AshaDii
Platinum Member
- Apr 16, 2011
- 16,189
- 18,102
nakuelewa sana unachosema my dear friend, lakini kuna mambo mengi sana hapa tunatakiwa kuyazingatia....
sisi ni binadamu na kama binadamu kuna mambo mengi sana ambayo tunatakiwa kuyafanya kukamilisha maisha yetu.
wakati nakua niliwahi kuishi na kakangu kwenye nyumba ya kupanga. kuna mama alikuwa anaishi na mumewe, huyo mama alikuwa mama wa nyumbani mwenye watoto. alikuwa anaishi na wasichana wa kazi wamsaidie watoto. mimi ni shuhuda, wasichana wake walikuwa wanafanya kazi za watoto tu, lakini yule dada alikuwa anapata shida sana na wasichana wa kazi sababu mumewe alikuwa anatembea na kila msichana anayemleta.
sisi wamama au hata hao wababa, kuna kipindi wanalazimika kuwa nje ya nyumbani kikazi au masomo, tuwe tunaambatana na wenzetu?
Kuna mipaka ya vitu. Siwezi mjudge huyo mama sababu sina all the details, ila mwisho wa siku alikua ni mdhaifu mno kwa mumewe. Mwanaume afanye makosa kama hayo mara moja, usamehe na isitokee tena! Anapofanya kwa kurudia tena kwa makusudi kabisa ndani mwako mwenyewe, anakutafuta ubaya... Believe me you.
Sasa hapo kwa huyo mama FP huoni kuwa kulikuwa ni muhimu kufanya udhibiti? So in this case unaona ni sawa tu mwanamke kumwachia mumewe kufanya maamuzi na hali anajua tabia yake fika?
Pengine alikua hadhibiti, ndio maana mume alikua na uwezo wa kulala na binti zake wa kazi. Ingawa naona ni disclaim kuwa kudhibiti haimaanishi hatafanikiwa lengo, ila unalipunguza makali.
Likija suala la kua mbali na mwenza, huwezi kwenda nae FP. Ila unapo ondoka unaenda kwenye kisomo unajua kabisa unakaa mwaka, huna haja ya kuacha mdogo wako wa kike au house gal ndani ya nyumba else by the time unarudi atakua tayari ni mke mwenzako. So hapo unadhibiti pale nyumbani, akitoka nje huko you can't help it, yale yaliyo ndani ya uwezo do it.