Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
View: https://www.facebook.com/share/v/1B2qhgYhck/?mibextid=wwXIfr
Historia hii ya Mkapa kuchaguliwa kuwa mgombea ili ikae vizuri inahitaji utafiti kujua wagombea wengine mfano wa Kikwete wanasema nini kuhusu mchango wa Mwalimu katika ugombea wao wa kutaka kupendekezwa kupeperusha bendera ya CCM.
Hili la kwanza lakini inabidi pia uangalie hali ya siasa nchini ilikuwaje na hapa nakuomba tumwingize Prof. Malima kama mgombea Urais ambae hakuona haja ya kuungwa mkono na Mwalimu Nyerere.
Kabla ya kwenda mbele tujiulize kwa nini Malima hakwenda kwa Nyerere?
Hapa sasa tumtazame mgombea Augustino Mrema na chama cha NCCR Mageuzi ambae alikuwa anamwaga vumbi jingi.
Hapa sasa unakuwa na wagombea watatu: Mkapa, Kikwete na Mrema.
(Kwa makusudi kabisa simjumuishi Prof. Malima tutamleta baadae).
Hawa katika jamii ya wapiga kura unadhani kundi gani lilikuwa linawaunga mkono na kwa sababu zipi?
Wagombea hawa watatu wote walikuwa na agenda makhsusi ambayo wangewaeleza wananchi na walikuwa na baba wanaemtegenea.
Katika wagombea hawa mtoto yatima alikuwa Prof. Malima.
Agenda ya Prof. Malima ilikuwa tofauti kabisa na agenda za wagombea wenzake.
Agenda ya Prof. Malima lau alikuwa bingwa katika mambo ya IMF na World Bank hayo si aliyokuwa amenuia kuwaelezà wananchi.
Mwalimu Nyerere hili akilijua fika na lilimtisha kwani ni agenda ambayo wale aliowakuta katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika wakiitumia kupambana na ukoloni wa Mwingereza.
Agenda hii ilikuwa nyepesi mno kueleweka haivurugi akili kwa mtu wa kawaida Baba Kabwela kama kumweleza mikopo ya IMF na World Bank.
Hebu tutazame hali ya siasa Tanganyika ilikuwaje wakati ule?
Tanganyika ilikuwa katika mgawanyiko mkubwa wa kidini haujapata kutokea.
Nchi ingeingia katika uchaguzi katika hali hii kama Prof. asingefikwa na umauti wa ghafla kabla ya uchaguzi na yeye akiwa mgombea wa Urais wa Tanzania.
Wakulima na vyama vya wafanyakazi siyo khasa waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Vyama vya wafanyakazi vilivyokuwapo baada ya uhuru vilikuwa dhaifu sana na havikuwa na uwezo wowote wa kutingisha serikali.
Mkapa naamini akiujua ukweli huu na anawajua wapigania uhuru wa Tanganyika kwani wakati ule alikuwa kijana na kayaona yote kwa macho yake.
Swali kubwa la kujiuliza ni, "Je Mwalimu Nyerere na nchi kweli ilikuwa tayari kumpokea kwa mfululizo Rais Muislamu?"
Wala hili si la kupuuza kwani ni swali linalohitaji jibu la kweli.
Yaliyotokea Dodoma kwenye kura za kuwapitisha wagombea Urais wa CCM yanafahamika.
Kikwete alishinda duru ya kwanza.
Umepata kujiuliza kwa nini alishinda?
Umepata kujiuliza Mwalimu Nyerere aliupokeaje ushindi wa Kikwete?
Ushapata pia kujiuliza ingekuwaje kama katika uchaguzi wa Rais wa Tanzania Prof. Malima angekabiliana na Mkapa?
Inamisha kichwa kutafuta jibu.