Elections 2010 KUMEKUCHA - 5: Ushindi wa Nani Igunga na kwanini..

Ndugu yangu Kigarama, unapoamua kuwa mkweli siku zote, ujue pia kuna price to pay, yaani kuna Vigharama utaingia. Hivyo unapoikosoa Chadema humu kwenye jf, pia ujiendae kupokea malipo ya ukosoaji huo!.

Niliwahi kuposti hii...
[h=3]
CCM Imechokwa
; CHADEMA Haijajipanga!
[/h]
Nilichoambulia niliambulia lakini kwa vile huu ndio ukweli wangu, kila unapotimia nitakuwa nakumbushia.

 

1. Kutokana na maelezo yako hapo juu ina maana umekubaliana na hoja kuwa wizi wa kura upo?
2. Kwenye hoja yako hapo juu kipengele b. naomba nikusahihishe kuwa chombo chenye mamlaka kisheria kutangaza matokeo ni NEC kwa maana hiyo uhuru wa vyombo vya habari hautakiwi kuingilia/kukiuka sheria za nchi i.e vyombo vya habari haviko juu ya sheria.
3. Kumbuka wewe huna mamlaka kisheria ya kutangaza matokeo so ukifanya hivyo itakuwa kwa kujifurahisha tu kama alivyofanya Zitto kwenye Uchaguzi B'haramulo
 

Nimeisoma hiyo thread kama CHADEMA wangeichukulia serious leo Igunga tungeshuhudia chama siyo kundi la watu Maarufu wanaojitahidi kumsaidia mtu aliyegombea kwenye chama chao. watu wengi huwa hatujali kama kwa kuwatumia watu maarufu na siyo mfumo wa chama tunajenga madikteta badala kujenga mifumo mbadala.

Najua kwa hakika kwamba kabla ya RA kujiuzulu Igunga haikuwa kwenye mpango mkakati wa vyama vyote vilivyoko igunga. Si CCM, CUF au CHADEMA ambavyo kwenye ratiba zao za mwaka huu kulikuwa na safari ya igunga kwenda kuimarisha chama kwa kiwango cha Gharama hizi wanazozitumia kwenye uchaguzi huu.

Hata Igunga kwenyewe mikakati ya uchaguzi haipangwi tena na viongozi wa vyama hivyo wa Ngazi ya wilaya bali na "wataalamu' kutoka makao makuu ya vyama hivyo Dar es salaam. Wakati mwingine huwa najiuliza hivi vurumai yote hii ni kwa ajili ya Mbunge wa Igunga au ni kwa sababu ya hadhi ya hawa kina Mbowe na kikwete.

Si CCM wala CDM ambao kwa sasa wanaonekana kuukimbia mtego wa kuamini kuwa kazi pekee ya siasa ni kushinda uchaguzi. Nimempenda sana Makongoro Nyerere ambaye amesema wazi kwamba uchaguzi wa Igunga ni kazi ya uongozi wa CCM ngazi ya Mkoa na Wilaya.
 
Kwa kweli, matokeo yanavyozidi kuonesha sasa hivi ndivyo ambavyo nilikuwa nadhania. Wapigaji kura wamekuwa wachache sana na kama nilivyosema hiyo itainufaisha CCM zaidi. Na kwa sababu suala la matokeo litaamuliwa kwa namba naamini hakuna atakayepata kura zaidi ya asilimia 50. CCM so far wana edge.
 

Naona nilichokisema mwanznoni kuhusu CUF kinatimia, Prof. Lipumba sijui ataficha wapi uso wake!!!!!! Annywayz ndiyo siasa lakini..., CUF ndiyo imeenda hivyo ligi yao sasa ni ile ya akina TLP, DP, UPDP, SAU etc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…