Kumbukumbu ya kuzama kwa MV Bukoba tarehe 21 May, 1996

Kumbukumbu ya kuzama kwa MV Bukoba tarehe 21 May, 1996

Had I
View attachment 159510
Meli ikiwa inazama na ikiwa imezungukwa na mitumbwi pamoja na boti ambazo zilisaidia kwenye uokoaji

RIPOTI ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha ajali ya mv Bukoba, inasema usiku wa kuamkia siku ya ajali, meli hiyo ilipakia abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37.

Kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana.

Kila mwaka, ifikapo Mei 21, serikali inayosema haina dini, huongozana na viongozi wa madhehebu ya dini na waganga, kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu.

Serikali ilishitaki aliyekuwa nahodha wa mv Bukoba, Jumanne Rume-Mwiru, (sasa marehemu), Mkaguzi wa Mamlaka ya Bandari Gilbert Mokiwa; aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Bukoba, Alphonce Sambo, na aliyekuwa Maneja wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila.


View attachment 159511
Meli ya Mv Bukoba ikiwa inazama.

Kesi hiyo Na. 22 ya mwaka 1998, ilianza kusikilizwa Mei 14 mwaka 2001. Miongoni mwa waendesha mashitaka katika kesi hiyo ni Eliezer Feleshi.Hukumu ya kesi ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Juxton Mlay (sasa mstaafu), Ijumaa, 29 Novemba 2002, majira ya saa sita mchana.

Washitakiwa wote walishinda kesi, kufuatia hukumu ya kurasa 118 iliyosomwa kwa dakika 160 na Jaji Mlay kusema, mv Bukoba ilizama kwa sababu haikuwa na uwiano wa majini na siyo uzembe wa washitakiwa.

Serikali iliahidi kukata rufaa; lakini hadi leo majaliwa ya rufaa hiyo hayajulikani; na baadhi ya washitakiwa wamefariki dunia bila kujua hatma ya kesi hiyo wala stahili zao.

Kwa kipindi kirefu, mv Bukoba ilikuwa ‘kaburi' lenye kuelea katika Ziwa Victoria. Ilikwishapigwa marufuku kufanya safari kwa kuwa haikuwa na viwango vya ubora wa kuwa majini.


View attachment 349558
Makaburi ya Igoma ambako wahanga wa Mv Bukoba walikozikwa

Meli hii ilijengwa na kampuni ya Kibelgiji; ikazinduliwa 27 Julai 1979. Siku ya uzinduzi, ilibainika haikuwa thabiti na ilikosa uwiano.
Hadi leo sitasahau marehemu 332 kwamba hawakupatikana..
Huzuni ilitanda nchi nzima.
Pia ilitoka taarifa ya kutokula Samaki kwa kipindi fulani.
Serikali iwe makini na wakandarasi wanaounda miundombinu ya kujenga Meli mpya pia wakati wa uundaji vipimo vizingatie hesabu na michoro..
 
MIAKA 23 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?
by MASSHELE


MAAFA YA MV BUKOBA
KILA KIFO NA SIKU YAKE

May 21 kila mwaka tunakumbuka maafa ya MV BUKOBA 😿
Kila binadamu atakufa, lakini kila kifo kina siku yake. Nyaisa Simango, katika makala haya ana tudhihirishia hivyo. Vinginevyo ni vipi mtu anaweza kuelezea alivyo nusurika wakati mamia ya wenzake walio kuwa katika meli moja walishindwa kujiokoa. Ilikuwa sio siku yake.
Ziwa victoria limekuwepo kwa karne na karne, watu wanaoishi kuzunguka ziwa hilo wamekuwa wakijishughulisha na shughuli mbalimbali. Kuvumbuliwa kwa Ngalawa, Jahazi, Boti, na meli kumewezesha kazi za usafirishaji kuwa rahisi.
Bila shaka Simango alipo itwa na mkuu wake wakazi na kuarifiwa kuwa itabidi aende Bukoba kumpeleka mfungwa kusikiliza rufaa ya kesi yake alifurahi kwani angeweza kuona mandhari nzuri njiani. Ijapokuwa yeye anatoka katika nmkoa unao pakana na ziwa bado angefurahia kula samaki. Nakwavile hakuwahi kufika bukoba, safari ingempa fursa nzuri ya kutalii mjini huko, na pia baada ya kumfikisha mfungwa huko alikotumwa na yeye angepata fursa nzuri ya kwenda kijijini kwake kuwatembelea jamaa. Inawezekana hayo yote yalimjia katika fikra zake
Kwahiyo safari yakwenda mwanza haikuwa na mashaka yeyote.
Ugumu wa safari ya kwenda Bukoba ulianza pale alipofika forodhani Mwanza, kwani waliokuwa wanaingoja MV BUKOBA walikuwa wengi kupindukia. Tofauti na safari ya barabara ambapo ikitokea ajali, na mtu kama hakuumia sana , anaweza kujizoa zoa na kwenda zake, ajali ya baharini inabidi mtu ajue kuogelea. Nyaisa alikuwa hajui kuogelea
MV BUKOBAilifika bukoba, lakini katika safari ya kurudi haikufika Mwanza, bali ilizama na kuteketeza maisha ya mamia ya watu. Ilikuwa ni moja ya ajali kubwa kutokea nchini na hata Afrika ya masharikui.
Nyaisa amejaribu kutuelezea hapa ninini kilitokea wakati meli inazama polepole. Lakini sidhani kwamba hata yeye ameweza kuipata taswira kamili ya nini kilikuwa kinatokea katika meli nzima, kwani yeye binafsi alikuwa katika hekaheka ya kuokoa maisha yake.
Taifa lilipigwa na butwaa, vilio vilisikika kutokea pande zote za nchi. Na cha kusikitisha zaidi nikule kutokuwepo kwa uwezo wa haraka wa kuwaokoa watu walio kuwemo kwenye meli ile. Hata nchi jirani hazikuwa na nyenzo za uokoaji. Afrika ya kusini ilisaidia, lakini masafa yanayo tenganisha nchi hizi mbili pamoja na kutoweza kuleta vifaa kwa haraka ili kuisimamisha mele hii isizame kabisa haikuwezekana, maisha ya wale waliokuwemo ndani ya meli wakaangamia. Tukabaki tukishuhudia maisha ya wananchi wenzetu yakiyoyoma . Sura kamili ya umasikini na udhaifu wan chi ilionekana.
Maafa haya yalikuwa ni pigo kubwa kwa serikali ya awamu ya tatu iliyo ongozwa na raisi Benjamin Mkapa, kwani ilikuwa bado haijatimia hata mwaka mmoja tangu iundwe kwahiyo bado ilikuwa katika fungate. Taifa lili ukabili msiba huu kwa ujasiri mkubwa. Maelfu ya wananchi wa kawaida, viongozi wa kidini, kijamii na kisiasa , wakuu wan chi, na baba wa taifa wote walimiminika mwanza kuomboleza. Na mazishi ya wale walioweza kupatikana yalifanyika Igoma nje kidogo ya jiji la Mwanza. Kuna wengi ambao Mv bukba ilibidi iwe kaburi lao
Kuna mengi ambayo taifa ilibidi lijifunze kutokana na tukio hilo kubwa, lakini je tumejifunza chochote?
Sehemu zilizo unda MV BUKOBA, zilitengenezwa Ubelgiji na kuja kuunganishwa mjini mwanza, mnamo mwaka 1978, na meli hiyo kuanza kazi mnamo mwaka 1979. Kiwango cha abiria ambacho kilitarajiwa kuchuliwa na meli hiyo ni abiria 400 tu na wafanya kazi 36 na tani 200 za mizigo. Hati ya usalama ya kusafiri baharini ( serficate of seaworthiness) ambayo meli hiyo ilikuwa nayo iliruhusu abiria 400, wafanya kazi 22, na tani 85 za mizigo.
Lakini meli hii ilikuwa na abiria mara mbili zaidi ya hao. Mbali na shehena ya mizigo iliyo kuwemo, hatujui kama meli hiyo ilikuwa ikikaguliwa kila wakati, na kufanyiwa matengenezo kikla inapo bidi. Simango anatueleza wazi kuwa wakati inaondoka Mwanza kwenda Bukoba ilionesha wazi uchakavu wake na kwamba ilikuwa katika hali mbaya. Sasa ilikuwaje meli hiyo ikapata hati ya kusafiria (sertificate of sea worthiness) linakuja pia suala la uadilifu na uamunifu wa nahodha wa meli hiyo. Ilikuwaje akachukua dhamana ya kuendesha meli iliyojaa abiria na shehena kubwa ya mizigo kwa kiasi hicho wakati meli ilionesha wazi kuwa sii madhubuti?
Serikali chini ya ibara ya 266 ya sharia ya meli za kibiashara ya mwaka 1967 (merchant shipping Act , 1967) iliunda tume ya watu 13 ikiongozwa na jaji wa mahakama ya rufaa, mh, Robert Kisanga, kuchunguza sababu ya ajali ya meli ya Mv Bukoba. Tume hiyo ilizinduliwa na waziri wa mawasiliano june 13/1996.
Kwanza alipewa wiki sita kufanya kazi hiyo, na kuongezewa wiki mbili. Ripoti iliyotolewa na tume hiyo ilikisia kwamba watu waliokufa kutokana na ajali hiyo walifika 700 na walio nusurika walifika 114, na meli ilitoweka katika macho ya dunia
Ripoti inaonesha kwamba utaratibu wa kununua Mv Bukoba ulipingana na taratibu za kimataifa kwamba serikali na shirika la reli nchini (TRC) HAVIKUMLAZIMISHA MTENGENEZAJI WA MELI KUITENGENEZA KWA MUJIBU WA MATAKWA YA NCHI
Mtu anaweza akafikiria kwamba kumbe haya tunayo yaona leo kuhusu machimbo ya madini, TANESCO, IPTL, na kadhalika yalianza zamani? Bila ya kutaka kuitetea serikali ya awamu ya kwanza au waziri wa mawasiliano na uchukuzi wa wakati ule mh Amir Jamal, bora ikumbukwe kwamba, katikati ya miaka 1970 ndipo jumuiya ya Afrika mashariki ilipovunjika.
Nchi ilikuwa katika wakati mgumu wa kuendeleza huduma zilizokuw azikitolewa na jumuiya wakati ule kama usafiri wa ndege, bahari, reli, nk. Kilichokuwa katika nchi moja hakikuvuka mpaka. Ndio maana , labda, baadhi ya mikataba ya wakati ule ya kununua vitu kama vile MV BUKOBA, au kukodi ndege ilikuwa haina miguu wala vichwa.
Lakini cha kujiuliza ni, nini kimefanywa kwa takribani miaka 20 tangu meli ile ilipo nunuliwa mpaka kuja kuzama? Ripoti inaonesha kwamba shirika la reli la taifa( TRC) ilikuwa ikijua fika juu ya hitilafu zilizo kuwemo katika meli
Lakini badala yake shirika liliingia katika mlolongo mrefu wa barua na watengenezaji wa meli na hayo hayakuleta tija yeyote mpaka meli hii ikizama. Ripoti inaonesha dhahiri kwamba katika shirika la reli la taifa ambalo ndilo lililokuw alikiendesha MV BUKOBA, MV victoria na meli nyinginezo, milkuwa na uzembe, ubadilifu na kulijaa rushwa.
Ripoti ya tume ya jaji kisanga imelaumu wengi kwa ajali hii, shirika la reli la taifa (TRC) watengenezaji wa meli ubelgiji, BSC na serikali ya Ubelgiji kwa kuto timiza ahadi ya kutoa misaada katika kugharamia matengenezo ya meli yenyewe.
Taswira aipatayo mtu ni kwamba kulikuwa na hali ya kutojali kwa upande wa uongozi wanchi na kwa upande wa wafanyakazi wa MV BUKOBA na maafisa usalama wa TRC. Kulikuwa na hali ya kutojali kuwakamua wananchi mpaka tone la mwisho la damu yao kwakuwa kulikuwa na shida ya usafiri.
Kwenye nchi zinazoenzi demokrasia na utawala bora ajali kubwa mfano wa MV bukoba, viongozi huwajibika, na wanapo sitasita, basi wakuu wao huwawajibisha au wananchi, kwa kelele zao huwataka wawajibike.
Itakubukwa kwamba ilipotokea vifo vya watu wawili walio wekwa rumande na polisi kule Mwanza, waziri wa mambo ya ndani wa wakati huo, mzee Ally Hassan Mwinyi (Ambaye alikuja kuwa raisi wa zanzibari na Tanzania alijiuzulu) pamoja na waziri aliye husika na usalama wa taifa na mkuu wa mkoa wote walijiuzulu na raisi Julius Nyerere akawakubalia.
Walipotoroka watuhumiwa wawili wa kesi ya uhaini katika gereza la Ukonga na kukimbilia Kenya, waziri wa mambo ya ndani ya wakati ule Maj-Gen Said Abdalah na mkuu wa gereza la Ukonga walijiuzulu na raisi akawakubalia . Kinacho staajabisha umma na ulimwengu kwa ujumla wakati ilipo tokea ajalia ya Mv BUKOBA, sii waziri wa mawasiliano wala uchukuzi wala mkurugenzi mkuu wa TRC walio ona haja ya kujiuzulu.
Kikubwa zaidi ni kwamba raisi wa nchi ambaye ndiye aliwateua watu hawa hakuona haja ya kuwawajibisha . Kelele za wananchi na vyombo vya habari za kuwataka viongozi hao wawajibike zilipuuzwa. Kujiuzulu kwa waziri hakungekuwa na maana kuwa alihusika moja kwamoja katika ajali ile, bali ni ustaarabu uliojengeka katika nchi nyingi duniani(political responsibility)
Ajali ya Mv Bukoba imeonesha wazi kabisa kuwa nchi yetu haikujiandaa kwa maafa kwanamna yeyote ile. Ijapokuwa kumekuwepo na sharia na 9, ya mwaka 1990 ya utaratibu na utoaji wa misaada ya maafa na kuundwa kwa kamati ya maafa ya taifa.
Sera ya maafa inaeleza kwa ufasaha sana kuwepo kwa kamati ya maafa , kamati ya kitaalamu, asasi ongozi, timu ya kukabili maafa, na kadhalika . lakini kila yatokeapo maafa vyombo hivyo havionekani wala havisikiki. Sijui kama viwanja vya ndege vya Kilimanjaro, pemba na tanga vimejiandaaje na janga lolote linaloweza kutokea
Nyaisa anafaa kushukuriwa kwa kazi hii nzuri na adhimu kunusurika kwake kutokana na kifo andiko kumetuwezesha leo kujua nini ni kilitokea.
Ikiwa hatujajifunza kutoka na makosa yaliyofanyika na kusababisha ajali hii, basi Tanzania itakuwa ni taifa lisilojifunza na lisilotathimini maisha ya watu wake. Waswahili husema kosa haliwi ni kosa isipokuwa likiwa limerejewa.

Prof Haroub Othman
Chuo kikuu cha Dar es salaam
Agost , 2007.

My contacts +255766605392 mwandishi
 
Sasa hiv usafiri wa meli Kati ya bukoba na mwanza umekufa kabisa.
 
Mpaka leo tunasubili yale yaliyohaidiwa kupata usafiri uliyo imara ziwa Victoria lakini tunabaki kwenye ahadi hatuoni kuimarisha meli ya MV VICTORIA wananchi wa Kagera usafiri bado ni wa ghari vitu ni ghari kwa kutumia usafiri wa barabara.Wakina mama waliokuwa wanafanya biashara yao ya ndizi,samaki,maharage ,kahawa nk kati ya Bukoba na Mwanza hawawezi mzunguko wa hela huko chini sana Kagera imebaki masikini,tunaomba viongozi wetu watuonee huruma warudishe haraka usafiri wa meli zilizo imara haraka maana Kagera tunaumia .
 


Leo ni kumbu kumbu ya kuzama kwa meli ya mv bukoba bonyea link kusikia zaidi
 
Tarehe 21 Mei 1996 ilizama kwenye njia ya kuelekea Mwanza.[2] Abiria wengi walikufa na idadi yao imekadiriwa kuwa 1,000 hivi, lakini idadi iliyotangazwa rasmi ilikuwa 894.
 
wapumzike kwa Amani marehemu na pole ndugu na jamaa kwa kupoteza wapendwa wao
 
Nakumbuka siku hii kabla RTD hawajatangaza hili tukio tayari nilishaliona kwenye tv ya CNN
 
Nakumbuka taarifa tuliipata tulipotoka mapumziko ya saa 4, nilikuwa form 3!
 
HIKI NDICHO CHANZO CHA AJALI YA MV BUKOBA.

Ajali hii ilitangazwa kuwa ni msiba wa kitaifa na kufuatia rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, kutangaza siku tatu za maombolezo na bendera kupepea nusu mlingoti.

Meli hiyo ambayo ilizinduliwa mwaka 1979 na Rais wa kwanza wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Nyerere, ilidumu kwa miaka 17 tu, na kupinduka ikiwa katika safari zake za kawaida, ikitokea katika bandari ya Bukoba kupitia Kemondo.

Meli hiyo ya MV Bukoba ilipinduka na kuzama ndani ya Ziwa Victoria Siku ya Jumanne alfajiri Mei 21, 1996. Kuzama kwa meli hiyo kulisababisha watu zaidi ya 800 kupoteza maisha baada ya kufa maji.

MV Bukoba ilizama ikiwa imebakisha umbali wa maili moja na nusu ili iweze kutia nanga katika bandari ya Mwanza Kaskazini, hali ambayo ilikwishawapa abiria matumaini ya kufika salama kwa abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo.

Ilikuwa tayari iko jirani kabisa na ufukwe wa Shule ya Sekondari Bwiru, ambako sasa kumejengwa mnara wa kumbukumbu ya wahanga wa ajali hiyo mbaya kuwahi kutokea katika Ziwa Victoria. Ukosefu wa vifaa vya kuokolea majini ulikuwa ni chanzo cha kuongezeka kwa vifo vya abiria, waokoaji wa ajali hiyo walisubiriwa kufika nchini kutokea Afrika ya Kusini, ambao waliweza kuogelea na kuokoa baadhi ya maiti chache zilizokuwa zimezama umbali wa mita 25 chini ya maji.

Ajali hiyo imebaki kuwa kumbukumbu mbaya kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa na mikoa jirani na Watanzania kiujumla. Kila mwaka ifikapo Mei 21 hapa Tanzania, siku hiyo hukumbukwa kwa kuomboleza vifo vya abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo.

Baadhi yao miili yao haikupatikana na kusababisha maziko yao kufanyika humo humo majini huku meli hiyo ikigeuzwa kuwa kaburi lao la pamoja.
Makaburi ya wahanga wengine yapo katika Kitongoji cha Igoma umbali wa kilometa nane kutoka katikati ya Jiji la Mwanza.

Katika ajali ya meli hiyo mali ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania (MSC) iliyokuwa chini ya Shirika la Reli (TRC), hadi leo bado ni kitendawili kilichokosa mteguaji, kuhusu idadi kamili ya abiria waliokuwamo ndani ya meli hiyo.

Yapo madai kuwa ilikuwa imebeba zaidi ya abiria 1,200 na mizigo iliyokuwemo ikiwa inakadiriwa kuwa zaidi ya tani 200. Inadaiwa kuwa watu 1,000 walipoteza maisha huku abiria 112 tu wakinusurika katika ajali hiyo.

Wakati tukielezwa kuwa meli ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 430, kwenye daraja la kwanza na la pili, wakati daraja la tatu ambazo kwa kawaida hubeba abiria wengi zaidi hakukuwepo rekodi yoyote.

Meli hiyo ambayo ilikuwa ya pili kwa ukubwa kati ya meli zinazofanya safari zake katika Ziwa Victoria, ajali yake iliacha simanzi na majonzi makubwa miongoni mwa familia nyingi ambazo ndugu zao walikuwa miongoni mwa abiria waliokuwa ndani.

Hadi sasa hakuna sababu rasmi zilizokwishatolewa na Serikali kuhusu chanzo cha ajali ya MV Bukoba ingawa wapo baadhi ya watu na viongozi wanaosema ilitokana na meli hiyo kujaza abiria na mizigo kupita kiasi, na kwamba ilikumbwa na dhoruba kali ziwani.

Meli hiyo ambayo ilijengwa na kampuni ya Kibelgiji, tangu kuzinduliwa kwake ilikuwa na tatizo la uwiano.

Aidha, yapo madai kuwa kabla ya safari hiyo ya mwisho kwa meli ya MV Bukoba ilikuwa mbovu, na hakuna mtu ambaye amewahi kutajwa kuiruhusu kufanya safari zake huku ikiwa mbovu, tofauti na kubebeshwa mzigo wa lawama nahodha wake, Jumanne Lume Mwiru ambaye alifunguliwa kesi na wenzake kwa kosa la uzembe, kusababisha vifo vya watu 400, kujeruhi na upotevu wa mali zisizofahamika.

Kesi hiyo iliahirishwa mara sita, baada ya kusikilizwa na hatimaye Ijumaa Novemba 29, 2002 aliyekuwa Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Mwanza, aliwachilia huru washitakiwa wote wanne.

Aliwachia baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka yao. Hukumu hiyo yenye kurasa 118 iliyoandikwa kwa mkono, ilisomwa kwa zaidi ya dakika 160, ikianza tangu saa sita mchana hadi saa tisa adhuhuri.
Washitakiwa wa kesi hiyo walikuwa nahodha huyo, Mkuu wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila, Mkuu wa Bandari ya Bukoba, Alfred Sambo, ambaye sasa ni marehemu na Mkaguzi wa Mamlaka ya Bandari (THA), Gilbert Mokiwa.

Kutokana na ajali hiyo, serikali iliunda SUMATRA kwa ajili ya kukabiliana na matatizo ya ajali ikiwa na lengo la kufanya ukaguzi kwa vyombo vyote vya usafiri wa majini na nchi kavu. Pamoja na kuwepo kwa chombo hicho, bado ajali zimeendelea kutokea kila kukicha.

Kuanzia mwaka 1996 ajali ya MV Bukoba na 2001 ajali ya treni, tumekuwa tukishuhudia ajali nyingi za majini na nchi kavu kama ajali ya meli ya MV Nyamageni iliyotokea Aprili 28 mwaka 2006 na kusababisha vifo vya watu 50 ambapo miili 6 ilipatikana nchini Uganda na wengine kutopatikana ikiwa ni pamoja na meli yenyewe, sasa kubwa zaidi ni ajali ya MV Spice Islander ambayo iliua zaidi ya watu 2000.

Pamoja na ajali ya MV Bukoba, ambayo haiwezi kusahaulika Mamlaka za kudhibiti au Kusimamia vyombo vya majini kama vile bandari, SUMATRA na mashirika mengine na hata wananchi wa kawaida bado hatujajifunza chochote. Tungekuwa tumejifunza kuhusu ajali hiyo ajali zingine zingeepukika na tungekuwa tunaziepuka kutokana na kwamba abiria tunapokuta chombo kimejaza kupita kiasi, yatupasa kusubiri kingine.

Hata hawa watu wa bandarini hizi meli, boti na mitumbwi zinapokuwa zinapakia abiria wao huwepo eneo hilo na pia tumekuwa tukishuhudia safari hizo zikiambatana na baadhi ya wafanyakazi wa vyombo vya dola, kwanini wasizuie mrundikano wa watu wengi wanaosafiri katika chombo kimoja.

Kwa mantiki hiyo ni kwamba serikali, mamlaka zinazoshughulika na usafiri wa majini, mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo pia yanashughulikia suala hilo pamoja na sisi wananchi wa kawaida, hatujajifunza lolote katika ajali ya MV Bukoba iliyotokea mwaka 1996 ambayo pamoja na kupoteza ndugu zetu wengi, tulilia, tukaomboleza na sasa tumesahau tukio.
 
Back
Top Bottom