Kumbukumbu ya kuzama kwa MV Bukoba tarehe 21 May, 1996

Kumbukumbu ya kuzama kwa MV Bukoba tarehe 21 May, 1996

Miaka 19 leo, Mungu alaze roho za marehemu mahali pema peponi.
 
Siku kama yaleo hii 21.5.1996. Nisiku ambayo ndugu zetu wapendwa,baba zetu,mama zetu,kaka zetu,dada zetu,wadogo zetu na jamaa na marafiki wanapoteza maisha yao ktk ziwa victoria,kufuatia kuzama kwa meli hii ya mv bukoba.ni majonzi makubwa sana.Tunakukumbusha rais wetu mpendwa jk kabla huja ng'atuka mwaka huu 2015 tunakuomba utufute machozi sisi watanzania hasa wa kanda ya ziwa kwa kutimiza ahadi yako ya kutununulia meli kubwa ktk ziwa victoria.Tutawakumbuka sana ndugu zetu wapendwa waliotutoka .
 
Tumejifunza nini kwa tukio kama hili? Mungu wapumzishe kwa amani marehemu wote
 
Kila nafisi ipumzike mahali inapostahili, ajari kama hizi ziwe funzo kwa wasimamizi wa sheria za usalama wa vyombo vyetu vya usafiri.
 
Wakati tukiendelea kuwakumbuka ndugu zetu waliopoteza maisha baada ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba!

Tunaikumbusha serikali itekeleze ahadi iliyotolewa na rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa ya kuwapatia watu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa meli mbadala ya iliyozama, maana hata iliyokuwepo MV. Victoria, hivi sasa inasumbuliwa na homa kali ya malaria!!!
 

Attachments

  • MV BUKOBA.jpg
    MV BUKOBA.jpg
    9.3 KB · Views: 805
Kazi kwelikweli ila ngoja tuwasubiri na ahadi za mwakahuu tuone maana wamekalili watz wajinga kila siku, mwakahuu hata wakikaa magogoni mwezi wa 11 wakuwa wamejifunza vitufulani
 
Mimj mpaka leo najiuliza ni akili gani ilitumika kuitoboa meli ikiwa kwenye maji ,bado inaelea na ndani bado kuna watu ?....physics ya wapi sijui hiyo
 
mungu awape raha ya milele marehemu wote wa ajali hii.aendelee kuwapa amani wwatanzania waliopoteza wapendwa wao
 
Wapo wanaodai ilikua kafara ya mkapa ctaki kuamin juu ya hilo
na kumbuka nilimpoteza mjomba Wang Aliamin abubakary kachwamba...mungu amulaze mahali pema peponi.. ameen

ni ubovu wa chombo uchakavu kukosa umakini wa wahusika
 
Wapumzike kwa amani marehemu wote,kwakweli ni tukio la kusikitisha hasa kwa watu waliopoteza ndugu na jamaa zao katika ajali hiyo.
Nakumbuka familia ya Lutanjuka
aliyekuwa principal wa chuo cha benki iringa
ilipotea yooote.Walikuwa wakitoka msibani.
 
JK alisema atawapa meli mpya wamefikia wapi

Tuliambiwa kuna ahadi za mgombea na ahadi za chama. Hiyo ya meli ilikuwa ahadi ya mgombea, sio lazima itimizwe na hamtamfanya kitu kwa vile atakuwa Msoga anachunga mbuzi ukwereni
 
Sitoisahau siku ile. Mungu aendelee kuwapumzisha wahanga wote kwenye mwanga wa milele.
 
Back
Top Bottom