Kumbukumbu ya kuzama kwa MV Bukoba tarehe 21 May, 1996

Kumbukumbu ya kuzama kwa MV Bukoba tarehe 21 May, 1996

Kuna jamaa alikua fundi seremala kipindi hicho na nilimpatia oda ya kitanda. Alipotea ghafla na siku nilipokutana nae huyo bwana alikua tajiri wa kutisha.nilimkumbusha oda yangu na advance niliyompa akaenda kuninunulia kitanda kipya on the spot.
Ouch!
 
Poleni sana wote mliofikwa na janga hili,poleni watanzania wote pia, Mungu azidi kuwapumzisha kwa amani wapendwa wote [emoji25].Miaka 22 sasa
 
Miaka 19 leo, Mungu alaze roho za marehemu mahali pema peponi.

Hesabu zenu mnapigaje leo ni miaka 22 tangu wapendwa wetu watwaliwe katika ulimwengu huu, huwa sitaki kukumbuka hii siku, nilichokionaga nyamagana......acheni Mungu aitwe Mungu
 
Kuna jamaa alikua fundi seremala kipindi hicho na nilimpatia oda ya kitanda. Alipotea ghafla na siku nilipokutana nae huyo bwana alikua tajiri wa kutisha.nilimkumbusha oda yangu na advance niliyompa akaenda kuninunulia kitanda kipya on the spot.
Kaaazi kweli kweli
 
je tumeweza kujifunza lolote kutokana na ajali ile?hakika ni blah blah tu, walale kwa amani wahanga wote wa ajali ile, lakini vile vile napenda kuwapa pole nyingi na faraja wale wote ambao waliondokewa na wapendwa wao, na kuondoka kwao likawa pigo kubwa, Mungu wa rehema nyingi azidi kuwatia nguvu na ujasiri wa kusonga mbele, aamen
hivi leo hii likitokeaj janga kama hili tuna vifaa na wazamiaji wetu wenyewe?
Hakika hatukujifunza lolote na leo tumewapoteza tena wapendwa wetu wengi!
 
Maswali magumu sana..Serikali imefanya nini kuepusha ajari za namna hii? Je imeweka kitengo cha uokozi kama ikitokea Meli ikazama ziwani jinsi ya kuokoa watu? Je Bandari za Bukoba na Kemondo zimeimalishwa kuzuia watu wasiokuwa na ticket na wazamiaji kupanda Meli?..Je MV Victoria imefanyiwa lini matengenezo makubwa ili kuokoa roho za watu zisije angamia tena?..Usafiri wa Basi toka Bukoba kuja Mwanza ila changamoto ya Kivuko inajulikana? Kuna mhindi "inasemekana" alipiga simu Mwanza kwa wenzie na kutangaza mtu atayeokoa Maisha yake atapewa Nusu ya Mali zake ndo maana Wajanja wakakikimbilia kutoboa meli ili kumuokoa ili waweze kutajirika...Je serikali iliwachukulia hatua gani hao walitoa uamuzi wa kutoboa meli na kusababisha izame kabisa!??

Wapumzike kwa Amani watu wote walitangulia mbele ya haki!!!
Inasikitisha sana! Ifikie mahali tujifunze kutokana na makosa, tutaendelea kupoteza wapendwa wetu mpaka lini?
 
Inasikitisha sana! Ifikie mahali tujifunze kutokana na makosa, tutaendelea kupoteza wapendwa wetu mpaka lini?
Tusiache kuwakumbusha maana wajibu wetu ni huu.. Mungu awapumzishe kwa amani walitangulia na Mv Nyerere..Inaumiza sana kupoteza nguvu ya Taifa namna hii
 
Mv bukoba enz za uhai wake
tapatalk_1558384342082.jpeg
 
Kazi yake mola haina mokosa...
Na kila mmoja atatoka kwenye dunia hii kwa staili yake peke yake..
 
Leo ni mwaka wa 23 tangu ndugu zetu mamia walipo tutoka kwa kuzama kwenye ziwa Victoria wakiwa ndani ya meli ya mv Bukoba mwaka 1996

Naomba tuwakumbuke angalau kwa kusema Amina.

FB_IMG_1558421765131.jpeg
 
Back
Top Bottom