Kumbukumbu za UDSM from 1970s to 1990s: Poisoned Letters na Mzee Punch

Zamani walikua hawataki ujinga.

Vichwa vilikua sawa. Saiz umbea umbea tu na kujipemdekeza kiboya. Ushe.. nz na maujinga jinga tu mengi
 
Hao wanafunzi walikuwa hawana kazi ya kufanya zaidi ya udaku na umbea?

What is the point? Kuanika mbunye za watu hadharani?

Na mimi nashangaa ilikuwaje mpaka watu wajinga wakapata nafasi ya kufanya ujinga wote huo na bado wakaendelea kuonekana mashujaa?

Kama una tatizo na mtu fuata njia halali za kumuwajibisha zinazozingatia utu na sio kuanika ****** wake kwenye mbao za matangazo.

No wonder we have such people today. Mazombi zombi tu, udaku na upashkuna ndo kitu wanaweza.

Ukiwaambia wajenge barabara wanajikuna vinyeo, kumbe chuo kikuu walienda kusomea udaku na ushangingi.

Cc: Lamomy cocastic Seran ephen_ Monetary doctor Tlaatlaah
 
Alikuwa Jaji sasa huyo jaji ni nani?
Wanasema sio mtu ni crew...!
Na msanifu wa hizo michoro ni "mama yetu Tanzania" thus hakumaliza kabisa udsm (banned) na wengine...
According to radio mbao.
 
Kama hiko chuo ndio kimetoa wasomi wa nchi hii ndio maana nchi ipo ilipo sasa.

Waambieni watoto wenu wasifanye huo upuuzi na mkatubu.

🚮
 
Na lugha, hakika walijua kuandika lugha/kingereza chenye viwango
 
Mzee Punch kilikuwa ni kikundi cha wanafunzi, “Wapanchi” na ni secret society

Inasemekana ilianzia mwaka 1970 hasa baada ya kucheleweshewa boom baada ya Nyerere kukataa kuogeza
Mzee wangu alimaliza hapo mwaka huo na kina Mu7 na ndiyo ilikuwa inaanza. Wengi walitoka Faculty of Engineering (FoE) a.k.a mafundi na wachache wa Law, Arts, etc a.k.a mangwini

Mie nilisoma 1990s tunaikuta inaanza kupungua nguvu na kufa baada ya Chuo kufungwa walipo mpanchi Mzee Mwinyi, enzi za kina James Mbatia

Ukijifanya kuwatafuta uwajue unawekwa kwenye ‘pipeline’ yaani next punch umatokea wewe, na wanaandika taarifa zako zote kuanzia kijijini, wazazi mpaka ndugu, kwa kashfa na matusi makubwa mno na kuutangaza mwili wako hasa kama ni mwanamke
Ukishakuwa kwenye pipeline au ukijaa kwenye punch wanafunzi wengi wanakutenga kuogopa wao wasiingie kwenye anga za “Mzee”

Kuna aunt yangu walimpiga punch kali sana miaka ya 80 , sasa yeye bint wa mjini hakujali akaenda kuicopy kama ilivyo na mpaka leo anayo na mpanch mmoja akawa mshkaji wake baada ya kumshuku na kutishia kumshtaki
Wanawake wenye misimamo walipigwa sana punch ila wengine walishindwa kuvumilia kama yule Levina Mukasa alijiua

Asubuhi mkiamka kama kuna Punch mnakuta karatasi vyumbani zenye alama ya hatari ile ya skulls and bones wanpitisha chini ya mlango na nyingine wanabandika kila sehemu za public
Siku inaanza kwa hofu kubwa na shauku sana kila mtu anawahi kujiandaa kwenda kusoma “gazeti”

Punch ilikuwa inaandikwa kwenye manila sheets kwa marker pens halafu Inabandikwa pale cafeteria inaitwa Sheraton/Havard wakati ule juu kabisa ambapo katika hali ya kawaida huwezi kupanda bila kuonekana lakini hawakuwahi kukamatwa kwenye tukio
Miaka ya mwanzoni walitumia mkaa kuandika ukutani
Kuna siku walinzi walikuwa wanalia timing, umeme ulikatika dk 5 tu wakakuta bango la punch tayari!
Imagine wakati huo hakuna simu lakini wapanchi waliweza kuwasiliana na kufanya tukio la kubandika matangazo kwenye mabweni yote na kusambaza karatasi kila chumba kwa wakati mmoja

Aliitwa “Mzee” na wanafunzi waliitwa kama “Grandchildren”
Sifa kubwa ni
1. kutojulikana ‘Mzee is incognito’
2. Mzee “has microscopic eyes and ultra-sensitive ears”
3. kuwa kila sehemu ‘Mzee is Omnipresent, Omniscient and Omnipotent’
4. kutomaliza chuo, “Mzee Never Graduates and is never discontinued”
Wengi baadae walikuja kuingia kwenye system na wakawa viongozi kuanzia wahadhiri, Maprofesa, Makatibu Wakuu, Majaji, Ma MD na DG, wabunge, Mawaziri na viongozi wa juu jeshini na serikalini kwa ujumla

Kwa kiasi fulani ilikuwa kama Big Brother, kuchunga tabia za wanafunzi, hasa ulevi, uzinzi, umalaya, udokozi, uchafu (hairuhusiwi kuvaa sandals au kofia na hata kaptula cafeteria) au kugombea chakula, lazima mpange foleni ingawa wanafunzi wa FoE tulikuwa hatupangi foleni na tunakaa high table, meza za mbele cafeteria ila kuna unyanyasaji mkubwa wa wanawake, hawakuruhusiwa kunywa chai ya saa kumi jioni, kuvaa kanga, nguo fupi au za kubana na pia kila mwanamke alijulikana boyfriend wake na tabia yake

Kuna jamaa aliwahi kukutwa anawachungilia Hall 3 , la wanawake tupu wakati huo, muda wa mchana kipindi cha joto wengi wamejiachia na gaguro na
sidiria, wale wanafunzi wa kike wakampa kichapo kumshuku kuwa mmoja wa wapanchi

Kulikuwa na Ten Holy Commandments za maelekezo ya kuishi Chuo hasa kwa freshers kila moja ikianza na neno “Thou Shall” au “Thou Shall Not”

FoE ndio walikuwa wababe wa Chuo miaka hiyo na kwa wengi kukosekana kwa wanafunzi wa kike kule ilichangia aina fulani ya misogynistic na male chauvinism behaviour, wengi wakitokea boys only schools na hasa kama “fundi” akimtongoza demu “ngwini” halafu amtolee nje kama ilivyotokea kwa Mukasa
(Mzee expresses regrets for the passing of his Granddaughter Revina Mukasa but do not accept the responsibility of her fate!)
mpaka Getrude Mongella wakati huo kama Gwajima wa sasa ikabidi aje na kuongoza maombolezo halafu aka panda juu ya ile meza ya “Mzee” na kutoa speech
Hapo ndio kifo cha Punch (natural na enforced death) kilipoanzia rasmi mpaka walipokuja kumpanch vibaya Rais Mwinyi ikapigwa search ya door to door kutafuta material za “Mzee” na wahusika walioshukiwa wakafukuzwa na Chuo kikafungwa mwaka mzima watu wakakaa nyumbani na kucheleweshwa kuingia first year wapya


Miaka ya nyuma ilikuwa sana michoro ila baadaye ndiyo wakaanza kutumia sana lugha (wall literature) hasa English na maneno mengi ya kilatini hasa yanayotumika kwenye Law na Medicine

Kwa kiasi kikubwa mwanzoni wanasema ilkuwa kama forum ya kupiga vita rushwa, wizi wa mitihani, upendeleo chuoni ila miaka ya mwishoni ilikuwa ni insecurity ya wanafunzi wa kiume, hasa Engineering kushindwa kupata mademu mangwini na pia kuanza kwa vyombo vya habari huru na vyama vingi kukamfanya “Mzee” kupoteza ushawishi wa mwanzoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…