Kumekucha: DAWASA yatoa ratiba ya mgao wa maji Dar es Salaam

Kumekucha: DAWASA yatoa ratiba ya mgao wa maji Dar es Salaam

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mamlaka ya maji safi na maji taka Dar es Salaam imetangaza mgao wa maji jiji la Dar es Salaam kanda ya Kinondoni ili kupunguza kero kwenye maeneo yanayotajwa kuwa na msukumo mdogo.

Katika ratiba hiyo wakaazi wa Masaki, Mikocheni na Obey wameula, watapata maji saa 24 siku saba za wiki. Baadhi ya maeneo sijayaona kabisa pia tangazo halina mwanzo wala ukomo wa mgao.

Anyways tunawasubiri Tanesco nao watoe ratiba badala ya kwenda kimya kimya pia wasisahau majenereta ya IPTL, tuko tayari kuchangia akaunti ya Tegeta Escrow..

Dawasa.jpg

 
JPM alisema mtamkumbuka, mtamkumbuka tu... sio ombi! Pale samaki wenu watakapoanza kuoza kwa kukosa umeme wa mafriji, pale mtakapoanza kukosa maji ya kufanyia shughuli za kila siku...
Sasa hapo obei na masaki wanatumia mfumo tofauti??
Bora kukosa Maji na umeme kuliko kutekana kidwanzi na mtu mmoja kujifanya ndio mungu mtu nchi nzima.
 
Kuna wilaya haziguswi na DAWASA kabisa wilaya ya Kigamboni, Ubungo, Temeke na Ukonga wao wamejizoelea kunywa maji ya madimbwi wanayojichimbia na Maji ya mvua.

Ukiwaangalia hata muonekano wa sura wanaotoka maeneo hayo yasiyo na ratiba wako tofauti na huko kwenye ratiba ya Dawasa sura zao zimekakamaa hasa

Ratiba haiwahusu
 
Nchi imefunguliwa.
Eeh nchi inafunguliwa bwana toka kwa dhalimu jiwe 😅!

Dhalimu ambaye hajawahi kuwalaza gizani zaidi ya masaa 24 katika siku zote ambazo alikuwa madarakani! Maji hayakuwahi kukatika katika namna yeyote isioeleweka😅

“Sote tu watu wazima haina haja ya kufatiliana na kutumbuana kila mtu afanye majukumu yake kwa moyo”~Amiri jeshi

Ha ha ha ha ha ha! Wacha nifike mlimani nikajipooze na AC za umma kwanza😅 hii joto ya huku uswahilini haifai!
 
Back
Top Bottom