Kumekucha! Bifu la Watangazaji wa Shilawadu na RC Makonda lafikia patamu na limenoga sasa

Lakini leo si ilikuwa fools day? Yaani thread zote za leo wala siziamini.
 
halafu nilisikia na neno "jini mkata kamba" sijui walikuwa wana maana gani
 
Wadada sio...[emoji23]
 
Mbona ni mipasho tu hata kwenye taarabu na singeli ipo? Mvamizi anaweza kwenda kuwasalimia, ule ulikuwa mchezo tu na umepita.Kwani kulikuwa na mtifuano gani usioisha? Wale na mvamizi wao ni marafiki wakubwa na hawana shida
 
Shilawadu ni watoto wa kishua.Hawana shida na mshua mwenzao katika kupeana ubuyu.Lile varangati lilikuwa ni dili feki lilishindikana kuchezwa ndiyo washua wakatofautiana.By the way wale bado ni marafiki wakubwa Pomoja na kutofautiana katika ngawira yao hiyo.Si ajabu mshua wao huyo siku moja ataenda kuwapa hai
 
Jana na Mimi nimeangalia kipindi inaonekana kweli mkuu GENTAMYCINE huyu Daudi Bashite ananuka miguu na mdomo nimeona Yale madongo kwa Paul Makonda

Nashukuru kwa kunielewa Mkuu ila na Yeye RC Makonda kayataka mwenyewe haya yote kwani nakumbuka alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na hadi hivi kuwa RC wa Dar es Salaam alikuwa akipenda mno kushinda pale Clouds Media Group muda wote na pengine haya matatizo yake ya Soksi, Miguu na Mdomo walishayajua ' Kitambo ' na walikuwa wanampa tu kiaina ' ushirikiano ' wa ' kumchunia ' ila Jamaa alipowatibua tu wiki mbili tu zilizopita na Wao wakaona isiwe taabu ' watuanikie ' Watanzania ' siri ' zake na hakika Watangazaji wa SHILAWADU jana wamemuanika mno Makonda na kwa jinsi nilivyowaona nahisi kuna ' siri ' zake zingine zaidi tena ' nyeti ' kabisa madogo hawa akina Soud Brown na Kwissa wanazijua na pengine tusishangae hata katika Kipindi kijacho cha SHILAWADU tunakapata ' series ' nyingine ya ' mapungufu ' yake ya aibu.

Pole sana Makonda hata hivyo uliyataka haya mwenyewe kwani kama unakumbuka kuna ' uzi ' mmoja humu niliwahi kuuandika na kukuonya kuhusu ukaribu wako usio wa kifani na hawa Clouds na jinsi gani ya kuwa makini nao ila kama kawaida ukaona GENTAMYCINE huwa nikiwa humu JF huwa napoteza tu muda wakati kumbe Mimi ni ' Malaika ' niliyetukuka ambaye Kazi yangu Kuu ni kukushauri, kukuongoza na kukuepusha na mabaya ambayo huwa nayaona mapema mno.

Mfano huyu Dada Shyrose Bhanji kama kweli angeusoma na kuuelewa kwa umakini mkubwa ule ' uzi ' wangu ambao niliuanzisha humu JF mwaka jana ambapo kwanza nilianza kwa ' kumponda ' kiaina na baadae nikamshauri mambo fulani sidhani kama angepata ile aibu ya juzi iliyompata huko Dodoma kwani katika ule uzi niliandika kwa kiasi kikubwa mno mapungufu yake ambaye tena nikasema wazi kuwa kama asiposhtuka na kuyafanyia Kazi mapema yatakuja kumgharimu siku moja katika safari yake ya Kisiasa na bahati ndicho kilimchomtokea Dada wa Watu.

Akhsante sana Mwenyezi Mungu kwa ' kunibariki ' huko na kunifanya kweli niwe ' talented and charismatic '.
 
Eti marinda yakishaondoka unakabiliwa na matatizo mengi likiwamo la kunuka mdomo na miguu.

Ha ha ha ha ha ha ha ....... madogo ' wameua ' sana jana. Jamaa ama hakika ' kaumbuka ' sana na sijui Jamii itamwonaje sasa kwani nahisi sasa atakuwa kila akiwa anahutubia tu zile mic ziwe zinaoshwa kwanza kwa kulowekwa katika maji ili kuondoa ' bacteria ' wanaosababishwa harufu ya ' Ndomo ' na kuna uwezekano hata Watu wakawa wanakaa nae mbali ili kuepuka harufu yake kali ya ama Soksi au Miguu.

Rais JPM yote haya umeyataka mwenyewe kwani tulikuambia mapema sana kuwa ' mtumbue ' Makonda kwani yawezekana kuna ' makombora ' mengine Watu walikuwa wameyahifadhi kwa muda tu ila sasa baada ya kukuona Wewe ' ukidinda ' kumtumbua nao wameamua ' kufunguka ' kama hivi.

Kweli nimeamini kuwa Watu ' wakikutafuta ' hawakukosi hakyanani!
 
Hawana ubunifu kwa ninapokutana na kusoma juu yao na udaku wa uongo ambao haujaenda shule, wanaishia kutunga kama walivyozoea ya mambo juu ya watu. Wanajua hakuna wa kuhakikisha uongo wao kama nilivyowasoma kabla wakimsingizia Diamond mambo, ila baadae ukweli uonekana.

Wangekuwa wagumu na wanaakili wasinge tafuta kiki ya kujifanya waliumizwa, huku walikuwa salama kabisa na kurudi na kuongelea ujinga. Gemu lao lilibuma lazima uwaume

Sijawahi kuangalia kipindi chao na sitakiangalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…