Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii ilifanywa na wachaga (huko kwetu) miaka hiyo
Alileta mapinduzi makubwa ya computerMFAHAMU BABA WA COMPUTER SCIENCE:
[emoji3579]Leo nakusogezea makala hii fupi ya miongoni mwa binadamu wenye akili Sana kuwahi kutokea japo na mafanikio yote aliyopata kwenye sayansi aliishia kujiua , twende sawa tujifunze vitu kutoka kwa mwanasayansi huyu nguli na hodari:
[emoji3579]Mwaka 1912 June 23 uko ktk Kijiji Cha Maida vale -Uwingereza alizaliwa mtoto mwenye akili ya ajabu aitwae Alan Turing , wazazi wake walifahamika kwa majina ya Mathison Tuling na Ether Sara , akiwa na Miaka 5 alianza kuonyesha uwezo wa kubuni vitu mbalimbali kutokana na mazingira yaliyokuwa yakimzunguka apo ndipo wazazi wake walianza kushituka na kumuwaisha shule , Baba yake Tuling alikuwa akifanya kazi km mtumishi wa umma Mzee Mathison alikuwa akimpenda Sana mtoto wake ivyo alipata mda mrefu kumchunguza mwanae na kugundua mtoto ake ana kitu special na uwezo mkubwa wa kufikilia , acha hapa Bongo Baba kila siku unaludi umelewa auna mda wakucheza na wanao Wala kuwatathimini watoto wako wakihalibika ukubwani utasikia aisee nimezaa mikosi , mkosi ni wewe Baba mtu umeshindwa kutengeneza base ya mwanao na kwa Mungu una kesi ya kujibu we acha bhana
[emoji3579] Mnamo 1918 Alan alienda Shule ya Msingi ya St Michael huko Playden . Alipoondoka miaka mitatu baadaye mwalimu mkuu alisema: "Nimekuwa na wavulana wajanja na wavulana wanaofanya kazi kwa bidii, lakini Alan ni fikra." Japo alikuwa hafanyi vizuri darasani ila mwalimu mkuu huyo akimpenda Sana Alan
[emoji3579] Alipokuwa na umri wa miaka kumi alipelekwa katika Shule ya Maandalizi ya Hazel Hurst.Hata Ivo Alan alikuwa akipata marks za chini katika masomo yake ya Hesabu na sayansi hivyo Mama yake alimshauli ni Bora akazane na masomo ya lugha na utamaduni yaliyokuwa hot Sana wakati huo uko Uwingereza,ilifikia hatua Alan Turing alitaka kusimamishwa kufanya mitihani ya Taifa kwa kuhofia ata feli Ivo Mara kwa Mara wazazi wake waliitwa shuleni kuelezwa hali halisi ya Mwanao , miongoni mwa nukuu zinazoish mpaka Leo ni ile ya Baba yake Alan kumwambia mwalimu wake wa darasani namuamini Sana kijana wangu itafika mda uwezo wake utaonekana , Mzee Mathison alikuwa karibu Sana na kijana wake japo performance yake ya masomo haikuwa ikiridhisha alimtia moyo aendelee kusoma kwa bidii bila kujali hali yake ya mda uo , hapa tuulizane wazazi ni Mara ngapi umemtia moyo kijana wako shuleni kwa matokeo yake mabovu yakitaaluma au ni mwendo wa bakola tu , actually fimbo azijengi akili ya mtoto ila ukaribu na Maneno ya hekima yanajenga mliwaze mtie nguvu mtengenezee mazingira ya yeye kusoma kwa nguvu Kisha utaona matokeo yake : Ndivo hivo ilivyokuwa kwa Mzee Mathison na mwanae Tuling , mda ulifika Tuling akawa kijana Bora sana darasani
[emoji3579]Aliingia Chuo Kikuu cha Cambridge kusomea hesabu mwaka wa 1931. Baada ya kuhitimu mwaka wa 1934, alichaguliwa kujiunga na chuo cha King's College kwa kutambuana kyheshimu tafiti zake, mbali na hapo Tuling alikuwa mwana riadha hodari na alishiliki mashindano ya Olympic, alikuwa akikimbia kila siku kutoka nyumban kwake mpaka sehemu aliyokuwa akifanyia kazi
Mmoja wa washiriki wa klabu yake ya riadha alipouliza kwa nini alifanya mazoezi kwa nguvu hivyo, alijibu, "Nina kazi yenye mkazo sana hivi kwamba njia pekee ninayoweza kuiondoa akilini mwangu ni kukimbia kwa bidii." Bwana wee ata usome vipi unakumbushwa kutokuacha kipaji chako
[emoji3579]Kazi maarufu zaidi ya Turing leo ni kama mwanasayansi wa kwanza wa kompyuta. Mnamo mwaka wa 1936, alianzisha wazo la Universal Turing Machine, msingi wa kompyuta ya kwanza. Na alianzisha jaribio la akili ya bandia mnamo 1950, ambalo bado linatumika hadi leo.
[emoji3579]Huyu mwamba alisoma haswa physics . Alisoma Sana nadharia za Einstein, na mara moja akajaza daftari na mawazo na maoni yake juu ya mada za Einstein . Alijishughulisha na mechanics ya quantum, uwanja mpya wakati huo, na vile vile biolojia, kemia na neurology baada ya vita. Mengi ya kazi hii ilihusiana na kuunda mashine ambazo zinaweza kujifunza na "kufikiri", yaani roboti uyu mzee ndo mtu wa kwanza kuja na theory za uundwaji wa roboti
[emoji3579]Kama haitoshi 1950 uyu jamaa alikuja na utangulizi wa morphogenesis ikawa uwanja mpya kabisa wa bilojia ya Hesabu kipindi kile yaani maelezo ya kihisabati jinsi mambo yanvyokuwa ambayo ndiyo Siri kubwa ya sayansi, miongoni mwa karatasi zake za msingi juu ya mada hii iliitwa "Muhtasari wa ukuzaji wa Daisy uyu jamaa alikuwa kichwa bhana acha sisi uko shuleni tulikuwa tunalukaluka juu ya madawati kama ngedere na kupiga walimu mawe achilia mbali kuvuta bange na mawazo yakuandika matusi Kuta za shule , Alan Tuling alikuwa anajuwa Nini kilimpeleka kusoma
[emoji3579]Itoshe kusema uundwaji wa KOMPYUTA ya kwanza ulitegemea Sana nguvu za uyu mwamba kwa asilimia 90 , na yeye ndiye mwanzilishi wa field ya " computer science "au tuseme ivi icho kilaptop chako kimetokana na nguvu ya Alan Turing , ila sisi hapa kwetu tuliowengi tunajua computer ni kusikiliza mziki movie , kupiga virtual dj mageton bila kusahau kuangalia porno , we acha bhana computer Ina mambo mengi mbali na ayo we fukunua utajua tu sa mtu una laptop ata kupiga window ujui ukimuuliza kwa Nini ujui oh ayo mambo Yana wenyewe akina Nani hao !? ukisema ivi wabongo watakuuliza ayaa tuonyshe na wewe ulichofanya kwenye computer bongo bhana
[emoji3579] hapa Nchini kwetu baadhi ya vyuo wanatoa , kozi ya computer science na ni miongoni mwa kozi Bora kweli kweli kwenye maendeleo ya Teknolojia , Cha ajabu serikali aitii mkazo hivi kweli Tanzania hii ni ya kukosa maabara official ya Taifa ya Computer iliosheheni kila kitu kuhusian na field ya computer kweli!? Sasa Kuna maana gani ya vyuo vetu kutoa hii kozi kwa sababu aitolewi ipasavyo ,juzi tu hapa serikali ndo imeingiwa Imani ikaanzisha SoMo la kompyuta kwenye tahasusi lakini tembelea izo shule zenye tahasusi ya computer mtakuta wanafunzi 10 computer moja duh , kinachotokea watu wachache wanaomaliza wenye wazazi wanao jiweza wanawapeleka kusoma China , marekani , Uwingereza, Japan na wakionekana bora waZungu wanawangangania , wachache wanaobaki wanaomba ajira na wengine wanakosa wanafungua ofisi zao mtaani na uko mtaani panya road usiku wanabomoa wanaiba laptop za watu walioleta kutengeneza asubuhi yake anapelekwa polisi anakula lungu zakutosha akitoka uko ka nyooka kama moja kwa hali hii saa ngapi tutapata wataalamu wa computer maana kama computer science inatolewa ipasavyo kwa Miaka yote tangu hii kozi nchini basi walau kila mkoa tungekuwa na maabara za kompyuta, na kwa Miaka Fulani tungeanza kutengeneza kompyuta zetu ila vijana wa kompyuta sayansi wakimaliza wanaachwa walande lande , ebu fikilia mtu kama Moudy Swema watu Kama awa walipaswa wawe na vituo sehemu wapewe sapoti mbona Miaka 100 ijayo tungekuwa mbali sana katika sayansi za Anga ila akina kaka moudy swema Wana achanizwa tu hii sio sawa wazee .
[emoji3579]Anyway tumalizie kwa mtaalamu Turing , uyu jamaa mbali na uwezo wake wa hali ya juu kwenye sayansi na kupelekea kutokea kwa vitu muhimu Leo kama kompyuta huyu jamaa alikuwa SHOGA , wakati ule Uwingereza watu walikuwa wakisali sana ivyo USHOGA ulipigwa marufuku na ulibainishwa kama uhalifu 1952 Turing alkuutwa na hatia za USHOGA hivyo jamii ilimtenga kitu kilichopelekea kutokufanya shughuli zake ipasavyo 1954 Turing alijiua kwa kula tofaa [emoji520]lenye sumu akiwa na Miaka 41 dah dunia ikampoteza mtu muhimu kweli kweli , ama kweli kizuri akikosi kasolo! Uyo ndo Alam Turing
[emoji3579]miongoni mwa vitu ambavyo Dunia aitosahau kwa Tuling , uyu jamaa alipigana kwenye vita ya pili ya dunia bila yakuvaa gwanda wala kushika mtutu: Bali kwa kutumia akili zake , ikapelekea Hitler na chawa wake kupigwa Sana na kushindwa, Sasa alifanya Nini ungana na Mimi sehemu ya pili ya maisha ya Alan Tuling the father of computer science
Mwandishi : Calvin Renatus
source : Alan Turing - the Engma: book by Andrew Hodges
.View attachment 2278708