Kumdhibiti mpenzi wako!!...ni woga au ndo mapenzi??

Kumdhibiti mpenzi wako!!...ni woga au ndo mapenzi??

ni juzi kati tu hapa mke wa rafiki yake msukuma amenitafuta kuniuliza nimemfanyaje mbona siku hizi msukuma katulia kwake ndio kumekucha sasa, nimsaidie, nikamwambia sina hata nililomfanya, yeye akinywa bia kule mie nakunywa ballantin huku, najiwahia nyumbani natulia na wanangu, sina habari nae na sitakuwa tena na habari nae, ajiheshimu/ajitunze!
ha haaa, kwa raha zako rafiki....
na hivi huna mpango wa kuondoka, kwa nini umkimbize?
 
Nimependa hii paragraph ya habari ya hapa
I wish Blue G na [MENTION]asakusa kunte[/MENTION] wangeisoma pia..

Binafsi ni mtu mzima na akili zangu timamu, nina jua jema na baya, so nikifanya kinyume na kumuudhi mwingine, itakuwa nimeamua tu kufanya hivyo, kuna mambo ya kumkosea mwenzio bila ya kujua, umefanya jambo kwako unaona uko sahihi lkn yy halikumpendeza hapo sawa, yaweza kuwa kwa kuongea imetokea umeropoka km mnavyojua ulimi, pengine umezidisha chumvi kwa chakula na ww bila ya chumvi nyingi huwezi kula na mengine yanayo fanana na hayo,
 
Last edited by a moderator:
dahhhhh hongera sana dada Fixed Point kwanza kwa kujitambua na kujua sehemeu yako kama mke na pili kwa kupata mume mwelewa na tatu kwa kuithamni familia yako kwa ujumla.

ila tu dadaangu kwa mimi udhibiti ule wa kiasi wala haumaanishi kuwa humwamini mwenzi wako ila tu kama alivyofafanua dada AshaDii udhibiti wakati mwingine husaidia kutukumbusha pale ambapo huenda tumelega lega au tunaanza kujisahau au kusahau sehemu katika ndoa zetu na hii ni kwa sababu hatujakamilika so nadhani utakubaliana nami kuwa kutokana na kutokamilika kwetu tunahitaji kukumbushwa nyakati nyingine,na ndio maana makanisa na misikiti ipo si kwa kuwa wanadamu tunafanya dhambi nyakati zote kila saa,dk na sekunde,la ila ni kwa lengo la kutukumbusha mara kwa mara kwa kuwa tuna mapungufu mengi kama wanadamu.sijui point yangu kuhusu udhibiti imeeleweka hapo dada yangu?
mimi ni mke, na ninajua kuwa ni mke wa mtu....
hata nilipokuwa kwa wazazi sikuwahi kurudi saa 8 usiku bila kuwaambia wazazi wangu kuwa naenda wapi na nitachelewa kurudi. nyumbani kwangu napenda (mimi pia nafanya hivyo) ninapoona nitachelewa kurudi nyumbani hata kama kwa nusu saa, huwa natoa taarifa kuwa nitachelewa kurudi. huwa nafanya hivi hata kwa msichana wa kazi. ikitokea mume kasafiri na nitachelewa kurudi huwa nampigia dada wa kazi kumwambia kuwa nitachelewa kurudi nyumbani.
huwa napenda kutoa taarifa siyo sababu nisifikiriwe vibaya, ila sababu mtu asiwe na wasiwasi kuwa nipo salama au la. mimi ni binadamu, chochote kinaweza nipata. mtu ajue kuwa nipo salama ila nimechelewa tu kurudi.
mdogo wangu, asilimia kubwa sana ya rafiki zangu ni wakaka, nje na ofisini. kwa hiyo huwa anajua kabisa nawasiliana/kutoka zaidi na wakaka kuliko wadada, na yupo sawa tu kwa hilo.
 
Last edited by a moderator:
AshaDii swala la mahousegirl limekuwa overated sana, kiasi kwamba wanaume ndio wamepatia utetezi wao kwa ubazazi wao.
Mbona wanatembea na ndugu au step daughters wao, Mbona hawatembei na wahudumu wa hoteli wanaowatandikia vitanda? Uhusiano wa kutandika kitanda na mwanaume kutembea na dada ni upi? Kuna tofauti gani na kufuta vumbi tv, au kusafisha choo. Wanawaonea helpless n sometimes innocents maids kwa udhalimu wao tu.

mwanaume yoyote anaetembea nje ya ndoa yake ni bazazi, atembee na housegirl,dada wa saloon sijui bar sijui Manager, wote ni ubazazi/ulafi tu, na wanatupeleka pabaya sana na haya mambo yao, mie sasa hivi nimemwachia aisee, sitafuti mjukuu wa mtu ooh sijui uko wapi oooh mpaka saa hizi, nimeshakuwa mie.
 
Nawaachaje bila msichana wa kazi?

Katika the career world wanawake tuna disadvantage kubwa sana. Naamini kuna wanawake wengi tu walio ndani ya ndoa walipata opportunities za kuendeleza career zao na walikwama sababu tu ya nafasi na majukumu yao ndani ya familia.

Inategemea age ya watoto, circumstances and the like. You would understand why sometimes I would prefer to kijana wa kazi wa kiume, na why sometimes I would prefer kua na ndugu wa kike upande wa mume ndie aje abaki hapo nyumbani. Like you say, haya mambo ni magumu sana.
 
Unadhani ukishajenga dhana ya ukaguzi utaacha kufikia hapo nilipobold?..
Ukishalijenga mawazoni wazo la kuwa huyu ataniumiza soon..huwezi kujizuia kushika simu yake..believe me!

...Kudhibiti kwapaswa mtu ajue wapi mpaka wake. Suala la kukagua kagua simu kila mara ni kujitafutia tu matatizo.
 
ha haaa, kwa raha zako rafiki....
na hivi huna mpango wa kuondoka, kwa nini umkimbize?

tulipofikia nadhani yeye ndio aondoke aniachie nyumba, aende kwa amani ya bwana Yesu! kama vipi tutatafutana uzeeni huko, lakini cha kushangaza sasa hivi yeye anaumia sana, anahisi mambo yasiyokuwepo, ile mtafutano kumbe ulikuwa unampa kichwa? sasa hivi anahisi kama namtenga fulani au nina mambo yangu, mie mtoto wa watu sina hili wala lile, ni kwamba hata akirudia tabia zake za kurudi saa 8 za mausiku hataona call/sms yangu ya kumuuliza, amalize starehe zake arudi nyumbani.
 
….JF ni kisima cha fikra, experiences na busara….

Okay..kwa hiyo unachosema ni 'scale' ya udhibiti kupishana..ryte?
Lakini tukatae tukubali kwenye aina yeyote ya udhibiti woga na kutojiamini kunakuwa kukubwa kuliko hata mapenzi yenyewe..hivi
kama najitambua mkewangu anashindwaje kuniamini hata ninapokuwa na wadogo zake?
Ni kwa vipi nisiamini tu kuwa mkewangu yupo jf kwa nia njema
Kwa nini nihangaike na mi'passwords'?...lazima kuna sehemu lipo tatizo
Aidha ni woga ulonijaa/wivu ulopevuka au mwenzangu ni kicheche..

….hayo unayojiuliza, yamejibiwa vyema kabisa na….

lakini ilinipa fundisho/ujasiri/kujiamini sana, sasa hivi mpaka mwenyewe anashangaa kwanza ndio ana wasiwasi na mie balaa,ameshangaa yule mcharuko wake amekuwaje siku hizi, anahisi yasiyopo na matisho juu.
 
Unadhani ukishajenga dhana ya ukaguzi utaacha kufikia hapo nilipobold?..
Ukishalijenga mawazoni wazo la kuwa huyu ataniumiza soon..huwezi kujizuia kushika simu yake..believe me!

SnowBall, aidha hujanielewa au unafanya makusudi.... Lol

Sijasema mahala popote I support ukaguzi, so far from what I know kudhibiti na ukaguzi ni vitu viwili tofauti. Tabia ya kugagua kagua kwa taarifa yako wengine si tu wanafanya sababu ya wivu, wengine ni tabia. Mtu mwingine hata akipata mgeni nyumbani kwake akaenda washroom atataka kukagua kwenye pochi kuna nini, yaani yeye furaha yake ni kupekua pekua tu.

Suala la kupekua simu si msingi na wala si afya kwa mahusiano, sababu hata kama mpenzi wako hafanyi lolote anakua hapendi na kujisikia vibaya wamchukulia sivyo. Ila kuna rare cases kitu kinaweza kutokea na kukusukuma kutaka kujua zaidi kwa kuangalia simu. Hilo ni tofauti kabisa na kujenga tabia ya kukagua kagua simu kila mara na kila siku bila sababu za msingi.

It should be noted however, si kila mara mpenzi wako akishika simu anakua anakagua. Simu za sasas zina features nyingi, saa ingine unaweza shika simu with genuine reasons wala hata una interest na chats or msgs.
 
dahhhhh hongera sana dada Fixed Point kwanza kwa kujitambua na kujua sehemeu yako kama mke na pili kwa kupata mume mwelewa na tatu kwa kuithamni familia yako kwa ujumla.

ila tu dadaangu kwa mimi udhibiti ule wa kiasi wala haumaanishi kuwa humwamini mwenzi wako ila tu kama alivyofafanua dada AshaDii udhibiti wakati mwingine husaidia kutukumbusha pale ambapo huenda tumelega lega au tunaanza kujisahau au kusahau sehemu katika ndoa zetu na hii ni kwa sababu hatujakamilika so nadhani utakubaliana nami kuwa kutokana na kutokamilika kwetu tunahitaji kukumbushwa nyakati nyingine,na ndio maana makanisa na misikiti ipo si kwa kuwa wanadamu tunafanya dhambi nyakati zote kila saa,dk na sekunde,la ila ni kwa lengo la kutukumbusha mara kwa mara kwa kuwa tuna mapungufu mengi kama wanadamu.sijui point yangu kuhusu udhibiti imeeleweka hapo dada yangu?
yaani mdogo wangu, na utu uzima wangu huu, ukiona nasaliti ujue nimeamua, sihitaji kukumbushwa kuwa sipaswi kusaliti... na nikiona unanifwatilia nisisaliti nitatafuta njia nyingine ya kupita ili usinikamate. kwa hiyo wewe kila siku kazi yako itakuwa kufwatilia mbinu zangu mpya za kunikamata? utaweza?
 
hapo nilipobold SnowBall ndipo wengi wanapoharibu hiyo tunaita ni kutomwamini yule uliyenaye na ni udhibiti uliopita kiasi ambao haufai na unaweza kumpelekea mtu kufanya kweli,lakini udhibiti ninaouunga mono hapa ni ule aliojaribu kuudadavua vizuri sana pale dada AshaDii,wanadamu hatujakamilika na kwa hiyo huenda kuna wakati unaweza anza lega lega na hivyo kuhitaji kikumbusho na hapo ndipo ule udhibiti wa kiasi unapokuwa unahitajika.

wakati kasheshe yangu inaisha isha, ile kumsamehe na kusonga na maisha alinianziaga hizo, umeshafika nyumbani? basi nipe "nanihii" niongee nae, nilikuwa namwambia piga simu ya mezani uongee na wanao kwanini yangu? ujinga mtupu we nimeshakuambia nipo nyumbani ndio utake kuhakiki ukiwa bar kwamba nipo nyumbani via kuongea na mwanao?
 
kweli kabisa unaamini ukiwa unapekua simu ya mpenzio ataacha kukusaliti? kweli kabisa?
umeshawahi kuwasikia watoto wakikatazana kufanya kitu fulani sababu mama kakataza?
mara nyingi napendaga sana kufanyia kazi zangu nyumbani, huwa najifungia chumbani kwangu kiasi kwamba watoto hawajui kama nipo ndani. utasikia tu huko nje wanaonyana "wewe usishike hapo mama anasema utanaswa", natabasamu tu kuona somo limeingia

naamini ataacha mawasiliano ya hovyo hovyo yasiyokuwa na muelekeo mzuri na hata akifanya atayafanya kwa tahadhari sana..................

hakuna uhuru usiokuwa na mipaka,,,,,,,,,,, kubali kataa vishawishi vipo na mpenzi wako kukulinda hupunguza Risk ya kutumbukia kwenye vishawish.

na je kwasababu watoto wenu wanatambu kuwa ukishika sehemu mama alisema tutanaswa basi tutawaachia tu wawe karibu na hatari hizo?
 
mimi ni mke, na ninajua kuwa ni mke wa mtu....
hata nilipokuwa kwa wazazi sikuwahi kurudi saa 8 usiku bila kuwaambia wazazi wangu kuwa naenda wapi na nitachelewa kurudi. nyumbani kwangu napenda (mimi pia nafanya hivyo) ninapoona nitachelewa kurudi nyumbani hata kama kwa nusu saa, huwa natoa taarifa kuwa nitachelewa kurudi. huwa nafanya hivi hata kwa msichana wa kazi. ikitokea mume kasafiri na nitachelewa kurudi huwa nampigia dada wa kazi kumwambia kuwa nitachelewa kurudi nyumbani.
huwa napenda kutoa taarifa siyo sababu nisifikiriwe vibaya, ila sababu mtu asiwe na wasiwasi kuwa nipo salama au la. mimi ni binadamu, chochote kinaweza nipata. mtu ajue kuwa nipo salama ila nimechelewa tu kurudi.
mdogo wangu, asilimia kubwa sana ya rafiki zangu ni wakaka, nje na ofisini. kwa hiyo huwa anajua kabisa nawasiliana/kutoka zaidi na wakaka kuliko wadada, na yupo sawa tu kwa hilo.

Hii post yako FP ni sababu tosha ya kufanya udhibiti. Si wanaume wote wamebahatika kama alivyo bahatika mume wako kwa kuoa mwanamke anae jitambua hivi. Huwa inapendezana kuleta saana raha; mwanamke anapo kua anajielewa kwa kiasi hiki.

Wengine walioa wanawake waliokutana nao Disco saa 8 usiku. Hao wakioana; kudhibitiana muhimu Lol
 
…..mimi nakwambia, akheri uachie Upepo uchukue mkondo wake badala ya wewe kuanza 'kuutegea!'
kama hujajua machungu ya kupekua simu ya mwenzio, tegea halafu ukute messages ulizozitegemea #Zimefutwa!

….acha kabisa
hata kuikagua hiyo simu….maana hatua itayofuatia huenda ukaenda hata TiGo au Voda kuomba printout!
Kama sio #Uchizi ni nini hiyo sasa?….

Unadhani ukishajenga dhana ya ukaguzi utaacha kufikia hapo nilipobold?..
Ukishalijenga mawazoni wazo la kuwa huyu ataniumiza soon..huwezi kujizuia kushika simu yake..believe me!
 
Labda kwanza tujue udhibiti ni nini SnowBall,udhibiti ni ile hali ya kuwekeana mipaka labda au vigezo fulani vya namna ya kuendesha maisha yenu kama vile saa za kurudi nyumbani,kampani yenu na hata aina ya mavazi.

Lakini linapokuja swala la kupekua simu ya mume/mke au kutaka mapassword na hata kushindwa kumuamini mke/mume wako hata anapokuwa hata na baadhi ya ndugu zake/zako hapo tumeshatoka kwenye udhibiti na kuja kwenye kumchunga mtu au kukosa kumuamini yeye kama yeye na jinsi anvyoishi na wewe na kuhisi labda kuna aina nyingine ya maisha zaidi anayoishi pengine nyuma yako na kwenye hayo mapassword au akiwa na watu wengine tofauti na wewe

Na hii huchangiwa pengine na nyendo za mmojawapo kwenye uhusiano kuonyesha dalili za hatari au kubadilisha namna fulani ya kuishi kulikozoleka ndani ya ndoa yenu nadhani hapo hata kama nini wewe SnowBall ni lazima taa nyekundu iwake kichwani ukiona mke kabadilisha mtindo maisha mliouzoelea na kuanza kuishi kivingine tena kinamna isiyokuridhisha hapo lazima uchunguzi utaanza kufanyika hata kama si kuomba mapassword yake,labda hata kwa kuanza kuchunguza anashinda na watu gani anatembela maeneo gani kimyakimya kwanza ili hatimaye ujue nini chanzo cha hiyo transformation,sijui nimeelekwa kaka SnowBall?

Na linapotokea swala la kuanza kumchunguza mwenzi mara baada ya kuona mabadiliko yanayomtishia mtu amani au mtindo maisha uliozoeleka ndani ya nyumba wala hakuna ubaya kwani hapo mtu anajaribu kupigania penzi lake,lakini kwa yule ambaye ye ni asili yake tu yaani aone asione mabadiliko mibano ipo pale pale huyo ndo tunamuweka kwenye kundi la watu wasiojiamini na walio na woga.
Okay..kwa hiyo unachosema ni 'scale' ya udhibiti kupishana..ryte?
Lakini tukatae tukubali kwenye aina yeyote ya udhibiti woga na kutojiamini kunakuwa kukubwa kuliko hata mapenzi yenyewe..hivi kama najitambua mkewangu anashindwaje kuniamini hata ninapokuwa na wadogo zake?
Ni kwa vipi nisiamini tu kuwa mkewangu yupo jf kwa nia njema
Kwa nini nihangaike na mi'passwords'?...lazima kuna sehemu lipo tatizo
Aidha ni woga ulonijaa/wivu ulopevuka au mwenzangu ni kicheche..
 
Last edited by a moderator:
Katika the career world wanawake tuna disadvantage kubwa sana. Naamini kuna wanawake wengi tu walio ndani ya ndoa walipata opportunities za kuendeleza career zao na walikwama sababu tu ya nafasi na majukumu yao ndani ya familia.

Inategemea age ya watoto, circumstances and the like. You would understand why sometimes I would prefer to kijana wa kazi wa kiume, na why sometimes I would prefer kua na ndugu wa kike upande wa mume ndie aje abaki hapo nyumbani. Like you say, haya mambo ni magumu sana.

tuseme hivi, haya mambo hayatabiriki, kabisaaa, mwanaume mlafi ni mlafi tu hata ufanyaje, ndugu wa mume? ndugu wenyewe hao ni wale wa damu ya kiumbali kidogo, atashindwa kutembea nae? hujasikia hizo kesi mbona kibao sana na kuna mada nilichangiaga kitambo fulani kwamba rafiki yangu alimleta mtoto wa dada yake mume amsaidie kazi za nyumbani na mwanaume alimla? kwenye hili simuamini mwanaume kabisa akiamua kufanya ufirauni ataufanya tu.
 
.Nilitolea mfano..kwa sababu huwa inatokea wenzi wanakuwa tayari wako kwenye udhibiti..
Hujawahi kusikia kwamba..'kama uko sehemu flani basi nipe flani niongee naye'?
Na nimeongelea udhibiti wa wazi ambapo mlengwa anajua kabisa anachungwa..
Sikatai kuwa na 'doubts' na mwenzio..lakini je umejiridhisha vya kutosha?
Na kama umejiridhisha uko tayari kwa maamuzi magumu in case...

kwa njia moja au nyingine kila mmoja hapa ameshakuwa kwenye mahusiano mengi mpaka ufikie utu uzima,,,,,,,,,,,,,

kuna yale mahusiano unaachiwa free kujifanyia mambo yako na kuna yale yaliyokuwa na ufuatiliaji wa upendo,,,,,,,,,,, sijui umeshalinganishwa matendo/mienendo yako kwenye hayo mahusiano mawili..................

na pia kumuacha mtu free haitoshi kudhani kuwa hatayafanya atakayo kuyafanya,,,,,,,,,,,,

binafsi nitakuwa mstari wa mbele kumlinda mpenzi wangu na hatari mbalimbali kwenye maisha yake ikiwemo hiyo ya kumuweka mbali na vishawishi.
 
Katika the career world wanawake tuna disadvantage kubwa sana. Naamini kuna wanawake wengi tu walio ndani ya ndoa walipata opportunities za kuendeleza career zao na walikwama sababu tu ya nafasi na majukumu yao ndani ya familia.

Inategemea age ya watoto, circumstances and the like. You would understand why sometimes I would prefer to kijana wa kazi wa kiume, na why sometimes I would prefer kua na ndugu wa kike upande wa mume ndie aje abaki hapo nyumbani. Like you say, haya mambo ni magumu sana.
Naomba kila mtu anayesoma hapa anisamehe tu......
kati ya vitu niliwahi kusema sita-compromise katika maisha yangu ni career yangu.... kwa kitu chochote kile.
Nilipozaliwa, nikiwa na miezi mi3 mama alipata nafasi ya kwenda kusoma, aliniacha akaenda shule. mpaka leo namshukuru kwa nuniacha nyumbani na kuchagua kwenda shule.
Nimeolewa nikiwa undergraduate, tena mwaka wa kwanza, na nikazaa mtoto wangu muda huo huo..... mpaka leo sijutii kuacha wanangu na kuendelea na masomo...... napenda sana wanangu, na nitafanya kila kitu kwa ajili yao, nafanya yote kwa ajili ya familia yangu.
kuna wamama wengi sana walioacha kujiendeleza sababu ya familia zao (kuna watu wa karibu sana na mimi waliofanya hivyo) mpaka sasa wanajutia maamuzi yao.
hapa tuelewane kuwa sijasema kukaa nje ya familia ni bora kuliko kuwa na familia
unaweza kaa na familia na mambo yasiwe kama vile unavyotaka yawe, fanya kitu unachoona kinafaa kwa manufaa ya familia yako
 
….JF ni kisima cha fikra, experiences na busara….

….hayo unayojiuliza, yamejibiwa vyema kabisa na….

ndipo hapo ninaposema, siku hizi msukuma amepata uhuru mpaka anajishtukia mwenyewe, achia mbali kuwa na ndugu zangu hata aniambie sijui kakutana na rafiki yangu bar gani wanapata moja wala mshipa haunishtuki, ni mtu mzima/ajichunge/ajilinde/ajiheshimu.
 
haaaaahaaaaaaaahaaaaaaa umetisha dada yangu na nimekuelewa vizuri sina nyongeza na kwa kweli ndivyo ilivyo kumlinda linda mtu wala si tija mtu mwenyewe akishajua kipi kinafaa na kipi hakifai bassiii mambo yote yanaenda vizuri tu.

Back
Top Bottom