Kumdhibiti mpenzi wako!!...ni woga au ndo mapenzi??

Kumdhibiti mpenzi wako!!...ni woga au ndo mapenzi??

tulipofikia nadhani yeye ndio aondoke aniachie nyumba, aende kwa amani ya bwana Yesu! kama vipi tutatafutana uzeeni huko, lakini cha kushangaza sasa hivi yeye anaumia sana, anahisi mambo yasiyokuwepo, ile mtafutano kumbe ulikuwa unampa kichwa? sasa hivi anahisi kama namtenga fulani au nina mambo yangu, mie mtoto wa watu sina hili wala lile, ni kwamba hata akirudia tabia zake za kurudi saa 8 za mausiku hataona call/sms yangu ya kumuuliza, amalize starehe zake arudi nyumbani.
ha haaa, na yeye haondoki, basi mmebaki mmegandana kama luba, lol!
ila mkishafikia uzeeni raha sana..... mnabaki kuwa marafiki tu
 
Dadaangu nakuelewa ila nataka tupanue mjadala na tuguse maeneo yote.
Kwa mfano hapa sidhani kama neno 'mipaka' linaweza kuwa sawa kwa watu wote.
Mfano unaposema kumdhibiti mwenzio ni ruksa mradi kuwe na 'mipaka'...Sasa mwengine aweza kuhoji mipaka hapa ni ipi?..Kwa mfano..kuna mwingine anataka kila jina kwenye phonebook ya mwenzi wake alijue ni la nani?..kwake huyu naye atakuambia sijavuka mipaka nalinda ndoa yangu..nadhani tafsiri ya 'udhibiti' ni pana sana.
Lengo kuu la mada yangu lilikuwa kujua hii 'motive' ya udhibiti inatokana na nini?..woga? au hisia mbaya tu?
Nashukuru umeieleza kwenye posts za mwanzo..lakini (kiuchokozi lakini) huoni kuwa mara nyingi 'woga' unaotokana na matukio ya wenzetu ndio unatupelekea huku kwenye udhibiti kuliko matuko halisi yaliyo kwenye mahusiano yetu???


SnowBall, aidha hujanielewa au unafanya makusudi.... Lol

Sijasema mahala popote I support ukaguzi, so far from what I know kudhibiti na ukaguzi ni vitu viwili tofauti.
Tabia ya kugagua kagua kwa taarifa yako wengine si tu wanafanya sababu ya wivu, wengine ni tabia. Mtu mwingine hata akipata mgeni nyumbani kwake akaenda washroom atataka kukagua kwenye pochi kuna nini, yaani yeye furaha yake ni kupekua pekua tu.

Suala la kupekua simu si msingi na wala si afya kwa mahusiano, sababu hata kama mpenzi wako hafanyi lolote anakua hapendi na kujisikia vibaya wamchukulia sivyo. Ila kuna rare cases kitu kinaweza kutokea na kukusukuma kutaka kujua zaidi kwa kuangalia simu. Hilo ni tofauti kabisa na kujenga tabia ya kukagua kagua simu kila mara na kila siku bila sababu za msingi.

It should be noted however, si kila mara mpenzi wako akishika simu anakua anakagua. Simu za sasas zina features nyingi, saa ingine unaweza shika simu with genuine reasons wala hata una interest na chats or msgs.
 
tuseme hivi, haya mambo hayatabiriki, kabisaaa, mwanaume mlafi ni mlafi tu hata ufanyaje, ndugu wa mume? ndugu wenyewe hao ni wale wa damu ya kiumbali kidogo, atashindwa kutembea nae? hujasikia hizo kesi mbona kibao sana na kuna mada nilichangiaga kitambo fulani kwamba rafiki yangu alimleta mtoto wa dada yake mume amsaidie kazi za nyumbani na mwanaume alimla? kwenye hili simuamini mwanaume kabisa akiamua kufanya ufirauni ataufanya tu.

Nyamayao unadhani sijui hilo dear?

Nikimwacha mdogo wangu wa kike atahalalisha kuwa ni mke na jamii inaweza ona sawa, na hata ndugu zake wanaweza wasiingilie kivilee, nikimwacha ndugu yake wa kike watafanya siri - ndugu zao wakijua panaweza kuwa hata padogo, na believe me you once najua narudi moja kwa moja huyo mwanadada namtafutia utaratibu ambao ni bora zaidi kwake - kama some sort of shukrani kwa kunilelea familia wakati sipo. For sababu najua tabia ya wanaume deep down within me naweza nikawa najiuliza kama they did it or not.

Mie najua, nikiwa mbali na mwanaume wangu for more than 6 months, yeye kuwa hajagusa mwanamke mwingine siwezi kuamini. Suala ambalo kwa kweli sipendi na linaweza niuma ni mwanamke aliyelala nae awe ndugu yangu. Alale tu anavyotaka (kwa heshima na nisijue) but ndugu zangu wa karibu naomba awaache tu. Inauma sana.
 
naamini ataacha mawasiliano ya hovyo hovyo yasiyokuwa na muelekeo mzuri na hata akifanya atayafanya kwa tahadhari sana..................

hakuna uhuru usiokuwa na mipaka,,,,,,,,,,, kubali kataa vishawishi vipo na mpenzi wako kukulinda hupunguza Risk ya kutumbukia kwenye vishawish.

na je kwasababu watoto wenu wanatambu kuwa ukishika sehemu mama alisema tutanaswa basi tutawaachia tu wawe karibu na hatari hizo?
sidhani kama utataka hicho kwenye RED kitokee...
niliwahi soma hapa kuwa kuna watu wana simu zinakaa ofisini tu, hiyo namba wenzi wao hawaijui, ni special kwa ajili ya kuchakachulia mahusiano....
 
hapa tuelewane kuwa sijasema kukaa nje ya familia ni bora kuliko kuwa na familia unaweza kaa na familia na mambo yasiwe kama vile unavyotaka yawe, fanya kitu unachoona kinafaa kwa manufaa ya familia yako

Nilikuelewa kabisa, na lile halikua applicable wala si maelezo ya kua wanao kaa mbali na familia wanakosea. Nilikua nagusia vitu kama hivyo ni moja ya sababu huwakwamisha baadhi.
 
wakati kasheshe yangu inaisha isha, ile kumsamehe na kusonga na maisha alinianziaga hizo, umeshafika nyumbani? basi nipe "nanihii" niongee nae, nilikuwa namwambia piga simu ya mezani uongee na wanao kwanini yangu? ujinga mtupu we nimeshakuambia nipo nyumbani ndio utake kuhakiki ukiwa bar kwamba nipo nyumbani via kuongea na mwanao?
hapana dada yangu hata mi hayo maisha ya hivyo yananichefua na wala hayafai hata kidogo na huyo mzee wako alipitiliza na mara nyingi ukikuta mtu anamchunga sana mwenzie wallahi ukija kuambiwa yake unaghairi kusihi naye siku hiyo hiyo,pole dada Nyamayao ila tena hongera maanake naona uliamua kuuvaa uso wa mbuzi na kuwa an iron woman hapo nilipobold nimepapenda kwa kweli maanake kuna watu wanazidi aisee.
 
Last edited by a moderator:
Hii post yako FP ni sababu tosha ya kufanya udhibiti. Si wanaume wote wamebahatika kama alivyo bahatika mume wako kwa kuoa mwanamke anae jitambua hivi. Huwa inapendezana kuleta saana raha; mwanamke anapo kua anajielewa kwa kiasi hiki.

Wengine walioa wanawake waliokutana nao Disco saa 8 usiku. Hao wakioana; kudhibitiana muhimu Lol
ha haaaa, sisi hatukukutana disco lakini anajua wazi kuwa napenda mno disco......
yaani atakuwa hajanitendea haki kama kasafiri kwa muda halafu ategemee siku zote hizo nisiende disco. kwa hiyo ni bora awe na amani tu aniruhusu.
na kuna siku kabisa inatokea tupo wote, yeye anatamani kwenda disco but miimi sijisikii kabisa. au yeye ana rafiki zake wamepanga kwenda disco halafu nianze kuambatana naye, hasa kama wenzie hawapo na wake zao.
ni sawa tumeoana, lakini kila mtu ni mmoja (wanatuambiaga tu kuwa tumekuwa mwili mmoja, lol!), kila mtu anaweza fanya lolote popote, la maana ni kujitambua, na hasa kujiheshimu...... yaani nikiwazaga kufanya upuuzi, jambo linalonijia kichwani kwanza wala siyo mume wangu, ni mimi mwenyewe.... hivi sioni aibu kufanya hayo? yaani aibu ikinijia tu akili inarudi, ingawa najua kabisa uwezekano wa kukutwa hapo haupo.
 
Kama kuna kitu unataka kuthibitisha ..unaweza weka huo udhibiti ili ujiridhishe
Ila kama ni hisia mbaya tu..inaweza pelekea mwenzi wako kujishrukia zaidi..
Na hata kile unachokipigania unaweza usikipate..

...Na linapotokea swala la kuanza kumchunguza mwenzi mara baada ya kuona mabadiliko yanayomtishia mtu amani au mtindo maisha uliozoeleka ndani ya nyumba wala hakuna ubaya kwani hapo mtu anajaribu kupigania penzi lake,lakini kwa yule ambaye ye ni asili yake tu yaani aone asione mabadiliko mibano ipo pale pale huyo ndo tunamuweka kwenye kundi la watu wasiojiamini na walio na woga.
 
Nilikuelewa kabisa, na lile halikua applicable wala si maelezo ya kua wanao kaa mbali na familia wanakosea. Nilikua nagusia vitu kama hivyo ni moja ya sababu huwakwamisha baadhi.
nilikuelewa pia.....
nilikuwa natoa changamoto tu kwa wadogo zangu ambao watapatwa na vishawishi vya kuogopa kujiendeleza sababu ya familia....
Pamoja sana!
 
Naomba kila mtu anayesoma hapa anisamehe tu......
kati ya vitu niliwahi kusema sita-compromise katika maisha yangu ni career yangu.... kwa kitu chochote kile.
Nilipozaliwa, nikiwa na miezi mi3 mama alipata nafasi ya kwenda kusoma, aliniacha akaenda shule. mpaka leo namshukuru kwa nuniacha nyumbani na kuchagua kwenda shule.
Nimeolewa nikiwa undergraduate, tena mwaka wa kwanza, na nikazaa mtoto wangu muda huo huo..... mpaka leo sijutii kuacha wanangu na kuendelea na masomo...... napenda sana wanangu, na nitafanya kila kitu kwa ajili yao, nafanya yote kwa ajili ya familia yangu.
kuna wamama wengi sana walioacha kujiendeleza sababu ya familia zao (kuna watu wa karibu sana na mimi waliofanya hivyo) mpaka sasa wanajutia maamuzi yao.
hapa tuelewane kuwa sijasema kukaa nje ya familia ni bora kuliko kuwa na familia
unaweza kaa na familia na mambo yasiwe kama vile unavyotaka yawe, fanya kitu unachoona kinafaa kwa manufaa ya familia yako

kidude cha like mie kwangu sikioni jamani, hizi hofu za kuwalinda hawa wanaume zinatupeleka mbali sana!
 
Ninachojiuliza hapa ni kuwa ..je,wakti unaweka huo udhibiti wa kulinda ,ali yako na yeye mlengwa anakuwa anajua kuwa hiki alichonifanyia mwenzi wangu ni kwa kuwa ananipenda?..au kaniona ni 'easy go' nisiyeweza kujisimamia..kuna uzuri wa mkubwa sana wa kuhakikisha mali yako inabaki kuwa ya kwako..Tatizo linaweza kuwa njia unazotumia 'kudhibiti' hiyo mali ibakie kuwa ya kwako..je, zinawaweka karibu au zinaacha maswali mengi kuliko majibu..Fikiria unamzuia mkeo kwenda hata kwenye vikao vya kina mama kisa atakutana na 'mishangingi' ya mjini..

kwa njia moja au nyingine kila mmoja hapa ameshakuwa kwenye mahusiano mengi mpaka ufikie utu uzima,,,,,,,,,,,,,

kuna yale mahusiano unaachiwa free kujifanyia mambo yako na kuna yale yaliyokuwa na ufuatiliaji wa upendo,,,,,,,,,,, sijui umeshalinganishwa matendo/mienendo yako kwenye hayo mahusiano mawili..................

na pia kumuacha mtu free haitoshi kudhani kuwa hatayafanya atakayo kuyafanya,,,,,,,,,,,,

binafsi nitakuwa mstari wa mbele kumlinda mpenzi wangu na hatari mbalimbali kwenye maisha yake ikiwemo hiyo ya kumuweka mbali na vishawishi.
 
hapana dada yangu hata mi hayo maisha ya hivyo yananichefua na wala hayafai hata kidogo na huyo mzee wako alipitiliza na mara nyingi ukikuta mtu anamchunga sana mwenzie wallahi ukija kuambiwa yake unaghairi kusihi naye siku hiyo hiyo,pole dada Nyamayao ila tena hongera maanake naona uliamua kuuvaa uso wa mbuzi na kuwa an iron woman hapo nilipobold nimepapenda kwa kweli maanake kuna watu wanazidi aisee.

baada ya kumbania akalegeza kidogo, alivyopumzika kufanya ule ufirauni wake, akaanza kuniletea za "ubaba ubaba" kwamba hakuna kwenda huko, mbona mitoko imekuwa mingi, nilimwambia weee hii mitoko ndio iliniliwaza kipindi cha masika, sasa hivi yupo level, nikimwambia leo nikitoka job ntaenda mahali fulani kupiga moja atakuambia poa, na mie napiga sijui wapi huku, basi siku zinaenda maisha yanasonga.
 
kidude cha like mie kwangu sikioni jamani, hizi hofu za kuwalinda hawa wanaume zinatupeleka mbali sana!
ha haaa, pole...
reflesh page kitakuja.
kuna dadangu mpaka leo anajuta kupoteza nafasi ya masomo sababu ya mume (siyo watoto)....
mume kamuacha na walikuwa wanabanana kila wanakoenda...... anabaki kunishangaa tu.......
 
sidhani kama utataka hicho kwenye RED kitokee...
niliwahi soma hapa kuwa kuna watu wana simu zinakaa ofisini tu, hiyo namba wenzi wao hawaijui, ni special kwa ajili ya kuchakachulia mahusiano....

hakuna mwanadamu anayependa au anayetaka kitu kinachomuumiza kitokee............kumbuka ule usemi "if you dont know ,it doesnt exist",,,,,,,,,,,,,, na kwa dhana ile ile ya kumuacha mtu free kwa kusema binadamu hachungiki , lakini hapo ameenda extra mile kwa kuyaacha hayo mawasiliano ya hovyo hovyo huko nje ya nyumba na akifika nyumba ni mimi na yeye na siyo mawasiliano na mtu mwingine na zaidi kwasababu kuna tahadhari basi , she/he cant bring the shits at the door steps............ at least ndani ya nyumba amani inakuwepo.
 
Ninachojiuliza hapa ni kuwa ..je,wakti unaweka huo udhibiti wa kulinda ,ali yako na yeye mlengwa anakuwa anajua kuwa hiki alichonifanyia mwenzi wangu ni kwa kuwa ananipenda?..a

ha haaaaa, kama unanipenda, utanilinda..... siyo kunidhibiti, lol!
 
lakini hapo ameenda extra mile kwa kuyaacha hayo mawasiliano ya hovyo hovyo huko nje ya nyumba na akifika nyumba ni mimi na yeye na siyo mawasiliano na mtu mwingine na zaidi kwasababu kuna tahadhari basi , she/he cant bring the shits at the door steps............ at least ndani ya nyumba amani inakuwepo.
wow!
hiki ndo unataka?
I thought unataka kwa kumdhibiti basi aachane na wasiliano yasiyofaa, kumbe ruksa kuyafanyia nje ya nyumba?
 
Nyamayao unadhani sijui hilo dear?

Nikimwacha mdogo wangu wa kike atahalalisha kuwa ni mke na jamii inaweza ona sawa, na hata ndugu zake wanaweza wasiingilie kivilee, nikimwacha ndugu yake wa kike watafanya siri - ndugu zao wakijua panaweza kuwa hata padogo, na believe me you once najua narudi moja kwa moja huyo mwanadada namtafutia utaratibu ambao ni bora zaidi kwake - kama some sort of shukrani kwa kunilelea familia wakati sipo. For sababu najua tabia ya wanaume deep down within me naweza nikawa najiuliza kama they did it or not.

Mie najua, nikiwa mbali na mwanaume wangu for more than 6 months, yeye kuwa hajagusa mwanamke mwingine siwezi kuamini. Suala ambalo kwa kweli sipendi na linaweza niuma ni mwanamke aliyelala nae awe ndugu yangu. Alale tu anavyotaka (kwa heshima na nisijue) but ndugu zangu wa karibu naomba awaache tu. Inauma sana.

mie nadhani wote ni wanawake, alale na nduguyo, nduguye, housegirl etc kwa upande wangu wote itaniuma sana, mana nilitoka huko hakuwa ndugu ila niliumia sanaa, hata kwa ndugu yake unadhani hiyo fedheha ya familia yake haitakuumiza, maneno ya familia yake, unadhani hawatasema/hawatakusema? zamani nilikuwa nikisafiri napeleka watoto na dada kwa dada yangu, kwasasa nawaacha hapo jinsi walivyo, dada aandae kila kitu cha ndani, aweke panapostaili, msukuma abebe funguo zote kuanzia za room kwetu mpaka getini/milangoni, akichelewa afanye yake bila kusumbua wengine, kitanda changu afanyie usafi yeye mpaka nitakaporudi, wakafanya yao "nisigundue tu" dada ni mtu mzima kwangu, nilishamuita kama dada nikaongea nae kiutu uzima, nadhani wote walinielewa, wakiamua wameamua kunifanyia, sitataka tena kuteseka kwa kuhofia "kitaliwa" kisipoliwa ndani "kitalia hata huko nje" nahitaji heshima/adabu yake nyumbani kwangu, akishindwa hilo nadhani nitafikia tamati, kama anahisi ni lazima kufanya basi akafute hukoooo sio kwa kiumbe chochote kilichopo ndani ya nyumba yangu, nina amani kwasasa.
 
…..mimi nakwambia, akheri uachie Upepo uchukue mkondo wake badala ya wewe kuanza 'kuutegea!'
kama hujajua machungu ya kupekua simu ya mwenzio, tegea halafu ukute messages ulizozitegemea #Zimefutwa!

….acha kabisa
hata kuikagua hiyo simu….maana hatua itayofuatia huenda ukaenda hata TiGo au Voda kuomba printout!
Kama sio #Uchizi ni nini hiyo sasa?….

katika watu walisumbukaga basi ni mimi, yaani wakati ule ningeendelea na ile tabia ningechizika, simu yake ikiita roho ilikuwa inanipaa, vidole vinawasha kusoma msg, na nilikuwa nazikuta, hahaha nikikuta msg ninayoihisi na save no kwangu, lol phonebook yangu ilijaa kuliko ya mtuhumiwa, siku nilivyoenda kuleta vagi, ndio siku nilikuwa nikafutilia mbali ma namba yote, sasa hivi hata akisahau simu itaitaaa mpaka akome, hata nikiona ni no ya landline ya ofisini kwake, sipokei apige kwangu aniambie nimpitishie.
 
Back
Top Bottom