Nimeshindwa kwenda chuo kwa sababu sina maji siku ya nne, sijaoga, maji ghetto yameisha, foleni ya maji yanayopatikana sijui inaanza lini na kuisha lini kila nikienda watu wanachota haijalishi ni saa 5 usiku au saa 11 alfajiri. Mtu anakuja na dumu 30 anapanga mstari na hawa ni wengi, sisi tumehamia hosteli kufua, vyoo na kuongea uko. Alafu nako ni foleni.
Nimepika jana mchana nikaja cheki maji ya kuoshea vyombo hakuna nikaviacha. Jioni nimeenda kula chips at least ndio vyakula vya kukaanga havina madhara sana maji yasipokuwepo ila nikakuta maji yanayooshea viazi ni machafu kuliko ambayo ningeoshea viatu.
Nikatoka zangu kuja kwa family relative mmoja mitaa ya Tabata ana visima nikaambiwa gari zinasomba maji kupeleka Masaki.
Miaka 60 ya uhuru, waliozaliwa tunapata uhuru ndio wanastaafu ila hatuna vyanzo vya uhakika vya maji kwenye jiji kuu la biashara na mji mkuu