Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi majuzi niliipanda MV VICTORIA, meli pekee ya abiria iliyosalia kwa safari za Mwanza - Bukoba, aisee ni majanga! Meli hiyo ikiendelea kufanya safari zake bila kufanyiwa ukarabati wa hali ya juu, watanzania tujiandae kupokea msiba mkubwa kuzidi ule wa MV BUKOBA! Eee.. Mungu baba igutushe serikali na ikaikarabati meli hii, nayo ikaepusha janga la kupoteza roho za watanzania wengine wengi zaidi, kwani meli hii ni kubwa na inabeba abiria wengi zaidi ya ile MV BUKOBA!
kiswahili kinakupiga chenga ,unajua maana ya "wahanga"
Mungu uwapokee wote waliopoteza maisha siku hiyo
Inahusianaje na kuzama kwa meli!?
Serikali ya ccm au?Je, kwanini serikali haifanyii kazi mapendekezo ya tume ya M.V Bukoba?
na wengineo wote!!mama yake na flaviana Matata,Antony matata, binamu yangu T-Mjahili Mungu awarehemu
ameen...miaka 20 sasa.Wapumzike kwa aman ndug.zetu
Umenikumbusha Mwalimu Paschal. Bado yupo Nyamagana?Hii ni kumbukumbu nzito sana. Wakati huo 1996, nilikuwa nasoma darasa la saba Nyamagana primary school na nilikuwa nasoma darasa moja na Haji Rume, Mtoto wa captain wa meli hiyo. Alikuja mwalimu mkuu, Mr. Paskal na kwa sauti akaita...Haji, Kuja hapa Baba!!....na kumpa taarifa ya ajali. Darasa lilitahamaki kwa taarifa hizo na wakati huo kama mnajua Nyamagana primary school iko pembeni ya kilima. Wanafunzi wengi tulienda kilimani angalau kuweza kuangalia ziwani kama tunaweza iona meli hiyo kwa mbali.
Kwa muda wa week nzima maeneo ya nyamagana yalizizima na shule ilikuwa haisomeki tena....Kibaya zaidi, kulitokea report ya misiba mingi mtaani nilioishi....
Wapumzike kwa amani..