Kumbukumbu za ulimwengu (World Archives)

Kumbukumbu za ulimwengu (World Archives)

View attachment 3107778
FOOTBALL _ SOCCER-LL.jpeg
 
Hii ilifanywa na wachaga (huko kwetu) miaka hiyo
Mtu anapokufa huzikwa ndani ya nyumba akiwa amekalishwa kwa kufungwa vizuri miguu na mikono,
Baada ya mwaka mmoja kuna kitu tunaita (wari wa mengelenyi) yaani pombe ya kichumini inafanyika kama hafla inayokuwa na mbege pamoja na kuchinja ng'ombe na mbuzi,baada ya zoezi hilo anafukuliwa vizuri kwa kuanza kutoa kichwa na kinahifadhiwa na kisha mifupa mingine yote na inahifadhiwa mahali maalum ambapo ya waliomtangulia ilihifadhiwa pia(mara nyingi ni katika masale maalum).
Niliwahi kusikia huko uru nao wanafanya hivi na hadi leo,kama yupo mtu wa uru atatuambia
 
Archaeologists dine in the tomb of Pharaoh Ramses XI in 1923.
FB_IMG_1727841625040.jpg
 
A New York City Police Officer poses hanging over Times Square, 1920. (Dobblet exposure image)
FB_IMG_1727888984391.jpg
 
Kiatu cha ngozi chenye umri wa miaka 5500—moja ya viatu vya zamani zaidi duniani—kiligunduliwa katika pango la Areni huko #Armenia.

Kiatu hicho kilipatikana katika hali nzuri
FB_IMG_1728772003990.jpg
kabisa kutokana na hali ya ubaridi na ukame ndani ya pango hilo na safu nene ya kinyesi cha kondoo ambacho kilikuwa kama muhuri thabiti. Vyombo vikubwa vya kuhifadhia vilipatikana katika pango lilelile, ambalo nyingi lilikuwa na ngano iliyohifadhiwa vizuri, shayiri, parachichi, na mimea mingine inayoweza kuliwa.

Imehifadhiwa kwenye Jumba la Makumbusho la Historia ya Armenia.
 
MFAHAMU BABA WA COMPUTER SCIENCE:

[emoji3579]Leo nakusogezea makala hii fupi ya miongoni mwa binadamu wenye akili Sana kuwahi kutokea japo na mafanikio yote aliyopata kwenye sayansi aliishia kujiua , twende sawa tujifunze vitu kutoka kwa mwanasayansi huyu nguli na hodari:

[emoji3579]Mwaka 1912 June 23 uko ktk Kijiji Cha Maida vale -Uwingereza alizaliwa mtoto mwenye akili ya ajabu aitwae Alan Turing , wazazi wake walifahamika kwa majina ya Mathison Tuling na Ether Sara , akiwa na Miaka 5 alianza kuonyesha uwezo wa kubuni vitu mbalimbali kutokana na mazingira yaliyokuwa yakimzunguka apo ndipo wazazi wake walianza kushituka na kumuwaisha shule , Baba yake Tuling alikuwa akifanya kazi km mtumishi wa umma Mzee Mathison alikuwa akimpenda Sana mtoto wake ivyo alipata mda mrefu kumchunguza mwanae na kugundua mtoto ake ana kitu special na uwezo mkubwa wa kufikilia , acha hapa Bongo Baba kila siku unaludi umelewa auna mda wakucheza na wanao Wala kuwatathimini watoto wako wakihalibika ukubwani utasikia aisee nimezaa mikosi , mkosi ni wewe Baba mtu umeshindwa kutengeneza base ya mwanao na kwa Mungu una kesi ya kujibu we acha bhana

[emoji3579] Mnamo 1918 Alan alienda Shule ya Msingi ya St Michael huko Playden . Alipoondoka miaka mitatu baadaye mwalimu mkuu alisema: "Nimekuwa na wavulana wajanja na wavulana wanaofanya kazi kwa bidii, lakini Alan ni fikra." Japo alikuwa hafanyi vizuri darasani ila mwalimu mkuu huyo akimpenda Sana Alan

[emoji3579] Alipokuwa na umri wa miaka kumi alipelekwa katika Shule ya Maandalizi ya Hazel Hurst.Hata Ivo Alan alikuwa akipata marks za chini katika masomo yake ya Hesabu na sayansi hivyo Mama yake alimshauli ni Bora akazane na masomo ya lugha na utamaduni yaliyokuwa hot Sana wakati huo uko Uwingereza,ilifikia hatua Alan Turing alitaka kusimamishwa kufanya mitihani ya Taifa kwa kuhofia ata feli Ivo Mara kwa Mara wazazi wake waliitwa shuleni kuelezwa hali halisi ya Mwanao , miongoni mwa nukuu zinazoish mpaka Leo ni ile ya Baba yake Alan kumwambia mwalimu wake wa darasani namuamini Sana kijana wangu itafika mda uwezo wake utaonekana , Mzee Mathison alikuwa karibu Sana na kijana wake japo performance yake ya masomo haikuwa ikiridhisha alimtia moyo aendelee kusoma kwa bidii bila kujali hali yake ya mda uo , hapa tuulizane wazazi ni Mara ngapi umemtia moyo kijana wako shuleni kwa matokeo yake mabovu yakitaaluma au ni mwendo wa bakola tu , actually fimbo azijengi akili ya mtoto ila ukaribu na Maneno ya hekima yanajenga mliwaze mtie nguvu mtengenezee mazingira ya yeye kusoma kwa nguvu Kisha utaona matokeo yake : Ndivo hivo ilivyokuwa kwa Mzee Mathison na mwanae Tuling , mda ulifika Tuling akawa kijana Bora sana darasani

[emoji3579]Aliingia Chuo Kikuu cha Cambridge kusomea hesabu mwaka wa 1931. Baada ya kuhitimu mwaka wa 1934, alichaguliwa kujiunga na chuo cha King's College kwa kutambuana kyheshimu tafiti zake, mbali na hapo Tuling alikuwa mwana riadha hodari na alishiliki mashindano ya Olympic, alikuwa akikimbia kila siku kutoka nyumban kwake mpaka sehemu aliyokuwa akifanyia kazi
Mmoja wa washiriki wa klabu yake ya riadha alipouliza kwa nini alifanya mazoezi kwa nguvu hivyo, alijibu, "Nina kazi yenye mkazo sana hivi kwamba njia pekee ninayoweza kuiondoa akilini mwangu ni kukimbia kwa bidii." Bwana wee ata usome vipi unakumbushwa kutokuacha kipaji chako

[emoji3579]Kazi maarufu zaidi ya Turing leo ni kama mwanasayansi wa kwanza wa kompyuta. Mnamo mwaka wa 1936, alianzisha wazo la Universal Turing Machine, msingi wa kompyuta ya kwanza. Na alianzisha jaribio la akili ya bandia mnamo 1950, ambalo bado linatumika hadi leo.

[emoji3579]Huyu mwamba alisoma haswa physics . Alisoma Sana nadharia za Einstein, na mara moja akajaza daftari na mawazo na maoni yake juu ya mada za Einstein . Alijishughulisha na mechanics ya quantum, uwanja mpya wakati huo, na vile vile biolojia, kemia na neurology baada ya vita. Mengi ya kazi hii ilihusiana na kuunda mashine ambazo zinaweza kujifunza na "kufikiri", yaani roboti uyu mzee ndo mtu wa kwanza kuja na theory za uundwaji wa roboti

[emoji3579]Kama haitoshi 1950 uyu jamaa alikuja na utangulizi wa morphogenesis ikawa uwanja mpya kabisa wa bilojia ya Hesabu kipindi kile yaani maelezo ya kihisabati jinsi mambo yanvyokuwa ambayo ndiyo Siri kubwa ya sayansi, miongoni mwa karatasi zake za msingi juu ya mada hii iliitwa "Muhtasari wa ukuzaji wa Daisy uyu jamaa alikuwa kichwa bhana acha sisi uko shuleni tulikuwa tunalukaluka juu ya madawati kama ngedere na kupiga walimu mawe achilia mbali kuvuta bange na mawazo yakuandika matusi Kuta za shule , Alan Tuling alikuwa anajuwa Nini kilimpeleka kusoma

[emoji3579]Itoshe kusema uundwaji wa KOMPYUTA ya kwanza ulitegemea Sana nguvu za uyu mwamba kwa asilimia 90 , na yeye ndiye mwanzilishi wa field ya " computer science "au tuseme ivi icho kilaptop chako kimetokana na nguvu ya Alan Turing , ila sisi hapa kwetu tuliowengi tunajua computer ni kusikiliza mziki movie , kupiga virtual dj mageton bila kusahau kuangalia porno , we acha bhana computer Ina mambo mengi mbali na ayo we fukunua utajua tu sa mtu una laptop ata kupiga window ujui ukimuuliza kwa Nini ujui oh ayo mambo Yana wenyewe akina Nani hao !? ukisema ivi wabongo watakuuliza ayaa tuonyshe na wewe ulichofanya kwenye computer bongo bhana

[emoji3579] hapa Nchini kwetu baadhi ya vyuo wanatoa , kozi ya computer science na ni miongoni mwa kozi Bora kweli kweli kwenye maendeleo ya Teknolojia , Cha ajabu serikali aitii mkazo hivi kweli Tanzania hii ni ya kukosa maabara official ya Taifa ya Computer iliosheheni kila kitu kuhusian na field ya computer kweli!? Sasa Kuna maana gani ya vyuo vetu kutoa hii kozi kwa sababu aitolewi ipasavyo ,juzi tu hapa serikali ndo imeingiwa Imani ikaanzisha SoMo la kompyuta kwenye tahasusi lakini tembelea izo shule zenye tahasusi ya computer mtakuta wanafunzi 10 computer moja duh , kinachotokea watu wachache wanaomaliza wenye wazazi wanao jiweza wanawapeleka kusoma China , marekani , Uwingereza, Japan na wakionekana bora waZungu wanawangangania , wachache wanaobaki wanaomba ajira na wengine wanakosa wanafungua ofisi zao mtaani na uko mtaani panya road usiku wanabomoa wanaiba laptop za watu walioleta kutengeneza asubuhi yake anapelekwa polisi anakula lungu zakutosha akitoka uko ka nyooka kama moja kwa hali hii saa ngapi tutapata wataalamu wa computer maana kama computer science inatolewa ipasavyo kwa Miaka yote tangu hii kozi nchini basi walau kila mkoa tungekuwa na maabara za kompyuta, na kwa Miaka Fulani tungeanza kutengeneza kompyuta zetu ila vijana wa kompyuta sayansi wakimaliza wanaachwa walande lande , ebu fikilia mtu kama Moudy Swema watu Kama awa walipaswa wawe na vituo sehemu wapewe sapoti mbona Miaka 100 ijayo tungekuwa mbali sana katika sayansi za Anga ila akina kaka moudy swema Wana achanizwa tu hii sio sawa wazee .

[emoji3579]Anyway tumalizie kwa mtaalamu Turing , uyu jamaa mbali na uwezo wake wa hali ya juu kwenye sayansi na kupelekea kutokea kwa vitu muhimu Leo kama kompyuta huyu jamaa alikuwa SHOGA , wakati ule Uwingereza watu walikuwa wakisali sana ivyo USHOGA ulipigwa marufuku na ulibainishwa kama uhalifu 1952 Turing alkuutwa na hatia za USHOGA hivyo jamii ilimtenga kitu kilichopelekea kutokufanya shughuli zake ipasavyo 1954 Turing alijiua kwa kula tofaa [emoji520]lenye sumu akiwa na Miaka 41 dah dunia ikampoteza mtu muhimu kweli kweli , ama kweli kizuri akikosi kasolo! Uyo ndo Alam Turing

[emoji3579]miongoni mwa vitu ambavyo Dunia aitosahau kwa Tuling , uyu jamaa alipigana kwenye vita ya pili ya dunia bila yakuvaa gwanda wala kushika mtutu: Bali kwa kutumia akili zake , ikapelekea Hitler na chawa wake kupigwa Sana na kushindwa, Sasa alifanya Nini ungana na Mimi sehemu ya pili ya maisha ya Alan Tuling the father of computer science

Mwandishi : Calvin Renatus

source : Alan Turing - the Engma: book by Andrew Hodges
.View attachment 2278708
Alileta mapinduzi makubwa ya computer
 
Wazo la kwamba milima fulani kwa kweli inaweza kuwa mabaki ya vishina vya kale vya miti ambavyo vimepitia mchakato wa kuoza inahakikisha uchunguzi mkubwa. Jugurtha Tableland nchini Tunisia, ambayo inainuka karibu futi 2,000 (mita 600) juu ya tambarare zinazoizunguka, inatoa kisa cha kustaajabisha. Mesa hii pana hupima takriban futi 4,900 (mita 1,500) kwa urefu na futi 1,600 (mita 500) kwa upana, ikijumuisha karibu hekta 80. Wazo la majitu ya zamani yaliyoharibiwa huibua athari za kupendeza kuhusu historia ya kijiolojia ya sayari yetu na michakato ambayo inaweza kusababisha malezi ya kushangaza kama haya.

FB_IMG_1730599576845.jpg
 
Bonde la Sayari nchini Libya

Ni moja ya maajabu ya dunia, kupata katika sayari ya Dunia na katika jangwa, kile kinachofanana na sayari na miili ya mbinguni, yote haya yenye mawe na mawe hata mchanga huko yana umbo sawa na nafasi na asili. ya sayari kama tunavyoiona kwenye picha na video, kama ilivyoripotiwa na wanaastronomia.

Mahali hapa paliitwa Bonde la Sayari katika mkoa wa Kufra wa Libya, na eneo hili ni moja ya hazina za Jimbo la Libya na jangwa lake, ingawa sio watu wengi wanaojua juu yake.

Iko karibu na Al-Uwainat Al-Gharbia karibu na mji wa Ghat kusini magharibi mwa Libya katika jangwa la mbali, kwenye bonde linalojulikana kama "Wan Tkufi", katika eneo linaloenea kutoka Hamada hadi miinuko ya Ghat.
Labda ni ya kushangaza zaidi nchini Libya, ikiwa sio ya kushangaza zaidi ulimwengun
FB_IMG_1731934273405.jpg
FB_IMG_1731934273405.jpg
i, katika bonde hili ambalo liko mbali na eneo la Al-Owainat (takriban kilomita 1130 kusini mwa Tripoli), miamba mikubwa huchukua fomu ya sayari, ili wale wanaotembelea eneo hili. bonde huhisi kana kwamba wako angani.
Kipenyo cha wastani cha kila mwamba ni kama mita 10, kwani miamba hii ya spherical imewekwa kando kwa umbali wa takriban kilomita 30.
Pia inajulikana kama "wan taufi" katika lugha ya Tuareg. Kinachotofautisha pia bonde hilo ni kwamba lina ardhi yenye miamba imara isiyo na maji wala kilimo.
 
Back
Top Bottom