Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #21
Kura alizopata mgombea wa CUF zilikuwa ni za wapinzani wote.Ngoja nichukulie mfano huu....Kuna wanaCDM waliompigia Mahona (CUF) simply CDM haikuwa na mgombea,na sasa kwakuwa CDM ina mgombea,watampigia na hvyo kuufanya mtaji wa Mahona (CUF) kupungua so unapofanya tathmini hilo nalo ni la kuzingatia.@Mzee Mwanakijiji
Fikiria kama CCM itapata 20,000 tu ya hizo ilizopata mwaka jana; hiyo ina maana gani kwa CDM na CUF?
Sijui hao vijana waliofikisha miaka 18 kuanzia octoba10 na sept.11 ni asilimia ngapi lakini ni insignificant ukilinganisha na vijana waliojiandikisha uchaguzi uliopita kati ya 170,000. Ukitaka kuangalia hivyo basi kuna factors nyingi sana itabidi ku-consider mfano wazee wangapi wamefariki, waliopoteza vitambulisho nk nk. Tuongelee waliopo ambao walipiga kura(50,000) na ambao hawakupiga kura wale 120,000 lets say at least quarter of 120,000 yaani 30,000 wajitokeze + 50,000 waliopiga mwaka jana to make 80,000 voters. Sasa kati ya hao 80,000 tuangalie ni asilimia ngapi ya vijana watakaopiga kura.Una tatizo hapo; vijana wengi sidhani kama wamepiga kura; wengi waliotimiza miaka 18 kuanzia Oktoba hadi Septemba mwaka huu hawapigi kura. Wengi waliokuwa shule wameenda shule au vyuoni. Watakaoamua kupiga kura ni watu wazima zaidi kuliko vijana. Vijana ni washingiliaji zaidi.. kama kungekuwa na uandikishwaji tena wa wapiga kura basi vijana wengi wangejitokeza.
Hata kama CDM haitashinda Igunga mm sijali .
"When Nature has work to be done, she creates a genius to do it. "
The guy who changed this world by inventing electricity did million of trials but succeed only once. And now here we are . ELECTRICTY.
We will try , and try and try until they can not afford not to accept us ....Peoples pawaaaaaaaa
Sijui hao vijana waliofikisha miaka 18 kuanzia octoba10 na sept.11 ni asilimia ngapi lakini ni insignificant ukilinganisha na vijana waliojiandikisha uchaguzi uliopita kati ya 170,000. Ukitaka kuangalia hivyo basi kuna factors nyingi sana itabidi ku-consider mfano wazee wangapi wamefariki, waliopoteza vitambulisho nk nk. Tuongelee waliopo ambao walipiga kura(50,000) na ambao hawakupiga kura wale 120,000 lets say at least quarter of 120,000 yaani 30,000 wajitokeze + 50,000 waliopiga mwaka jana to make 80,000 voters. Sasa kati ya hao 80,000 tuangalie ni asilimia ngapi ya vijana watakaopiga kura.
Nakubaliana na wewe kuna walio mashuleni sijui ni asilimia ngapi ila kumbuka umri wa kuwa shuleni ni 18-22(wapiga kura) zaidi ya hapo vijana wengi ni jobless wako mitaani-Igunga. Mimi bado nafikiri vijana watakuwa wengi ikichangiwa na elimu iliyotolewa huko na mwamuko wa uelewa wa mambo ya siasa unavyozidi kukua, hata huo ushangiliaji unaousema ni hamasa na kampeni tosha kuwafanya watu waliojiandikisha kujitokeza siku ya kupiga kura. Hata hivyo haya yote tunayojadili yanategemea iwapo uchaguzi unakuwa free and fair.
Yaani CCM ingekuwa ni chama cha mastrategistS na wanaoongozwa na principles basi wangekubali kuupoteza uchaguzi huu, lakini sio sasa. Wangekubali toka mwanzo kwa vitendo. Kwanza wangemfukuza Rostam, pili wasingemteua Kafumu kugombea na ufunguzi ule usingefanywa na Mkapa. Hapa ndiyo wangeipigilia vizuri ile dhana yao ya kujivua gamba na kweli vigogo mafisadi wangetishika na wengine wangejiondoa wenyewe. Sasa ilipofika mahali wakaanza kukompromize principles, mara ooh Nape, Kilango, Sitta, Mwakyembe wasiende huko. RA yuleyule waliyemwita Gamba wakampigia magoti awepo ufunguzi wa kampeni ni Bao lakudumu walilojipiga CCM.
CCM: Kwa mambo yalivyoenda mpaka sasa CCM ishinde au isishinde imeshajimaliza
1. CCM wamepoteza ile commanding lead kwenye uchaguzi, uchaguzi wowote kuanzia sasa itakuwa ndiyo mwendo huu, sasa tusijeshangaa siku JK anenda kumpigia kampeni diwani wa Kawe.
2. CCM haiaminiki tena, hata wale waliokuwa sometimes in sometimes out, kwa matukio hayo ya Igunga ndiyo basi tena.
3. CCM is not for us but against us, hii ndiyo msg inayoresonate kwa vijana wa kitanzania.
4. CCM ni lazima inunue affection kwani ile natural is gone, gone in Igunga.
5. Uchaguzi huo wa Igunga ni mwanzo tena wa migogoro mingine, utawasikia watakapoanza kutuhumu wenzao watakaodaiwa kuhujumu.
6. Stori ya Gamba ndiyo imeenda hivyo, I will alwayz remember ile thread yako ya Mapacha watatu should stay put, CCM hana cha kuwafanya.
CUF:
1. Uchaguzi huu pia una maana kubwa sana kwa chama cha CUF kwani mgombea wao akipata say chini ya 10% of the votes ndiyo kitakuwa kimepoteza relevance machoni pa watanzania.
2. Habari ya ndoa ya CUF na CCM imeonekana kuresonate vizuri sana huko Igunga, na hii ndiyo hasa sababu ya CUF ku-retract kuishambulia CHADEMA kama walivyoonekana mwanzo. Wapiga kampeni wa CUF wakiiandama CHADEMA hata logically inaonekana aah! si ni CCM B hao.
3. Habari kwamba huku ni kwao Lipumba na CUF kuwa na influence mkoa wa Tabora inatakiwa ithibitishwe na uchaguzi huu otherwise watajikuta wanaingia ile ligi ya akina TLP, DP, UDP etc.
CHADEMA:
1. Amini usiamini na tuweke mbali ushabiki, chama chenye advantage kubwa uchaguzi huu ni CHADEMA all they need hata ikitokea bahati mbaya hawajashinda ni kupata kura very close na atakayetangazwa mshindi. Ikumbukwe kuwa wao hawakusimamisha mgombea hapo 2010 lakini kwa fair analysis wameihenyesha CCM mpaka aibu.
2. CHADEMA wakitangazwa washindi uchaguzi huu basi ndiyo itakuwa referendum 2015 na chaguzi nyingine kabla ya hapo zitakuwa na ahueni kidogo maana inaonyesha mbinu za CCM zimeshajulikana. Hii itafanya hata zile kesi za kipuuzi puuzi za kupinga matokeo ya wabunge wa CDM zisiingiliwe na watawala maana inajulikana wazi kwamba nafasi kwa CCM ni ndogo mno hata kama kutafanyika re-election.
3. CHADEMA baada ya uchaguzi huu itakuwa imejiongezea mtaji mkubwa kisiasa hasa kwa yale majimbo ambayo bado ni loyal kwa CCM.
Hivyo basi kwa majumuisho ya hoja, atakayetangazwa mshindi kwenye uchaguzi huu bado ni kitendawili. Lakini kama nilivyoainisha hapo juu CCM ndiyo ataibuka looser atangazwe awu asitangazwe mshindi unless it is a clear margin of say more than 30%. Any signs of that?
Kama hii ingekuwa kweli watu wengi zaidi pia wangejitokeza kumpigia mgombea wa Urais wa CDM. lakini Dr. Slaa alipata kama kura 6000 hivi Igunga na mgombea wa Uais wa CUF alipata kiasi gani?
Nilibahatika kushughudioa chaguzi ndongo kadhaa na ikiwemo Busanda na Biharamulo na kushuhudia jinsi wananchi wa mijini walivyohamanika na Chadema, lakini siku ya siku, kilichofuatia sote tunakijua, na matokeo mliyaona, hivyo kwa Igunga, sio tofauti ya Biharamulo na Busanda.
Amen...@Mageuzi