SnowBall
JF-Expert Member
- Sep 13, 2011
- 3,052
- 2,842
Wanabodi natumaini nyote hamjambo!
Kwa muda mrefu stori nyingi zinazohusu mapenzi zimegubikwa na migogoro mingi inayotokana na wapenzi husika kuhisiana kukosa uaminifu baina yao. Kwa kuhisi kuwa wanaweza kuibiwa, wapenzi wengi wamekuwa wanawekeana 'njia' nyingi za kudhibitiana. Tumesikia 'stori' za kuwekeana 'tego' baina ya wapendanao..ili kwamba kama mmoja atatoka 'nje' basi anasie. Lakini sio hivyo tu..tunashuhudia pia wapenzi/wanandoa 'wanakagua' simu na pochi za wenza wao kwa nia ya kuhakikisha 'haibiwi mtu'. Kuna cases za baadhi ya wenza kuwafuata wenzi wao kwenye sehemu zao za kazi kwa nia ya kuji'expose' ili wajulikane. Kuna wenzi ambao wamepeana hadi 'password' za accounts zao za kwenye mitandao ya kijamii. Alimradi kinafanyika kila kiwezekanacho kuhakikisha 'udhibiti' upo.
Binafsi naamini 'binadamu hachungwi' na kwamba ukishaanza kumdhibiti au kumchunga mwenzio ni wazi kuwa wewe ni muoga wa mapenzi. Kama anakupenda anakupenda tu na kama anakuzuga atajulikana tu...Kuku wako mwenyewe manati la nini??...Lakini kuna wanaosema 'abiria chunga mzigo' hawa wanasema binadamu ni kiumbe asiyetabirika ..hivyo kufuatilia nyendo zake inasaidia 'kumstua' na kumrudisha kwenye mstari.
Hivi jamani kweli kuchungana na kudhibitiana ndio kuonyesha kuwa una mapenzi ya dhati kwa mwenzio?? au ni woga tu na kutojiamini!!!
Wasalaam!