Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Huyu mzee anazingua, watu ambao wasiohoji na upungufu wa elimu ukiongezea ndugu wa imani lazima wamkubalie kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyiokunda,
Mimi naelewa tabu wanayopata wengi kuhusu historia ya TANU.

Shida hii ya akili kutaabika baada ya ukweli kudhihirika ndiyo iliyomfanya Prof. Haroub Othman kuzungumza na Baba wa Taifa ili amsikie Mwalimu anasemaje.

Hii ilikuwa baada ya kusoma kitabu cha Abdul Sykes.

Haya kanieleza kwa kinywa chake.

Uamuzi uliotoka baina yao ni kuwa Mwalimu na yeye azungumze.

Ikaamuliwa itengenezwe kamati ya wasomi na Mwalimu Nyerere atazungumza maisha yake na wao wataandika historia yake.

Hili halikukamilika kwa kuwa Mwalimu alikuwa anaugua.

Ndiyo baada ya kifo chake hivi sasa kinaandikwa kitabu hicho na Jopo la Prof. Shivji.

Jopo limeshapita kwangu na kunihoji.

Nimewapa Nyaraka za Sykes na picha za kipindi kile cha kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Tusubirini kitabu hiki.

Sijapatapo kumdhalilisha Baba wa Taifa kwa namna yoyote si hapa JF wala kwengineko na laiti maandishi yangu yangefanya hivyo nisingefikia katika kushirikishwa katika miradi miwili mikubwa ya kuandika historia ya Afrika, mradi wa Oxford University Press Nairobi 2007 na mradi wa Harvard na Oxford University Press New York 2011.

Hata hawa waliponisoma kwa mara ya kwanza walipigwa na butwaa kama nyie.

BBC mwaka 2014 waliniomba nishiriki katika kuadhimisha miaka 100 ya Vita ya Kwanza ya Dunia lakini nilishindwa kwa kuwa muda ule sikuweza kupatikana.

BBC walitaka niwasomee na kuzieleza War Diaries alizoandika Kleist Sykes wakati akiwa askari wa Wajerumani akipigana dhidi ya Waingereza chini ya Kamanda Von Lettow Vorbeck 1914 - 1918.

Niko mbali na Maktaba yangu nikirejea ofisini In Shaa Allah nitakuwekeeni hapa hizo shajara nanyi mzisome.

Sina tatizo la kukubalika katika historia hii.

Chembelecho Maalim Faiza, Elimu bila Khiyana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengine wanasoma au wanasikiliza bila kujua kuna kitu kinaitwa critical thinking

Kuna hoja mbili kuhusu hili

1.Mohamed ameondoa ushiriki wa watu makusuadi katika historia anayosema ni ya Tanganyika, ingawa mambo yakibana husema ya wazee wake na ikiwa ngumu zaidi husema ya Waislam

Kosa ambalo Kivukoni walifanya kwa kutotambua michango mingine, kwake lina uhalali

2. Historia ina formula, kuieleza au kuiandika kwa mujibu wa matukio na wakati kama ilivyo
Jaribio la ku ''interject'' personal feelings or ideas, historia husota madole ya machoni dhahir shahir

Kwa waliosikiliza video, Mohamed anasema Kleist Sykes aliunda AA na kisha Jamii fil Islamiya 1933. Mohamed hakueleza chochote kuhusu Cecil Matola.

Kumtaja Cecil ni kumtaja Rais wa kwanza na hivyo hoja ya Kleist kuunda AA inakufa.
Katika maandishia anasema, Kleist aliunda kwasababu alikuwa na pesa na mashuhuri.

Mohamed haelezi Cecil Matola alikuwa msomi na 'immunity' dhidi ya Wakoloni kuliko Kleist
Tendo la kutomtaja Matola, historia haikukaa kimya imemnyooshea kidole

3. Mohamed anasema Abdul Aliunda TANU, Nyerere akiwa Rais wa TAA kabla ya 1954.

Kitendo cha kumuondoa Nyerere, historia inamzaba kibao Mohamed.
Huwezi kuwa Rais wa chama asiyejua transformation. Abdul hakuunda TANU, alishiriki

1929 cecil akiunda AA hadi uchaguzi katika miaka ya 1950 Abdul ni takribani miaka 23.
Kleist na Mwanawe Abdul walibaki na uana harakati kwa miaka 23.

Nyerere aliandika katiba ya TANU katika transformation ya chama kuwa ya kisiasa
Akafungua milango UN kwa kutumia usomi, na kupata Uhuru katika miaka 10

Mohamed hasemi hilo, lakini historia inamsuata bila mtu kuandika kitabu kingine

Miaka 23 Kleist na mwanae Abdul Sykes hawakuwa na wazo la kuandika katiba
Wazo amekuja nalo Nyerere. Ndio maana Mohamed hajibu hoja za nani aliandika katiba
Hataki kumsikia Nyerere mtu anayemchukia sana katika dunia hii

Mohamed anasema hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na kamati ya watu watano.
Katika hao Mohamed hamtaji Nyerere aki back date kuandikwa kwake.

Historia inamshataki Mohamed, kama hotuba iliandikwa kabla ya Nyerere ni nani aliyetarajiwa kwenda UN?

Historia inasema kama kamati iliandika hotuba, kulikuwa na tatizo gani ikiwa lilikuwa suala la chama?
Kuna shida gani chama kuandika hotuba kubwa kama ya UN na kumkabidhi mhusika!

Mohamed anaingiza hoja kuonyesha Nyerere alisoma tu bila kujua maudhui ili kumdhalilisha.

Historia inamtetea Nyerere. Wakati hotuba inaandikwa yeye ni mmoja wa watu wachache sana waliokuwa na degree katika kiwango cha Master. Alishakuwa exposed katik siasa za dunia

Mohamed anaweza kumdhalilisha Nyerere atakavyo, wanaosoma kwa critical thinking watakuwa na rafiki yao mmoja anayeitwa Historia atakayewasaidia kuchambua chuki na ukweli
Huu ndio ukweli mchungu kwa Mohamed Said
 
Yericko,
Mimi sina uchungu katika nafsi yangu na ndiyo unaona hapa najadili na kueleza yale niyajuayo pasi na ghadhabu wala kutoa matusi.

Nimeweka hapa kazi zangu na nilioshirikiananao katika kuhifadhi historia hii.

Nyie kwa chuki ndiyo mnaokuja na kejeli na mna ujasiri hata wa kukejeli vyuo vikuu vyenye hadhi duniani ambao wamechapa vitabu nilivyoandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3efaace6db4615104e72dcced5d17640.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
Kulikuwa na ubishi mzito kuhusu katiba ya TANU pale niliposema kuwa ilinakiliwa kutoka katiba ya Convention People's Party (CPP) ya Kwame Nkrumah.

Msomeni Judith Listowel, "The Making of Tanganyika," anaeleza katiba ya TANU ilipotoka.

uYFTmZdKe0wOy6bfZB0fkLvrgrgOpRoKLVAZEqwpy0v0DQhqATCRkCeU44X0Gg3GG21J9gzhpTvflCZtcu-X3fnwiuMezDSKdyQmJW13KVwe0223n0p2up3pLYmn3n7Gyz5zx16Xe_MM4i-3NbLmQeoeHit8htq2Y_2tDbqJPnuR9onc5vRrK6kSUu2H9JTN8Dd0cwTkTLYSqtjaHX5yRxG09GNg7ylsOp8e9F1S68XggRz0nr6ETNPBUGplBOJfijzSc_VM0Epbj9i7WH619-i7lDNKwyDO2vKIyopbTqB9jXvf_mw7h42QM-UVa0PGiFZg1BN1cM8l2saORe1fexKbxSJIl281ErPKeg6XmdWbxHaPtFkA8IdDlpe0X59Z-FyOO7fXrs_uOXoHyw41M1_iGREcuvOSqgHsGhDfB_RJhL5NhqS6CRIRut_pWD-dZfebXKAYB-xQVcEEvuJnVj2RkfW52TS-qfTzsKd7IuvfA81fNNPLbYGAHg1TwWE9OLhKjQ8dnOcbsj4C8dSGVzuCJHMHs1gBQIKGrN5LjK6S3kRhBUUTuJibS8B4TW0pdNoIrGt05ljzyk2E7U-_j5FnuJBdNmZXsimmJKdRC3EYXqtrVRT_zA=w354-h629-no
 
Shukran sana Sheikh Mohamed Said.

Hii bayana yako umekata mzizi wa fitina.

Labda kwa wale waliokuwa wanapinga kuwa katiba ya TANU iliandikwa na Nyerere, sababu alikuwa msomi peke yake ni vizuri waje na ushahidi kwa faida ya huu ukumbi wa JF.

Kumekucha.
 
Ritz,
Mimi nimesoma kila kitabu kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nimezungumza na waasisi wenyewe wa TANU na wanachama wa mwanzo wa chama hiki.

Hawa wote wamenisomesha mengi.

Tewa Said Tewa ndiye aliyenipa habari za katiba ya TANU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anababaika tu hajui aseme nini. Anatafuta visababu vya kitoto kabisa

Jamvi linashuhudia fadhaiko lingine, na tulimuasa mapema sana akiona tupo kimya asiamshe 'dude'
Tulipokaa pembeni akaanza kutamba 'jamvi kimyaa' na kila tambo. Jamvi linashudia ubabaikaji na hili ndilo watu waelewe. Ukiona mapicha na maneno meengi ni kubabaisha usisome between the lines
Mtu anaadhirika
3efaace6db4615104e72dcced5d17640.jpg

Mipicha yenyewe ndiyo kama hiyo.
 
View attachment 574747
Mipicha yenyewe ndiyo kama hiyo.
Ritz,
Moja katika ibra ya kitabu hiki ni kughadhibisha.

Mimi sijaona wapi nimefedheheka.

Zaidi nimefanikiwa sana kwanza kusomesha mengi ambayo wengi hawakuyajua lakini kubwa zaidi ni kuuza nakala nyingi za kitabu.

Hadi hii leo hakuna aliyekuja hapa jamvini na historia hata iliyokaribia na yangu hata kwa mbali.

Wako kimyaa...

Wakija hapa wameghadhibika hawana uwezo wa kufanya mjadala kistaarabu.

Tusubiri kitabu cha Jopo la Prof. Shivji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyiokunda,
Mimi naelewa tabu wanayopata wengi kuhusu historia ya TANU.

Shida hii ya akili kutaabika baada ya ukweli kudhihirika ndiyo iliyomfanya Prof. Haroub Othman kuzungumza na Baba wa Taifa ili amsikie Mwalimu anasemaje.

Hii ilikuwa baada ya kusoma kitabu cha Abdul Sykes.

Haya kanieleza kwa kinywa chake.

Uamuzi uliotoka baina yao ni kuwa Mwalimu na yeye azungumze.

Ikaamuliwa itengenezwe kamati ya wasomi na Mwalimu Nyerere atazungumza maisha yake na wao wataandika historia yake.

Hili halikukamilika kwa kuwa Mwalimu alikuwa anaugua.

Ndiyo baada ya kifo chake hivi sasa kinaandikwa kitabu hicho na Jopo la Prof. Shivji.

Jopo limeshapita kwangu na kunihoji.

Nimewapa Nyaraka za Sykes na picha za kipindi kile cha kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Tusubirini kitabu hiki.

Sijapatapo kumdhalilisha Baba wa Taifa kwa namna yoyote si hapa JF wala kwengineko na laiti maandishi yangu yangefanya hivyo nisingefikia katika kushirikishwa katika miradi miwili mikubwa ya kuandika historia ya Afrika, mradi wa Oxford University Press Nairobi 2007 na mradi wa Harvard na Oxford University Press New York 2011.

Hata hawa waliponisoma kwa mara ya kwanza walipigwa na butwaa kama nyie.

BBC mwaka 2014 waliniomba nishiriki katika kuadhimisha miaka 100 ya Vita ya Kwanza ya Dunia lakini nilishindwa kwa kuwa muda ule sikuweza kupatikana.

BBC walitaka niwasomee na kuzieleza War Diaries alizoandika Kleist Sykes wakati akiwa askari wa Wajerumani akipigana dhidi ya Waingereza chini ya Kamanda Von Lettow Vorbeck 1914 - 1918.

Niko mbali na Maktaba yangu nikirejea ofisini In Shaa Allah nitakuwekeeni hapa hizo shajara nanyi mzisome.

Sina tatizo la kukubalika katika historia hii.

Chembelecho Maalim Faiza, Elimu bila Khiyana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wana Majlis,
Nilikuwa nje ya maktaba kwa muda kidogo sasa Alhmadulilah nimerejea.
Hebu tuanze na haya hapo chini:

Pol Pot,
Wajib wetu kuhifadhi historia ya wazee wetu.

Kipande hiki cha Vita Vya Pili Vya Dunia nilikipata kwa njia ya ajabu kidogo.
Mimi nilikuwa nishakamilisha utafiti na kuandika.

Mswada ulikuwa unasubiri mchapaji (publisher).

Katika mahojiano yangu na marehemu Bwana Ally Sykes wakati wa utafiti
kila mara alikuwa akitaja jalada la moja ambalo alikuwa akinambia kuwa lina
taarifa muhimu.

Alikuwa akinambia kuwa jalada hili lilikuwa mikononi kwa marehemu kaka
yake Bwana Abdulwahid Sykes.

Siku moja nikakutana na Ally Sykes Msikiti wa Manyema katika maziko.
Ally Sykes akanambia, ''Mohamed njoo ofisini lile ''file'' la Bwana Abdu
nimelipata.

Katika jalada lile ndipo nilipokutana na mengi na mojawapo ni hizi ''War
Diaries,'' za Lance Corporal Kleist Sykes.

Nikarudi tena mezani kuongeza yale niliyokwishaandika.

Ndipo nilipojua kwa nini jalada lile lilimtaabisha sana Bwana Ally Sykes
hadi alipoliona tena.

Nimesoma hapa jamvini kuna mtu kaghadhibishwa na kumbukumbu hii
na kaandika mistari ya kukejeli hizi ''Shajara za Vita Kuu Vya Kwanza
Vya Lance Corporal Kleist Sykes,'' ameziita ''hekaya.''

Mara nyingi kila nilipokuwa nikizungumza na Mzee Kitwana Kondo
alikuwa na msemowake akipenda kuusema, ''It takes all sorts of people
to make the world go round.''

Kwa hiyo mimi namtia Bwana ''Hekaya,'' katika kundi hilo.
Kama si Bwana, ''Hekaya,'' nisingepata hamu ya kuandika haya.

In Sha Allah nitaweka hapa jamvini maandishi ya mjukuu wa Kleist,
Bi. Daisy Aisha Sykes aliyoandika mwaka wa 1968 kuhusu maisha ya
babu yake akiwa vitani kati ya mwaka wa 1914 na 1918.

Huenda Bwana ''Hekaya,'' akaamini kuwa hiyo ni historia ya kweli na
wala si ''hekaya.''
 
Bi. Daisy Aisha Sykes
aliyoandika mwaka wa 1968 kuhusu maisha ya

MAADHIMISHO YA MIAKA 100 VITA VYA KWANZA VYA DUNIA 1914 - 1918 : SHAJARA ZA LANCE CORPORAL KLEIST SYKES

Miezi michache kabla vita haijaanza Ujerumani ilimteua Lettow-von Vorbeck kama Kamanda wa Majeshi ya Ulinzi ya Ujerumani katika Tanganyika. Askari wa zamani Waafrika waliopigana chini yake, pamoja na Kleist wanamkumbuka kwa mapenzi kama mtu mwema na askari shujaa. Kleist aliingizwa ndani ya jeshi la Wajerumani tarehe 13 November 1906 akiwa kijana mdogo sana wa umri miaka kumi na mbili na akapigana katika vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914 - 1918). Katika jeshi Kleist alipata mafunzo ya mawasiliano. Baada ya miezi mitatu alihamishwa na kupelekwa Bataliani ya Pili kama karani katika Makao Makuu ya Jeshi Dar es Salaam. Alibakia hapo hadi mwaka 1914. Vita vilipoanza, bataliani ya Kleist iliondoka Ukonga ikaelekea Mwakijembe, Tanga ambako kulikuwa na mashambulizi kutoka majeshi ya Waingereza kupitia mpaka wa Kenya. Katika bataliani hiyo alikuwapo Schneider, mtoto wa Affande Plantan.

Kleist alikuwa anazungumza Kijerumani na juu ya yote hayo alikuwa vilevile mtoto wa Affande Plantan, kiongozi wa askari wa Kizulu katika utawala wa Wajerumani. Kwa ajili hii Kleist alipewa heshima ya pekee na akapewa nafasi kuwa mpambe wa von Lettow Vorbeck. Kumshuhudia kijana wa Kiafrika katika sare ya jeshi la Kijerumani akiongea Kijerumani huku anatembea nyuma ya von Lettow-Vorbeck, Mkuu wa Majeshi ya Wajerumani Tanganyika, bila shaka kuliwavutia wengi, hata Wajerumani wenyewe. Hii ilikuwa nafasi hasa iliyostahili mtoto wa askari ambae baba yake aliwasaidia Wajerumani kuiteka Tanganyika. Kama mpambe kazi yaje ilikuwa kushughulikia mambo yote ya Kamanda Mkuu. Alikuwa na jukumu la kuangalia chakula na usafi wa sare za von Lettow-Vorbeck, pamoja na mahitaji yake mengine. Alikuwa ndiye mtu wa kwanza Lettow-Vorbeck kukutananae asubuhi na wa mwisho kabla hajalala. Ilikuwa kazi yenye kumpa hadhi, mamlaka na heshima mbele ya askari wenzake. Utanashati wa Kleist katika mavazi na nidhamu yake katika maisha yake ya kawaida tu, yalitokana na kipindi hiki alichokuwa jeshini. Inaaminika kuwa hata ile hulka yake ya kuweka shajara na kuandika kumbukumbu muhimu ya mambo yake, yanatokana na uzoefu aliopata katika kipindi hiki akiwa jeshini. Inasemekana hii ndiyo miaka ambayo ilijenga silka na maisha ya Kleist.

Shajara zake za vita ni kielelezo binafsi kuhusu kampeni za Wajerumani na Waingereza wakati wa Vita Kuu Vya Kwanza. Shajara hizo zinaeleza kwa ukamilifu hali ya mambo yalivyokuwa kwa askari wa Kiafrika katika mapambano waliyoshiriki dhidi ya Waingereza. Kupitia maandishi ya Kleist unaweza ukaelewa ile chuki ambayo Waarabu walikuwanayo dhidi ya Wajerumani. Pambano la Kleist la kwanza dhidi ya Waarabu waliokuwa washirika wa Waingereza lilikuwa katika sehemu moja ijulikanayo kama Mwele Juu karibu ya Tanga.

Mbinu ya Lettow Vorbeck ilikuwa kuvuka mpaka wa Tanganyika na Kenya ili kukata mawasilano ya reli kati ya Mombasa na Kisumu. Reli hii ilikuwa jirani na mpaka wa Tanganyika. Ilikuwa mwendo wa siku chache kuifikia reli hii na kuikata Kenya na njia yake kuu kutoka Mombasa. Lakini jeshi la wanamaji wa Kiingereza lilikuwa Mombasa kwa hiyo bandari ya Mombasa ilikuwa imesalimika na manowari za Kijerumani. Ilikuwa wakati bataliani ya Kleist ipo Korogwe, mji uliopo maili chache kutoka Tanga, katika kijiji kiitwacho Semanya ndipo Kleist alipopokea habari kuwa Affande Plantan, baba yake Schneider na mlezi wake amefariki Dar es Salaam. Plantan alikuwa amekufa kwa homa ya matumbo tarehe 11 December 1914. Wajerumani walisimamisha vita kwa siku saba kwa heshima ya Affande Plantan.Wajerumani hawakuwa wezi wa fadhila walitambua kuwa alikuwa Affande Plantan waliekujanae kutoka Msumbiji kuja kuiteka Tanganyika. Alistahili kila aina ya heshima aliyostahili askari shujaa, hata kama alikuwa mamluki. Baada ya hapo Kleist na kamapani yake walielekea Tanga ambako kulikuwa makao makuu ya jeshi la Wajerumani wakati wa vita. Hapo hakukaa kwa muda mrefu kwa kuwa ilibidi kuomba likizo kurudi Dar es Salaam kumuangalia mama yake aliyekuwa mgonjwa. Alikaa Dar es Salaam kwa siku kumi akimuuguza mama yake kisha akarejea Tanga na akapewa kuongoza askari wanane katika divisheni ya kampani. Tarehe 24 December, 1915 kamapani yake iliamuriwa kwenda Mwakijembe na kisha Mwele Ndogo kuipokea 4th Reserve Company.

Waarabu walichukua nafasi hii ya msahambulizi ya Waingereza dhidi ya Wajerumani kulipiza kisasi dhidi yao. Waarabu waliungana na Waingereza kuwatimua Wajerumani Tanganyika. Bado baadhi yao walikuwa na kumbukumbu ya kitendo cha kikatili cha Wajeruani kwa shujaa wao Abushiri ambae walimnyonga mwaka 1889. Historia ikajirudia upya; Kleist na Schneider waliingia katika mapigano Mwele Ndogo dhidi ya adui wa zamani wa baba yao na adui wa Wajerumani ñ Waarabu. Mapambano haya yalifanyika siku ya mkesha wa Krismasi mwaka wa 1915 katika sehemu ile ile ambayo Sykes Mbuwane na Affande Plantan mamluki wa Kizulu waliteremka kwenye meli kuja kuwaongezea nguvu Wajerumani waliokuwa wakipigana na Waarabu na machifu wenyeji. Kwa saa kumi kuanzia alfajir hadi muda mchache kabla ya jua kuchwa, Wajerumani walibanwa katika mashambulizi makali. Kleist akapandishwa cheo na kuwa Lance Corporal kwa mchango wake katika pambano lile. Siku mbili baada ya pambano hilo Kleist na kampani yake waliamuriwa kwenda Kahe. Kleist Alibakia Kahe kwa mwezi mmoja kisha wakapata amri ya kwenda Voi,Kenya mji uliopo mpakani. Wakati wakiwa njiani kuelekea Voi, Kleist akaugua na ikabidi arudishwe Mombo, mji uliokuwa na mbu wengi kwa ajili ya mto uliokuwa unakatiza hapo mjini. Kleist alibaki akiugua hapo Mombo hospitalini kwa miezi miwili. Kutoka Mombo akaelekea Handeni. Mwezi Aprili 1916 habari zikamfikia bado akiwa katika uwanja wa mapambano kuwa mama yake amefariki dunia.

Mwaka wa 1916 Jeshi la Kiingereza lilikuja kuungwa mkono na askari kutoka Afrika ya Kusini walioshuka na meli Mombasa. Chini ya uongozi wa Jenerali Smutswalivuka mpaka wakaingia Tanganyika kupitia Namanga na Taveta. Haukupita muda mrefu mji wa Moshi ukatekwa. Batalioni ya Kleist ikawa sasa inarudi nyuma kuelekea Dodoma kulipokuwa na boma la Wajerumani. Si tu kuwa kikosi cha Kleist kilikuwa kinaandamwa na majeshi ya Waingereza, vikosi vya Wabelgiji navyo vilikuwa vimevuka mpaka kutoka Belgian Congo na kuingia Tanganyika. Wabelgiji waliteka Kigoma, Ujiji na Tabora. Mambo yalikuwa yamewachachia Wajerumani. Afya ya Kleist kwa wakati ule ikawa mbaya sana. Alifanyiwa uchunguzi Morogoro na akaonekana hawezi kuendelea kuitumikia katika kampeni yake. Afya yake haikumruhusu kupigana vita na ikabidi aachwe nyuma Mahenge wakati wenzake wakikimbia huku wakifukuzwa na adui. Kampani ya Kleist ilikwenda Chenene ambako walipambana kwa bunduki na vikosi vya Afrika ya Kusini kwa saa mbili. Kampani ile ikakimbilia Gode Gode, wakiponea chupu chupu. Kleist akakamatwa mateka mwezi Septemba 1917. Von Lettow Vorbeck mwishowe alifanikiwa kuvuka reli ya kati akavuka mpaka na kuingia Msumbiji, wakati huo ikijulikana kama Portuguese East Africa, akanusurika kutekwa yeye na askari wake. Kwa askari wa Kizulu hii ikawa ni nusra kwao kwa kuwa walikuwa wamerudishwa nyumbani.

Wakati von Lettow Vorbeck amefanikiwa kuponyoka kukamatwa, mpambe wake Kleist alitekwa na jeshi la Wabelgiji na wao wakamkabidhi kwa Waingereza. Waingereza walimtia Kleist kifungoni katika kambi ya mateka wa vita. Askari waliokuwa mateka pamoja na wagonjwa walichukuliwa na Waingereza na kutiwa kwenye kambi iliyokuwapo Kilosa. Kleist alikubali ukweli kuwa sasa yeye amepoteza hadhi yake kama askari, ni mateka, kwa hiyo akawa anasubiri hatima yake. Alibakia ndani yake kambi ile na yeye mwenyewe anaeleza katika kumbukumbu zake kuwa hakuwa na kinyongo chochote kwa maadui zake. Kleist aliweza hata kufanya urafiki na maadui zake ambao walikuwa wamemtia kifungoni. Kutokana na hali yake ya afya, Kleist hakuweza kufanya kazi zote za sulubu kama ilivyo desturi kwa wafungwa. Hali yake ya afya haikuwa inaonyesha dalili zozote za kupata nafuu, Kleist aliachiwa mwaka 1917 kwa hisia labda akiwa nje ya kambi, afya yake itarudi. Mwezi Novemba 1918 vita vikaisha huko Ulaya.

(Kutoka, ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)...''
 
3efaace6db4615104e72dcced5d17640.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
Kulikuwa na ubishi mzito kuhusu katiba ya TANU pale niliposema kuwa ilinakiliwa kutoka katiba ya Convention People's Party (CPP) ya Kwame Nkrumah.

Msomeni Judith Listowel, "The Making of Tanganyika," anaeleza katiba ya TANU ilipotoka.

uYFTmZdKe0wOy6bfZB0fkLvrgrgOpRoKLVAZEqwpy0v0DQhqATCRkCeU44X0Gg3GG21J9gzhpTvflCZtcu-X3fnwiuMezDSKdyQmJW13KVwe0223n0p2up3pLYmn3n7Gyz5zx16Xe_MM4i-3NbLmQeoeHit8htq2Y_2tDbqJPnuR9onc5vRrK6kSUu2H9JTN8Dd0cwTkTLYSqtjaHX5yRxG09GNg7ylsOp8e9F1S68XggRz0nr6ETNPBUGplBOJfijzSc_VM0Epbj9i7WH619-i7lDNKwyDO2vKIyopbTqB9jXvf_mw7h42QM-UVa0PGiFZg1BN1cM8l2saORe1fexKbxSJIl281ErPKeg6XmdWbxHaPtFkA8IdDlpe0X59Z-FyOO7fXrs_uOXoHyw41M1_iGREcuvOSqgHsGhDfB_RJhL5NhqS6CRIRut_pWD-dZfebXKAYB-xQVcEEvuJnVj2RkfW52TS-qfTzsKd7IuvfA81fNNPLbYGAHg1TwWE9OLhKjQ8dnOcbsj4C8dSGVzuCJHMHs1gBQIKGrN5LjK6S3kRhBUUTuJibS8B4TW0pdNoIrGt05ljzyk2E7U-_j5FnuJBdNmZXsimmJKdRC3EYXqtrVRT_zA=w354-h629-no
Nani alikupinga katika hili?

Nadhani hoja ilikuwa je AA na TAA vilikuwa na Katiba?

Kama ilikuwepo, ilikuwaje Julius Nyerere akachukue nakala ya katiba kwa rafiki yake kipenzi Kwame Nkurumah na kuinakili iwe ya TANU?
 
Ikiwa hamkupinga basi si neno.
 
Nani alikupinga katika hili?

Nadhani hoja ilikuwa je AA na TAA vilikuwa na Katiba?

Kama ilikuwepo, ilikuwaje Julius Nyerere akachukue nakala ya katiba kwa rafiki yake kipenzi Kwame Nkurumah na kuinakili iwe ya TANU?
Kwa hiyo tunakubaliana kuwa Mwalimu Nyerere hakuandika katiba ya TANU alichofanya na kunakili tu katiba ya kina Nkurumah.
 
Kabla ya Nyerere kwanini haikunakiliwa katiba hiyo toka Ghana?
 
MAADHIMISHO YA MIAKA 100 VITA VYA KWANZA VYA DUNIA 1914 - 1918 : SHAJARA ZA LANCE CORPORAL KLEIST SYKES

Miezi michache kabla vita haijaanza Ujerumani ilimteua Lettow-von Vorbeck kama Kamanda wa Majeshi ya Ulinzi ya Ujerumani katika Tanganyika. Askari wa zamani Waafrika waliopigana chini yake, pamoja na Kleist wanamkumbuka kwa mapenzi kama mtu mwema na askari shujaa. Kleist aliingizwa ndani ya jeshi la Wajerumani tarehe 13 November 1906 akiwa kijana mdogo sana wa umri miaka kumi na mbili na akapigana katika vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914 - 1918). Katika jeshi Kleist alipata mafunzo ya mawasiliano. Baada ya miezi mitatu alihamishwa na kupelekwa Bataliani ya Pili kama karani katika Makao Makuu ya Jeshi Dar es Salaam. Alibakia hapo hadi mwaka 1914. Vita vilipoanza, bataliani ya Kleist iliondoka Ukonga ikaelekea Mwakijembe, Tanga ambako kulikuwa na mashambulizi kutoka majeshi ya Waingereza kupitia mpaka wa Kenya. Katika bataliani hiyo alikuwapo Schneider, mtoto wa Affande Plantan.

Kleist alikuwa anazungumza Kijerumani na juu ya yote hayo alikuwa vilevile mtoto wa Affande Plantan, kiongozi wa askari wa Kizulu katika utawala wa Wajerumani. Kwa ajili hii Kleist alipewa heshima ya pekee na akapewa nafasi kuwa mpambe wa von Lettow Vorbeck. Kumshuhudia kijana wa Kiafrika katika sare ya jeshi la Kijerumani akiongea Kijerumani huku anatembea nyuma ya von Lettow-Vorbeck, Mkuu wa Majeshi ya Wajerumani Tanganyika, bila shaka kuliwavutia wengi, hata Wajerumani wenyewe. Hii ilikuwa nafasi hasa iliyostahili mtoto wa askari ambae baba yake aliwasaidia Wajerumani kuiteka Tanganyika. Kama mpambe kazi yaje ilikuwa kushughulikia mambo yote ya Kamanda Mkuu. Alikuwa na jukumu la kuangalia chakula na usafi wa sare za von Lettow-Vorbeck, pamoja na mahitaji yake mengine. Alikuwa ndiye mtu wa kwanza Lettow-Vorbeck kukutananae asubuhi na wa mwisho kabla hajalala. Ilikuwa kazi yenye kumpa hadhi, mamlaka na heshima mbele ya askari wenzake. Utanashati wa Kleist katika mavazi na nidhamu yake katika maisha yake ya kawaida tu, yalitokana na kipindi hiki alichokuwa jeshini. Inaaminika kuwa hata ile hulka yake ya kuweka shajara na kuandika kumbukumbu muhimu ya mambo yake, yanatokana na uzoefu aliopata katika kipindi hiki akiwa jeshini. Inasemekana hii ndiyo miaka ambayo ilijenga silka na maisha ya Kleist.

Shajara zake za vita ni kielelezo binafsi kuhusu kampeni za Wajerumani na Waingereza wakati wa Vita Kuu Vya Kwanza. Shajara hizo zinaeleza kwa ukamilifu hali ya mambo yalivyokuwa kwa askari wa Kiafrika katika mapambano waliyoshiriki dhidi ya Waingereza. Kupitia maandishi ya Kleist unaweza ukaelewa ile chuki ambayo Waarabu walikuwanayo dhidi ya Wajerumani. Pambano la Kleist la kwanza dhidi ya Waarabu waliokuwa washirika wa Waingereza lilikuwa katika sehemu moja ijulikanayo kama Mwele Juu karibu ya Tanga.

Mbinu ya Lettow Vorbeck ilikuwa kuvuka mpaka wa Tanganyika na Kenya ili kukata mawasilano ya reli kati ya Mombasa na Kisumu. Reli hii ilikuwa jirani na mpaka wa Tanganyika. Ilikuwa mwendo wa siku chache kuifikia reli hii na kuikata Kenya na njia yake kuu kutoka Mombasa. Lakini jeshi la wanamaji wa Kiingereza lilikuwa Mombasa kwa hiyo bandari ya Mombasa ilikuwa imesalimika na manowari za Kijerumani. Ilikuwa wakati bataliani ya Kleist ipo Korogwe, mji uliopo maili chache kutoka Tanga, katika kijiji kiitwacho Semanya ndipo Kleist alipopokea habari kuwa Affande Plantan, baba yake Schneider na mlezi wake amefariki Dar es Salaam. Plantan alikuwa amekufa kwa homa ya matumbo tarehe 11 December 1914. Wajerumani walisimamisha vita kwa siku saba kwa heshima ya Affande Plantan.Wajerumani hawakuwa wezi wa fadhila walitambua kuwa alikuwa Affande Plantan waliekujanae kutoka Msumbiji kuja kuiteka Tanganyika. Alistahili kila aina ya heshima aliyostahili askari shujaa, hata kama alikuwa mamluki. Baada ya hapo Kleist na kamapani yake walielekea Tanga ambako kulikuwa makao makuu ya jeshi la Wajerumani wakati wa vita. Hapo hakukaa kwa muda mrefu kwa kuwa ilibidi kuomba likizo kurudi Dar es Salaam kumuangalia mama yake aliyekuwa mgonjwa. Alikaa Dar es Salaam kwa siku kumi akimuuguza mama yake kisha akarejea Tanga na akapewa kuongoza askari wanane katika divisheni ya kampani. Tarehe 24 December, 1915 kamapani yake iliamuriwa kwenda Mwakijembe na kisha Mwele Ndogo kuipokea 4th Reserve Company.

Waarabu walichukua nafasi hii ya msahambulizi ya Waingereza dhidi ya Wajerumani kulipiza kisasi dhidi yao. Waarabu waliungana na Waingereza kuwatimua Wajerumani Tanganyika. Bado baadhi yao walikuwa na kumbukumbu ya kitendo cha kikatili cha Wajeruani kwa shujaa wao Abushiri ambae walimnyonga mwaka 1889. Historia ikajirudia upya; Kleist na Schneider waliingia katika mapigano Mwele Ndogo dhidi ya adui wa zamani wa baba yao na adui wa Wajerumani ñ Waarabu. Mapambano haya yalifanyika siku ya mkesha wa Krismasi mwaka wa 1915 katika sehemu ile ile ambayo Sykes Mbuwane na Affande Plantan mamluki wa Kizulu waliteremka kwenye meli kuja kuwaongezea nguvu Wajerumani waliokuwa wakipigana na Waarabu na machifu wenyeji. Kwa saa kumi kuanzia alfajir hadi muda mchache kabla ya jua kuchwa, Wajerumani walibanwa katika mashambulizi makali. Kleist akapandishwa cheo na kuwa Lance Corporal kwa mchango wake katika pambano lile. Siku mbili baada ya pambano hilo Kleist na kampani yake waliamuriwa kwenda Kahe. Kleist Alibakia Kahe kwa mwezi mmoja kisha wakapata amri ya kwenda Voi,Kenya mji uliopo mpakani. Wakati wakiwa njiani kuelekea Voi, Kleist akaugua na ikabidi arudishwe Mombo, mji uliokuwa na mbu wengi kwa ajili ya mto uliokuwa unakatiza hapo mjini. Kleist alibaki akiugua hapo Mombo hospitalini kwa miezi miwili. Kutoka Mombo akaelekea Handeni. Mwezi Aprili 1916 habari zikamfikia bado akiwa katika uwanja wa mapambano kuwa mama yake amefariki dunia.

Mwaka wa 1916 Jeshi la Kiingereza lilikuja kuungwa mkono na askari kutoka Afrika ya Kusini walioshuka na meli Mombasa. Chini ya uongozi wa Jenerali Smutswalivuka mpaka wakaingia Tanganyika kupitia Namanga na Taveta. Haukupita muda mrefu mji wa Moshi ukatekwa. Batalioni ya Kleist ikawa sasa inarudi nyuma kuelekea Dodoma kulipokuwa na boma la Wajerumani. Si tu kuwa kikosi cha Kleist kilikuwa kinaandamwa na majeshi ya Waingereza, vikosi vya Wabelgiji navyo vilikuwa vimevuka mpaka kutoka Belgian Congo na kuingia Tanganyika. Wabelgiji waliteka Kigoma, Ujiji na Tabora. Mambo yalikuwa yamewachachia Wajerumani. Afya ya Kleist kwa wakati ule ikawa mbaya sana. Alifanyiwa uchunguzi Morogoro na akaonekana hawezi kuendelea kuitumikia katika kampeni yake. Afya yake haikumruhusu kupigana vita na ikabidi aachwe nyuma Mahenge wakati wenzake wakikimbia huku wakifukuzwa na adui. Kampani ya Kleist ilikwenda Chenene ambako walipambana kwa bunduki na vikosi vya Afrika ya Kusini kwa saa mbili. Kampani ile ikakimbilia Gode Gode, wakiponea chupu chupu. Kleist akakamatwa mateka mwezi Septemba 1917. Von Lettow Vorbeck mwishowe alifanikiwa kuvuka reli ya kati akavuka mpaka na kuingia Msumbiji, wakati huo ikijulikana kama Portuguese East Africa, akanusurika kutekwa yeye na askari wake. Kwa askari wa Kizulu hii ikawa ni nusra kwao kwa kuwa walikuwa wamerudishwa nyumbani.

Wakati von Lettow Vorbeck amefanikiwa kuponyoka kukamatwa, mpambe wake Kleist alitekwa na jeshi la Wabelgiji na wao wakamkabidhi kwa Waingereza. Waingereza walimtia Kleist kifungoni katika kambi ya mateka wa vita. Askari waliokuwa mateka pamoja na wagonjwa walichukuliwa na Waingereza na kutiwa kwenye kambi iliyokuwapo Kilosa. Kleist alikubali ukweli kuwa sasa yeye amepoteza hadhi yake kama askari, ni mateka, kwa hiyo akawa anasubiri hatima yake. Alibakia ndani yake kambi ile na yeye mwenyewe anaeleza katika kumbukumbu zake kuwa hakuwa na kinyongo chochote kwa maadui zake. Kleist aliweza hata kufanya urafiki na maadui zake ambao walikuwa wamemtia kifungoni. Kutokana na hali yake ya afya, Kleist hakuweza kufanya kazi zote za sulubu kama ilivyo desturi kwa wafungwa. Hali yake ya afya haikuwa inaonyesha dalili zozote za kupata nafuu, Kleist aliachiwa mwaka 1917 kwa hisia labda akiwa nje ya kambi, afya yake itarudi. Mwezi Novemba 1918 vita vikaisha huko Ulaya.

(Kutoka, ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)...''
Nashukuru kwa kitabu hiki ambacho kimsingi ni mawazo ya mtu mmoja tu anayebeba hata ya wengine...
 
Wana Majlis,
Nilikuwa nje ya maktaba kwa muda kidogo sasa Alhmadulilah nimerejea.
Hebu tuanze na haya hapo chini:

Pol Pot,
Wajib wetu kuhifadhi historia ya wazee wetu.

Kipande hiki cha Vita Vya Pili Vya Dunia nilikipata kwa njia ya ajabu kidogo.
Mimi nilikuwa nishakamilisha utafiti na kuandika.

Mswada ulikuwa unasubiri mchapaji (publisher).

Katika mahojiano yangu na marehemu Bwana Ally Sykes wakati wa utafiti
kila mara alikuwa akitaja jalada la moja ambalo alikuwa akinambia kuwa lina
taarifa muhimu.

Alikuwa akinambia kuwa jalada hili lilikuwa mikononi kwa marehemu kaka
yake Bwana Abdulwahid Sykes.

Siku moja nikakutana na Ally Sykes Msikiti wa Manyema katika maziko.
Ally Sykes akanambia, ''Mohamed njoo ofisini lile ''file'' la Bwana Abdu
nimelipata.

Katika jalada lile ndipo nilipokutana na mengi na mojawapo ni hizi ''War
Diaries,'' za Lance Corporal Kleist Sykes.

Nikarudi tena mezani kuongeza yale niliyokwishaandika.

Ndipo nilipojua kwa nini jalada lile lilimtaabisha sana Bwana Ally Sykes
hadi alipoliona tena.

Nimesoma hapa jamvini kuna mtu kaghadhibishwa na kumbukumbu hii
na kaandika mistari ya kukejeli hizi ''Shajara za Vita Kuu Vya Kwanza
Vya Lance Corporal Kleist Sykes,'' ameziita ''hekaya.''

Mara nyingi kila nilipokuwa nikizungumza na Mzee Kitwana Kondo
alikuwa na msemowake akipenda kuusema, ''It takes all sorts of people
to make the world go round.''

Kwa hiyo mimi namtia Bwana ''Hekaya,'' katika kundi hilo.
Kama si Bwana, ''Hekaya,'' nisingepata hamu ya kuandika haya.

In Sha Allah nitaweka hapa jamvini maandishi ya mjukuu wa Kleist,
Bi. Daisy Aisha Sykes
aliyoandika mwaka wa 1968 kuhusu maisha ya
babu yake akiwa vitani kati ya mwaka wa 1914 na 1918.

Huenda Bwana ''Hekaya,'' akaamini kuwa hiyo ni historia ya kweli na
wala si ''hekaya.''
Yale yale ya from Sykes to Sykes
 
Wana Majlis,
Nilikuwa nje ya maktaba kwa muda kidogo sasa Alhmadulilah nimerejea.
Hebu tuanze na haya hapo chini:

Pol Pot,
Wajib wetu kuhifadhi historia ya wazee wetu.

Kipande hiki cha Vita Vya Pili Vya Dunia nilikipata kwa njia ya ajabu kidogo.
Mimi nilikuwa nishakamilisha utafiti na kuandika.

Mswada ulikuwa unasubiri mchapaji (publisher).

Katika mahojiano yangu na marehemu Bwana Ally Sykes wakati wa utafiti
kila mara alikuwa akitaja jalada la moja ambalo alikuwa akinambia kuwa lina
taarifa muhimu.

Alikuwa akinambia kuwa jalada hili lilikuwa mikononi kwa marehemu kaka
yake Bwana Abdulwahid Sykes.

Siku moja nikakutana na Ally Sykes Msikiti wa Manyema katika maziko.
Ally Sykes akanambia, ''Mohamed njoo ofisini lile ''file'' la Bwana Abdu
nimelipata.

Katika jalada lile ndipo nilipokutana na mengi na mojawapo ni hizi ''War
Diaries,'' za Lance Corporal Kleist Sykes.

Nikarudi tena mezani kuongeza yale niliyokwishaandika.

Ndipo nilipojua kwa nini jalada lile lilimtaabisha sana Bwana Ally Sykes
hadi alipoliona tena.

Nimesoma hapa jamvini kuna mtu kaghadhibishwa na kumbukumbu hii
na kaandika mistari ya kukejeli hizi ''Shajara za Vita Kuu Vya Kwanza
Vya Lance Corporal Kleist Sykes,'' ameziita ''hekaya.''

Mara nyingi kila nilipokuwa nikizungumza na Mzee Kitwana Kondo
alikuwa na msemowake akipenda kuusema, ''It takes all sorts of people
to make the world go round.''

Kwa hiyo mimi namtia Bwana ''Hekaya,'' katika kundi hilo.
Kama si Bwana, ''Hekaya,'' nisingepata hamu ya kuandika haya.

In Sha Allah nitaweka hapa jamvini maandishi ya mjukuu wa Kleist,
Bi. Daisy Aisha Sykes aliyoandika mwaka wa 1968 kuhusu maisha ya
babu yake akiwa vitani kati ya mwaka wa 1914 na 1918.

Huenda Bwana ''Hekaya,'' akaamini kuwa hiyo ni historia ya kweli na
wala si ''hekaya.''
Watu wengine wanasoma au wanasikiliza bila kujua kuna kitu kinaitwa critical thinking

Kuna hoja mbili kuhusu hili

1.Mohamed ameondoa ushiriki wa watu makusuadi katika historia anayosema ni ya Tanganyika, ingawa mambo yakibana husema ya wazee wake na ikiwa ngumu zaidi husema ya Waislam

Kosa ambalo Kivukoni walifanya kwa kutotambua michango mingine, kwake lina uhalali

2. Historia ina formula, kuieleza au kuiandika kwa mujibu wa matukio na wakati kama ilivyo
Jaribio la ku ''interject'' personal feelings or ideas, historia husota madole ya machoni dhahir shahir

Kwa waliosikiliza video, Mohamed anasema Kleist Sykes aliunda AA na kisha Jamii fil Islamiya 1933. Mohamed hakueleza chochote kuhusu Cecil Matola.

Kumtaja Cecil ni kumtaja Rais wa kwanza na hivyo hoja ya Kleist kuunda AA inakufa.
Katika maandishia anasema, Kleist aliunda kwasababu alikuwa na pesa na mashuhuri.

Mohamed haelezi Cecil Matola alikuwa msomi na 'immunity' dhidi ya Wakoloni kuliko Kleist
Tendo la kutomtaja Matola, historia haikukaa kimya imemnyooshea kidole

3. Mohamed anasema Abdul Aliunda TANU, Nyerere akiwa Rais wa TAA kabla ya 1954.

Kitendo cha kumuondoa Nyerere, historia inamzaba kibao Mohamed.
Huwezi kuwa Rais wa chama asiyejua transformation. Abdul hakuunda TANU, alishiriki

1929 cecil akiunda AA hadi uchaguzi katika miaka ya 1950 Abdul ni takribani miaka 23.
Kleist na Mwanawe Abdul walibaki na uana harakati kwa miaka 23.

Nyerere aliandika katiba ya TANU katika transformation ya chama kuwa ya kisiasa
Akafungua milango UN kwa kutumia usomi, na kupata Uhuru katika miaka 10

Mohamed hasemi hilo, lakini historia inamsuata bila mtu kuandika kitabu kingine

Miaka 23 Kleist na mwanae Abdul Sykes hawakuwa na wazo la kuandika katiba
Wazo amekuja nalo Nyerere. Ndio maana Mohamed hajibu hoja za nani aliandika katiba
Hataki kumsikia Nyerere mtu anayemchukia sana katika dunia hii

Mohamed anasema hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na kamati ya watu watano.
Katika hao Mohamed hamtaji Nyerere aki back date kuandikwa kwake.

Historia inamshataki Mohamed, kama hotuba iliandikwa kabla ya Nyerere ni nani aliyetarajiwa kwenda UN?

Historia inasema kama kamati iliandika hotuba, kulikuwa na tatizo gani ikiwa lilikuwa suala la chama?
Kuna shida gani chama kuandika hotuba kubwa kama ya UN na kumkabidhi mhusika!

Mohamed anaingiza hoja kuonyesha Nyerere alisoma tu bila kujua maudhui ili kumdhalilisha.

Historia inamtetea Nyerere. Wakati hotuba inaandikwa yeye ni mmoja wa watu wachache sana waliokuwa na degree katika kiwango cha Master. Alishakuwa exposed katik siasa za dunia

Mohamed anaweza kumdhalilisha Nyerere atakavyo, wanaosoma kwa critical thinking watakuwa na rafiki yao mmoja anayeitwa Historia atakayewasaidia kuchambua chuki na ukweli
 
Kwa hiyo tunakubaliana kuwa Mwalimu Nyerere hakuandika katiba ya TANU alichofanya na kunakili tu katiba ya kina Nkurumah.

Watu wengine wanasoma au wanasikiliza bila kujua kuna kitu kinaitwa critical thinking

Kuna hoja mbili kuhusu hili

1.Mohamed ameondoa ushiriki wa watu makusuadi katika historia anayosema ni ya Tanganyika, ingawa mambo yakibana husema ya wazee wake na ikiwa ngumu zaidi husema ya Waislam

Kosa ambalo Kivukoni walifanya kwa kutotambua michango mingine, kwake lina uhalali

2. Historia ina formula, kuieleza au kuiandika kwa mujibu wa matukio na wakati kama ilivyo
Jaribio la ku ''interject'' personal feelings or ideas, historia husota madole ya machoni dhahir shahir

Kwa waliosikiliza video, Mohamed anasema Kleist Sykes aliunda AA na kisha Jamii fil Islamiya 1933. Mohamed hakueleza chochote kuhusu Cecil Matola.

Kumtaja Cecil ni kumtaja Rais wa kwanza na hivyo hoja ya Kleist kuunda AA inakufa.
Katika maandishia anasema, Kleist aliunda kwasababu alikuwa na pesa na mashuhuri.

Mohamed haelezi Cecil Matola alikuwa msomi na 'immunity' dhidi ya Wakoloni kuliko Kleist
Tendo la kutomtaja Matola, historia haikukaa kimya imemnyooshea kidole

3. Mohamed anasema Abdul Aliunda TANU, Nyerere akiwa Rais wa TAA kabla ya 1954.

Kitendo cha kumuondoa Nyerere, historia inamzaba kibao Mohamed.
Huwezi kuwa Rais wa chama asiyejua transformation. Abdul hakuunda TANU, alishiriki

1929 cecil akiunda AA hadi uchaguzi katika miaka ya 1950 Abdul ni takribani miaka 23.
Kleist na Mwanawe Abdul walibaki na uana harakati kwa miaka 23.

Nyerere aliandika katiba ya TANU katika transformation ya chama kuwa ya kisiasa
Akafungua milango UN kwa kutumia usomi, na kupata Uhuru katika miaka 10

Mohamed hasemi hilo, lakini historia inamsuata bila mtu kuandika kitabu kingine

Miaka 23 Kleist na mwanae Abdul Sykes hawakuwa na wazo la kuandika katiba
Wazo amekuja nalo Nyerere. Ndio maana Mohamed hajibu hoja za nani aliandika katiba
Hataki kumsikia Nyerere mtu anayemchukia sana katika dunia hii

Mohamed anasema hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na kamati ya watu watano.
Katika hao Mohamed hamtaji Nyerere aki back date kuandikwa kwake.

Historia inamshataki Mohamed, kama hotuba iliandikwa kabla ya Nyerere ni nani aliyetarajiwa kwenda UN?

Historia inasema kama kamati iliandika hotuba, kulikuwa na tatizo gani ikiwa lilikuwa suala la chama?
Kuna shida gani chama kuandika hotuba kubwa kama ya UN na kumkabidhi mhusika!

Mohamed anaingiza hoja kuonyesha Nyerere alisoma tu bila kujua maudhui ili kumdhalilisha.

Historia inamtetea Nyerere. Wakati hotuba inaandikwa yeye ni mmoja wa watu wachache sana waliokuwa na degree katika kiwango cha Master. Alishakuwa exposed katik siasa za dunia

Mohamed anaweza kumdhalilisha Nyerere atakavyo, wanaosoma kwa critical thinking watakuwa na rafiki yao mmoja anayeitwa Historia atakayewasaidia kuchambua chuki na ukweli
 
Yale yale ya from Sykes to Sykes
Yericko,
Hakika katika historia ya Waafrika katika Tanganyika chini ya ukoloni toka
Wajerumani hadi Waingereza ni lazima yawe, ''yale yale Kleist Sykes to
Abdulwahid Kleist Sykes to Ally Kleist Sykes.''

Hakuna njia unayoweza hata kwa mbali kuikwepa historia hii katika kuunda
African Association, TANU na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ikawa wewe utaandika historia ya uhuru wa Tanganyika na TANU ukawaruka
hawa...

Angalia balaa lililowafika Chuo Cha Kivukoni kwa kujaribu kufanya hivyo.
Leo Jopo la Prof. Shivji wanaiandika historia ile ile upya.

Harvard waliponiandikia kunishirikisha katika mradi wa Dictionary of African
Biography waliniletea orodha ya majina ya wanasiasa wengi wa Tanzania
na kuniomba ushauri kama wanazo sifa za kuingizwa katika hilo kamusi.

Moja ya majina lilikuwa jina la Kleist Abdulwahid Sykes Meya wa Jiji la
Dar es Salaam.

Nikamweleza Prof. Emmanuel Ekyeampong kuwa nimeona jina la Kleist
Sykes
lakini kama umemkusudia Kleist Abdulwahid Sykes (1950 - ) mimi
namtoa katika orodha namweka babu yake Kleist Sykes (1894 - 1947).

Nikamwambia pia kuwa ikiwa unataka tumtie Kleist katika kamusi itabidi
kwanza tumtangulize baba yake Abdulwahid na baba yake mdogo Ally.

Nikamweleza hawa ndiyo waliopigania uhuru wa Tanganyika bega kwa bega
na Nyerere.

Nikamweleza kuwa hii ni familia maarufu katika siasa za kikoloni Tanganyika.

Prof. Akyeampong akaniomba niandike kitu nimpelekee.

Hivyo ndivyo Kleist Sykes akaingia katika kamusi lile yeye pamoja na wanae
wote.

Siku hiyo nilipokwenda kuiangalia medali ya Abdul Sykes ya ''Mwenge wa
Uhuru,'' nikamweleza Kleist nikamwambia, ''Harvard walikutaka wewe ndiye
uingie katika kamusi yao mimi nikakufanyia, ''fitna,'' nikamtia somo yako.''

Inawezekana kuwa na nyie mna historia yenu ya African Asociation na
TANU na pia historia yenu jinsi mlivyoikomboa Tanganyika.

Mimi sina ugomvi na historia hiyo.

Tumeishi miaka mingi na historia ya Chuo Cha Kivukoni hapajakuwa na
tatizo wala sikuwatafuta niwatolee kejeli na jeuri asilani.

Nilinyanyua kalamu nikaandika historia ya African Asociation, TANU na
historia ya uhuru wa Tanganyika kama ninavyoifahamu.

Msemaji mmoja baada ya kusoma kitabu cha Abdul Sykes alisema,
''Wengi walioandika historiaya TANU hawakuwa wanaijua.''

Basi mimi nakuchukulieni nyie kuwa hamkuwa mnayajua haya.

ehbUAwfAkWf4oCgt8bdYOJvUR-H67JxixLcTum_PsQd0LErJmXM3dN8LvGjIqXBLc1XJeIlZDKdM4axOcrfaXIQ9_wrf8GK6M_3xnAg7kKSumtfO9jW3tCZacbnQDdDKwlbkEjoTbFhvEwl3Lgw2KiYYL1vtLfoovZJxfR_gSiGPZUq5ilA4U252iTlZa-3DnbtRNULVlzRG5UiGua4Nm2NSOl8djBkaBEg6d-75o6zQEQ3YazyR_I1y0u-7pE1sSaIgS6RrW6iOpWc9esbTJzFCPd1DlzrP5JqZuyRZ7R68j1iwMoN8ydbSPVLurKoDAYFzyzBGYFtKDR2fDv5XY6oJlzT0cK3x-02xqjri36KVmz1j7ZpeuzPd9oRDKHJS-3Gfvys5GPPYoqkU49OIAA5drlZYBY6xMJT0O9eAScsF2N282fK_YQPDItIgV9_VMjfxOHqheFl0PFSsNjPuX5xMgAnhLPnjlAj_8FGo_NhiBgwkWuwNK7AjXRFKbX2QVPNIRCQ9dqt9b67Zu6ctjzmlBBVqunXmBkBbfPXrPYkfpo53YU6IG7MR4KXw3iDbDsse8br5seyzBjwRQQXy7vy5ZHJN4sY5QPjmeZeHizMie08y_EEE6mdiFytY79OJJk9h4iw-jwxqnF3kmw9BoTRTySKPr8_85sidMjLvLyOnZP4=w932-h629-no

Kulia waliokaa: Abdul Mtemvu, Wendo Mwapachu, Kedi.
Kulia waliosimama: Mwandishi, Yusuf Zialor, Kleist Sykes,
Bubby, Abdallah Tambaza
(1968).

Katika picha hiyo hapo hayo majina katika nyekundu yanajieleza,
wazee wetu ni maarufu katika historia ya AA, TANU na kupigania
uhuru wa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom