Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aisee bado nakushangaa sana kwenye hilo hapo (kwenye red). Mbona kuna ushahidi wa kimahakama kuwa CCM ni wezi wa kura na ruling kadhaa za mahakama zimeshadhibitisha hilo..? Au unataka kuniambia mahakama iliionea CCM...? ili iweje..?Mkandara, umesema kitu kizito ambacho wengi tunakijua kwa karibu miaka mitano sasa. Kuna vitu ambavyo mimi nilishakataa - siamini katika nadharia ya "wizi wa kura" wala siamini kuwa "CCM walitumia vyonmbo vya dola" n.k CDM na vyama vingine vilienda kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana vikijua mfumo uliopo uko vipi kama walivyokwenda kwenye chaguzi ndogo zote za Busanda, Biharamulo, Tarime, n.k Japo natamani sana kuona CDM inashinda Igunga lakini isiposhinda itakuwa ni somo ambalo ningependa waeleze sababu zake ni nini tena. Kushinda kwa kutumia nguvu kubwa sana siyo mfumo mzuri.
GeniusBrain,
Ni rahisi sana. Rejea kesi ya Uchaguzi (Election Petition Joseph Haymu and others vs Attorney General and Others), 2005 Corum Makaramba (Unreported). Utajua mbinu zote ya jinsi kura zinavyoibiwa. It is no longer hypothetical. It has been tested in a court of law.
CCM inashinda kwasababu kura 20,000 tu inatosha..zingine mgawane vyama vingine[/kwa njia za wizi lakini
Nimejitahidi kukuelewa unataka kusema nini lakini nimeambulia patupu.Kwa nini pale umeandika Lowassa for Chairman? Unataka Lowassa awe Chairman wa nini? Kwa nini usiandike mada kwamba unataka Lowassa awe Chairman?
Kwa nini unasema ''ili CCM ishinde Igunga lazima itimize masharti haya na haya?'' Yaani CCM inaweza kushinda Igunga hata baada ya High Court kusema kwamba Dowans walipwe zile heka? Hata mshabiki wa CCM wa namna gani ataweza kuona kwamba huyo hakimu aliyeamua hivyo amekwishaizika CCM as far as Igunga is concerned. Lakini it does not mean that uamuzi wake ulilengwa kwa huu uchaguzi wa Igunga.
Maneno mengi yanasemwa kuhusu huyu Lowassa;kwamba analipia kampeni za wabunge,kwamba labda wabunge wachache,au wabunge wengi sana wameingia bungeni kwa msaada wake. Certainly,siku ile Waziri Sitta alipokuwa anakaimu Ukuu wa Bunge badala ya Pinda,alisema maneno kuwapinga wafisadi,halafu lile Bunge lilikuwa just one third full. You wonder what it was all about.
Siasa za Tanzania,CCM ni kama CCP,Chinese Communist Party au Russia United Party,chacha Putin. Wanabishana,wagombana wenyewe,halafu baadaye kabisa ndio wananchi wanfahamu nani atakuwa kiongozi.
Sisi wengine tutaona tu majina yanatajwatajwa,tunakuwa hatufamu kwa nini ''haya majina ya kipumbavu '' yanatajwa. Kumbe,we do not have our ear on the ground. Wale wengine ambao tunadhani ni ''majina ya kipumbavu'' ni watu wakubwa sana katika Chama.
View attachment 37966
Uchaguzi wa Igunga utaamuliwa siku chache zijazo. Mshindi atashinda siyo kwa uzuri wa hoja tu bali pia kwa mbinu na mikakati. Kama nilivyosema kwenye makala nyingine uchaguzi wa Igunga utaamuliwa na idadi ya watu watakojitokeza kupiga kura. Naamini kabisa kuwa hadi hivi sasa kwa kuangalia mwelekeo wa joto la uchaguzi ushindi unaweza kwenda kwa yeyote. Lakini ni CCM na CDM ambao wanaweza kujikuta wote wawili wanapoteza Igunga - yote kutegemeana na idadi ya wanaojitokeza kupiga kura.
Ila CCM Ishinde:
Ila chama cha Mapinduzi kishinde Igunga formula ile ile lazima itumike nayo ni kuhakikisha idadi ndogo zaidi ya watu wanajitokeza kupiga kura. Ila inachohitaji ni idadi kubwa ya wanachama wake wajitokeza katika ile idadi ndogo ya wapiga kura. Hii ndiyo kanuni iliyotumika kwa kiasi kikubwa mwaka jana. Kati ya watu 170,000 waliojiandikisha kupiga kura ni kama watu 49,000 tu waliojitokeza kupiga kura sawa na asilimia kama 23 hivi. Lakini katika hao mgombea wa CCM Rostam alishinda kwa asilimia 73 akikusanya kura 35,000 hivi. Kama "trend" hii itarudiwa basi CCM yaweza kuwashangaza watu kwa kushinda siyo kwa wizi kama wengi wanavyofikiria bali kwa kutumia mbinu ya suppression of votes - yaani kugandamiza upigaji kura. Hii - kwa mtu anayefuatilia - imeshaanza na kwa kweli naamini inafanikiwa sana. Baadhi ya mbinu ambazo zinatumika kwa kiasi kikubwa ni za Kisaikolojia.
KIMSINGI: Ili CCM iweze kushinda kwa kuwepo wapiga kura wachache hofu inahitajiwa. Hivyo, siku hizi zinavyokwenda matuko na kauli za kuwatia hofu wananchi wasijitokeze kwenda kupiga kura kwa hofu ya kudhurika au kujikuta kwenye matatizo. Hofu hii itawazuia kina mama na wanawake kwenda kupiga kura. Lakini pia itawatisha wazee na baadhi ya vijana ambao wamelelewa katika "amani" kama hali ya kutokuwa na vurugu na hivyo matukio mbalimbali yaliyoripotiwa sana kabla ya uchaguzi yatawafanya waone kabisa kuwa siyo Utanzania kwenda na kuwa sehemu yenye vurugu. Endapo upigaji kura utakuwa chini ya asilimia 25 (kama mbinu hizo zitafanikiwa sioni upigaji kura zaidi ya asilimia hiyo), CCM itashinda kwa karibu asilimia 60.
- - Kutishia umwagikaji damu - hii ni mbinu ya kuwafanya watu wahofie kujitokeza kupiga kura
- - Kutishia uwezekano wa kutokea vurugu siku ya kupiga kura - hii ina lengo la kuwatisha kina mama na wazee kwenda kupiga kura
- - Vituo kuwa mbali sana na maeneo ya makazi - hii inawafanya watu wafikirie mara mbili kwenda kupiga kura hasa kama kuna uwezekano wa hayo mambo mawili ya kwanza.
- - Kutokana na mawili ya kwanza kumwaga polisi na hata jeshi ili kuonesha kuwa kuwa hali ya hatari yaweza kutokea - lengo ni kuwafanya watu wawe na hofu ya kujitokeza - hii inawatisha vijana hasa wasichana ambao kukurukakara za polisi hawajazizoea.
- - Udini - hii ni mbinu nyingine mbaya sana hasa kwenye mazingira ya Igunga ambapo wagombea karibu wote ni Wakristu. Hii ni mbinu ya kugandamiza kura za Waislamu na hivyo kuwafanya wengi wao wasite kujitokeza kupiga kura Igunga. Lakini pia inaweza kutumika - naamini kihalali kabisa - kuongeza kura za CCM kwa kutaka zipigwe kura za kundi (group voting). Bahati mbaya kura za namna hii pia huwa zinamatokea yasiyotakiwa - tuliona kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana - kwamba makundi mengine nayo yatapiga kura za kidini.
- - Msaada mkubwa huja siku ya kupiga kura hasa kama NEC inaanza kuwa na matatizo na hivyo watu wanakuja kupiga kura na kukutana na matatizo kibao na kuamua kukata tamaa kwa sababu wanashughuli zao mbalimbali.
Ili CDM ishinde
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinaweza kushinda vizuri kabisa na kuweka historia nchini. Lakini kushinda kwake kutategemea sana idadi ya watu watakaojitokeza kupiga kura. Hivyo siku hizi chache zilizobakia CDM ina kazi kubwa ya kuwatia moyo wapiga kura wajitokeze kupiga kura "no matter what". Hapa patakuwa pagumu. Haitoshi kuwataka watu wasubirie kura wazilinde kazi kubwa iko katika kuwafanya watu watoke majumbani mwao kwenda kupiga kura bila kutishwa na mtu yeyote. Kwa maneno mengine CDM ni lazima iwahakikishie watu usalama na utulivu kwenda kupiga kura.
- CDM iihakikishe kuwa inashirikiana na polisi kuhakikisha usalama na isikubali polisi watumie mbinu za kuwatisha wananchi
- CDM ihamasishe vijana - hasa mwanzo wa siku yenyewe wajitokeze kwenda kupiga kura. Kama watu wanaogopa kuanza kutoka mapema ni rahisi sana kwa watu wengine nao kufuatia. Hivyo, viongozi na makada wa CDM watumie muda mwingi uliobakia kuhamasisha watu kupiga kura na kuwaambia wasiogope kupiga kura siyo tu kwa sababu ni haki yao (kitu ambacho wengi wanakijua) bali kwa sababu ndio sauti yao na wasikubali kunyamazishwa iwe kwa baruti au suti.
- CDM kuhamasisha watu kusaidiana kusafirishana kwenda kwenye vituo vya kupigia kura. Hii ni pamoja na watu wenye baskeli, vibajaji au magari yao. Ikumbukwe kuwa Sheria inakataza kukodisha (kwa malipo) magari kwenda kupiga kura; lakini haikatazi magari kutolewa bure kwa ajili ya shughuli hiyo - one of those loopholes za sheria ya gharama za uchaguzi. CDM ihakikishe kwa upande wake kuwa yeyote anayetaka kupiga kura siku hiyo anapiga kura hata kama kwa kusindikizwa, kubebwa, kuendeshwa au kushikwa mkono.
KIMSINGI ili CDM iweze kushinda ni lazima iwape wananchi ujasiri na kuwatia moyo wajitokeze kwa wingi kupiga kura. Wasitishwe, wasiogopeshwe wala wasihofia lolote. Tanzania bado ninchi huru na kila mtu ana haki kama mwingine. Suti, polisi, jeshi au watu wenye ving'ora hawana haki zaidi kuliko wananchi wengine. Hivyo, kazi kubwa iko kwa CDM kuwahamasisha watu kupiga kura - haijalishi kama inahamasisha wanachama wake - kwani haiwezi kushinda kwa kura za wanachama. Bila KUHAMASISHA WATU kujitokeza kupiga kura na kuweza CDM itakuwa na kazi nzito kweli ya kushinda.
Hivyo, endapo watu watajitokeza kupiga kura kwa kiwango chochote kufikia asilimia 30 au zaidi CDM itashinda kwa kiasi cha 53-57%
Ili CUF ishinde
Kwa upande wa CUF ushindi wake unategemea kwa kiasi kikubwa idadi wapiga kura isibadilike sana kama ilivyokuwa mwaka jana. Kwa CUF endapo upigaji kuta urakuwa kama mwaka jana ni wazi kwamba kura zitakazoleta mabadiliko sana zitakuwa ni zile za CDM. Mwaka jana CUF ilipata kama kura 11,000 endapo CCM na CDM zitagawana sana kura zile 40,000 hivi na CUF ikaendelea na kiasi kama hicho basi inaweza kushinda kwa kushangaza watu lakini kwa less then 50 percent.
Kinyume na watu wanavyofikiria CUF ina faida ambayo CDM haina:
a. Mgombea wake alisimama kugombea mwaka jana na hivyo jina lake tayari linajulikana na tayari alijitengenezea mashabiki
b. Mgongano wa CCM na CDM waweza sana kuinufaisha CUF zaidi kwani kama upigaji kura ukifikia hata hiyo 50,000 (kitu ambacho binafsi sitarajii) vyama vya CCM na CDM vinaweza kugawana hata kura 35,000 kati yao!!!
LA MSINGI hapa ni kuwa CUF inaweza kujikuta inashinda kiti hicho kwa kupata kura chache zaidi kulinganisha na wagombea wengine wakijumlishwa.
Hata hivyo, kama yaliyotokea kwenye kura za Urais ni ishara ni wazi kuwa Igunga wako huru zaidi kumchagua mtu wanayemtaka kuliko inavyofikiria. Kwa hiyo la kuangalia Igunga ni matokeo ya CUF kwani ndio yataamua kama CCM au CDM inashinda au vyote viwili ambavyo vimepiga kelele sana kujikuta vikiwa nje. Msemo wa "Vita vya Panzi..." waweza kuwa kweli.
Zaidi kuhusu Igunga na Habari jisomee kijarida chako ukipendacho siku chache kabla ya Uchaguzi Mdogo wa Igunga. Kumbuka wakati wengine wamelala.....
Tatizo letu limelala hapo kwenye kufikiri kwenye kujiokoa kila kinachoparamiwa ni kitu salama. kuna methali ya kiswahili inayosema 'mfa maji haishi kutapatapa.lUsichanganye watu kuchoshwa na majaribio yao ya kujiokoa. Mtu anapozama ziwani kitu chochote kinachoonekana kuelea hukiparamia kujaribu kujiokoa. Na kile ambacho kinaonekana kinaweza kuchukua watu wengi ndio hukimbiliwa zaidi hata kama chenyewe si imara kihivyo au salama kihivyo. Think about it.
Nimejitahidi kukuelewa unataka kusema nini lakini nimeambulia patupu.
Tatizo letu limelala hapo kwenye kufikiri kwenye kujiokoa kila kinachoparamiwa ni kitu salama. kuna methali ya kiswahili inayosema 'mfa maji haishi kutapatapa.
Mimi sijaona kama nao CDM wako makini kwa wanachokifanya na wala kama wanajua kwa usahihi wapi wanataka kutupeleka kama chama tawala baada ya CCM. Mfano maandiko mengi humu ndani yanaonyesha kwamba wana JF wanaamini kwamba Waislamu(Viiongozi wao?) wanaishabikia CCM kuliko CDM. Lakini sijaona karipio kali kutoka kwa viongozi wa CDM dhidi ya tabia ya sehemu kubwa ya washabiki wao kudhania CDM ni chama kilicho dhidi ya uislamu.
Viongozi wengi wa CDM (Mbowe amejitoa) wanaamin kwamba Peoples powers inamaanisha ni matumizi ya nguvu kwenye kudai "haki" na "Ukamanda" ni ukakamavu kwenye kutokutii sheria na mapambano na Polisi hata bila ya sababu za msingi. hata humu ndani ukisema CDM wamekosea utarukiwa kama kibaka aliyekamatwa akitaka kuiba simu Kariakoo.
CDM kama chama hakina Oganaizesheni ya uhakika kwenye mambo yake ya kila siku na hakuna anayeonyesha kujali.Ukiwauliza watu CDM Makao Makuu ni kiasi gani fedha chama kitatumia kwenye uchaguzi wa Igunga na chaguzi ndogo za Madiwani inawezekana hawajui kabisa kwani fedha nyingi za kuendeshea chama ama "wanakopeshwa" na Mbowe au wanapewa "msaada" na Mzee Ndesamburo.
kWELI?? You got it wrong yourself!!You got it all wrong!!!!!!
kWELI?? You got it wrong yourself!!
Yes i agree!!Mere allegations do not become facts just by bold and red highlighting hahaha ahaha ahahahaha ahahah!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mzee Mwanakijiji, sahihisho dogo hapo kwenye Red.Sidhani kama kitakuwa na chaguo jingine unless kimwage damu. Uzuri wa uchaguzi wa Ubunge ni kuwa matokeo yanatangazwa rasmi pale pale Bungeni hayahitaji kutangazwa na Tume ya Uchaguzi kama ilivyo kwa matokeo ya Urais. Lakini uzuri zaidi ni kuwa kama unaweka wasimamizi kwenye kila kituo unaweza kuwa na matokeo yako wewe mwenyewe kabla RO hajatangaza rasmi.
Kama CCM imeweza kuweka wasimamizi kwenye vituo vyetu na CDM kisiweze basi mwanya wa watu kuchezea kura waweza kutokea wakati huo. Lakini kinyume cha hapo ni vigumu sana kubadilisha matokeo ndio maana kina Masha, Marmo na wengine walianguka mwaka jana. Si kwamba hawakuweza kuiba iila ilikuwa ngumu sana kumanipulate kura za ubunge.
Mzee Mwanakijiji, sahihisho dogo hapo kwenye Red.
1. Kwanza matokeo ya kila kituo, hubandikwa hapo hapo kituoni mara baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika na sio Bungeni! (I know you mean kituoni). Angalizo matokeo hayo hubandikwa tuu na sio kutangazwa!. Hata baada ya zoezi la kuhesabu kura kwenye vituo vyote kukamilika, hayo bado sio matokeo rasmi.
2. Matokeo rasmi ya jumla hutangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Returning Officer, ambaye hapa ni ajenti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, hivyo atakapoyatangaza, natangaza kwa niaba ya NEC, hivyo sio kweli kuwa matokeo hayatangazwi na NEC!.
4. Kwa case ya Igunga, zoezi la kuhesabu kura vituoni litakamilika by saa 3 usiku, hivyo within that time, kama Chadema itafanikiwa kuweka mawakala wake kote, then watakuwa wameshayajua matokeo ila hawaruhusiwi kuyatangaza mpaka yatakapotangazwa rasmi na msimamizi wa uchaguzi siku ya Jumatatu saa 4:00 asubuhi.
5. Kwa kumbukumbu ya zoefu wa uchaguzi mdogo wa Biharamulo, Chadema waliwapa simu za mkononi mawakala wao wote, huku laptop ya Zitto ikitumika kuhifadhi kumbukumbu. Kufikia saa 4 usiku walishapokea matokeo yote isipokuwa ya vituo sita vya kata ya Nyakananazi walikodai mawakala wao wametekwa. Wakajijumlishia wenyewe na kukuta margin ni kubwa kati ya ushindi wao na CCM, hivyo kuasume hata kama vituo vyote sita wataichagua CCM kwa asilimia 100%, wao bado ni washindi, wakajitangazia ushindi na mji wa Biharamulo ukalipuka kwa nderemo na vifijo kushereherea ushindi ambao ulidumu kwa muda mfupi tuu. Ilipofika saa 6:00 usiku CCM nao wakalipuka kwa ushindi!. Asubuhi CCM ikatangazwa imeshinda!.
4. Kitendo cha vyama kujitangazia matokeo yao kabla ya RO, ndiko kuhatarisha usalama wenyewe, nashukuru Mungu watu wa Bimulo ni wapole, hata baada ya kupokwa tonge mdomoni walitulia tuu, na hivyo ndivyo walivyo watu wa Igunga, lakini kuna maeneo ukishatangaza umeshinda ndio umeshinda, matokeo ya RO yakiwa ni tofauti, panakuwa hapakaliki!.
Asante Mzee Mwanakijiji, jumapili jioni macho na masikio yetu ni Igunga, hivyo tutakutembelea sana kule Mwanakijiji.com.Asante kwa masahihisho.
a. Kwenye demokrasia na kwa mtindo wa mfumo wetu wa uchaguzi mtu yeyote kama anajua kujumlisha anaweza kumjulisha na kujua matokeo kabla ya kutangazwa. Huu ni mfumo unaotumika hata baadhi ya nchi japo wenzetu huwa wanatumia zile exit polls (kuwahoji waliokwishapiga kura) na kutoka hapo wanaweza kukisia matokeo ya jumla yatakuwaje.
b. Kosa kubwa liko kwa vyombo huru vya habari kwani vinategemea tume navyo kutangaza matokeo badala ya kuweka watu wao kila kituo au kufuatilia kila kituo na kujumlisha. Kwa kutumia vyombo vya habari huru kuweza kutangaza mshindi (to call the election) inazuia watu wengine kuchakachua kwa sababu vyombo vya habari itabidi vielezee tofauti ya hesabu yake na ile ya tume. Kosa kubwa la mwaka jana - hasa kwenye kura za urais - ni kuwa vyombo vya habari vilikatazwa kutangaza matokeo ya Urais kwa kadiri walivyoyapata. I believe it was one of the most shameful moment ya uhuru wa habari nchini.
Binafsi nimejiweka sawa hapa kuwa nitatangaza matokeo ya Igunga kwa kadiri yanavyokuja.
Kosa kubwa la mwaka jana - hasa kwenye kura za urais - ni kuwa vyombo vya habari vilikatazwa kutangaza matokeo ya Urais kwa kadiri walivyoyapata. I believe it was one of the most shameful moment ya uhuru wa habari nchini.