Asante Mwanakijiji kwa uchambuzi makini wa namba, asilimia na hoja. Mimi narudia ule ubashiri wangu nilioutoa mara tuu baada ya RA kujivua gamba.
CCM itashinda kwa kishindo kwa sababu watu wa Igunga ni watu wa ajabu sana!. Nimesema ni watu wa ajabu sana kwasababu nawafahamu fika ndugu zangu Wanyamwezi (mtanisamehe sana!), sio watu wa msimamo!. Natamani wangekuwa kama watu wa Tarime kwenye ule uchaguzi mdogo, lakini very unfortunately, they are not!. Kwa Wanyamwezi ninaowafahamu mimi, T.shirt, kofia, doti ya kanga na shibe ya siku moja tuu inatosha kumaliza kila kitu kesho yake!
RA alipojivua gamba, nilisema mbunge mpya wa Igunga, ni yule tuu atakayenyanyuliwa mkono na RA. Pia nikasisitiza, hata CCM ikimvua gamba, AC na EL, chama chochote watakacho simama, hata kiwe unknown vipi au insignifant vipi, watashinda simply kwa sababu watu wao, wanawaambudu!. Hawa ni miungu watu. Niliangalia jinsi walivyopokelewa kwao baada ya kuyafanya walioyafanya, ni kama walivyompokea Jairo pale wizarani kwake, kama mfalme fulani!, RACHEL nao ni wafalme maeneo yao, hivyo kwa Igunga, mwana mfalme ni Dr. Kafumu, tena sio tuu ni mwana mfalme, bali ni mwana wa mungu mtu, RA!.
Nimefuatilia ule utabiri wa idadi ya wapigakura wa uchaguzi wa 2010 Igunga, wale wengine wote ambao hawakujitokeza, wengi wao ni waumini wa mungu yule yule, hivyo 2010 hawakuona haja ya kujitokeza kwa sababu walisha muaminia mungu mtu wao kwa ushindi wa asilimia 100%, wale waliojiotokeza, walijitokeza tuu ili kumuendorse!. Kwa vile kwa sasa mgombea wa mungu wao na chama chake ambacho wanaamini ndio kimeubwa kuitawala milele, anapokumbana na kitisho cha Chadema, then this time, watajitokeza kwa wingi, mamia kwa maelfu, kwenda kuokoa jahazi!, nani hapendi pilau, tisheti na kofia!.
Nilibahatika kushughudioa chaguzi ndongo kadhaa na ikiwemo Busanda na Biharamulo na kushuhudia jinsi wananchi wa mijini walivyohamanika na Chadema, lakini siku ya siku, kilichofuatia sote tunakijua, na matokeo mliyaona, hivyo kwa Igunga, sio tofauti ya Biharamulo na Busanda.
Angalizo, nawaombeni sana, wana JF wenzangu, msihamanike na umati kwenye mikutano ya kampeni, wengi kwenye umati hizo sio wapiga kura.
Kwa kawaida, mimi hujitambulisha kama mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge, hivyo binafsi ningependa sana kuona Chadema ikiongeza jimbo, lakini nimeishajiandaa kupokea taarifa za maumivu!.
Pasco.