SoC02 Kumbukumbu zangu

SoC02 Kumbukumbu zangu

Stories of Change - 2022 Competition

King Nabora

New Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
2
Reaction score
3
Umuhimu wa chakula uonekana palipo na njaa vivyo hivyo umuhimu wa amani huonekana pasipo na amani, giza lilitanda upande wa kazkazini mwa Tanzania maskani pa majirani zetu wa nchi ya kidemokrasia ya Congo, Giza hilo liloletwa na kundi la waasi wa kundi la M27.

Kama ilivyo desturi ya ujirani mwema basi hapakuwa na budi ila kupeleka mwanga upya kwa msaada wa kijeshi kwa lengo la kulinda Amani. Huwa ni wakati mgumu kuona nyumba ya jirani inaungua halafu ukajifanya huoni, kati ya vikosi vichache vya jeshi la ulinzi la Tanzania basi kama ilivyoada palitakiwa wanajeshi wa kwenda kuweka sawa hali ya kiusalama katika eneo lile lililotekwa na waasi wa kundi la M27 ambao wamekua wakitekeleza mauaji na uhalifu wa kibinadamu.

Ninayekuandikia simulizi hii ni kati ya manusura wa kifo kilichotokana na vita hivi vya ndani vya majirani zetu. Kwa majina naitwa David Mwamunyange, ni mwanajeshi kijana mwenye umri wa miaka 26 katika Jeshi la Wananchi la Tanzania ni luteni wa kikosi namba 442KJ naandika simulizi hii angali bado nipo katika hali mbaya ya kiafya ambayo ni madhara ya mejeraha niliyopata nikiwa napambana na kundi la waasi la M27, lengo kuu la simulizi hii nikuwaasa vijana na raia wote kupenda na kulinda Amani tuliyo nayo katika taifa letu la Tanzania, najua Tumekua nayo kwa muda mrefu ila ni matokeo ya utawala bora wenye kujua umuhimu wa tunu hii muhumu kwa taifa letu. Basi turejee katika simulizi yetu hii ambayo itatukumbusha umuhimu wa utawala bora na umuhimu wa kulinda tunu hii muhimu tuliyonayo.

David ni miongoni mwa maofisa wachache waliohitimu mafunzo ya kiofisa katika levo ya nyota mbili, ni kati ya maafisa wasomi mwenye shahada ya Sheria, nilipangiwa katika kikosi namba 442KJ na pia kupangiwa majukumu ya kua kiongozi wa kombania C, mapema katika umri wa miaka 26 angali bado ni kiongozi wa kombania na afisa wa kikosi namba 442KJ nilifunga ndoa na mpenzi wangu wa mda mrefu aliyejulikana kwa jina la Magreti.

Ndani ya muda mfupi mke wangu alipata ujauzito ivyo ilikua ni furaha tele kwenye familia yetu, Ghafla furaha hii kuu ilitoweka baada ya kupata taarifa za kupangiwa majukumu ya kulinda Amani katika nchi ya Jirani zetu wa Taifa la Congo, ulikua ni wakati mgumu sana kwangu na familia yangu kwakua hakuna asiyejua matokeo ya kwenda kwenye mizozo ya kivita kama hii kuna kurudi hai, kufa au majeruhi.

Basi hakukua na sababu ya kupinga amri halali ya jeshi na mapema nikaagana na familia yangu kwa machozi ya uchungu huku bado nikiwa na hamu kubwa ya kua karibu na mke wangu. Basi safari ilianza mara moja kwa kutumia ndege za kijeshi na mda mchache tulikua tayari tumefika eneo la tukio.

Naamini ninyi wengi mlishawahi kutizama filamu za kivita au unaweza ukarejea filamu ya korea kusini ya mwaka 2010 ijulikanayo kama “Road Number 1”. Mwaka 2014 niliwahi kutizama filamu hii hakika ilikua ya kusisimua sana sikujua kua ipo siku ntakuja kuyaishi maisha niliyoyaona katika filamu hiyo.

Mapambano na kundi hili yalikua ni makali mno kutokana na uzoefu wao na kutokua na kujali kwa uharibu wowote, hali ilikua ngumu sana kwa vijana wangu maana katika operesheni hii ya kulinda amani na kuzibiti kundi hili kubwa la waasi nilipewa kusimamia seksheni namba 2, ambapo eneo letu lilikua nje kidogo ya mji wa Goma upande wa kusini ambapo ilikua ni ngome ya muda ya kundi hili la M27, Mapambano yalikua ni makubwa na yenye kutumia silaha nzito maana waasi hawa walikua na shehena kubwa ya silaha nzito za kivita kitendo kilichofanya majeshi ya kulinda amani kua kwenye wakati mgumu sana ivyo kuhitaji usaidizi wa Zaidi wa vikosi vya kulinda Amani vya Umoja wa mataifa.

Hali ya mapigano ilizidi kupamba moto na ndani ya muda mfupi katika seksheni yangu nikawa nimepoteza wanajeshi wanne na wawili walikua wamejeruhiwa vibaya kwa bomu la kurusha kwa mkono, nilijawa na uchungu mkubwa kuwaona vijana wenzangu wakipoteza maisha yao mbele ya macho yangu simanzi ilitanda na hofu pia uchungu ulizidi nlipokua nikiiwaza familia yangu haswa mke wangu akiwa mjamzito uchungu ule ulinifanya niwe makini na kuongeza ubunifu wa mapigano.

Ikumbukwe kwamba wajeshi wa taifa letu huwa tumezoea kuishi kwa amani ivyo katika uwanja wa vita mambo hua tofauti haswa unapokutana na watu wazoefu wa vita kama makundi haya ya waasi, ivyo kuwadhibiti upande ule wa kusini haikua kazi rahisi na wakati huo huo tumeshapoteza vijana sita katika seksheni yetu ivyo nikiwa na vijana wangu wanne tuliweza kubadilisha mbinu na kutumia mbinu ya kuvizia na kujificha au kwenye mchezo wa mpira tunaiita ‘counter attack’ kwa kutumia mbinu hii tuliweza kuwapunguza maadui kwa kiwango kikubwa huku sisi tukiwa wa tano tu katika upande ule kusini.

Tulizidi kuomba msaada kwa wakuu wetu na pia kufanya mawasiliano na mkuu wa operesheni wa umoja wa mataifa kutuongezea nguvu ya watu pamoja na silaha pia na madakari ili kuwatibu wanajeshi wetu wawili waliojeruhiwa ila bahati mbaya walipoteza damu nyingi ivyo walifariki kabla msaada wa umoja wa mataifa kufika.

Licha ya kutumia mbinu nzuri ila idadi yetu ilikua ndogo sana kuweza kupambana na kundi kubwa kiasi kile ivyo ilifika mahali tukawa tumechoka uku maadui wakizidi kufanya mashambilizi ya hovyo ya silaha nzito, niliona umauti ukininyemelea akili yangu na moyo wangu ukiwa unaiwaza familia yangu mara ghafla sikutambua kilichoendelea wakati ule akili zilirudi nikiwa kwenye helkopta ya umoja wa mataifa nikiwa kwenye maumivu makali huku nikipatiwa matibabu.

Nimeendelea kupata matibu katika hospitali ya jeshi hapa hapa Tanzania baada yakurudishwa na vikosi vya Umoja wa mataifa hadi wakati huu naandika andiko hili bado nipo nauguza mwili wangu uliojeruhiwa pakubwa na bomu la kurushwa kwa mkono lilidondoka eneo tulilokua tumejificha na wenzangu huku nikipata taarifa vijana wengine watatu walipoteza maisha pale pale.

Niwasihi tu Watanzania Amani tuliyonayo tusiizoe tukaona haina maana tuzidi kuweka mbele Amani yetu uku tukitafuta suluhu za changamoto zetu kwa njia za amani, vita zinaua, utawala mbaya unazaa makundi ya waasi ivyo ni vyema viongozi kutawala kwa hekima na kuweka maslahi ya wananchi mbele ili kudumisha Amani yetu.

KUMBUKUMBU ZANGU
Imendaliwa na kuchapishwa na Bernard E. Nabora.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom