Kumbukumbu za UDSM from 1970s to 1990s: Poisoned Letters na Mzee Punch

Kumbukumbu za UDSM from 1970s to 1990s: Poisoned Letters na Mzee Punch

Zamani walikua hawataki ujinga.

Vichwa vilikua sawa. Saiz umbea umbea tu na kujipemdekeza kiboya. Ushe.. nz na maujinga jinga tu mengi
 
Hao wanafunzi walikuwa hawana kazi ya kufanya zaidi ya udaku na umbea?

What is the point? Kuanika mbunye za watu hadharani?

Na mimi nashangaa ilikuwaje mpaka watu wajinga wakapata nafasi ya kufanya ujinga wote huo na bado wakaendelea kuonekana mashujaa?

Kama una tatizo na mtu fuata njia halali za kumuwajibisha zinazozingatia utu na sio kuanika ****** wake kwenye mbao za matangazo.

No wonder we have such people today. Mazombi zombi tu, udaku na upashkuna ndo kitu wanaweza.

Ukiwaambia wajenge barabara wanajikuna vinyeo, kumbe chuo kikuu walienda kusomea udaku na ushangingi.

Cc: Lamomy cocastic Seran ephen_ Monetary doctor Tlaatlaah
 
Alikuwa Jaji sasa huyo jaji ni nani?
Wanasema sio mtu ni crew...!
Na msanifu wa hizo michoro ni "mama yetu Tanzania" thus hakumaliza kabisa udsm (banned) na wengine...
According to radio mbao.
 
Kama hiko chuo ndio kimetoa wasomi wa nchi hii ndio maana nchi ipo ilipo sasa.

Waambieni watoto wenu wasifanye huo upuuzi na mkatubu.

🚮
 
Katika miaka ya 1980 na miaka ya nyuma yake, machapisho na barua za siri au za asiyekuwa na jina zilizokuwa zikifichua kashfa, udaku, na masuala mbalimbali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Mlimani) zilifahamika sana kama "Poisoned Pens" (au Poison Letters).

Mwandishi au waandishi wa machapisho hayo walikuwa hawatumii majina yao halisi na walibaki kuwa watu wasiojulikana (anonymous).
Sifa kuu za mwandishi/waandishi hao wa siri:
Mtindo wa Usambazaji:
Wsshkaji walikuwa wakiandika barua au vipeperushi hivyo kwa mashine ya chapa (typewriter) na kuvibandika usiku mzito kwenye mbao za matangazo (noticeboards) za mabweni na idara mbalimbali Mlimani, au kuvipenyeza chini ya milango ya vyumba vya wanafunzi na mihadhara.

Mada Zilizochapishwa: Barua hizo zilikuwa zikigusia kashfa za mapenzi kati ya wahadhiri na wanafunzi, tuhuma za rushwa ya mak certain (maki/alama), majungu ya ndani ya idara, na migogoro ya kisiasa na kiutawala chuoni hapo.

Sababu ya Kutojulikana: Kutokana na hofu ya kufukuzwa chuo, kuchukuliwa hatua za kisheria, au kufukuzwa kazi kwa wahadhiri na wafanyakazi, utambulisho wa waandishi hao ulibaki kuwa siri kubwa na waandishi hao walijulikana tu kwa majina ya bandia au kama sauti za siri za Mlimani.

Kisa cha Mr. Punch au Mzee Punch

"Mr. Punch" (au maarufu kama "Mzee Punch") hakuwa mtu mmoja halisi, bali lilikuwa ni jina la fumbo au kikundi cha siri cha wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM - Mlimani) kilichoendesha mfumo wa utamaduni wa fasihi ya ukutani (wall literature) kuanzia miaka ya 1970 hadi miaka ya 1990.
Hapa kuna mambo makuu kuhusu Mzee Punch:

Sifa na Utendaji Kazi: Kikundi hiki kilijifanya kuwa na uwezo wa kujua kila kinachoendelea chuoni ("Omnipresent & Omniscient"). Walikuwa wakiandika vipeperushi au michoro kwa kutumia mashine ya chapa (typewriter) au mikono na kuvibandika usiku sana kwenye kuta za cafetaria, mbao za matangazo (noticeboards), na mabwenini.

Dhumuni la Punch: Mwanzo lilipozuka, lilichukuliwa kama chombo cha kurekebisha maadili, kukosoa utawala, rushwa, au tabia zisizofaa chuoni. Hata hivyo, mara nyingi walilenga zaidi wanafunzi wa kike kwa kashfa na kejeli (kutoa majina ya uswahilini, kuwachora vibaya na kufichua siri zao za mapenzi au maisha binafsi).

Sheria 10 za Mzee Punch: Kundi hili lilikuwa na sheria zao (mfano: kutokaa kwenye meza ya Punch cafeteria, kutovaa malapa au msuli cafeteria, nk). Mwanafunzi yeyote aliyetenda kinyume alipigwa "Punch" (alilengwa kwenye machapisho hayo ya kashfa).

Athari na Mwisho wake: Kitendo cha "kupigwa Punch" kilileta shinikizo kubwa sana la kisaikolojia na aibu kwa waathirika, kiasi cha baadhi ya wanafunzi kuacha chuo. Baada ya tukio la masikitiko la mwanafunzi wa kike kujiua miaka ya 1990 kutokana na unyanyasaji wa Punch, utawala wa chuo ulichukua hatua kali za kisheria na nidhamu ambazo zilileta mwisho wa utamaduni huo Mlimani.


Mr. Punch/ Mzee Punch alikuwepo UDSM kabla halijalazwa jiwe la kwanza kwenye msingi wa jengo la kwanza la chuo.
CC:-
Pascal Mayalla
Na lugha, hakika walijua kuandika lugha/kingereza chenye viwango
 
Mzee Punch kilikuwa ni kikundi cha wanafunzi, ā€œWapanchiā€ na ni secret society

Inasemekana ilianzia mwaka 1970 hasa baada ya kucheleweshewa boom baada ya Nyerere kukataa kuogeza
Mzee wangu alimaliza hapo mwaka huo na kina Mu7 na ndiyo ilikuwa inaanza. Wengi walitoka Faculty of Engineering (FoE) a.k.a mafundi na wachache wa Law, Arts, etc a.k.a mangwini

Mie nilisoma 1990s tunaikuta inaanza kupungua nguvu na kufa baada ya Chuo kufungwa walipo mpanchi Mzee Mwinyi, enzi za kina James Mbatia

Ukijifanya kuwatafuta uwajue unawekwa kwenye ā€˜pipeline’ yaani next punch umatokea wewe, na wanaandika taarifa zako zote kuanzia kijijini, wazazi mpaka ndugu, kwa kashfa na matusi makubwa mno na kuutangaza mwili wako hasa kama ni mwanamke
Ukishakuwa kwenye pipeline au ukijaa kwenye punch wanafunzi wengi wanakutenga kuogopa wao wasiingie kwenye anga za ā€œMzeeā€

Kuna aunt yangu walimpiga punch kali sana miaka ya 80 , sasa yeye bint wa mjini hakujali akaenda kuicopy kama ilivyo na mpaka leo anayo na mpanch mmoja akawa mshkaji wake baada ya kumshuku na kutishia kumshtaki
Wanawake wenye misimamo walipigwa sana punch ila wengine walishindwa kuvumilia kama yule Levina Mukasa alijiua

Asubuhi mkiamka kama kuna Punch mnakuta karatasi vyumbani zenye alama ya hatari ile ya skulls and bones wanpitisha chini ya mlango na nyingine wanabandika kila sehemu za public
Siku inaanza kwa hofu kubwa na shauku sana kila mtu anawahi kujiandaa kwenda kusoma ā€œgazetiā€

Punch ilikuwa inaandikwa kwenye manila sheets kwa marker pens halafu Inabandikwa pale cafeteria inaitwa Sheraton/Havard wakati ule juu kabisa ambapo katika hali ya kawaida huwezi kupanda bila kuonekana lakini hawakuwahi kukamatwa kwenye tukio
Miaka ya mwanzoni walitumia mkaa kuandika ukutani
Kuna siku walinzi walikuwa wanalia timing, umeme ulikatika dk 5 tu wakakuta bango la punch tayari!
Imagine wakati huo hakuna simu lakini wapanchi waliweza kuwasiliana na kufanya tukio la kubandika matangazo kwenye mabweni yote na kusambaza karatasi kila chumba kwa wakati mmoja

Aliitwa ā€œMzeeā€ na wanafunzi waliitwa kama ā€œGrandchildrenā€
Sifa kubwa ni
1. kutojulikana ā€˜Mzee is incognito’
2. Mzee ā€œhas microscopic eyes and ultra-sensitive earsā€
3. kuwa kila sehemu ā€˜Mzee is Omnipresent, Omniscient and Omnipotent’
4. kutomaliza chuo, ā€œMzee Never Graduates and is never discontinuedā€
Wengi baadae walikuja kuingia kwenye system na wakawa viongozi kuanzia wahadhiri, Maprofesa, Makatibu Wakuu, Majaji, Ma MD na DG, wabunge, Mawaziri na viongozi wa juu jeshini na serikalini kwa ujumla

Kwa kiasi fulani ilikuwa kama Big Brother, kuchunga tabia za wanafunzi, hasa ulevi, uzinzi, umalaya, udokozi, uchafu (hairuhusiwi kuvaa sandals au kofia na hata kaptula cafeteria) au kugombea chakula, lazima mpange foleni ingawa wanafunzi wa FoE tulikuwa hatupangi foleni na tunakaa high table, meza za mbele cafeteria ila kuna unyanyasaji mkubwa wa wanawake, hawakuruhusiwa kunywa chai ya saa kumi jioni, kuvaa kanga, nguo fupi au za kubana na pia kila mwanamke alijulikana boyfriend wake na tabia yake

Kuna jamaa aliwahi kukutwa anawachungilia Hall 3 , la wanawake tupu wakati huo, muda wa mchana kipindi cha joto wengi wamejiachia na gaguro na
sidiria, wale wanafunzi wa kike wakampa kichapo kumshuku kuwa mmoja wa wapanchi

Kulikuwa na Ten Holy Commandments za maelekezo ya kuishi Chuo hasa kwa freshers kila moja ikianza na neno ā€œThou Shallā€ au ā€œThou Shall Notā€

FoE ndio walikuwa wababe wa Chuo miaka hiyo na kwa wengi kukosekana kwa wanafunzi wa kike kule ilichangia aina fulani ya misogynistic na male chauvinism behaviour, wengi wakitokea boys only schools na hasa kama ā€œfundiā€ akimtongoza demu ā€œngwiniā€ halafu amtolee nje kama ilivyotokea kwa Mukasa
(Mzee expresses regrets for the passing of his Granddaughter Revina Mukasa but do not accept the responsibility of her fate!)
mpaka Getrude Mongella wakati huo kama Gwajima wa sasa ikabidi aje na kuongoza maombolezo halafu aka panda juu ya ile meza ya ā€œMzeeā€ na kutoa speech
Hapo ndio kifo cha Punch (natural na enforced death) kilipoanzia rasmi mpaka walipokuja kumpanch vibaya Rais Mwinyi ikapigwa search ya door to door kutafuta material za ā€œMzeeā€ na wahusika walioshukiwa wakafukuzwa na Chuo kikafungwa mwaka mzima watu wakakaa nyumbani na kucheleweshwa kuingia first year wapya


Miaka ya nyuma ilikuwa sana michoro ila baadaye ndiyo wakaanza kutumia sana lugha (wall literature) hasa English na maneno mengi ya kilatini hasa yanayotumika kwenye Law na Medicine

Kwa kiasi kikubwa mwanzoni wanasema ilkuwa kama forum ya kupiga vita rushwa, wizi wa mitihani, upendeleo chuoni ila miaka ya mwishoni ilikuwa ni insecurity ya wanafunzi wa kiume, hasa Engineering kushindwa kupata mademu mangwini na pia kuanza kwa vyombo vya habari huru na vyama vingi kukamfanya ā€œMzeeā€ kupoteza ushawishi wa mwanzoni.
 
Back
Top Bottom