Nyaka-One
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 4,730
- 6,736
Namkumbuka sana huyu mzee. Na mke wake Mwalimu Makoye.namkumbuka mzee makoye, meneja wa tanesco mwanza kipindi hicho
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Namkumbuka sana huyu mzee. Na mke wake Mwalimu Makoye.namkumbuka mzee makoye, meneja wa tanesco mwanza kipindi hicho
Na katika hiyo ajali kuna bwana mmoja miaka kadhaa nyuma alikuwa kamwambia baba yake katika ugomvi wao kuwa "Mimi si mwanao tena. Hata nikifa usinizike". Mzee nae akamjibu "Haya. Na sitakuzika mwanangu". Matokeo yake yule bwana hakuzikwa kweli na baba yake kwa sababu alikuwa ni mmoja wa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo lakini mwili wake haukupatikana kabisa.Hii ajali imenikumbusha usemi wa baadhi ya watu wanapogombana aliyechukia zaidi humwambia mwenzake HATA NIKIFA SITAKI UJE KUNIZIKA. Inabidi usemi huu ukome kwa sababu waweza zama baharini na wala mwili wako usionekane na huta zikwa kweli.Mungu awapumzishe kwa amani waliokufa kwa ajali hii.
Haya mambo buana achana nayo, Serikali imelala doro wamemuachia Matata.Hivi hii siku ya kumbukumbu ya ajali ya MV Bukoba kwa sasa imeachwa chini ya usimamizi wa Flaviana Matata Foundation au bado serikali inatimiza wajibu wake ipasavyo kwenye haya maadhimisho?
Yule mmiliki wa vivuko vya kamanga wakati ule alipinga kabisa wazo la kutoboa meli, alitaka ivutwe mpaka maji mafupi, Lakini hao magenius wetu walifosi matokeo yakawa hayo tena...hii meli ilizama basi tu sababu ya umasikini wetu,ilikuwa inazama taratibu km tungekuwa na vifaa vya uokoaji naamini wangepona watu wengi sana.Halafu mbaya zaidi akatokea "genius" akashauri itobolewe!, yani wenyewe ndio tukaharakisha upotevu wa uhai wa watu wetu?!
...so sad indeed!
R.I.P.
....tutawakumbuka daima.
Hivi hii siku ya kumbukumbu ya ajali ya MV Bukoba kwa sasa imeachwa chini ya usimamizi wa Flaviana Matata Foundation au bado serikali inatimiza wajibu wake ipasavyo kwenye haya maadhimisho?