Elections 2010 KUMEKUCHA - 5: Ushindi wa Nani Igunga na kwanini..

Elections 2010 KUMEKUCHA - 5: Ushindi wa Nani Igunga na kwanini..

CCM iko kwenye hali mbaya, inner circles wanasema kwa uwazi kabisa!!! Makundi yanawamaliza. Waliyaanzisha wenyewe, sasa yame kua hayakamatiki, rate yake ni kubwa kiasi wamechoka ku-control!!!

Time will tell, all in all MAGAMBA are evil anything can happen in Igunga!!!
 
Wakuu msisahau kuwa majimbo kama ya RA ndio ambayo CCM 2010 waliweka kura nyingi sana za wizi kwa ajili ya margin ya ushindi wa Urais, Muhimu ni kama Mwanakijiji alivyosema CDM ihakikishe wapiga kura wote waliopo wanapiga kura na ikiwezekana pia wasio wakazi wa Igunga hawapigi kura katika huo uchaguzi waamashishe watu wa Igunga kujitokeza kwa wingi sana na pia kutambua watu ambao sio wakazi wa Igunga hili wasipige kura hapo vitambulisho vihakikiwe pale ambapo watoa taarifa watawashituwa wasimamizi wa vituo juu yawapiga bandia
 
Kama "trend" hii itarudiwa basi CCM yaweza kuwashangaza watu kwa kushinda siyo kwa wizi kama wengi wanavyofikiria bali kwa kutumia mbinu ya suppression of votes - yaani kugandamiza upigaji kura...
Kwenye analysis zako za uchaguzi hasa ile ya 2010 na hii ya Igunga umekua uki rule out possibility ya wizi wa kura. Tunaomba utuelezee kwanini unaamini /unataka tuamini kuwa CCM hawashindi kwa kuiba Kura...?
 
Mwanakijiji asante kwa analysis yako.

Mapema niliwahi kufanya analysis yangu kuwa kama wapigakura watajitokeza kama walivyokuwa uchaguzi uliopita 50,000 Chadema itashinda kwa 46% kura 23,000 na CCM itapata 35% kura 17,500, CUF 11% kura 5,500, kifupi ni kuwa Chadema kitachukua nusu ya kura ya kila chama CCM na CUF walizopata kwenye uchaguzi uliopita, safari hii wakijitokeza watu wengi zaidi kupiga kura itakuwa advantage kwa Chadema.

Nikirudi kwa analysis yako kwa vile CCM inategemea wazee na wanawake kitendo chochote cha kuwatia hofu aidha kwa kumwaga polisi au kutumia vijana kuanzisha fujo wazee hasa kina mama wengi hawatajitokeza hivyo kuipunguzia CCM kura. Kwa hali hiyo CDM kitakuwa na advantage kubwa kwa vile ni vijana wengi watakaojitokeza.

Suala la udini pia halitaisaidia sana CCM kwa sababu kura za waislamu ni fixed ambazo hizo hizo CUF inaziwinda achilia mbali chache watakazopata CDM, kwa msingi huo huo wa udini kuna kura za wakristo zitakazobaki zitaonekana kama sympathy kwa Chadema au counter attack, bila kusahau wagombea wote wa vyama vikuu vitatu ni wakristo hivyo kuwafanya waislamu wengi kutokuwa na interest kwa yeyote na kuwafanya hata wengine kutokwenda kabisa kupiga kura. Hiyo ndiyo analysis yangu.

Asante mkuu, nakubaliana nawe.

Nafikiri hii karata ya udini tutakuja ona impact yake siku zijazo. Maadam imeingizwa rasmi na CCM ktk siasa basi tusitegemee kuwa itapotea hivi hivi, lazima tutaona impact yake ktk siasa za Tz.

Mi nadhani ingewekwa sheria ya dharura kuwa ikitokea taasisi/kikundi/mwanasiasa/chama cha siasa ambacho si tu kitatumia hii karata ya udini kwamba kifukuzwe kwenye uchaguzi husika bali kifutwe kabisa. Na wahusika wakutane na Mahakama kwa kosa la uhaini na uvunjifu wa amani na umoja wa Tz.

Weledi wa watu wengine ni mdogo wa kuwawezesha kujisaidia, kuvuka barabara nk lakini si ktk kuchambua hoja na mambo. Pia wengi wao wana njaa so wametumika kirahisi sana na CCM.

Nakemea udini na ukabila kwa nguvu zote ktk nyanja zote ikiwemo siasa.
 
Hii imekaa vizuri sana well said man, we will keep the fire burning as usual

Mwanakijiji asante kwa analysis yako.

Mapema niliwahi kufanya analysis yangu kuwa kama wapigakura watajitokeza kama walivyokuwa uchaguzi uliopita 50,000 Chadema itashinda kwa 46% kura 23,000 na CCM itapata 35% kura 17,500, CUF 11% kura 5,500, kifupi ni kuwa Chadema kitachukua nusu ya kura ya kila chama CCM na CUF walizopata kwenye uchaguzi uliopita, safari hii wakijitokeza watu wengi zaidi kupiga kura itakuwa advantage kwa Chadema.

Nikirudi kwa analysis yako kwa vile CCM inategemea wazee na wanawake kitendo chochote cha kuwatia hofu aidha kwa kumwaga polisi au kutumia vijana kuanzisha fujo wazee hasa kina mama wengi hawatajitokeza hivyo kuipunguzia CCM kura. Kwa hali hiyo CDM kitakuwa na advantage kubwa kwa vile ni vijana wengi watakaojitokeza.

Suala la udini pia halitaisaidia sana CCM kwa sababu kura za waislamu ni fixed ambazo hizo hizo CUF inaziwinda achilia mbali chache watakazopata CDM, kwa msingi huo huo wa udini kuna kura za wakristo zitakazobaki zitaonekana kama sympathy kwa Chadema au counter attack, bila kusahau wagombea wote wa vyama vikuu vitatu ni wakristo hivyo kuwafanya waislamu wengi kutokuwa na interest kwa yeyote na kuwafanya hata wengine kutokwenda kabisa kupiga kura. Hiyo ndiyo analysis yangu.
 
Mzee Mwanakijiji,

Nimekusoma vizuri lakini kuna hoja yangu ambayo sijui kama umeifikiria..Kwa jinsi ulivyoandika kuhusu CCM wala sina ubishi hapo kwa sababu ndivyo wakoloni na hata Makaburu walitumia mbinu hizo na tusingeweza kuwashinda kupitia sanduku la kura. Labda niziorodheshe tena kama ulivyobandika.

- Kutishia umwagikaji damu - hii ni mbinu ya kuwafanya watu wahofie kujitokeza kupiga kura

- Kutishia uwezekano wa kutokea vurugu siku ya kupiga kura - hii ina lengo la kuwatisha kina mama na wazee kwenda kupiga kura

- Vituo kuwa mbali sana na maeneo ya makazi - hii inawafanya watu wafikirie mara mbili kwenda kupiga kura hasa kama kuna uwezekano wa hayo mambo mawili ya kwanza.

- Kutokana na mawili ya kwanza kumwaga polisi na hata jeshi ili kuonesha kuwa kuwa hali ya hatari yaweza kutokea - lengo ni kuwafanya watu wawe na hofu ya kujitokeza - hii inawatisha vijana hasa wasichana ambao kukurukakara za polisi hawajazizoea.

- Udini - hii ni mbinu nyingine mbaya sana hasa kwenye mazingira ya Igunga ambapo wagombea karibu wote ni Wakristu. Hii ni mbinu ya kugandamiza kura za Waislamu na hivyo kuwafanya wengi wao wasite kujitokeza kupiga kura Igunga. Lakini pia inaweza kutumika - naamini kihalali kabisa - kuongeza kura za CCM kwa kutaka zipigwe kura za kundi (group voting). Bahati mbaya kura za namna hii pia huwa zinamatokea yasiyotakiwa - tuliona kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana - kwamba makundi mengine nayo yatapiga kura za kidini.

- Msaada mkubwa huja siku ya kupiga kura hasa kama NEC inaanza kuwa na matatizo na hivyo watu wanakuja kupiga kura na kukutana na matatizo kibao na kuamua kukata tamaa kwa sababu wanashughuli zao mbalimbali.

Sasa nikitazama Chadema na CUF naona umejaribu kuwapa nafasi wakitumia zaidi nguvu za kichama ktk uchaguzi badala ya wananchi wenyewe wapiga kura kukubali mabadiliko. Mimi nadhani ili kuwashinda CCM ni swala la Chadema na CUF kuhakikisha wanawaelimisha wananchi vya kutosha kwa sababu ushindi leo haupo ktk sanduku la kura..

Chadema na CUF wamejaribu vya kutosha na hakika uchaguzi huu wa Igunga ndio utakao toka picha halisi na pengine kuwafungua akili kwamba huwezi kupambana na utawala dhalimu wenye kutumia mbinu chafu kwa kutegemea sanduku la kura wakati mfumo wenyewe umeoza. haiwezekani wananchi waliojiandikisha kupiga kura Igunga kuwa 170,000 lakini waliojitokeza kupiga kura walikuwa 43,000 na watu wakaamini takwimu hizo, leo wanaingia katika uchaguzi mwingine pasipo kufanyiwa uchunguzi na marekebisho kuhusiana.

Mzee mwanakijiji

Heshima yako mkuu uchambuzi wako mzuri sana lakini nina hoja juu ya uchambuzi wakokama ifuatavyo

1.Uchambuzi huu unatokana na maono yako binafsi na huja fanya utafiti wowote unaweza kutupa taswila halisi ya sample ulio tumia,methodology uliyo tumia na assumption ulizo tumia kufikia hitimisho

Well sijadai kuwa ni uchambuzi wa kisayansi wala sijadai kuwa hauna makosa; msingi wake ni uelewa wa kawaida tu unaotokana na uzoefu wa kufuatilia siasa za Tanzania. Wanasema "it walks like a duck, squak like a duck and swim like a duck then its a duck".. Ni observation tu wala siyo prediction written in stone.

2.Siasa Zatanzania hazitabiliki hata kidogo kwa sababu hatuna ukabila,urangi na udini ulio wazi kabisa ingawa wakubwa wanajaribu kuutumia kama kete ya kisiasa

3.Uchambuzi wako hauja chukulia hata kidogo misingi ya mageuzi na harakatizake kisiasa katika taifa hili na hauja eleza hata kidogo upepo wa mageuzi uliopo nchini kwa sasa na mwelekeo uko vipi juu ya upepo huu

Hakuna uchaguzi unaotabirika sana kama wa Tanzania. Kama taifa tuna fikra za aina fulani na tunashare sentiments fulani fulani. Matokeo yake ni rahisi sana kuwapredict kutokana na kujielewa hasa ukijaribu kujiweka katika nafasi yao.

4.Uchambuzi wako hauja eleza hata kidogo mabadiliko ya kifikra katika jamii yaleo ukilinganisha na mwakajana ambapo umeweka msingi mkuu wa hoja yakoya kura na wagombea Igunga.

Well.. labda najua sana kuhusu mabadiliko ya kifikra kuliko unavyofikiria nikiwa muasisi wa mapambano ya kifikra. Najua ni katika level gani watu wetu wengi wamefikia - naona sana katika mazungumzo na maandishi yao na kuwafuatilia - kinyume na unavyofikiria mabadiliko ya kifikra yapo lakini hayajawa mahali ambapo panatosha kutaka mabadiliko makubwa ya kisiasa kwa gharama yoyote.

5.Na kama utazungumzia mageuzi ya kifikra katika jamii hii toka mwakajana 2010 wakati wa uchaguzi mpaka leo utajua nichama gani kime wekeza katika hili,ukitambua hili hutapata shida kujua mshindi igunga ninani kwasababu hoja ya msingi unayo

Of course.. najua ni nani lakini misingi na mifumo haijabadilika. hivi unafikiria kama wangekuwa wanaruhusu kujiandikisha hadi mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu, uchaguzi wa mwaka jana ungekuwa kama ulivyokuwa?

6. Bila ushabiki wowote huwezi kupata shida kujua wananchi wa naamini chama gani na chenye mlengo gani juu ya taifa hili kama utakosa kabisa mwelekeo na kutambua nichama gani wananchi wanakiamini jiulize kwanini siri za serikali zinavuja sana na zina vuja kuelekea chama gani

Usichanganye watu kuchoshwa na majaribio yao ya kujiokoa. Mtu anapozama ziwani kitu chochote kinachoonekana kuelea hukiparamia kujaribu kujiokoa. Na kile ambacho kinaonekana kinaweza kuchukua watu wengi ndio hukimbiliwa zaidi hata kama chenyewe si imara kihivyo au salama kihivyo. Think about it.
 
Chadema na CUF wamejaribu vya kutosha na hakika uchaguzi huu wa Igunga ndio utakao toka picha halisi na pengine kuwafungua akili kwamba huwezi kupambana na utawala dhalimu wenye kutumia mbinu chafu kwa kutegemea sanduku la kura wakati mfumo wenyewe umeoza. haiwezekani wananchi waliojiandikisha kupiga kura Igunga kuwa 170,000 lakini waliojitokeza kupiga kura walikuwa 43,000 na watu wakaamini takwimu hizo, leo wanaingia katika uchaguzi mwingine pasipo kufanyiwa uchunguzi na marekebisho kuhusiana.

Mkandara, umesema kitu kizito ambacho wengi tunakijua kwa karibu miaka mitano sasa. Kuna vitu ambavyo mimi nilishakataa - siamini katika nadharia ya "wizi wa kura" wala siamini kuwa "CCM walitumia vyonmbo vya dola" n.k CDM na vyama vingine vilienda kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana vikijua mfumo uliopo uko vipi kama walivyokwenda kwenye chaguzi ndogo zote za Busanda, Biharamulo, Tarime, n.k Japo natamani sana kuona CDM inashinda Igunga lakini isiposhinda itakuwa ni somo ambalo ningependa waeleze sababu zake ni nini tena. Kushinda kwa kutumia nguvu kubwa sana siyo mfumo mzuri.
 
Kwenye analysis zako za uchaguzi hasa ile ya 2010 na hii ya Igunga umekua uki rule out possibility ya wizi wa kura. Tunaomba utuelezee kwanini unaamini /unataka tuamini kuwa CCM hawashindi kwa kuiba Kura...?

Kwa sababu mfumo wetu wa uchaguzi ukizingatiwa unaondoa hiyo possibiilty. Jamani, Tanzania imekuwa ikifanya chaguzi kuanzia wakati wa chama kimoja na watu walikuwa wanaanguka tena vigogo wakubwa tu. Hatujaanza kupiga kura baada ya vyama vingi. Mfumo wa kupiga kura uko very transparent kuliko watu wanavyofikiria. Niliandika mwaka jana kuwa ni vigumu sana kuiba kura Tanzania. Ni rahisi kumanipulate matokeo hasa ya Urais kuliko kuharibu matokeo ya Ubunge.
 
mwanakijiji umejikita sana kwenye namba
kuna vitu vingi sana viko upande wa CDM

1. performance ya wabunge wa CDM bungeni, watz wengi sana walikuwa wanafuatilia na hii kitu imeipeleka CDM to the next level
2. umeme
3. sukari
4. experince ya CDM kwenye uchaguzi, uchaguzi huu CDM wamepambana na ccm kila kona.
5. time iko na CDM - budget ya kwanza tokea uchaguzi imeisha juzi kwa hiyo hata kama kitu kime allocatiwa hela basi kitakuwa hakijaanza hata kutendeka, hii ina maana ccm haijatimiza ahadi yoyote kwa wana Igunga.
6. watz sasa hivi wana uelewa kuliko 10 months ago
7. CDM sasa hivi wana hela zaidi ya waliyokuwa nayo wakati wa busanda
6. ukimwona magufuli anaaidi daraja kwenye mkutano uliojaa watoto ujue kuna kazi.
7. jana ccm wameshindwa kuleta helikopta kwa wakati na hii imepelekea malumbano makubwa baina ya viongozi wa ccm waliokuwa kwenye campaign wanajiuliza inakuaje hata helikopta wanashindwa kuandaa. helikopta ya CDM imefika kwa wakati na ina jina la CDM.
8. wiki iliyopita nimepokea watu wakitokea Igunga na ni wana ccm, wanasema hali ni tete wananchi wa Igunga wameamka.
9. siku hizi vijana wanashiriki uchaguzi sio kama zamani. vijana hawako emotionally attached to ccm
 
It's kinda hard to comprehend,
IN 2010 55,370 people who voted in Hai district.
Presidential, JK had 35,910, Slaa had 18,513: JK won almost twice as much.
PARLIAMENTARY, CCM had 23,349 while CDM had 28,585. the difference was 5,236.
Spoilt votes were astonishingly 176 and 3043 respectively, Hai had one of the best voter turnarround.
Can someone explain what went on (conclude statistically).
I think CDM stole some votes here.

Hapa kura za urais zimechakachuliwa ili kumweka JK juu.Mchezo mchafu ulikua unafanyika.Kuna sehemu ambazo Dr alikua chini akapandishwa na sehemu zingine JK yuko juu lakini kawekwa juu zaidi.So,CCM are expatries in this
 
mwanakijiji umejikita sana kwenye namba
kuna vitu vingi sana viko upande wa CDM

1. performance ya wabunge wa CDM bungeni, watz wengi sana walikuwa wanafuatilia na hii kitu imeipeleka CDM to the next level
2. umeme
3. sukari
4. experince ya CDM kwenye uchaguzi, uchaguzi huu CDM wamepambana na ccm kila kona.
5. time iko na CDM - budget ya kwanza tokea uchaguzi imeisha juzi kwa hiyo hata kama kitu kime allocatiwa hela basi kitakuwa hakijaanza hata kutendeka, hii ina maana ccm haijatimiza ahadi yoyote kwa wana Igunga.
6. watz sasa hivi wana uelewa kuliko 10 months ago

Hizi zote ni pointi nzuri sana lakini zina ukweli kwa kiasi chake. Hata hivyo factors zote hizo ukizingalia zilikuwepo kwa miaka mitano iliyopita. Na kwa kweli hazibadilika sana ndani ya miezi hii michache; umeme, sukari, na umahiri wa CDM unajuliakana kwa kiasi kikubwa. So.. hizi ni zile naweza kusema kuwa ni "constants" zilizopo. Hazijabadilika.

7. CDM sasa hivi wana hela zaidi ya waliyokuwa nayo wakati wa busanda

Hii naweza kukupa kuwa yawezekana kabisa kuwa ndio "game changer" kwa CDM. Lakini kwa kiasi hicho wataweza kuweka makawala kila kituo? Wataweza kuwapatia mawakala hao mfumo wa mawasiliano ya haraaka kuweza kujua wapi kuna tatizo mara moja na kurespond? Kwa mfano ukisikia CUF wanamawakala kila kituo na CDM haina utalielezaje hilo?

6. ukimwona magufuli anaaidi daraja kwenye mkutano uliojaa watoto ujue kuna kazi.

This is also a constant.. CCM imekuwa ikifanya hivi miaka yote. Tumeona Busanda na Ngeleja na tumeona hata Babati na Mbeya Vijijini. Ningeshangaa kama wasingefanya hivi - si umeona limekuja baada ya Kafumu kuboronga kwenye suala la daraja wakati wa mdahalo?

7. jana ccm wameshindwa kuleta helikopta kwa wakati na hii imepelekea malumbano makubwa baina ya viongozi wa ccm waliokuwa kwenye campaign wanajiuliza inakuaje hata helikopta wanashindwa kuandaa. helikopta ya CDM imefika kwa wakati na ina jina la CDM.

Helikopta hazishindi uchaguzi tena to be very very frank; I hate matumizi ya helikopter.. ni gharama sana, distracting na zinahatarisha sana maisha ya viongozi. Ningekuwa na uwezo ningepiga marufuku kabisa. They can easily being sabotaged.

8. wiki iliyopita nimep okea watu wakitokea Igunga na ni wana ccm, wanasema hali ni tete wananchi wa Igunga wameamka.

Of course.. ndivyo ilivyo uchaguzi mahali popote pale.

9. siku hizi vijana wanashiriki uchaguzi sio kama zamani. vijana hawako emotionally attached to ccm

Sema wanashiriki kampeni sana; kwani hujawaona maelfu ya vijana wanaokubali hata kupewa mafunzo ya kuitetea CCM? Au kina Nape siyo vijana wenyewe? Tena cha kushangaza zaidi utakuta vijana wasomi sana ndio wako CCM! you go figure!
 
Just thinking outside the box whilst in the box, say CHADEMA wakawa wa kwanza, CUF wa pili na CCM wa tatu!!!!!!!!!!! Je chama tawala kitayakubali hayo matokeo?????????
 
Just thinking outside the box whilst in the box, say CHADEMA wakawa wa kwanza, CUF wa pili na CCM wa tatu!!!!!!!!!!! Je chama tawala kitayakubali hayo matokeo?????????

Sidhani kama kitakuwa na chaguo jingine unless kimwage damu. Uzuri wa uchaguzi wa Ubunge ni kuwa matokeo yanatangazwa rasmi pale pale Bungeni hayahitaji kutangazwa na Tume ya Uchaguzi kama ilivyo kwa matokeo ya Urais. Lakini uzuri zaidi ni kuwa kama unaweka wasimamizi kwenye kila kituo unaweza kuwa na matokeo yako wewe mwenyewe kabla RO hajatangaza rasmi.

Kama CCM imeweza kuweka wasimamizi kwenye vituo vyetu na CDM kisiweze basi mwanya wa watu kuchezea kura waweza kutokea wakati huo. Lakini kinyume cha hapo ni vigumu sana kubadilisha matokeo ndio maana kina Masha, Marmo na wengine walianguka mwaka jana. Si kwamba hawakuweza kuiba iila ilikuwa ngumu sana kumanipulate kura za ubunge.
 
Yea umwagaji damu linaweza kuwa suluhisho kwa ushindi wa CCM, kwa sababu kuna kila dalili kwamba CCM haijajua bado hatima ya uchaguzi huu itakuwaje, looks like they keep on flip flopping to where they did bank at on votes. Pia kuna kila dalili kwamba the common machine iliyokuwa ikitumika kwenye chaguzi za zamani imeshindwa kabisa kufanya kazi this tyme. CCM hawajazoea fair platform na ndiyo maana tunawasikia kulalamika kila siku, quite uncommon kwa chama tawala in Africa.

Lingine naloliona ni kwamba uhai wa CCM Igunga ulikuwa entirely on RA na siyo chama chenyewe. Lolote linaweza kutokea katika uchaguzi huu na kama ulivyosema upinzani wanatakiwa wawe fast kukusanya matokeo na kwa vielelezo ikiwezekana zile form za matokeo pamoja na sahihi waweke na madole gumba pia.

All in all kama tunaikumbuka vizuri ile hotuba ya RA inaonyesha wazi the guy is laughing so much huko aliko!!!!
 
Nyambala.. think it this way - kama ingekuwa rahisi sana kuiba kura za ubunge kama watu wanavyofikiria CCM isingetumia nguvu kubwa sana kujaribu kulishikilia jimbo; Mkapa, jeshi n.k Kama ingekuwa rahisi hivyo hawa watu wasingehangaika sana na mambo ya tuhuma n.k Wangeweka tu mechanism yao na kusubiri kunyakua lakini haiwezi kuwa hivyo. Ndio maana naamini wao wanategemea sana suppression ya voting kuliko kitu kingine chochote. CCM ina count on its loyal supporters. Kama waliochamgua Rostam mwaka jana ni wana CCM damu na wakaamua kurudi tena basi vyama vyote vya upinzani vina kazi kubwa sana ya kupiku hilo. Fikiria kuwa watu 37,000 walimchagua RA wakati kama JK alipata kura chini ya hapo na kati yao wakija hata asilimia themanini tu ya hao upinzani wana kibarua kigumu sana.

Ndio maana miye napigania watu wengi wajitokeze kupiga kura zaidi ili kuoffset hiyo namba ya CCM.

Utokee muujiza tu kuwa upigaji kura uwe kama fifty percent ya waliojiandikisha - kitu ambacho hakijatokea kwenye chaguzi ndogo nchini kwa muda mrefu sana - ina maana karibu watu 85,000 watapiga kura. Hiyo namba itakuwa na advantage kubwa kwa upinzani kuliko CCM kama tukichukulia mambo mengine yote yaliyotajwa safari na yawezekana sana hasa kama walioipigia CUF wakaendelea kufanya hivyo basi ni CUF na CCM watagawana kuipa kura CDM. Kwa sababu vyama hivyo viwili tayari tunajua mvuto wake kwani vilishandana mwaka jana. Matokeo ya hilo ni kuwa CDM inaweza kweli kushinda lakini with the less than fifty percent of the votes.

Sijasikia sana (at least katika ripoti mbalimbali) viongozi wa CDM wakiwahimiza watu kujitokeza kupiga kura.
 
Back
Top Bottom