Kumdhibiti mpenzi wako!!...ni woga au ndo mapenzi??

Kumdhibiti mpenzi wako!!...ni woga au ndo mapenzi??

Wakati mwingine wasiwasi wangu unakuwa kwa yule unayehangaika kumchunga na kuweka mitego ya kumdhibiti..
Je, anaweza kuona 'cencern' yako au ataona ni usumbufu na kwamba 'humuamini' katika nyendo zake?
Je, huoni hii inaweza kupelekea mhisiwa kuamua kuwa 'victim' moja kwa moja kwa sababu mazingira ubayojenga yanaonyesha haaminiki. Kama ni mwanamke anaweza kuamua 'kukupa penzi la unafiki'...kumbuka pia mwanadamu anao utashi ambao hauondoki hata kama kaolewa/kaoa...Kuna mtu yeye ni msemaji tu...kuanza kumwekea mipaka ya usemaji wake ni kama kumdictate..ultimately ataishi na wewe a fake life kwa sababu hafanyi kile kilichomo ndani yake....

Ofcourse, mimi nikichunguzwa sana itanidisappoint pengine kuniuma; maana nitakitafsiri hicho kitendo ni kutoniamini. Na huenda nikaenda mbali zaidi, kuwa kama haniamini ina maana naye si muaminifu.

You are right, waweza hata mpa wazo la kucheat kwa kumfuatilia sana. Umeshamtuhumu au kumpaka shombe, kwanini asimle samaki kabisa.

Juu pale nilijaribu tu kutafakari kwanini watu wanakuwa na hofu inayowapelekea kuanza kufuatilia wenzi wao.
Binafsi huwa nasema as long as umenipenda mimi Kaunga, na the fact kwamba Kaunga niko peke yangu duniani basi sina shaka. Lakini pia si ulianza kunipenda, hivyo kuna siku utaacha kunipenda so mapenzi yako yakiisha basi niambie ili nikupe go ahead.
Huo msimamo wangu haufanyi kazi kama sababu ya kuwa pamoja sio mapenzi, mfano tumeunganika kwa ajili ya convinience (mimba), au makaratasi kwa wale wabeba maboksi, au wazazi etc.
 
mtu anatakiwa ajue mipaka yake yeye mwenyewe, utamdhibiti mara ngapi?
na akishazoea kudhibitiwa basi ikatokea mitego ambayo wewe hujaiona basi atanaswa, sababu hakuna wa kumdhibiti.
rafiki yangu jiulize hapo ulipo ni mara ngapi umekutana na mitego ambapo mpenzi wako hajui? uliingia au uliweza kujinasua? kama uliweza kujinasua bila yeye kujua huko ndo kunaitwa kujitambua, na binadamu anatakiwa awe hivyo, ajitambue, yeye mwenyewe.
mimi sikubaliani kabisa kusema kuwa mtu aliingia majaribuni, ina maana hakujijua wakati anaingia? ni kwamba huyu jamaa anaingia majaribuni kwa kila mtego? kama mingine anaweza kuidhibiti, kwa nini huu aingie?

Naamini pia katika mtu kujidhibiti mwenyewe. Ila kumbuka kuwa mahusiano ni team effort, mwanadamu is capable of anything na ndio maana kuna kusalitiana. Ndio maana nikatoa angalizo kua kuna mipaka ya kudhibiti. Ni ngumu kuelezea udhibiti kwa kutumia neno lenye udhibiti sababu linatoka vibaya na watu wengi wanalichukulia kana kwamba ni hali ya kuchunga. Sio hivyo.

Nakupa mfano wa kudhibiti. Unapokua wewe ni mke na waishi na mumeo na family members wengine ndugu na jamaa, linapokuja kwa mabinti lets say binti wa kazi; mwanamke una nafasi kubwa ya kuchangia mumeo alale ama asilale na huyo binti. Unapomwachia huyo binti ndie amhudumie mumeo, ndie awatandikie kitanda chumbani na kuwafanyia usafi na akazoea kuingia chumbani kwako mda wowote, unapo mwachia nyumba mda mrefu wewe mwenyewe mke haupo na she takes care of your husband unarahisisha mumeo kulala na huyo binti.

So kuna mipaka ambayo binti wa kazi inapaswa awe nayo kwa mume wako. Hiyo mipaka tayari ni moja ya namna ya kudhibiti. Na hio ni one of the cases ni applicable. As much as yeye mwanaume ndie hasa inapaswa kutovuka huo mstari kwa kulala na huyo binti wa kazi.

Nikija suala la kujitambua... FP bahati mbaya saana, watu wanajitambua ila morals of what they can do and not do zimepishana. Unaweza ukawa una mume/mke anajitambua vizuri tu, ila si sababu ya wewe kushindwa kumdhibiti. Kudhibiti kuna umuhimu katika mahusiano ili mradi iwe within reason na isivuke mpaka.
 
Well said Fixed Point
Na ndicho nilichomuambia Blue G kuwa..mapenzi lazima yaambatane na kuheshmu nidhamu ya maisha ya kila mmoja..Nidhamu ambayo inaambatana na uhuru wa kutenda na kuamua pasi na kushurutishwa...kuanza kudhibitiana inaweza kuonyesha 'udikteta' na kulazimishana kutenda hata yale tusiyoyaamini..huoni hii inatupeleka kwenye penzi la unafiki?
Na ukishakubali kudhibitika unaeza kujikuta unaishi maisha feki...

Last edited by a moderator:
Fixed Point na mimi ndo ninachokisema..unamdhibitije mwenzio?
Nadhani kuna haja ya kuwekana sawa na kila mtu amjue mwenzie beforehand..lakini hii habari ya 'uspy'..lolz
Kwa sisi wanaume naona hili limezidi sana..lakini kwa nini tufike huko?
Mie naona ile tu mwenzio kujua 'humuamini' inapunguza hata kile kilichokuwepo..
kama kweli huaminiki ni swala jingine, but kama najiamini mwenyewe sichepuki, halafu unaniletea zako za kukagua simu yangu, mbona itakula kwako!
kuna watu kama mimi tunapenda sana stori, na nikiri wazi kabisa sometimes sijui mipaka yangu ya kuongea na mtu as long as simuudhi. nje ya stori ni muoga saaanaaaa. sasa ukitaka kuchunguza stori zangu, utanihukumu kwa vitu ambavyo sivifanyi na wala hata sifikirii kuvifanya
 
AshaDii nimekusoma vizuri sana dadaangu..Kwanza hujambo?...long tyme ujue?
Back to the topic ..mie concern yangu ni kuwa hata kama tuko kwenye mahusiano/mapenzi..lakini as individuals kila mtu anao uhuru na nidhamu yake ya kutenda. Na beforehand natambua mtakuwa mshafahamiana vya kutosha kuhusu individuals characters..na kama mnaoana obvious kila mtu anakuwa amekubaliana na mwenzie.

Mie mzima kabisa SnowBall na nafurahi kukuona hapa.

Naomba niseme kuna kitu nadhani unachukulia for granted. Kana kwamba wanadamu wote tunaweza behave the same way. Sio kweli. Ingekua hivyo it would have been so simple.

Mahusiano ya mapenzi ni sawa tu na mahusiano hata ya kikazi. Unaweza kuwa una kampuni yako, una mfanyakazi mchapa kazi sana na utendaji wake ni mzuri, anakufurahisha na kukuridhisha kwa kila namna kiasi kwamba hata wateja na wafanya kazi wenzake wanamkubali. BUT unatambua ana madhaifu, na dhaifu moja kubwa kuliko zote ni yeye kupenda pesa na saa ingine kufanya maamuzi damaging sababu tu anapenda pesa - Utamwachia tu sababu anapenda pesa ambayo inamfanya awe na maamuzi mabovu? Nadhani to most itakua hapana.

Utajitahidi kumdhibiti kwa kuhakikisha unaweka mazingira ya yeye kuwa na pesa consistent, aidha kwa kumpa mshahara mkubwa anao deserve, kumpa marupu rupu, na once in a while kumpa hata lecture ya matatizo ya kuweka pesa mbele. 🙂 Else unaweza jikuta unamfukuza kazi, unaishia kupata mfanyakazi mwingine ambae kichwa gongana na kukuaribia kabisa biashara.
 
AshaDii swala la mahousegirl limekuwa overated sana, kiasi kwamba wanaume ndio wamepatia utetezi wao kwa ubazazi wao.
Mbona wanatembea na ndugu au step daughters wao, Mbona hawatembei na wahudumu wa hoteli wanaowatandikia vitanda? Uhusiano wa kutandika kitanda na mwanaume kutembea na dada ni upi? Kuna tofauti gani na kufuta vumbi tv, au kusafisha choo. Wanawaonea helpless n sometimes innocents maids kwa udhalimu wao tu.
 
Last edited by a moderator:
Of course ndicho ninachosema na mimi hapa Kaunga kuwa 'kimsingi kila afanyae jambo baya anajua kuwa ni baya' na ndio maana anajificha. Kumuwazia mtu vibaya kwa kutumia 'precedence' za watu wengine inaweza pia kumkwaza japokuwa inalenga kudumisha penzi...Kama ulivyoshauri..udhibiti unafaa sana hasa pale unapokuwa na 'clues' zinazoaashiria kutokuwepo kwa uaminifu kwa mwenzi wako..Ila u need to be careful..kwa sababu badala ya kutengeneza waweza kuta ndo unaharibu kabisa..

Ofcourse, mimi nikichunguzwa sana itanidisappoint pengine kuniuma; maana nitakitafsiri hicho kitendo ni kutoniamini. Na huenda nikaenda mbali zaidi, kuwa kama haniamini ina maana naye si muaminifu.

You are right, waweza hata mpa wazo la kucheat kwa kumfuatilia sana. Umeshamtuhumu au kumpaka shombe, kwanini asimle samaki kabisa.

Juu pale nilijaribu tu kutafakari kwanini watu wanakuwa na hofu inayowapelekea kuanza kufuatilia wenzi wao.
Binafsi huwa nasema as long as umenipenda mimi Kaunga, na the fact kwamba Kaunga niko peke yangu duniani basi sina shaka. Lakini pia si ulianza kunipenda, hivyo kuna siku utaacha kunipenda so mapenzi yako yakiisha basi niambie ili nikupe go ahead.
Huo msimamo wangu haufanyi kazi kama sababu ya kuwa pamoja sio mapenzi, mfano tumeunganika kwa ajili ya convinience (mimba), au makaratasi kwa wale wabeba maboksi, au wazazi etc.
 
Last edited by a moderator:
Kumdhibiti mtu? mzima wa afya? na akili zake timamu!
hii kazi sitaifanya, hata kwa wanangu.
mamangu alikuwa anatuambia sisi tumeshakuwa watu wenye akili timamu tangu tulipoanza sekondari, na kwa maana hiyo hatamfwatilia mtu nyendo zake nje ya nyumbani, hana huo muda na hataki kuwa kichaa. la maana alikuwa anatuambia madhara ya kuwa na matendo maovu..... kupata mimba zisizotarajiwa, kuambukizwa magonjwa, kushindwa kuendelea vizuri na masomo na vitu kama hivyo. kila mtu alipewa uhuru wa kuchagua analotaka kulifanya. na ukweli sikuwahi kufanya lolote ambalo nilijua mama hapendi, sababu sikutaka kuingia kwenye matatizo aliyoyasema....
hata sasa nilishasema sichungi mtu, namchungaje kwanza? simu? ofisini? bar? safarini? kwa nini haswa nimchunge?

mie nilijaribu hilo but madhara yake ni maumivu matupu, nilichunga/chunguza mpaka nikafumania, nikaumia sana, nimeacha kuchucga/chunguza kajituliza mwenyewe, sujui kwanini nilichungaga nikajiumiza vile.
 
Naamini pia katika mtu kujidhibiti mwenyewe. Ila kumbuka kuwa mahusiano ni team effort, mwanadamu is capable of anything na ndio maana kuna kusalitiana. Ndio maana nikatoa angalizo kua kuna mipaka ya kudhibiti. Ni ngumu kuelezea udhibiti kwa kutumia neno lenye udhibiti sababu linatoka vibaya na watu wengi wanalichukulia kana kwamba ni hali ya kuchunga. Sio hivyo.

Nakupa mfano wa kudhibiti. Unapokua wewe ni mke na waishi na mumeo na family members wengine ndugu na jamaa, linapokuja kwa mabinti lets say binti wa kazi; mwanamke una nafasi kubwa ya kuchangia mumeo alale ama asilale na huyo binti. Unapomwachia huyo binti ndie amhudumie mumeo, ndie awatandikie kitanda chumbani na kuwafanyia usafi na akazoea kuingia chumbani kwako mda wowote, unapo mwachia nyumba mda mrefu wewe mwenyewe mke haupo na she takes care of your husband unarahisisha mumeo kulala na huyo binti.

So kuna mipaka ambayo binti wa kazi inapaswa awe nayo kwa mume wako. Hiyo mipaka tayari ni moja ya namna ya kudhibiti. Na hio ni one of the cases ni applicable. As much as yeye mwanaume ndie hasa inapaswa kutovuka huo mstari kwa kulala na huyo binti wa kazi.

Nikija suala la kujitambua... FP bahati mbaya saana, watu wanajitambua ila morals of what they can do and not do zimepishana. Unaweza ukawa una mume/mke anajitambua vizuri tu, ila si sababu ya wewe kushindwa kumdhibiti. Kudhibiti kuna umuhimu katika mahusiano ili mradi iwe within reason na isivuke mpaka.
nakuelewa sana unachosema my dear friend, lakini kuna mambo mengi sana hapa tunatakiwa kuyazingatia....
sisi ni binadamu na kama binadamu kuna mambo mengi sana ambayo tunatakiwa kuyafanya kukamilisha maisha yetu.
wakati nakua niliwahi kuishi na kakangu kwenye nyumba ya kupanga. kuna mama alikuwa anaishi na mumewe, huyo mama alikuwa mama wa nyumbani mwenye watoto. alikuwa anaishi na wasichana wa kazi wamsaidie watoto. mimi ni shuhuda, wasichana wake walikuwa wanafanya kazi za watoto tu, lakini yule dada alikuwa anapata shida sana na wasichana wa kazi sababu mumewe alikuwa anatembea na kila msichana anayemleta.
sisi wamama au hata hao wababa, kuna kipindi wanalazimika kuwa nje ya nyumbani kikazi au masomo, tuwe tunaambatana na wenzetu?
 
nimekusoma vilivyo SnowBall lakini ninachojaribu kukiongelea hapa si kule kuchunguzana au kuwekeana ulinzi au kupelelezana kusiko na kichwa wala miguu,kama tu nilivyotangulia kusema udhibiti huja tu wenyewe automatically na hii ni kwa sababu udhibiti hutokana na wivu mara nyingi na they say there is no love without jelous,na udhibiti ambao mimi binafsi siuonei shida wala taabu ni kama ule wa kuwekewa limit labda ya kufika nyumbani hii ikionyesha anajali usalama wako,au udhibiti wa watu unaozumgumza nao mara kwa mara akitaka kujua ni wa aina gani na wana influence gani kwako hii ikiwa kama wonyesho wa kujali sana mwenendo wako na hali yako nzuri,vitu kama hivyo havimnyimi mtu uhuru bali vinamkubusha kuwa he or she belongs to someone and not to her or himself,sikui nimeeleweka kaka yangu?
Blue G kimsingi kila mwanadamu anapaswa kuwa na nidhamu aliojijengea kwenye maisha yake.
Nidhamu ile inaambatana na uhuru wa kutenda na kuamua pasi na kushurutishwa...kuanza kudhibitiana inaweza kuonyesha 'udikteta' na kulazimishana kutenda hata yale tusiyoyaamini..huoni hii inatupeleka kwenye penzi la unafiki?
Na ukishakubali kudhibitika unaeza kujikuta unaishi maisha feki....
 
Last edited by a moderator:
Wakati mwingine hapa huwa ndo panaleta hatari zaidi..
Unaweza kufikiri unajenga kumbe unabomoa..
Fikiria mkeo kakuambia niko nyumbani...mara hebu mpe mwanangu simu niongee naye!
Tayari vitu kama hvi vinaanza kumuonyesha kuwa humuamini..
Na akishajua kuwa humuamini anakosa 'confidence'..

mkuu namaanisha unafuatilia mwenendo wa maisha yake muda wote kujua yupo wapi anafanya nini yupo na kina nani , madhumuni ya matendo yake n.k................. njia unayotumia inaweza ikwa physically au kidigitalia zaidi...........

mkuu kuwa na mazoea ya kumuuliza mpenzi wako sasa hivi upo wapi , au kumjengea mazoea ya kuwa mnaagana kila unapotoka sehemu moja kwenda nyingine ni hatua kubwa sana katika kujua ukweli............

maswali ya kawaida , mepesi kujibu huwa yanatoa majibu magumu sana kwenye mahusiano............
 
Well said Fixed Point
Na ndicho nilichomuambia Blue G kuwa..mapenzi lazima yaambatane na kuheshmu nidhamu ya maisha ya kila mmoja..Nidhamu ambayo inaambatana na uhuru wa kutenda na kuamua pasi na kushurutishwa...kuanza kudhibitiana inaweza kuonyesha 'udikteta' na kulazimishana kutenda hata yale tusiyoyaamini..huoni hii inatupeleka kwenye penzi la unafiki?
Na ukishakubali kudhibitika unaeza kujikuta unaishi maisha feki...
umeona eeehhh! na binadamu tulivyo wabaya ukigundua unachunguzwa unatafuta njia nyingine ambayo itazidi kukuficha...
hii nimeshuhudia sana kwa watu wengi wanaochungwa..... ukichungwa ndo unapanua akili ya kujificha zaidi, what is the use?
 
AshaDii swala la mahousegirl limekuwa overated sana, kiasi kwamba wanaume ndio wamepatia utetezi wao kwa ubazazi wao.
Mbona wanatembea na ndugu au step daughters wao, Mbona hawatembei na wahudumu wa hoteli wanaowatandikia vitanda? Uhusiano wa kutandika kitanda na mwanaume kutembea na dada ni upi? Kuna tofauti gani na kufuta vumbi tv, au kusafisha choo. Wanawaonea helpless n sometimes innocents maids kwa udhalimu wao tu.

Kaunga, nimezungumzia housegal because ni rahisi. Kama mzazi au dada inauma sana kusikia mume katembea na mwanao or mdogo wako.

Hilo sasa ndio mfano mzuri saana. Kudhibiti ni muhimu saana, call me old fashioned or not, mdogo wangu wa kike, rafiki yangu wa kike azoeane but kwa heshima sana na mpenzi wangu. Siruhusu usasa wa watu kuwa karibu, wengine hadi kukumbatiana na kuhagiana wakijifanya ni utani wa mke mdogo...

Siruhusu mtoto wangu wa kike kakua na kavunja ungo kuwa karibu na babake kila saa pamoja ya kukumbatiana or uzungu zungu wa kwenda kuogelea pamoja na vitu vyote ambavyo vinawanya wawe private katika mazingira yanayo hamasisha ngono. Si kwamba naona kua babake anaweza kufanya hivyo na ni malaya - ila kwa sababu najua babake mwisho wa siku ni mwanaume ambaye anaweza kufanya hivyo.

Mimi kuto endekeza baadhi ya hayo nilotaja above ni moja ya namna ya kudhibiti. Na kwa mtazamo wangu naona kuwa ni muhimu kudhibiti. Narudia iwe within reason, isiwe udhibiti wa kero.
 
simuamini mwanake!wasiwasi ndo silaha kabla mambo hayajawa mabaya niyadhibiti
 
mie nilijaribu hilo but madhara yake ni maumivu matupu, nilichunga/chunguza mpaka nikafumania, nikaumia sana, nimeacha kuchucga/chunguza kajituliza mwenyewe, sujui kwanini nilichungaga nikajiumiza vile.

Umeona eeh, lengo la kuchunguza lilikuwa nini? Ujue, eh ukishajua? Umbadilishe? How? Can you real change him? Au umuache? Can you? Vipi kuhusu watoto, miradi?
 
mie nilijaribu hilo but madhara yake ni maumivu matupu, nilichunga/chunguza mpaka nikafumania, nikaumia sana, nimeacha kuchucga/chunguza kajituliza mwenyewe, sujui kwanini nilichungaga nikajiumiza vile.
ha haaaa, pole sana my dear.
rafiki yangu Kaunga kasema vizuri sana, unachunga ili iweje? kama unauhakika ukifumania utamuacha then endelea kuchunga, otherwise hakuna sababu ya kufanya hivyo.....
habari huwa zinakuja, hata kama huchungi. kama mtu wako anafanya mambo ya ovyo, hata baada ya miaka kadhaa, utapata taarifa, hakuna haja ya kujipotezea muda kumchunga mtu mzima mpaka unajisababishia maumivu
 
Last edited by a moderator:
Binafsi ni mtu mzima na akili zangu timamu, nina jua jema na baya, so nikifanya kinyume na kumuudhi mwingine, itakuwa nimeamua tu kufanya hivyo, kuna mambo ya kumkosea mwenzio bila ya kujua, umefanya jambo kwako unaona uko sahihi lkn yy halikumpendeza hapo sawa, yaweza kuwa kwa kuongea imetokea umeropoka km mnavyojua ulimi, pengine umezidisha chumvi kwa chakula na ww bila ya chumvi nyingi huwezi kula na mengine yanayo fanana na hayo,

Mfano kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja c pepo wala nini nikwamba nimeamua mwenyewe kwa akili zangu bila hata ya kushawishiwa na mtu nifanye hivyo, yawezakuwa ni tamaa ya kitu fulani (Pesa au haniridhishi au siwezi kuwa na mume mmoja) hata akinichunga atakuwa anajipa tabu tu,

Hivyo kwa mawazo yangu mtu hachungwi, mtu anajichunga mwenyewe, ukiona mtu anakuwa c mwaminifu ni yy mwenyewe kaamua kufanya wala hakushikwa mkono na mtu, katoka hme kaenda gesti kuzini na mke/mume mwingine nikwamba kaamua kufanya hicho kitendo mwenyewe kwa akili zake c pepo wa maimuna wala jini makata
 
AshaDii nimekusoma vizuri sana dadaangu..Kwanza hujambo?...long tyme ujue?
Back to the topic ..mie concern yangu ni kuwa hata kama tuko kwenye mahusiano/mapenzi..lakini as individuals kila mtu anao uhuru na nidhamu yake ya kutenda. Na beforehand natambua mtakuwa mshafahamiana vya kutosha kuhusu individuals characters..na kama mnaoana obvious kila mtu anakuwa amekubaliana na mwenzie.

Sasa wasiwasi wangu ni kile unachokiita 'ingredient muhimu ya penzi' kudhibitiana/kuchungana/kupelelezana..Na kimsingi hii inatokana na hofu..na hofu hapa ni kuwa umeshindwa kukubali kuwa mwenzi wako 'atavishinda' vishawishi?..Kwa nini umjengee hiyo dhana??. Bahati mbaya mwengine anakuspy bila hata kujua na anaweza ku-connect dots hata zisizokonektika..Unapendwa kuchungwa dadaangu??

hapo kwenye bold kwanini usimsaidie mwenzako kuvishinda hivyo vishawishi kuliko kumuacha kwa kuamini kuwa atavishinda?
 
hapo kwenye bold kwanini usimsaidie mwenzako kuvishinda hivyo vishawishi kuliko kumuacha kwa kuamini kuwa atavishinda?
kumchunga siyo kumsidia mtu, ni kumlazimisha.
kumsaidia ni kuongea naye kuhusu mema na mabaya bila kutafuta kuwa anafanya au la
 
ni kweli unachokisema kaka yangu SnowBall lakini unajua kutokana na huu ubinadamu wetu huu hata ikiwa mtu utaujua sana tu umuhimu wa kujiheshimu au kujitambua kuna wakati unaweza kujisahau au kupitiwa na kusahau majukumu yako au sehemu yako kama mume/mke ndani ya uhusiano wenu na hapo ndipo udhibiti unapoweza kukukumbusha kile unachostahili kukifanya kwa usahihi hata zaidi,ila kuishi maisha feki huletwa na ule udhibiti uliopitiliza kama wa kuwekeana walinzi na kujipeleka peleka kazini ili ujulikane na watu kuwa wewe ndo mmiliki,lakini ulio na kiasi hauna shida unawaweka wenzi angalau kwenye mstari unaotakiwa.

Back
Top Bottom