Kumbukumbu zangu za Jukwaa la Chitchat :
Miaka ile kunazia 2015 mpk 2018 Jf chitchat lilikuwa jukwaa la moto sana haipiti mtu siku bila kuja chitchat kuburudika na ilikuwa haipiti mda mrefu bila watu kugungulia nyuzi za kutakana na kujibebishana ila miaka ya siku hivi karibuni Jf chitchat hakuna nyuzi za kuburudisha kama zamani na inafika hata mwezi sitembelei .
Miaka ile kulikuwa na uzi pendwa na ilikuwa bonge la ubuunifu kutoka kwa
DJ SEPETU alikuwa na show yake ya interview kuwahoji members mbalimbali humu ,humo ilikuwa mtu unacheka mpk basi na alipata muitikio mkubwa sana ikawa watu wanasubiri kama wanavyosubiri mechi za mpira .Kama kawaida ya Jf haters wakaanzisha vuguvugu la kuwa jamaa interviews zake anadili na warembo tu na kuwa anaajenda za siri za kula kimasihara hatimaye shows zikapoteza mvuto na jamaa akapotea .
Jf kulikuwa kama kuna kujuana fulani na matabaka unakuta kama kikundi fulani wanachat sana wenywew kwa wenyewe nk mpaka kukuzuka harakati za makapuku kupinga na kuanzisha makapuku forum humu.
Nimekutia Jf together party ,ilikuwa inakuwatanisha wana Jf mbalimbali kusherekea na kubadilisha a mawili matatu na ilikuwa kila mwaka kabla ya kufa na sijui iliipotelewa wapi japo sijawahi kushiriki hata moja.