Katika kumbukumbu za mwaka huu, ni vizuri seriali ikaweka wazi kilichotokea badala ya kuwafumba watu n akuishia kusema Marehemu walazwe pema wakati kuna mengi ya kujifunza.
Si kwa vyombo vya majini bali kila chombo cha usafiri.
WAtu waliokufa ni wengi zaidi ya 800.
Meli ilioveload watu na mizigo kupita uwezo wake kwa hesabu isiyosemekana kana kwamba hapakuwa na wataalamu, wala chombo cha kusimamia compliance and usalama wa wateja.
Jambo hili linatokea kila sehemu hata katika mabus na daladala. Utakuta makondakta wamejaza abiria na mizigo ndani ya basi la abiria. WAsimamizi wako barabarani kuongea na wafanyakazi wa mabus pembeni na kuruhusu gari kuondoka bila kuzingatia usalama wa abiria. Ikitokea ajail iwatu wanakufa kwa kugongwa na mizigo ama kufunikwa na kushindwa kujiokoa. Matumizi ya malori ya midanani yakiwa yajeaza mizigo na abiria juu!. Pikipiki na ubebaji wa mishkakki. Bodaboda kuendeshwa bila kufuata taratibu kwa maana ya kuchomekea kulia kushoto, kati kati ili mradi anakwenda bila kujua athari zake kwa mwendeshaji na abiria wake huku wasalama wakiona kawaida.
MV Bukoba ilikuwa meli lya miaka mingi na kila wakati ilikuwa katika matengenezo including siku ya ajali. Matumizi ya vyombo vibovu katika usafirishaji ni tatizo. Hili ni pamoja na daladala, mabusi, ndege n.k. Serikali kuruhusu ununizi wa vitu vichovu bila kuwa na kiwango cha mwisho cha uchakavu. Kulipisha kodi kubwa kwa muagizaji wa chombo kibovu hakuwi mbadala wa usalama wa watumiaji wa chombo hicho. Matumizi ya magari mabaya, machovu, machkavu na yasiyofaa kwa kusarifisha abiria mijiini na vijinini ni kuvundika mauti. Utakuta gari limechunika maviti hayana mavazi, nondo zimejaa kutu, uchafu n aharufu iliyokithiriri, hadi mende, kunguni na kila aina ya ubaya lakini wasimamizi wa usafiri wanachojali awe amelipia njia na leseni, bila kuzingatia abiria wanaathirikaje. Ifike mahali chombo chochote cha kubebea watu kinapokuwa kimechakaa, hata kama engine inaonekana nzima , kipigwe marufuku kutumika. Auze scraper ama akifanyie ukarabati na uthibitishwe na wataalam kwamba liko katika kiwango sahihi kwa matumizi ya bidamu.
Serikali isioykubali kushauriwa na kukosolewa ni mzigo mzito. MV bukoba ilivyoanza kuzama, Genji aliwaona akasema anazo boat zake mbili zisaidiane moja ivute kwa mbele nyingine ibaki nyuma ya meli ili kwa pamoja ziisogeze meli kweli maji mafupi kwa sababu ilikuwa karibu na pwani. Wenye wammlaka wakakataa msaada na ushauri huo sijui kwa ego au hofu ya nini. Wakasema wataalmu wanakuja toka Dar Es Salaam watakuja shughulikia as if kwamba kama wangeliikuta meli imezogezwa kwenye kina kifupi cha maji wasingeonyehs umahili wao.
Bahati mbaya utaalamu ukabuma. Wakatoboa meli na hiyvo kuboresha kasi ya kuzama na hivyo kuliltea taifa na hsa wananchi hasara isiyosahaulika ya kupoteza ndugu na mali kiasi kischosemekeana.
Srikali ijifunze kufahamu kwamba uongozi ni dhamana. And ukpewa uongozi haina maaan wewe una uelewa wa mambo yote kuliko watu wote unaowangoza. Kiongozi mzuri ni yulte anatumia vipaji, uwezo na kila nyenzo walizonazo anaowangoza na kila maarifa yaliyopo ili kufikia malengo yaliyokubalika. MV Bukoba, laiti mamlka ingtetambua uzalendo wa Genji, na kupima wazo lake badala ya kuangalia nani anasema kama tunavyoona leo kwa wabunge wa ccm na bunge lao vile wanafanya, wananchi wasingepoteza maisha kwanye MV. Wataalam wangetoboa na kuwatoa watu bila kuwazamisha.
Ubishi, majivuno, ego, ubinafsi, dharau, na umbumbumbu wa wenye mamlaka na mitazamo mibovu inaligharimu taifa. Kina vipaji vingi, maarifa, uwezo, elimu, utaalam na nia njema za kutisha kama zingelipewa nafasi kwa usimamizi sahihi zikatumika katika kuboresha nchi yetu, bila shaka tungelikuwa mbali na kwa kasi ya ajabu.
Ninaomba kwa hili la Mwaka huu tusikumbukie MV kwa kuweka mashada baharini ila atuwe wakweli kuchukua mafunzo kwa ajili ya maisha yetu.[Umenigusa