Kumbukumbu zangu: Leo nimetimiza miaka mitano(5) tokea nijiunge Jf

Katika moja ya interviews "mrembo" mmoja akafichuliwa kuwa ana id ya kiume zikaunganishwa. Ikawa shida.
 
Jf kulikuwa kama kuna kujuana fulani na matabaka unakuta kama kikundi fulani wanachat sana wenywew kwa wenyewe nk
Ni kweli. Utakuta uzi unazungumza jambo jengine kuna wadau wanakuja wanaanza kupiga stori zao binafsi humo, wengine wanatongozana humo humo na mengineyo. Na zile enzi hizo ilikuwa ukiquote uzi wa mtu unatokea wote. Sasa mtu kama the Bold akiandika uzi wake mreeeefu mtu ana quote wote halafu anaandika "asante sana mkuu". Basi watu wanakasirika sana.
 
Siku hizi hizo pigo zimekufa zamani ukiandika uzi mahali popote wanakuja watu wanajichatisha huku wakiulizana hali na kuzungumza mambo binafsi ambayo hata mwenye uzi haulewi kipi kinazungumzwa uzi mpaka mtu uwafoke hapo wanaacha au wengine wanarundisha mashambulizi.
 
Nakumbuka miaka ile mpaka Le mutuz yupo humu Jf watu walikua wanamchokoza sana pamoja na DeoKisandu ambaye alikuwa akionekana kama dishi limeyumba vile .Upande wa wahuni kulikuwa na @Segrio B na 666 chata walikuwa wanatukana matusi ya wazi tena makubwa.
 
Hapo kwenye id zaidi ya moja najiuliza wengine wanawezaje..
 
Uzi wangu bora ni Jf bookworm wa Paula Paul umenipa hamasa ya kuwa msomaji wa vitabu kabla ya hapo ilikuwa kwa mwaka nasoma vitabu 5 mpk 10 baada ya hapo kwa kukadiri nimefikia uwezo wa kusoma vitabu 30-50 kwa mwaka.

Uzi mwingine nilioukubali na kuupenda ni ule wa Da'Vinci kuhusu Low latent inhibition jinsi jamaa alivyowasilisha na kutoa madini mule na wakati nasoma nilikuwa kama najiona mimi nazungumziwa.
 
Kwa hiyo ule uzi wetu pendwa we huupendi?
 
SEMA KITU NIMEGUNDUA JF UWEZI KUTANA NAYO KAMA HUWA UNASACH UJINGA MTANDAONI
 
SEMA KITU NIMEGUNDUA JF UWEZI KUTANA NAYO KAMA HUWA UNASACH UJINGA MTANDAONI
Ujinga utakutana kwenye comments kuna watu wana mizaha sana mfano kuna mtu aliuliza dawa ya kuongeza uume jamaa akajibu siriaz kuwa kama nyingu au nyuki wakali watatu unawaweka kwenye mfuko au boksi dogo kisha unaweka uume kupitia tundu na unukua unachekesha boksi ndani ya dakika chache kitu kinaongezeka .
 
Hiyo jf together party naomba irudi
Antonnia Poker Mjep cocastic Beesmom mzabzab Kelsea Wigelekelo Pau Bae Depal sophy27 Lenie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…