuwa kubwa lakini baadaye masharti ya udhamini yalikuwa muhimu.
Kwa mfano, hali ya Tanganyika kuwa eneo ka kudhaminiwa, ilisababisha Uingereza kutokubali walowezi wengi kuja hapa. Vivyo hivyo, hali ya Afrika ya Kusini Magharibi kuwa eneo la kudhaminiwa, ilizuia sehemu hii kuwa jimbo la Afrika Kusini kuwa msingi kwa uhuru wake kama nchi ya Namibia.
Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na shirika hilo la kijasusi (Jeisuiti) kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua. Lakini, lilikumbana na kiunzi/ukinzani hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya Ukristu, kufuatia nguvu ya Cambrige (Anglikana). Mgogoro huo ulikuzwa kwa kuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa shirika lao la kijasusi la Fabian Sociaty, maalumu kwa minajili ya kuwaandaa Vijana katika makoloni Uingereza hususani barani Afrika, kukabidhiwa nchi zao. Barani Afrika, Jeisuiti ilibadili mbinu kwa kuwa dola la Kiingereza, lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani. Haikujikita kwenye dola, bali ilisimama katika muundo wa shirika likifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri shahiri, ilikuwa lazima itimie, kama ilivyoelezwa mwanzoni kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu. Kwa hiyo, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo.
Katika Tanganyika, chini ya Udhamini wa Shirikisho la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.
Mwaka 1927 hadi 1929, kanisa Katoliki nchini, chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi wake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli. Tar. 12 Februari, mwaka 1929, Zelger alistaafu wadhifa wake kwa lazima. Ni mwaka huohuo wa 1927, ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron, maalumu kwa minajili ya kuratibu mambo ya sherehe za watu weusi pembeni ya mji, huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na akawapa jingo la ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini, historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA: Rais wa kwanza, Mwalimu, Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za Mjerumani kutoka kabila la Wayao), Katibu Mkuu wa kwanza, Klest Sykes (Mzulu, Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni kutoka Afrika Kusini), Mwekahazina, Ali Ramadhan (Mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania leo bahari ya Hindi). Hawa ndio mwaka 1927, waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933, Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho, Bw. Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948, yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest, aliyeitwa Abdulwahid Sykes.
Abdulwahid Sykes alitoka kupigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia, huko Burma. Aliporudi, alikuwa na mawazo ya ujana kutoka vitani, akampindua baba yake kwa vurugu na ngumi. Mapinduzi yaliyoitwa ‘ondoa wazee’. Kisha chama cha AA kikabadilishwa jina na kuitwa TAA ambapo Rais wake wa Kwanza, akawa Daktari wa binadamu Vedasto Kyaruzi (Mhaya), aliyekuwa anafanya kazi Kingolwila Mkoani Morogoro. Huyu ndie daktari wa binadamu wa kwanza kabisa wa Kiafrika, Tanganyika. Katibu Mkuu, akawa Abdulwahid Sykes mwenyewe na Mweka Hazina akawa Dosa Azizi. Miaka miwili tu ya chama kipya, yaani 1950, Daktari Vedasto Kyaruzi, kwa ghiriba za wakoloni, alihamishiwa Sengerema Mwanza, kama sehemu ya kumuondoa jijini Mzizima leo Dar es Salaam awe mbali na harakati.
Nafasi ya rais wa TAA ikakaimiwa na Bw. Adbulwahid, mpaka mwaka 1953, uchaguzi ulipofanyika na Julius Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo (Mnazimoja ya leo). Mwaka 1954, Mwl. Nyerere akabadili jina la chama cha TAA na kuwa TANU, jina ambalo lilibuniwa na Abdulwahid Sykes. TANU ilikwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM (Chama cha Mapinduzi), baada ya Muungano wa ASP na TANU.
Moja ya kisa cha kukumbukwa ni kile cha kufukuzwa kwa Kasisi Zelger kinanachosema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, na lilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika. Hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa Kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake. Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta, mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranta alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya Mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake. Mathalani mnamo tar. 23 Mei, mwaka 1938, wakati makanisa sabaa ya Kilutheri, yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu Maranta aliomba kuhudhuria kikao cha tar. 8 mwezi Juni kilichofanyika Mjini Arusha. Askofu Maranta aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana. Bali, uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamanufaa (ushahidi wa nyaraka za kumbukumbu za mkutano huo unaeleza).
Juhudi za kanisa kupigania mkataba wa Versailles ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana, kwa mfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950s, kanisa sasa lilikuwa tayari lina nguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika. Wakati hayo yakiendelea, tayari kanisa kupitia Shirika lake la Kijasusi (Jeisuiti), lilikuwa limewekeza kwa nguvu kubwa kumtafuta mtu imara mwenye weledi na vipawa kimkemu, atakayejengwa ili aje kuongoza nchi. Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki, tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na makasisi wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Ma-sheikh waliokuwa na ushawishi mkubwa. Mathalani tar. 5 Feb., mwaka 1948, Askofu Maranta alikutana na Sheikh Issa bin Amir, kiongozi wa kiroho katika Msikiti wa Ilala-Mchikichini.
Sheikh Issa Bin Amir, alizaliwa mwaka 1846 katika viunga vya Mzizima, Mchikichini, na kuhudumu katika wadhifa (k.m. Sheikh) katika msikiti uliokuwa hapohapo viwanja vya nyumbani kwake na alifariki mwaka 1953 akiwa na umri wa miaka mia moja na sabaa (107). Sheikh Issa Bin Amir, kwa kabila, alikuwa Mzaramo. Wakati wa uhai wake hadi kifo kilipomfika, aliishi Mchikichini, nyuma ya kilipo kiwanda cha bia leo (TBL). Sheikh Issa Bin Amir, rafiki kipenzi wa Padre Maranta, na mzee wa hekima za kilele cha zama hizo, mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya Uislamu na Ukristu, Mtu ambaye watu (Mwalimu Cesil Matola rais wa kwanza wa AA na Klest Sykes katibu mkuu wakwanza wa AA, na wanachama wengine waliokuwa AA) walimheshimu sana kwa hekima zake, akiwa mmoja wa wasisi wa Jumuiko la Uislamu Afrika Mashariki (EAMWS) ambapo Mazungumzo mengi ya Jumuiko la Uislamu, yalihusu harakati za ukombozi. Shekh Issa alimshauri Askofu Maranta kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi, basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono. Wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?
Siku chache baada ya makutano yake na Sheikh Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino, kasisi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa. Mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni: “Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa Biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo. Halafu, ndani ya Biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe.” Pendekezo hilo lilimvutia sana Askofu Maranta, hivyo akalipa baraka zake zote. Kwa hakika, pendekezo hilo lilifanikiwa na ndilo lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru. Mathalani Biblia ya lugha ya Kihehe, ilieleza wazi athari za kutawaliwa.
Harakati za Ukombozi za Mwl. Nyerere, akiwa na nguvu mpya ya kifikra kutoka Chuo kikuu, zililivutia kanisa na uungaji mkono ukachagizwa. Mfano, mwaka 1953, wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu kufuatia mabadiliko ya 1948 kutoka AA kwenda TAA. Askofu Maranta alimwalika Mwl. Nyerere ofisini pake. Walipokutana, walizungumza mengi lakini kubwa ni kuwa, alimsifu Mwl. Nyerere kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni. Ndipo, akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za kiraia viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru, na kanisa litasaidia kwa hali na mali.
Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mwl. Nyerere kisawasawa. Ndipo, mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa Kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi huku wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao ambayo ni Elimu na Woga. Ikumbukwe kuwa mwaka 1953, baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwl. Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena, Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ukashika mkondo wake.
Mnamo tar. 7 Julai, mwaka 1954, Vijana (wazee wa Kariakoo) wakiongozwa na Mwl. Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajeisuiti (Askofu Maranta) na Waislamu (Sheikh Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, hekima za Sheikh huyu ziliendelea kusaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwl. Nyerere ya kwenda UNO tar. 5 Machi, mwaka 1955, kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tikiti ya ndege ya kwenda na kurudi. Lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani.
Si hivyo tu, bali katika moja ya utani wa Mwl. Nyerere wenye ukweli ndani yake, aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni mabosi wake, akikumbuka malipo ya Shilingi mia sita (600/=) angali ameacha kazi ya ualimu, akiwa kijijini Butiama. Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Nyerere kuja kuiongoza Tanganyika mpya. Barua ya lugha ya Kilatini, ya kitume, Tot Tangaeque, ya Papa wa Roma, ya tar. 8 Novemba, mwaka 1984, kwenda kwa Kanisa Katoliki Tanzania, inautangazia ulimwengu kwamba Tanzania itakuwa chini ya himaya ya kanisa kwa mwavuli wa Bikira Maria Imakulata.
Miaka thelethini na mbili (32) baadae, Kanisa Katoliki Tanzania chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Askofu Tarcisius J.M. Ngalalekumtwa, linaijibu barua hiyo kwa barua yenye kumbukumbu nambari TEC/PR/1 ya tar. 10 Novemba, mwaka 2016, likikubaliana na kuitangazia dunia kuwa siku ya Uhuru wa Tanganyika, tar. 9, mwezi 12 ya kila mwaka itakuwa pia siku ya kuadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria Imakulata. MSIMAMIZI wa JAMHURI ya MUUNGANO wa TANZANIA........
Kutoka katika Kitabu: Ujasusi wa Kidola na kiuchumi.
Mwandishi: Yericko Nyerere
Sura ya pili: Uk 461-465. (Mashirika ya Kijasusi)