Elections 2010 KUMEKUCHA - 5: Ushindi wa Nani Igunga na kwanini..

analysis nzuri sana.............naamini matokeo yatakuwa hivyo bila shaka...................PEOPLES...POWER......
 
Aisee bado nakushangaa sana kwenye hilo hapo (kwenye red). Mbona kuna ushahidi wa kimahakama kuwa CCM ni wezi wa kura na ruling kadhaa za mahakama zimeshadhibitisha hilo..? Au unataka kuniambia mahakama iliionea CCM...? ili iweje..?
Rejea hapa Dr. Slaa alikua akimjibu GB:
 
CCM inashinda kwasababu kura 20,000 tu inatosha..zingine mgawane vyama vingine
 
Kwa nini pale umeandika Lowassa for Chairman? Unataka Lowassa awe Chairman wa nini? Kwa nini usiandike mada kwamba unataka Lowassa awe Chairman?
Kwa nini unasema ''ili CCM ishinde Igunga lazima itimize masharti haya na haya?'' Yaani CCM inaweza kushinda Igunga hata baada ya High Court kusema kwamba Dowans walipwe zile heka? Hata mshabiki wa CCM wa namna gani ataweza kuona kwamba huyo hakimu aliyeamua hivyo amekwishaizika CCM as far as Igunga is concerned. Lakini it does not mean that uamuzi wake ulilengwa kwa huu uchaguzi wa Igunga.
Maneno mengi yanasemwa kuhusu huyu Lowassa;kwamba analipia kampeni za wabunge,kwamba labda wabunge wachache,au wabunge wengi sana wameingia bungeni kwa msaada wake. Certainly,siku ile Waziri Sitta alipokuwa anakaimu Ukuu wa Bunge badala ya Pinda,alisema maneno kuwapinga wafisadi,halafu lile Bunge lilikuwa just one third full. You wonder what it was all about.
Siasa za Tanzania,CCM ni kama CCP,Chinese Communist Party au Russia United Party,chacha Putin. Wanabishana,wagombana wenyewe,halafu baadaye kabisa ndio wananchi wanfahamu nani atakuwa kiongozi.
Sisi wengine tutaona tu majina yanatajwatajwa,tunakuwa hatufamu kwa nini ''haya majina ya kipumbavu '' yanatajwa. Kumbe,we do not have our ear on the ground. Wale wengine ambao tunadhani ni ''majina ya kipumbavu'' ni watu wakubwa sana katika Chama.
 
Nimejitahidi kukuelewa unataka kusema nini lakini nimeambulia patupu.
 


You are very right Mwanakijiji kwa uchambuzi huo, na siku zote CCM hutumia sana hiyo mbinu kwani wanajua kuwa vijana wengi maneno mengi lakini wengi wao pia hawajajiandikisha na ukiwatishia kidogo hawaendi kupiga kura, huku wale wazee wao wanawahubiria kwamba wapitiane majumbani waende vituoni.

MUHIMU hapo vijana wote na wapenzi wa mageuzi wasitishike na wafike kwenye vituo vya kura hata kama kutakuwa na POLISI njia zote
 
Asante kwa analysis nzuri ila mwisho wa siku watu wa igunga tunawaachia kazi ya kutegua kitendawili hiki.
 
i wish chadema washinde huko Igunga maana haya magamba kila siku yanaboa
 
Tatizo letu limelala hapo kwenye kufikiri kwenye kujiokoa kila kinachoparamiwa ni kitu salama. kuna methali ya kiswahili inayosema 'mfa maji haishi kutapatapa.

Mimi sijaona kama nao CDM wako makini kwa wanachokifanya na wala kama wanajua kwa usahihi wapi wanataka kutupeleka kama chama tawala baada ya CCM. Mfano maandiko mengi humu ndani yanaonyesha kwamba wana JF wanaamini kwamba Waislamu(Viiongozi wao?) wanaishabikia CCM kuliko CDM. Lakini sijaona karipio kali kutoka kwa viongozi wa CDM dhidi ya tabia ya sehemu kubwa ya washabiki wao kudhania CDM ni chama kilicho dhidi ya uislamu.

Viongozi wengi wa CDM (Mbowe amejitoa) wanaamin kwamba Peoples powers inamaanisha ni matumizi ya nguvu kwenye kudai "haki" na "Ukamanda" ni ukakamavu kwenye kutokutii sheria na mapambano na Polisi hata bila ya sababu za msingi. hata humu ndani ukisema CDM wamekosea utarukiwa kama kibaka aliyekamatwa akitaka kuiba simu Kariakoo.

CDM kama chama hakina Oganaizesheni ya uhakika kwenye mambo yake ya kila siku na hakuna anayeonyesha kujali.Ukiwauliza watu CDM Makao Makuu ni kiasi gani fedha chama kitatumia kwenye uchaguzi wa Igunga na chaguzi ndogo za Madiwani inawezekana hawajui kabisa kwani fedha nyingi za kuendeshea chama ama "wanakopeshwa" na Mbowe au wanapewa "msaada" na Mzee Ndesamburo.
 

You got it all wrong!!!!!!
 
Mwanakijiji naomba twende sawa kwenye haya

Endapo kutakuwepo na fujo ama kuwepo umbali kwenda kupiga kura basi wazee na wake kwa ujumla wataudhuria kwa mashaka na hvyo itakuwa neg kwa CCM inayohitaji huruma ya akina mama na ujinga wa wazee ili ipate kura tofauti na CDM inawategemea vijana zaidi na kwa asilia vijana ni wabishi na ni wanamapinduzi wakubwa hivyo waweza kuiinua CDM

Nawashauri CDM waangalie hata jinsi ya kuyasaidia baadhi ya maeneo waliko na mitaji mikubwa ya wapiga kura waweze kupeleka usafiri ili iwe rahisi kwa watu kwenda kupiga kura pasipo kukosa,wakiweza katika hili watakuwa wametengeneza mkakati wa kupata kura kwa urahisi zaidi hata zile ambazo wasingezipata
 
Mzee Mwanakijiji, sahihisho dogo hapo kwenye Red.
1. Kwanza matokeo ya kila kituo, hubandikwa hapo hapo kituoni mara baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika na sio Bungeni! (I know you mean kituoni). Angalizo matokeo hayo hubandikwa tuu na sio kutangazwa!. Hata baada ya zoezi la kuhesabu kura kwenye vituo vyote kukamilika, hayo bado sio matokeo rasmi.
2. Matokeo rasmi ya jumla hutangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Returning Officer, ambaye hapa ni ajenti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, hivyo atakapoyatangaza, natangaza kwa niaba ya NEC, hivyo sio kweli kuwa matokeo hayatangazwi na NEC!.
4. Kwa case ya Igunga, zoezi la kuhesabu kura vituoni litakamilika by saa 3 usiku, hivyo within that time, kama Chadema itafanikiwa kuweka mawakala wake kote, then watakuwa wameshayajua matokeo ila hawaruhusiwi kuyatangaza mpaka yatakapotangazwa rasmi na msimamizi wa uchaguzi siku ya Jumatatu saa 4:00 asubuhi.
5. Kwa kumbukumbu ya zoefu wa uchaguzi mdogo wa Biharamulo, Chadema waliwapa simu za mkononi mawakala wao wote, huku laptop ya Zitto ikitumika kuhifadhi kumbukumbu. Kufikia saa 4 usiku walishapokea matokeo yote isipokuwa ya vituo sita vya kata ya Nyakananazi walikodai mawakala wao wametekwa. Wakajijumlishia wenyewe na kukuta margin ni kubwa kati ya ushindi wao na CCM, hivyo kuasume hata kama vituo vyote sita wataichagua CCM kwa asilimia 100%, wao bado ni washindi, wakajitangazia ushindi na mji wa Biharamulo ukalipuka kwa nderemo na vifijo kushereherea ushindi ambao ulidumu kwa muda mfupi tuu. Ilipofika saa 6:00 usiku CCM nao wakalipuka kwa ushindi!. Asubuhi CCM ikatangazwa imeshinda!.

4. Kitendo cha vyama kujitangazia matokeo yao kabla ya RO, ndiko kuhatarisha usalama wenyewe, nashukuru Mungu watu wa Bimulo ni wapole, hata baada ya kupokwa tonge mdomoni walitulia tuu, na hivyo ndivyo walivyo watu wa Igunga, lakini kuna maeneo ukishatangaza umeshinda ndio umeshinda, matokeo ya RO yakiwa ni tofauti, panakuwa hapakaliki!.
 

Asante kwa masahihisho.

a. Kwenye demokrasia na kwa mtindo wa mfumo wetu wa uchaguzi mtu yeyote kama anajua kujumlisha anaweza kumjulisha na kujua matokeo kabla ya kutangazwa. Huu ni mfumo unaotumika hata baadhi ya nchi japo wenzetu huwa wanatumia zile exit polls (kuwahoji waliokwishapiga kura) na kutoka hapo wanaweza kukisia matokeo ya jumla yatakuwaje.

b. Kosa kubwa liko kwa vyombo huru vya habari kwani vinategemea tume navyo kutangaza matokeo badala ya kuweka watu wao kila kituo au kufuatilia kila kituo na kujumlisha. Kwa kutumia vyombo vya habari huru kuweza kutangaza mshindi (to call the election) inazuia watu wengine kuchakachua kwa sababu vyombo vya habari itabidi vielezee tofauti ya hesabu yake na ile ya tume. Kosa kubwa la mwaka jana - hasa kwenye kura za urais - ni kuwa vyombo vya habari vilikatazwa kutangaza matokeo ya Urais kwa kadiri walivyoyapata. I believe it was one of the most shameful moment ya uhuru wa habari nchini.

Binafsi nimejiweka sawa hapa kuwa nitatangaza matokeo ya Igunga kwa kadiri yanavyokuja.
 
Asante Mzee Mwanakijiji, jumapili jioni macho na masikio yetu ni Igunga, hivyo tutakutembelea sana kule Mwanakijiji.com.
 
Kosa kubwa la mwaka jana - hasa kwenye kura za urais - ni kuwa vyombo vya habari vilikatazwa kutangaza matokeo ya Urais kwa kadiri walivyoyapata. I believe it was one of the most shameful moment ya uhuru wa habari nchini.

Kuna utaratibi fulani umezoeleka na CCM kwamba chochote wasichokipenda wao basi hupigwa ban. Lakini hao hao utasikia ooh nchi hii inaendeshwa kwa utawala wa sheria. Mara ooh! CCM inasimamia ustawi wa demokrasia wkati matendo yao yanaonyesha wazi kwamba demokrasia nik nzuri kwa mambo yale tu wanayoyapenda. Haiingii akilini mimi nipepiga kura kwenye kituo A, na matokeo yamebandikwa nje ya kituo, eti chombo cha habari kisitangaze, sasa wanabandika ya nini???????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…