Kumekucha DSTV, Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo na msaidizi wake wasimamishwa kwa rushwa!

Mpali ilikuwa ya moto pale mwanzoni bwana.

Alipozidi kuongeza wanawake hadi wazungu ikapoteza ladha.
Bora hata hao wameongeza wanawake,mi huba ndo sielewi mwelekeo wake kila siku watu wanaanzisha mapenzi hovyohovyo sijui maudhui yake ni yapi yaani hata direction haieleweki kila siku watu wanapendana

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Watu hawajui tu, hayo maigizo yamewashika watu sana.

Mimi nilikuwa nayadharau hadi nilipochangamana na watu ndio nikajua.
Watu wanachukulia poa..
Mm mwenyewe nilipoanza kufatilia nikatekwa.
Yaani heri mtu asile nyama ila aweke kifurushi 🤣🤣
Mabeki tatu ndo wadau namba Moja 🙌

Zile za kikorea na zingine zilizotafsiriwa sitaki kabisa kufatilia maana zimewashika watu balaa.

Zangu bongo movies tu,, so far tumepiga hatua watz.
 
Tz taifa la hongo!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Nimeshapoa.

Huo ubuyu wa moto ni next weekend, wala usijali kabati langu halikaukiwi ubuyu.

Tutakuwa na holidays nzuri, tuombe uzima na kukiombea chanzo changu pia.
Mtafanya na sisi Wazee tuhamie mitaa ya Watu maarufu(Celebrates forum) ili kuja kusoma huo Ubuyu.

Fanya hivyo ili kumuenzi mdau pamoja na kulipa uhai Jukwaa la Macelebrates maana tangu atutoke Warumi Jukwaa bado halijapata mrithi wake japo baadhi wanajaribu lakini inaonekana viatu vyake vimekosa mtu sahihi.
 
Wizi ni tabia za kiume?. Mbona siku hizi kuna wamama wezi wengi tu.
Nimemshangaa sana huyo member kwa kuihusishanisha tabia ya wizi na uanaume, huyo inaonekana ni mtu aliyelelewa kwa kuaminishwa kwamba wanawake siku zote ni innocent na waaminifu na hawana kabisa kasumba za udokozi wala ujambazi, na ndio maana ameonesha kushangazwa na hii habari.

Yaani jamaa ameshindwa kabisa hata kuangalia mifano ya akina Tibaijuka,Hawa Gasia,Angelina na mama Fulani nimemsahau jina alikuwa mkurugenzi wa MSD enzi za awamu ya nne hili aondokane na hiyo Imani aliyonayo na kutambua kwamba hata wanawake pia ni majizi vile vile na Tena ni majizi haswa wakiamua.
 

Hapo kwa maafande Huwa pananiumiza sana, hivi kwanini askari wabongo kutimiza wajibu wake mpaka umfurahishe kwa kumpa hongo kidogo? Kiukweli hakuna askari aliyewahi kunisaidia pasipo kumrefushia mkono!

Sasa huko kunaitwa kujiongeza na Wala sio upigaji huo maana mtoaji wa hela kaitoa bila manung'uniko ya aina yoyote[/red]
Kupiga pesa isivyo halali kwa namna yeyote ile ni kubaya.
Mbongo anakwambia pesa ni pesa haijalishi umeipata vipi maana hakuna sehemu utakayoenda kuitumia wataikataa kisa umeipata kwa njia isiyokuwa ya halali.
 
Nafikiri sababu umeijua leo sasa, huenda baada ya hili sakata hizo tamthilia zitaisha.
 
Shaka ondoa, pele limepata mkunaji.

Tuombe uzima tu, tutakuwa na wakati mzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…